Kikwete: Naomba yasinikute ya jaji Warioba

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Katika hali ya kushangaza, rais Jakaya Kikwete ameonesha kuunga mkono udhalilishaji aliofanyiwa mwenyekiti wa iliyokuwa tume ya kukusanya maoni ya kuandika katiba mpya jaji Joseph Warioba.

Akipiga kijembe kwa jaji Warioba, Kikwete alisema kuwa "Naomba sana yasije yakanikuta yaliyomkuta Warioba" bila kutoa ufafanuzi wa zaidi.

Jaji Warioba alifanyiwa vitendo vya kumdhalilisha wakati wa kongamano la katiba lililofanyika juzi jijini Dar es Salaam ambapo vijana 'wahuni' wa UVCCM wakiongozwa na kiongozi wao Paul Makonda walivamia kongamano hilo na kuanzisha fujo huku Makonda akimzaba kibao jaji Joseph Warioba.

Jaji Warioba amewahi kuwa makamu wa rais enzi za utawala wa awamu ya pili.
==============================================

Dar/mikoani. Rais Jakaya Kikwete amesema anaomba yasimkute ya Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba aliyeshambuliwa katika mdahalo wa katiba uliofanyika Dar es Salaam, juzi.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo Mwanza jana katika mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kupambana na Rushwa (Safac) unaojumuisha nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc).

"Naamini Katiba Inayopendekezwa itapitishwa, nina matumaini hayo. Nadhani na mimi nitakavyokuwa napiga kampeni hayatatokea yale ya jana(juzi), maana mie sioni haya kuipigia kampeni kama wale wenzetu ambao wanataka isipite," alisema Rais Kikwete kwa ufupi.

Juzi, Jaji Warioba alishambuliwa na kundi dogo la watu walioingia katika mdahalo ulioitishwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kutolewa chini ya ulinzi.

Vurugu hizo zilitokea wakati Jaji Warioba alipokuwa akihitimisha hotuba yake kwa kuhoji watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Julius Nyerere kupitisha hoja zao katika misingi isiyokubalika.

Miongoni mwa wanaotuhumiwa kumshambulia Jaji Warioba ni Katibu wa Hamasa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), Paul Makonda ambaye hata hivyo, jana alikana kufanya kitendo hicho.

Tukio lakemewa kila kona

Wasomi, wanasiasa na wananchi wa kada mbalimbali nchini wamelaani vurugu zilizotokea katika mdahalo huo na zaidi, kitendo cha Jaji Warioba kuvamiwa na kupigwa.

Mbali na kulaani, mjumbe wa iliyokuwa Tume hiyo, Profesa Mwesiga Baregu alimtaka Rais Kikwete kutoa tamko, huku wanaharakati na wasomi wakitaka ulinzi uimarishwe kwa viongozi wa kitaifa wakiwamo wastaafu.

Profesa Baregu alisema ni vizuri kwa Rais akatoa tamko kuhusu tukio hilo ili kunusuru mchakato mzima wa Katiba Mpya.

"Nashangaa mpaka sasa Serikali imekaa kimya licha ya kutokea kwa tukio hili la aibu kwa Taifa, ambalo unaweza ukahisi lilipangwa ili kuhatarisha usalama wa wananchi," alisema na kuongeza:

"Jaji Warioba kwa wadhifa wake, anatakiwa kupatiwa ulinzi wa kutosha kama walivyo viongozi wengine wastaafu, lakini cha kushangaza jana (juzi) mpaka tunaanza mdahalo hakukuwa na askari hata mmoja ndani ya ukumbi, badala yake walikuwa nje ya jengo lile."

Alisema kwa mwenendo uliopo sasa, itakuwa vigumu kupatikana Katiba Mpya kwani wananchi wanakoseshwa haki zao za msingi ikiwamo usalama.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee alilaani kitendo hicho na kuitaka Serikali kuwachukulia hatua kali waliohusika.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Nyalikungu Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Mdee alimtuhumu Makonda na wenzake kuwa wamefanya tukio ambalo limeidhalilisha nchi.

"Tunalaani vikali kilichomtokea Warioba ...nani asiyefahamu uadilifu wa Warioba? Eti wanampiga, hili hatuwezi kukubali litokee tena. Serikali iwachukulie hatua kali kwani waliofanya wanajulikana kwa nini kuwaficha au kosa la Warioba ni lipi?"

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema viongozi wa kitaifa wanatakiwa kupewa ulinzi wa kutosha na kitendo kilichotokea juzi ni aibu kwa Taifa zima.

Mwenyekiti wa PPT - Maendeleo, Peter Mziray alisema viongozi wastaafu wasijihusishe kabisa na masuala ya kisiasa badala yake wapumzike kama alivyoamua Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikataa kuzungumzia lolote akisema yupo nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba la Tanzania (Jukata), Deus Kibamba alisema vurugu hizo ni maafa na uhuni wa kutisha unaostahili kulaaniwa.

"Sitaki kuamini kuwa wale vijana wahuni walitumwa na CCM, sitaki kuamini hata kidogo… hali ile ni maafa. Ulinzi na usalama umekwisha kabisa," alisema na kuongeza: "Hii hali ya kusubiri mpaka maafa yatokee haifai. Warioba ana mlinzi mmoja na sisi jana tulikuwapo pale ilifikia kipindi hadi walinzi wa Jukata waliingia kumsaidia Warioba, ni aibu kubwa."

Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Patience Mlowe alisema vurugu hizo zimemshangaza kila mpenda amani na demokrasia.

"Ni fedheha kwa Taifa. Warioba ni Makamu wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, halafu vijana wanashindwa kumheshimu… hili ni janga kwa Taifa," alisema Mlowe.

Mbunge wa zamani wa Vunjo, Aloyce Kimaro alisema kitendo alichofanyiwa Jaji Warioba hakijawahi kufanywa tangu nchi ipate uhuru na kwamba waliofanya kitendo hicho wanataka kuharibu utawala wa Rais Kikwete ambaye amewapa Watanzania uhuru wa kuzungumza.

"Hao wahuni waliompiga Warioba walionekana vizuri kwenye runinga. Serikali iwachukulie hatua kali kwa kuwa wamedhalilisha nchi, pia Watanzania tujifunze kusikiliza maoni ya mtu hata kama yanakukera," alisema.

Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei aliwataka Watanzania kulaani kitendo hicho huku akimtaka Jaji Warioba asikate tamaa, bali aendelee kutetea maoni ya wananchi.

Mtei alisema kilichofanyika ni sawa na laana kwa vijana kwani haiwezekani kuwashambulia wazee wenye heshima kubwa katika Taifa bila sababu za msingi.

CUF kulinda midahalo


Chama cha Wananchi (CUF) mbali ya kulaani, kimekwenda mbali na kikisema kinachukua dhamana ya kuilinda midahalo yote itakayomhusu Jaji Warioba, waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko Katiba na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), kwa nia njema ya kutoa elimu ya uraia juu ya Katiba Inayopendekezwa.

Taarifa ya Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Abdul Kambaya ilisema chama hicho kimeamua kuchukua dhamana hiyo kwa kuwa polisi wameshindwa kutekeleza wajibu wao.

"Jaji Warioba ni kiongozi wa Taifa hili, hivyo kwa namna yoyote ile hawezi kudhalilishwa huku CUF kama wadau wa mambo ya siasa na elimu ya uraia tukiwa kimya," ilisema taarifa hiyo ya Kambaya.

Makonda ajitetea

Wakati wanasiasa na mitandao ya kijamii ikimlaani Makonda, kiongozi huyo jana aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema hakumpiga Jaji Warioba, bali alikuwa akimwokoa katika vurugu hizo.

Makonda alisema baada ya vurugu hizo kutokea, aliamua kumwokoa Mjumbe wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Amon Mpanju na Jaji Warioba ili wasijeruhiwe kwenye vurugu hizo. Picha zilizochapishwa jana zilimwonyesha Makonda akiwa amemshika Jaji Warioba.

"Nilipoingia ukumbini nilikwenda kukaa jirani na Mpanju, baada ya kutokea vurugu nikaona ni lazima nimwokoe kwa sababu ya ulemavu wake wa kutokuona. Jaji Warioba alituona na akanisogelea akaniambia nisimwache Mpanju asije akapata matatizo. Kwa hiyo nikawa niko karibu na Mpanju na Warioba ili kuhakikisha kuwa wanakuwa salama."

"Warioba ni kama baba yangu, kamwe siwezi kunyanyua mkono wangu na kumpiga, nitakuwa ninajitafutia matatizo, huu ni mchezo mchafu unaochezwa na baadhi ya wanasiasa wenye lengo la kunichafua.

"Leo (jana) asubuhi Warioba amenipigia simu akinipa pole kwa vurugu hizo, nami nikampa pole kwa yote yaliyotokea jana, sasa inakuwaje mtu uliyempiga halafu akakupigia simu ya kukupa pole?" alisema Makonda.

Hata hivyo, Jaji Warioba hakupatikana jana kuzungumzia nini hasa kilitokea kati yake na kada huyo wa CCM ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge la Katiba.

Kauli ya Polisi

Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba alisema bado viongozi wastaafu wanapatiwa ulinzi wa kutosha lakini hakutaka kufafanua zaidi vigezo vinavyoangaliwa kwa kile alichoeleza kuwa ni sababu za kiusalama," alisema.

Mwaka 2009 Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi alipigwa kibao shavuni alipokuwa akihutubia katika Baraza la Maulid.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema watu kadhaa ambao hata hivyo hakuwataja kwa majina wala idadi, walihojiwa ili kujua chanzo cha vurugu hizo na kuwa uchunguzi unaendelea.

Chanzo: Mwananchi
 
Na ayawezi mkuta kwa sababu hata yeye kuwa raisi ilikuwa siyo matakwa ya watanzania kwa hiyo kunatofauti kubwa Kati ya warioba na kikwete.
Naitakaa itoke kikwete kuwapigania wanyonge Kama anavyo Fanya warioba na kitu kingine kikwete atambue warioba akudhalilishwa hata kidogo bali alipewa ulinzi tena na vijana wazalendo wa taifa hili kuepuka uhuni uliofanywa na chama chake na ukizingatia yeye ndiye Mwenyekiti inamaana ilitoa Baraka kwa hao watoto wake kuja kuleta fujo
 
Uovu unafumbiwa macho na kushangiliwa badala ya kuukemea!!!!! Nchi ya ajabu sana
 
Yamkute mara ngapi kasahau Mbeya, walipo mtungua mawe...kikwete afungue kidogo akili yake...nafasi aliyo nayo ni kubwa kulinganisha na kauli anazo toa...kwana amesahau kama urais huu alionao sasa ni ilikuwa slaa awe kwenye kiti hicho...atafute mtu wa kuwa anamsemea maneno yaliyo na hekima kidogo!
 
Sishangai kabisa kauli ya Kikwete. Ni kauli ya CCM nzima. Lakini wakae wajue kwamba hii katiba ya Chenge ni kaburi lao. Tumeikataa na tutaitumia kuikataa CCM 2015. Aombe tu yasimkute ya Warioba kwa sababu hajui ya Kikwete yatakuwaje.

katiba mnaikataa nyinyi ukawa sisi wananchi wa tanzania wenye hekima na busara tunaikubali
 
Katika hali ya kushangaza, rais Jakaya Kikwete ameonesha kuunga mkono udhalilishaji aliofanyiwa mwenyekiti wa iliyokuwa tume ya kukusanya maoni ya kuandika katiba mpya jaji Joseph Warioba.

Akipiga kijembe kwa jaji Warioba, Kikwete alisema kuwa "Naomba sana yasije yakanikuta yaliyomkuta Warioba" bila kutoa ufafanuzi wa zaidi.

Jaji Warioba alifanyiwa vitendo vya kumdhalilisha wakati wa kongamano la katiba lililofanyika juzi jijini Dar es Salaam ambapo vijana 'wahuni' wa UVCCM wakiongozwa na kiongozi wao Paul Makonda walivamia kongamano hilo na kuanzisha fujo huku Makonda akimzaba kibao jaji Joseph Warioba.

Jaji Warioba amewahi kuwa makamu wa rais enzi za utawala wa awamu ya pili.

Kikwete aliyasema wapi hayo?
 
Najaribu kuwa Neutral, siamini kama maneno hayo yametoka kwa so called Mkuu wa Nchi...
 
Baadhi ya nchi wananchi wao wengi ni wajinga lakini angalao viongozi wao huwa ni werevu, wazalendo, wabunifu na wenye akili. Sisi tuna Rais mjinga kupindukia, viongozi wengi wajinga, na wananchi wengi wajinga.

Kiongozi aliyetegemewa kutoa kauli nzito dhidi ya fujo za kijinga halafu anaishia kusifia fujo, lazima awe ni kiongozi wa ajabu kupindukia. Huyu hakustahili kuwa hata Mwenyekiti wa mtaa.

Hii nadhani ni taarifa tosha ya nini Kikwete atafanya kukitokea vurugu wakati wa uchaguzi. UKAWA ni lazima agenda ya kujilinda, kulinda kura na kuwalinda wananchi iwe kipaumbele cha kwanza. Lazima wajue hatuna Rais katika ile maana halisi ya Rais kama mlinzi wa watu wote, na pia hatuna polisi katika ile maana ya kuwa ni chombo wa uhakikisho wa usalama wa mali na maisha ya watanzania wote.

Shame to Tanzania, shame to CCM, shame to Kikwete and his familiy!
 
katiba mnaikataa nyinyi ukawa sisi wananchi wa tanzania wenye hekima na busara tunaikubali

Katiba yenyewe hamuijui imeandikwa nini,imeongezwa nini, imepunguzwa nini, mnakubalitu, Elimu ikitolewa ili muijue vizuri ili muamue kwa busara, mnafanya vurugu kuzuia watu wasielimishwe, eti ndio mna busara na hekima,(maskini ya Mungu!)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom