JamiiForums Usiku wa manane
Nilikuwa nimerudi kutoka chuoni Eldoret, Kenya. Kwa hiyo nikawa nipo likizo nika kutana na rafiki yangu Cris. Jumamosi moja akanipigia simu. Akaniambia kesho twende kanisani kwao wanaibada nzuri. Tukakubaliana kesho yake jumapili nitaenda usiku nika nyoosha nguo zangu vizuri. Nikawahi kulala.
Nilishtuliwa na simu
"Halo"
"Halo bado umelala?"
"Eeh nimelala"
"Amkaa, ni saa mbili kasoro tayari"

Alikuwa ni Cris, Nika amka fasta nika oga, nika vaaa, tukaondoka mpaka kanisani kwa Cris.

HADITHI
 
Episode 2

Tulifika kanisani, watu walikuwa ni wengi, wa kila aina, Ibada ikaanza ukapigwa mziki mzuri na mimi na Chris hatukujizuia tukaenda mbele kucheza, mziki ulikuwa mzuri na waimbaji waliimba kwa ustadi. wakati tume maliza kucheza ili turudi kukaa upande wangu wa kushoto nikamuona msichana mrembo, mrefu wa wastani, amevaa gauni jekundu lenye urefu wa kawaida, amesuka rasta nyeusi na amezifunga kwa ustadi mkubwa. alikuwa ni mweupe pee! Hiyo namna hiyo ya uvaaji iliongeza umaridadi wa msichana yule, nilipigwa na butwaa. Wakati nina endelea kumshangaa Chris akanisukuma akisema
"Rudi kukaa, unazuia watu"
Nili rudi kukaa haraka lakini kwa kweli nilikuwa sielewi kinacho endelea, ninacho kumbuka nilimuona mchungaji anazungumza maneno ambayo sikuwa nayasikia vizuri akili yote ilihamia kwa dada yule mrembo.
Kuna time nili mwangalia na yeye akaniona akatabasamu hapo mimi moyoni nasema "Yees" 'baada ya ibada lazima niongee na huyu mrembo ni lazimaaaa
 
Nilikuwa nimerudi kutoka chuoni Eldoret, Kenya. Kwa hiyo nikawa nipo likizo nika kutana na rafiki yangu Cris. Jumamosi moja akanipigia simu. Akaniambia kesho twende kanisani kwao wanaibada nzuri. Tukakubaliana kesho yake jumapili nitaenda usiku nika nyoosha nguo zangu vizuri. Nikawahi kulala.
Nilishtuliwa na simu
"Halo"
"Halo bado umelala?"
"Eeh nimelala"
"Amkaa, ni saa mbili kasoro tayari"

Alikuwa ni Cris, Nika amka fasta nika oga, nika vaaa, tukaondoka mpaka kanisani kwa Cris.

HADITHI
...hadith njoo ukweli njoo utamu kolea
 
Episode 3
Wakati wa kufunga ibada mchungaji akasema wageni wote tulio fika kusali kwa mara ya kwanza tusimame. Tulisimama, tuka ambiwa tuchukue kila tulicho nacho tuelekee kwenye ukumbi mdogo wa kanisa kwa dakika 5 tuu. Nikataka nikaushe Chris akanilazimisha niende akasema uta enjoy.

Muda ule wageni tunatoka, mchungaji akawa anafunga ibada ila.natoka tuu nikasikie mchungaji anasema
"bwana awe nanyi"
washarika waka itikia "awe nawe pia"
aka waruhusu watawanyike. Moyo wangu ulilia 'paaa' nikasema basi nime kwisha mkosa mrembo.

Tuli ingia ndani ya ukumbi tukatambulishwa kanisa na kukaribishwa. Tulipewa Soda na sambusa ambazo kutokana na mawazo sikula. Tulipo ambiwa tutawanyike nikarudi fasta ndani ya kanisa. Nilimtafuta yule mrembo sikumuona, nika sikima mtu ana nigusa kwa nyuma, nikawa kama nimepigwa shot.
Nikageuka nika kuta ni Chris.
"Ulikuwa una nitafuta ee"
Nikasema "Ndio" huku nikiwa na hasira.
Tuka toka, kuelekea kwenye gari ya Chris tuliyo kuja nayo. Hapo am very mad....

IMG_20180419_004904.jpg
 
Episode 4
Wakati tuna toka kwenye geti la kanisa. Pembeni kulikuwa na bustani ndogo ina maua mazuri na kuna viti baadhi ya watu wamekaa au wamesimama wana piga story. Nikamuona yule sista mrembo, nika muuliza Chris
"una mfahamu yule dada mwenye gauni jekundu?"
Chris Akasema ana mfahamu ila huwa ana muona tuu, lakini ana wafahamu wale kina dada wengine anao zungumza nao. Kabla sija sema lolote, sauti ikatokea kule waliko wale kina dada,
"Chris, we Chris, leo uko na mgeni ndio hutusalimii eeh!?"
Chris akasema hebu twende tukawasalimie wale kina dada, moyoni nililipuka kwa furaha, iliyo changanyikana na woga
IMG_20180422_233726.jpg
 
Episode 3
Wakati wa kufunga ibada mchungaji akasema wageni wote tulio fika kusali kwa mara ya kwanza tusimame. Tulisimama, tuka ambiwa tuchukue kila tulicho nacho tuelekee kwenye ukumbi mdogo wa kanisa kwa dakika 5 tuu. Nikataka nikaushe Chris akanilazimisha niende akasema uta enjoy.

Muda ule wageni tunatoka, mchungaji akawa anafunga ibada ila.natoka tuu nikasikie mchungaji anasema
"bwana awe nanyi"
washarika waka itikia "awe nawe pia"
aka waruhusu watawanyike. Moyo wangu ulilia 'paaa' nikasema basi nime kwisha mkosa mrembo.

Tuli ingia ndani ya ukumbi tukatambulishwa kanisa na kukaribishwa. Tulipewa Soda na sambusa ambazo kutokana na mawazo sikula. Tulipo ambiwa tutawanyike nikarudi fasta ndani ya kanisa. Nilimtafuta yule mrembo sikumuona, nika sikima mtu ana nigusa kwa nyuma, nikawa kama nimepigwa shot.
Nikageuka nika kuta ni Chris.
"Ulikuwa una nitafuta ee"
Nikasema "Ndio" huku nikiwa na hasira.
Tuka toka, kuelekea kwenye gari ya Chris tuliyo kuja nayo. Hapo am very mad....

View attachment 780952
 
Back
Top Bottom