Ina maana Mbowe hana wahasibu na washauri wa kodi katika kampuni zake? Tusiichafue TRA kwa faida binafsi za kisiasa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,922
141,887
Ninavyofahamu hata mzee Mgaya na lile duka lake la Hardware ana mhasibu na mshauri wa kodi ambaye husimama kama wakili wa maswala yake ya kiuhasibu na kodi.

Ninavyojua ukiwa na kampuni ni lazima uwe na mhasibu na external auditor kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA.

Freeman Mbowe kuwa jela haimaanishi kwamba biashara zake na maswala yake ya kodi yamesimama.
Na siamini kama Freeman Mbowe huwa anakwenda yeye binafsi TRA kushughulikia maswala ya kodi kama Individual taxpayer kwa sababu biashara zake zimeshavuka level hiyo.

Sisemi kwamba Mbowe hajaonewa bali siyo sawa kulitumia jambo hili kujinufaisha kisiasa, anapaswa aongee kama mfanyabiashara mkubwa.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
 
Haujaelewa mantiki ya Mbowe, ni kwamba alipelekewa barua za madai wakati yupo Jela na akaambiwa atoe responses wakati bado yupo Jela, ile anatoka kushakuwa na time lapse na muda wa kujitetea haupo tena. Kilichofuata ni kuchukua pesa zake zote na kumfungia akaunti zake. Kimsingi plan ilipangwa ikapangika. Sasa katika mazingira hayo huyo Muhasibu wa kazi gani?
 
Wewe haujawahi kuwa hata na genge la kuuza mitumba, haya ya Mbowe unafanya shambulio la kiccm.
Hoja hii mkosaji si Mbowe (MTU), mkosaji ni KAMPUNI hivyo mtuhumiwa ni kampuni na hii ndivyo inavyofanyika kwa makampuni yote, iweje kwa Mbowe?
 
Haujaelewa mantiki ya Mbowe, ni kwamba alipelekewa barua za madai wakati yupo Jela na akahambiwa atoe responses wakati bado yupo Jela, ile anatoka kushakuwa na time lapse na muda wa kujitetea haupo tena. Kilichofuata ni kuchukua pesa zake zote na kumfungia akaunti zake. Kimsingi plan ilipangwa ikapangika. Sasa katika mazingira hayo huyo Muhasibu wa kazi gani?
Siyo kweli.

Mbowe anamiliki kampuni siyo kioski cha Mangi.

Kampuni za Mbowe zina wahasibu kwa mujibu wa sheria na hao hufanya kazi hizo za kushughulika na mambo ya kodi.
 
Kama jaji mkuu, mkurugenzi mkuu wa TRA na wengineo wengi walitiwa mfukoni na Tofali, hivi unadhani Wakili na auditor wa mbowe ni nani mpaka afurukute.

Kama ungekuwa unaepusha mapenzi ya kitoto kwa Tofali ungekuwa unamiliki hekalu yako Dubai
 
TRA walijichafua wenyewe. Badala ya kukusanya kodi, wakajiingiza kwenye kazi ya kulazimisha kodi tena mara nyingine kwa uonezi kabisa.

Ndio maana huwa nahisi wafanyakazi wa umma kufanya kazi kwa weledi. Mana muda ukibadilika lila kitu kinabadilika. Kisichobadilika ni ukweli tu. Unabaki vile ulivyo
 
Madai ya kodi yalitumwa kwenye email yake binafsi, na ilikuwa ni njama kwa kuwa walikuwa wakijua kuwa hatoiona maana yuko jela. Ilikuwa ni hujuma ambayo hao TRA walipewa maelekezo na yule mtu katili.

YESU NI BWANA.
Angeenda kuwashtaki TRA kwenye mahakama ya biashara.

Labda kama Freeman Mbowe ni individual taxpayer lakini kama anamiliki kampuni hawezi kutumiwa taarifa rasmi za kodi yeye binafsi.

Hata MO Dewji alivyotekwa biashara ziliendelea na kodi zililipwa bwashee!
 
Waliozoea kuitafuna nchi wanarudi kwa kasi
Tena warudi kwa kasi ya kutisha ili na mimi muuza mchicha nifaidike, na maisha yaende japo niwe na uhakika wa milo mitatu kwa siku!!kuliko tulivyokuwa tunaaminishwa kuwa upigaji hakuna chini ya jemedali meko, lakini tukishangaa mbona maisha yanazidi kuwa magumu, huduma za kijamii ni vile vile??kumbe tulikuwa tuna subilia meli uwanja wa ndege!!MUNGU NDIO IMEBIDI AINGILIE KATI, kutunusuru kwani daaa!!ila meko, meko, meko nakuita mala tatu bora MUNGU amekuona.
 
Tena warudi kwa kasi ya kutisha ili na mimi muuza mchicha nifaidike, na maisha yaende japo niwe na uhakika wa milo mitatu kwa siku!!kuliko tulivyokuwa tunaaminishwa kuwa upigaji hakuna chini ya jemedali meko, lakini tukishangaa mbona maisha yanazidi kuwa magumu, huduma za kijamii ni vile vile??kumbe tulikuwa tuna subilia meli uwanja wa ndege!!MUNGU NDIO IMEBIDI AINGILIE KATI, kutunusuru kwani daaa!!ila meko, meko, meko nakuita mala tatu bora MUNGU amekuona.
 
Ninavyofahamu hata mzee Mgaya na lile duka lake la Hardware ana mhasibu na mshauri wa kodi ambaye husimama kama wakili wa maswala yake ya kiuhasibu na kodi.

Ninavyojua ukiwa na kampuni ni lazima uwe na mhasibu na external auditor kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA.

Freeman Mbowe kuwa jela haimaanishi kwamba biashara zake na maswala yake ya kodi yamesimama.
Na siamini kama Freeman Mbowe huwa anakwenda yeye binafsi TRA kushughulikia maswala ya kodi kama Individual taxpayer kwa sababu biashara zake zimeshavuka level hiyo.

Sisemi kwamba Mbowe hajaonewa bali siyo sawa kulitumia jambo hili kujinufaisha kisiasa, anapaswa aongee kama mfanyabiashara mkubwa.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Unampangia nani wa kumuajiri as if ulimpa mtaji. Na unavyomuona hana tax consultant kabisa???
 
TRA wezi,Sana na wamekua na ukatili wa ajabu kwa wananchi hasa kwenye awam ya tano,na hii Kama aliyosema mh Mbowe ,ni WATU wengi yamewapata ,so serikali mjiandae kuja kulipa WATU mafidia,kwa ushenzi wa baadhi ya WATU wa TRA kisa maagizo kutoka juu,maana WATU watashitaki,mfano rafiki yangu mwaka jana alipigiwa lipa m300 wakati mtaji wake hata m60 hatufiki,TRA nchi hii ishakua shida,Bila kusukwa upya sijui Kama tutafika
Ninavyofahamu hata mzee Mgaya na lile duka lake la Hardware ana mhasibu na mshauri wa kodi ambaye husimama kama wakili wa maswala yake ya kiuhasibu na kodi.

Ninavyojua ukiwa na kampuni ni lazima uwe na mhasibu na external auditor kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA.

Freeman Mbowe kuwa jela haimaanishi kwamba biashara zake na maswala yake ya kodi yamesimama.
Na siamini kama Freeman Mbowe huwa anakwenda yeye binafsi TRA kushughulikia maswala ya kodi kama Individual taxpayer kwa sababu biashara zake zimeshavuka level hiyo.

Sisemi kwamba Mbowe hajaonewa bali siyo sawa kulitumia jambo hili kujinufaisha kisiasa, anapaswa aongee kama mfanyabiashara mkubwa.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
 
Haujaelewa mantiki ya Mbowe, ni kwamba alipelekewa barua za madai wakati yupo Jela na akahambiwa atoe responses wakati bado yupo Jela, ile anatoka kushakuwa na time lapse na muda wa kujitetea haupo tena. Kilichofuata ni kuchukua pesa zake zote na kumfungia akaunti zake. Kimsingi plan ilipangwa ikapangika. Sasa katika mazingira hayo huyo Muhasibu wa kazi gani?
Umeona barua au umesikiliza alichosema Mbowe?

Je kula pesa za chama ulishawahi kumuona akikanusha hata siku moja?
 
Back
Top Bottom