Jaji Warioba: Dkt. Bashiru ajibiwe kwa hoja, hajafanya kosa lolote acheni kumshambulia

Hapa ndipo unapotofautisha maoni ya msomi, na mashabiki wanaotafuta madaraka na vyeo kwa kumshambulia Bashiru kwa ajili ya matumbo yao.

Utashangaa mpaka kina Msukuma na Lusinde leo wanaonekana wa maana kisa wanamshambulia Bashiru, tuna taifa la mihemko sana, ambalo kila siku linazidi kupoteza muelekeo.
 
CCM hawanaga Uwezo wa kujibu hoja, watatumia Akina Kibajaji na wengine, ikishindikana watatumia Jeshi la Polisi, usalama na Mahakama. Ndio Mwisho wa akili zao. Ukibisha wewe ni nbwa
..Bashiru amejibiwa, hajashambuliwa.

..labda tuseme hatupendi jinsi alivyojibiwa.

..walioshambuliwa ni Lissu, Mdude, Roma Mkatoliki, na wanaharakati wengine.

Cc Erythrocyte, Nguruvi3
Saaaafi sana sana Kaka
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, ameeleza kuwa Balozi Bashiru Ally, hajafanya kosa lolote hakustahili kushambuliwa. Amesema, watu wajibu hoja badala ya kumshambulia yeye binafsi.

View attachment 2423235

Chanzo: Mwanahalisi
Katika wazee wachache mno waliobakia ndani ya CCM na wenye kuheshimika na kuaminika, basi mmoja wao ni Mzee Warioba. Kwa haraka haraka nafikiri watakuwa wamebakia wawili ama watatu tu.

Yaliyobakia ni majizi, maongo na yasiyoaminika kabisa. Mazee yaliyobakia ndani ya CCM ni laana kwa nchi na taifa letu.
 
Dr.Bashiru katika video hii fupi binafsi sijaona wala kusikia akiongea baya lolote, hasa kwa watu aliokuwa anaongea nao, hii kauli ya Bashiru tafsri yake ni kwamba lazima tuwawajibishe Watawala, wao kututumikia sio fadhila bali ni wajibu wao.
Msikilize Dr. Bashiru halafu uamue kama tumsimange au tufuate ushauri wake.
 
Asante Kwa kuja Mzee wetu WARIOBA.

RASIMU yetu uliyowakabidhi wameitia KAPUNI ni suala la muda tu itarudi mezani.

Nasubiri atakayekujibu Kwa HOJA CCM nami nimjibu😃😃😃😃
 
Nipe mfano mmoja wa kiongozi wa Chadema au ACT au CUF aliyekikosoa chama chake au kiongozi wake halafu akabaki salama kwa kigezo cha demokrasia. Unijibu ukimkumbuka Chacha Wangwe.
Ubaya mpya hauhalalishi ubaya wa zamani.muwe na hekima kama hamnazo basi jilazimisheni angalau.
 
Pia ajibiwe na aliowasema sio chawa wao.

Bashiru kamsema Samia Ila ajabu anajibiwa na wakina Kigwangala.

Kigwangala ana cheo gani serikalini Cha kumjibia Samia

Samia atoke ajibu hoja za bashiru mwenyewe sio kuwatuma mawakala wa unaupiga mwingi
Kabisa
 
..Bashiru amejibiwa, hajashambuliwa.

..labda tuseme hatupendi jinsi alivyojibiwa.

..walioshambuliwa ni Lissu, Mdude, Roma Mkatoliki, na wanaharakati wengine.

Cc Erythrocyte, Nguruvi3
Hebu tupe mfano wa mtu mmoja toka CCM, au wale wengine mashabiki wa walamba asali aliyejibu hoja za Dr. Bashiru ukiondoa hizo kelele za kina Lusinde na wenzake.

Halafu unawaingiza wakina Lissu na wengine sijui wanahusiana nini kwenye kujibu hoja za Dr. Bashiru, mimi naona ndio unataka apuuzwe kisa historia yake.

Mtambue whatever Dr. Bashiru alifanya kabla, hakumuondolei haki yake ya kuzungumza na hoja zake kujibiwa.

Hiki mnacholazimisha kuleta ndicho kinawakuta nanyi halafu mnalalamika, ndio maana mikutano ya siasa mmezuiwa japo ni haki yenu, mnaendelea kuwakomaza CCM wazidi kuvunja sheria bila kujua, amkeni; msiwe wabinafsi, haki haichagui rangi, historia, wala chochote..

Ukimnyima haki mwenzio mjue nanyi mtamyimwa, coz anayemnyima huyo ndie anaewanyima nyie, mjifunze kuihubiri demokrasia na kuitenda, sio mnaishia kuihubiri pekee, hii demokrasia yenu unayoileta ina exceptions, hamtaki fulani asikilizwe kisa historia yake, hii kitu haipo hapa duniani.
 
Mzee maisha yamempiga, anahaha tu kutafuta ajira kupitia wapiga debe wa katiba mpya.

Huyu alikaa na Nyerere kwa miongo kadhaa, hakumshauri kuhusu katiba, na aliiacha nchi imefilisika, kwa Sasa hivi hana la kutushauri, ni mtu wa hovyo tu, na pia alikula Hela katika kashfa ya meremeta.

Matapeli wa kisiasa waliobaki
JIBU HOJA popoma wewe!!! Nchi Iko gizani na matatizo lukuki, anaupigaje mwingi''!!!
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, ameeleza kuwa Balozi Bashiru Ally, hajafanya kosa lolote hakustahili kushambuliwa. Amesema, watu wajibu hoja badala ya kumshambulia yeye binafsi.

View attachment 2423235

Chanzo: Mwanahalisi
Yeah Dr Bashiru Ally Kakurwa ajibiwe kwa hoja. Sio chawa wamevimbiwa asali wanaanza kutukana mtu wala uwezo kumuelewa hawana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom