JamiiForums Usiku wa manane
Episode 4
Wakati tuna toka kwenye geti la kanisa. Pembeni kulikuwa na bustani ndogo ina maua mazuri na kuna viti baadhi ya watu wamekaa au wamesimama wana piga story. Nikamuona yule sista mrembo, nika muuliza Chris
"una mfahamu yule dada mwenye gauni jekundu?"
Chris Akasema ana mfahamu ila huwa ana muona tuu, lakini ana wafahamu wale kina dada wengine anao zungumza nao. Kabla sija sema lolote, sauti ikatokea kule waliko wale kina dada,
"Chris, we Chris, leo uko na mgeni ndio hutusalimii eeh!?"
Chris akasema hebu twende tukawasalimie wale kina dada, moyoni nililipuka kwa furaha, iliyo changanyikana na woga
View attachment 780953
hahaha aisee braza safi kwa story, na hivi vipicha vya hao watt na situation ya rafk yake chriss nacheka sana...
 
Episode 5
Tulisogea pale tuka salimiana, wale kina dada wakamwambia Chris awaambie naitwa nani nikawahi mwenyewe.
"Naitwa TJ " wakawa kama hawa amini "Just TJ" nika nika waambia ndio hivo just TJ na Chris naye akasema ni hilo hilo TJ ndo jina langu, wakajibu kwa tabasamu pana "woouw its good good name". Chris akaanza kunitambulisha dada mmoja mmoja, "huyu ni Maggie, huyu ni Karen, huyu ni Tusubilege huwa tuna muita white" (Tusu alikuwa ni mweusi sanaa kama sufuria yenye masizi kwa hiyo woote tuliangua vicheko pale).
Chris hakumalizia kuwatambulisha kina dada wawili akiwemo yule mrembo. Hivo tuka baki wote kimya, Karen akamwuliza Chris kwa nini asimalizie kutambulisha, Chris akasema hawa ni watu special wajitambulishe wenyewe. Akaanza dada mmoja pembeni ya yule mrembo akasema ana itwa Nina, ikafika zamu ya mrembo akasema "Mimi naitwa Cynthia" nilipoteza network kwa dakika chache kwani sauti ya Cynthia ilijuwa ni nyororo na ya upole yaan aliendelea kunichanganya zaid. Basi mimi sikuongea tena nikawa mkimya na akili ikahama kama nimepigwa na butwaa
IMG_20180519_013750.jpg
 
Back
Top Bottom