Dkt. Bashiru anahukumiwa kwa yale, si hili

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Kumekuwa na fukuto kubwa baina ya wanachama wa chama Cha Mapinduzi CCM wakimjia juu aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ally.

Wanachama hao wanamlaumu Bashiru kwa uchochezi na kutomheshimu Rais aliye madarakani Samia Suluhu ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala.

Bashiru ambaye ni Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, siku za hivi karibuni alitoa kauli inayo onyesha kuwa hakubalini na vikundi vinavyosifu Viongozi wa Serikali kwa kusema kiongozi fulani "anaupiga mwingi".

Akizungumza katika katika tukio lililoandaliwa na mtandao wa wakulima wadogo MVIWATA alisema, " Sauti yenu wakulima, iwatishe wanyonyaji wenu kama hatujafikia hatua hiyo na kutisha watawala, bado tutakuwa hatujafikia malengo".

Bashiru aliendelea kusema, "hatutakuwa tofauti na mawakala wao, wanaowapamba na wakati mwingine kuwadanganya kwamba wanaupiga mwingi. MVIWATA mkifika hatua ya kusema mnaupiga mwingi uhai wenu uko mashakani".

Baada ya siku kadhaa wanachama mbalimbali hasa ambao ni wabunge wa CCM wamejitokeza kumkosoa na kumuonya Bashiru kuwa hapaswi kuongea kuhusu Viongozi wakuu wa serikali kwakuwa hata yeye amepitia huko.

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku màarufu kama Msukuma ni miongoni mwa waliojitokeza kumkosoa Bashiru.

Msukuma amemtaka Bashiru kuomba radhi kwa kauli yake huku akisisitiza kuwa wakati wa utawala wa awamu ya tano Bashiru alikuwa karibu na Rais mambo mengi yalikuwa yanatendeka kinyume lakini hakuwahi kukemea kwanini leo hii awachukie wanao msifu Rais ambae wanaona anafanya vizuri.

Nae Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangala akiwa mbele ya waandishi wa habari mkoani Dodoma amesema kuwa Bashiru aheshimu mamlaka ya Ikulu iliyomteua hivyo anapaswa kujiuzulu nafasi ya ubunge na kuwapa nafasi watu wengine.

Aidha Kigwangalla amefunguka kuwa wao kama wanachama wa CCM hawajui kama Dk. Bashiru alikuwa na kadi ya chama.

"Hatujui kadi yake ya Chama Cha Mapinduzi aliichukua lini, hatujui hata kadi yake ya CUF aliirudisha lini? tulishangaa tu ameteuliwa kuwa Katibu mkuu wa CCM, lakini tuliheshimu mamlaka iliyomteuwa,sasa tulitegemea awe na Shukrani".

Sio hao tu nae mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mvumi Livingston Lusinde amemtaka Bashiru kujizulu nafasi yake ubunge.

"Jimbo la Bashiru ni lkulu kwasababu ndio imemteua, si kumbuki kama kuna siku aliwahi kumshukuru Rais Samia kwa kumteua, kwasababu anajisikia vibaya akisikia watu wanasema Rais Samia anaupiga mwingi anatakiwa aachie ngazi ili ateuliwe Mbunge mwingine ambaye atapendezwa na kile kinachofanywa na serikali ya awamu ya sita.” amesema.

Lusinde amesema Bashiru akiwa Katibu Mkuu wa CCM aliwafundisha kuimba mapambio ya kusifu na walifanya hivyo sasa kwanini wakati huu inamkera.

Wakati hayo yakiendelea mjadala huu umekuwa mkubwa na kuwaibua watu wengine ndani na nje ya chama Cha CCM Ambao wanakuja na mawazo tofauti kwa mtazamo wao.

Jaji Mstaafu, Joseph Warioba amesema badala ya Watu kumshambulia Dkt. Bashiru wajibu hoja zake kuhusu Watawala na hali za wakulima.

Warioba Amesema bado kuna mambo yana matatizo ikiwemo Ajira za Vijana, Wakulima na Wafugaji lakini hayazungumzwi.

Pia wanaharakati mbalimbali wametoa maoni yao wengi wakijikita kwenye umuhimu wa hoja alizo ziibua Bashiru na uhalisia ulivyo wengi wao wanamuunga mkono Bashiru kwa alichokisema lakini wanamhukumu kwa historia yake katika utawala wa awamu ya tano ambao yeye alikuwa karibu mkuu kiongozi Ofisini ya Rais Ikulu.

Wengine wanazungumzia mwenendo wa tabia ya kusifia viongozi "Uchawa" kuwa ilianza miaka michache iliyopita katika awamu ya tano kumsifia aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli.

John Pambalu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema yeye anaibua hoja kadhaa ambazo zinagusia madudu ya serikali ya awamu ya tano katika kusifia viongozi lakini Bashiru hakuwahi kukemea.

Nini kinamfanya Bashiru akemee kuabudu watawala, jambo ambao lilikuwa utamaduni wa kawaida katika utawala wa awamu ya 5?.

"Agrey Mwanri aliwahi kusema Mungu amshukuru Magufuli kwa uchapa kazi wake na wala sio Magufuli kumshukuru Mungu"

"Pia Profesa Kabudi aliwahi kumuita Mhe. Magufu Mhe. Mungu, Kangi Lugola aliwahi kusema Magufuli ni zaidi ya Yesu na Mtume Muhammad, Kufuru nyingi zilifanyika awamu ya 5 Bashiru alikuwa wapi" Pambalu anahoji.

Lakini mwisho wa yote watu wengi wanasema Bashiru anayo haki ya kutoa maoni hapaswi kushambuliwa na kuonekana mbaya kwa mawazo yake kwa sababu ni haki yake kikatiba na hajavunja sheria.

Peter Mwaihola ni Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii na kisiasa.
 
Perfectly well adressed. Anashambiliwa kwa hgili la kinafiki. A sensible man atajiuliza inakuwaje anashambuliwa yeye? alikuwa CEO wa mapambio ya magufuli? Hakuwahi kukemea haya uliyoyaweka
"
"Pia Profesa Kabudi aliwahi kumuita Mhe. Magufu Mhe. Mungu, Kangi Lugola aliwahi kusema Magufuli ni zaidi ya Yesu na Mtume Muhammad, Kufuru nyingi zilifanyika awamu ya 5 Bashiru alikuwa wapi" Pambalu anahoji".
 
Halafu pale ninapo ombea haya maccm kuendelea kuparuana, ili tuje kuona mwisho wake hapo baadaye! Kuna wapuuzi wachache eti wananuna!
 
Kumekuwa na fukuto kubwa baina ya wanachama wa chama Cha Mapinduzi CCM wakimjia juu aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ally.

Lakini mwisho wa yote watu wengi wanasema Bashiru anayo haki ya kutoa maoni hapaswi kushambuliwa na kuonekana mbaya kwa mawazo yake kwa sababu ni haki yake kikatiba na hajavunja sheria.

Peter Mwaihola ni Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii na kisiasa.
Mkuu Peter Mwaihola, thanks for this, a very good analysis, very objective!.
P
 
Wanasiasa wote wamejaa "unafiki" kupitiliza.
Mwanasiasa wa Tz akiwa "anakula na kushiba", utamsikia wakati wote akisifia na kuabudu waliomteua.

Mwanasiasa huyo huyo wa Tz akiwatupwa nje ya "system" utamsikia akikosoa na kuhoji watawala waliomtupa. This is crass hypocrisy!!!
 
Na hii ndiyo hufanya Vijana chipukizi kuona Kama siasa Ni mchezo usiofaa.
 
Asantee Sana, mkuu naomba namba yako tafadhali
emoji120.png
07(5/8)4 27 04 03 anza na sms or whatsapp
P
,
 
Back
Top Bottom