SoC03 Mambo haya yakifanyiwa kazi na wadau (TRA, wananchi wafanyabiashara, wizara husika) itaongeza uwajibikaji wa kila mdau kwenye makusanyo ya kodi

Stories of Change - 2023 Competition

TAJIRI MSOMI

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
477
495
NATAMANI KIKOSI KAZI KILICHOUNDWA NA WAZIRI MKUU,TRA na SERIKALI WANGEWEZA KUTATUA TATIZO LA PENATI KWA KUTO KUFANYA FILING ZA P.A.YE,SDL,VAT, MAKADIRIO, NA RITANI ZA MWAKA KWA KAMPUNI/BIASHARA ZENYE MTAJI CHINI YA BILIONI MOJA

Awali ya yote, mimi ni mdau na mfanyabiashara ndogondogo wa sector ya fedha,hivyo katika andiko hii utaona mifano mingi nitatoa kutoka sekta hio kwa sababu ndio eneo langu la uzoefu.

Muundo wa sasa katika ritani za Mapato

Mamlaka ya Mapato imetengeneza utaratibu kwa kampuni/wafanyabiashara wote kufanya filing za ritani za kodi P.A.YE, SDL, VAT, MAKADIRIO,na mapato ya mwaka etc na kulipa kodi accordingly kulingana na makadilio au mapato halisi.Kwa mujibu wa sheria sasa ritani nyingi kama vile PAYE, VAT,SDL zinahitaji ujaze kila mwezi either tarehe 7 au tarehe 20 ya mwezi ujao na usipofanya hivyo TRA wanapiga penalty ya 225,000 kwa kampuni na 75,000 kwa watu binafsi kwa mwezi, na pia kuna riba(Interest) ya kutolipa kodi kwa wakati

Kulipa kodi ni wajibu wa kila Mtanzania na kwa maendeleo ya taifa letu, tunanufaika sana kama taifa kutokana na Kodi, lakini pale utaratibu wa kukusanya kodi unapokuwa mbovu hupelekea watu kukwepa kulipa kodi, kuficha ama hata kukiuka taratibu za kulipa kodi.

Tatitizo lipo hapa kwa Kampuni ndogo/wafanyabiashara wadogo

Wafanyabiashara wadogo/kampuni ndogo nyingi zina mtaji chini ya Bilioni moja, Zaidi ni chini ya milioni 100. Kwa mtaji wa Bilioni moja kama ni faida kubwa utapata kwenye biashara kwa mwezi basi ni milioni 35,000,000 kabla ya kulipa gharama za kuendesha,Faida hii ni ndogo sana kulipa wafanyakazi, umeme, wafanyakazi, maji, pango, internet, riba za bank etc. Kwa sababu faida ni ndogo wafanyabiashara wengi huwa hawawezi kuajiri wahasibu wa kodi badala yake wamiliki wa biashara wanakomaa kufanya compliance ya ritani za TRA. Ukiajiri Mhasibu gharama zinaongezeka; kwa sababu wamiliki wa biashara wanakuwa busy sana kufanya core business(Biashara) hupelekea kusahau kujaza ritani Hizi.

Ukisahau filingi ya ritani hizi kwa miaka mitatu usishangae TRA wakaja na penalty na milioni 400+ wakati mtaji wa biashara yako hauvuki hata milioni 30. Kwa namna TRA walivyo, huwa wanakomaa na wewe mpaka wahakikishe mtaji wako wote umelipa Penati zao na pengine hata kuuza mali zako zingine kwa sababu tu ya kodi.Hali hii imeua au kurudisha nyuma biashara nyingi za watanzania. Mfano Microfinance Company statutory capital ni Milioni 20, na riba ambayo wanaambiwa watoze na BOT ni pungufu ya 3.5% kwa mwezi, kwa maana hio mfanyabiashara huyu kwa mwezi anapata 700,000 kabla ya gharama za uendeshaji provided that kila mkopaji amelipa, ukimwambia aajili mhasibu hata wa part time kwajili ya filing za ritani za kila mwezi unakuwa umeua biashara yake kabisa na hawezi kabisa. Hizi penalty hazijali hata level ya mtaji wa mafanyabiashara , mwenye mtaji wa bilioni 300 huko analipa sawa na mwenye mtaji wa milioni kumi, hii si sawa kabisa ni unyonyaji na uuaji wa biashara ndogondogo. Wafanyabiashara wengine wameacha na kujisemea liwalo na liwe (Wamemwachia Mungu)

