INSIDER MAN
JF-Expert Member
- Nov 7, 2018
- 1,736
- 15,856
Leo nitabase na walipakodi binafsi/ Individual taxpayers (Presumptive ). Kuna jambo ambalo nafikiri ni kilio kwa wengi ila wanakosa mahali pakusemea. Ukweli hili jambo TRA mliangalie ni namna gani mtaweza kulitatua.
Mlipakodi akifikisha mauzo ya milion 100 mnamsajili na VAT na pia mnamwambia afanye self assessment. Nashindwa kutambua ni sheria ipi ambayo inamlazimisha mlipakodi kufanya online self assessment (e-filling)?. Point yenu ni kwamba mteja akifika hayo mauzo anatakiwa kusajiliwa na VAT na kuanza kutuma return za VAT hivyo anakua account case, na pia afanye self assessment online. Kumbuka unavofanya self assessment kwenye huu mfumo itabdi uandae hesabu yaani financial statements.
Tunatambua TRA mnania njema na Taifa hasa katika makusanyo ya kodi na pia mnafata sheria Vat Act, 2014 (S.28). Hii sheria naona bado inahitaji maboresho zaidi (Amendement).
Tanzania tuna aina tatu (3) za walipa kodi
1. Walipakodi wadogo ( Presumptive)
2. Walipa kodi wa kati (Normal flow)
3. Walipakodi wakubwa ( Large taxpayers)
Lakini kundi kubwa hapo la walipakodi kwa Tanzania linaangukia kwenye namba moja (1). Asilimia kubwa ni wale ambao tunafanya biashara ili tuweze kujikwamua kimaisha tupate chakula, tusomeshe watoto na mahitaji mengine.
Mitaji pia ni ya kuunga unga na asilimia kubwa ya bidhaa tunapata kwa mali kauli, huko bank tunamikopo ya kutosha. Sasa Mlipakodi kama huyu unakuta kwa mwezi kauza 10million (mfano). Unakuta hapo million 9 inakwenda kulipa deni la watu anabaki na million moja hapo hujalipa kodi ya pango, gharama za umeme, maji, chakula, taka nknk.
Mlipakodi kama huyu unakuja kumtandika na VAT juu, hapo unamtoa kutoka presumptive kwenda kuwa mlipaji kodi wa kati (Normal flow). Mlipakodi atakiwa atafute mtu (mhasibu) wa kumsaidia kutuma ritani za VAT kila mwezi na bado atahitajika kuandaa hesabu zake Financial statements tayari gharama zimeongezeka kwenye biashara.
Ushauri wangu kwa TRA msikimbilie kusajili VAT embu fanyeni kwanza evaluation ya kutosha kwa Mlipakodi. Msikimbilie kusajili, lengo ni kupata Walipakodi bora lasivyo mnazalisha wakwepaji ( Non fillers). Fanyeni tathmini ya kutosha hata zaidi ya miaka 2 mjiridhishe na Mlipakodi. Kumuingiza mteja kwenye VAT mnampa gharama za kila mwezi za kutuma ritani pamoja na gharama za kuandaa hesabu kwa wahasibu biashara ndo inaanza kuyumba, sababu ni ndogo anategemea mali kauli. TRA mnaua biashara nyingi sana huku mitaani kama hamjui leo nawaambia.
Tuje upande wapili
Tatizo ni kwamba unakuta uyo mlipakodi mwaka jana 2022 mauzo yalishuka mpaka 50million kutokana na kuyumba kwa biashara. Mwaka huu Ukienda ofisini TRA kuomba kuondolewa na VAT na pia kuondolewa kwenye mfumo wa e-filling ni kipengele sana utapigwa danadana mpaka ukome. Na mnajua fika mteja akitumia E-filling lazima atatakiwa kuandaa hesabu za mwaka husika.
Sasa kama mteja alifika 100m akasajiliwa na VAT pindi mauzo yanaposhuka na kua chini ya hapo kwanini asitolewe kwenye VAT??. Inamaana hiyo mifumo yenu inashindwa kutambua??. Utaandika barua utazungushwa mpaka unakata tamaa , hapohapo ofisa anakwambia wewe mauzo yameshuka sababu hutoi risiti. Moja ya sababu ya kipumbavu ukimwuliza unaushahidi na unachosema atabaki anajiuma.
Biashara zinabadilika unakuta mtu alipata mauzo makubwa sababu alibahatika kupata tenda ndo ikaboost mauzo. Baada ya kumaliza mkataba mauzo yakashuka yakarudi kama zamani japo kuna ambao hawatoi risiti kweli. TRA hili suala mlitizame maana asilimia kubwa return za VAT ni repayment sababu ya masuala kama haya.
Na hili suala la e-filling kama mlipakodi aliambiwa afanye self assessment online akafanya kwanini kwenye kutoka inakuwa ngumu?. Kwanini kwenye system msiweke option ya kujiondoa?. Ofisa anakwambia mpaka makao makuu kutolewa, mbona tunavoingia kwenye mfumo hatukwenda makao makuu??. Mlipakodi akishakuwa chini ya 100m kwa individual huyu sio account case tena anatakiwa kuondolewa kwenye VAT arudi kuwa presumptive case, kama sheria inavyosema.
Kuna mambo mnafanya mazuri mnastahili pongezi ila kwa hili lina discourage sana walipa kodi. Nakutana na case kama hizi nyingi sana watu wanaumia maana inauwaumiza sana wafanyabiashara wadogo.
Unaweza kuwasiliana na mimi kwa mahitaji ya:
-Makadirio ya kodi (binafsi na kampuni)
-kufungua/kusajili TIN (binafsi na kampuni)
-kufungua business name na kusajili kampuni. BRELA
-Kutuma/kuandaa Ritani za VAT/SDL/PAYE nk
-Kuandaa hesabu (Financial statements)
-Driving license 🪪
-Leseni za Biashara.
-Tax payments receipt. nknk
Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Taifa letu.