Nini Kifanyike Kutatua changamoto Hii...

  • Ifanyike classification ya wafanyabiashara, mfanyabiashara mdogo Mtaji mpaka 1 billion, na wawekwe katika tier tofauti tofauti based kwenye level ya mtaji…hivyo hivyo wafanyabiashara wa kati na wafanyabiashara wakubwa
  • Compliance level iwe based kwenye group la wafanyabiashara na tier zao, mafano wafanyabiashara wadogo wafanye return za makadirio na return za mwisho wa mwaka, wafanyabiashara wa kati wafanye return zao based kwenye nusu mwaka na wa juu ndio wawe full compliance na return zote kama ilivyo sasa.
  • Kama ilivyo kwenye Compliance level hapo Juu, penalty nazo ziwe based kwenye group la wafanyabiashara , eg Wadogo inaweza kuwa 0-5 currency point (30,000) wa kati ikawa 6- 10 cp, na wakubwa ikawa hio 11-15 CP.Hii itasaidia kuona penaty unayopewa ni ya halali na uwezekano wa kulipa hio penalty utakuwa mkubwa kuliko ilivyo sasa , mfanya biashara akiona amepewa penalty ya non filing million 400+ na wakati yeye mtaji wake ni million 10 anaona njia rahisi ni kufunga biashara na kuacha ama kuacha kiwalo na lkwa (Hapa TRA,Mfanyabiashara,nan chi wote wanakuwa wamepoteza-wamepata hasara)
  • Iwekwe sheria ya lazima kwa makundi yote kutunza kumbukumbu sahihi za biashara zao, kwenye mfumo ambao TRA watakuwa weme-precribe ( Muundo uwe rahisi na simple-mtu wa kawaida darasa la saba uweze kutumia unaweza ukawa electronic au manual)
  • Kamata kamata kwasabau mtu hana EFD receipts iondoke badala yake utumike mfumo mwingine. Kamata kamata na EFD imesababisha wateja wengi kukimbia nchi yetu na udanganyifu mkubwa kwa wafanya biashara, umenunua vitu vya 200,000 unaandikiwa risiti ya 2000 hii si sawa; hili hufanyika kwakuwa TRA wanamuundo mbovu wa record za wafanyabiashara na kodi zilizopitiliza
  • Elimu itolewa ya filing ya ritani za mapato kwa kuzingatia kundi la wafanyabiashara. Huwezi kumchanganya mafanyabiashara mwenye million 10 na yule mwenye bilioni miambili huko ukadhani watatoka wameelewa wote sawa
  • Nguvu kazi ya kudai kodi au kuelimisha watoa kodi itatumika kwa kuzingatia group la wafanyabiashara
  • Haya mawazo yawe effective, restructuring za domestic revenue department ifanyake kuwako na wasaidizi wa commissioner wa mapato ya ndani kwa kuzingatia group la wafanyabiashara
Mwisho:

Wajibu wa kulipa kodi ni wa kila Mtanzania, na tupende kulipa kodi kwa wakati, na wajibu wa Mamlaka ya mapato-TRA ni kukusanya kodi sahihi kwa kuzingatia kodi za leo na za kesho yaani bila kuua biashara za walipa kodi. Bunge letu litunge sheria wezeshi za mapato kwa TRA na Walipa kodi.

Asanteni Sana
 
Back
Top Bottom