Imenishangaza - ina maana.......

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
Katika kupitia mabandiko na michango ya wadau mbalimbali JF nimevutika kuangalia ni vipi michango hiyo inapokelewa na wasomao. Kilichonishangaza ni pattern hii:

Katika mabandiko ni nadra sana hata kwa wale magwiji kupewa thanks katika asilimia zaidi ya 30 ya mabandiko yote. Mathalani kama mtu kabandika mara 10,000, asante atakazopokea zinacheza kwenye mabandiko yasiyozidi 3,000!!

Ina maana mabandiko 7,000 ni pumba? Hebu angalieni wenyewe - chukua id ya mtu yeyote hasa wale mahiri wa kubandika, angalia kabandika mara ngapi kisha kapongezwa mara ngapi mtajionea wenyewe - inacheza kati ya asilimia 10 na 30, haizidi 1/3 ya mabandiko yake.

Mimi mwenyewe nimebandika mara 61, nimepongezwa mara 32 lakini katika mabandiko 24 tu. Nimeshangaa kiaina!

Nitatoa mifano michache as of today 15/6/2010:

1. Mzizimkavu :
Posts: 3,906
Thanks : 605
Thanked 518 Times in 352 Posts

2. Anyisile Obheli
Posts:1,257
Thanks : 516
Thanked 466 Times in 311 Posts

3.Mbu
Posts:5,164
Thanks : 538
Thanked 666 Times in 402 Posts

4 Buchanan
Posts:3,795
Thanks : 817
Thanked 1,510 Times in 913 Posts

5.Abduhalim
Posts:8,700
Thanks : 505
Thanked 1,319 Times in 881 Posts


Hizi takwimu zinatuambia nini jamani? Wengine hatufanyi kitu bila kutathmini.
 
Kwa maoni yangu sidhani kama zinatwambia chochote. Kuna baadhi ya wanachama (nisingependa kuwataja) wana michango ya maana sana lakini hawapewi "thanks" kama inavyostahili. Pia kuna baadhi hapo juu walikuwa na thanks nyingi sana ziliminywa katika kurekebisha matatizo ya forum.

Wakati zilipominywa ilisemekana 'thanks" zile zingerudishwa baada ya kila kitu kukaa sawa lakini hadi hii leo hazijarudishwa na naweza kusema hazitarudishwa tena maana ni miezi mingi imepita sasa. Soma baadhi ya michango ya wanachama hao na kuamua kama wanabandika pumba kila leo au la, lakini ukiamua kama wanaweka pumba au la kwa kuangalia wana "thanks" ngapi na katika threads ngapi basi utaingia maboya.
 
Thread hii haijengi kitu kwa members, na vile vile metric unayotumia siyo sahihi.

Metric hii siyo sahihi kwa vile inategema ratio baina ya posts zote za mchangiaji na zile zilizokuwa credited with thanks. Hiyo siyo sahihi kwa vile post zote zilianza kuhesabiwa mwaka 2006 wakati credit za thanks unazoshesabu zilianza kuhesabiwa mwaka jana tu. Kuna hesabu ya credist za zamani iliyofutwa mwaka jana na kuondoa credits zote zilizokuwapo kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2009; katika hesabu ile, wenyeji wa forum kama Mzee Mwanakijiji, FMES, Mtanzania, Rev Kishoka, Bubu Ataka Kusema, SteveD, Mwafrika wa Kike, Brazameni, Masatu, Nungwi, Madela-wa-Madilu, Nyani Ngabu, Muchambuzi, Jasusi, Mwanasiasa, Dar Si Lamu, Joka Kuu na wengineo ambao inawezekana huwafahamu, walikuwa wameshafikisha zaidi ya credits 20,000.

Kwa vile umejiunga mwezi jana tu, unaweza kuwa hujui yote hayo. Ningekushauri uwe unatumia forum hii effectively kubadilishana mawazo na wanachama kwa namna mbalimbali kwa vile kuna wanachama wenye ujuzi wa aina mbalimbali na kwa caliber za ajabu sana. Hata kama usipochangia mada, unaweza kukaa kimya na kufuatilia mada mbalimbali kadri watu wanavyozichambua. Kwenye ukumbi kama huu kutakuwa na watoa pumba na watoa mchele; ni wajibu wako kuchambua mchele ni upi na pumba ni zipi. Ni jambo la kawaida sana hapa watoa pumba kupena credit na watoa mchele pia kupeana credit, kwa hiyo swala la kuangalia ni nani kapata credit nyingi linaweza lisikusaidie sana katika matumizi yako ya forum hii.
 
Asante BAK na Kichuguu kwa michango yenu - naweza nikakubaliana na maelezo yenu au pia kukataa.

Assuming kuwa thanks zilifutika wakati wa kurekebisha forum bado kuna hiyo trend. Iweje hata wageni kama siye bado tujikute tunapatikana na trend hii?

Kwamba thread haijengi nadhani ndugu Kichuguu hayo ni mawazo yako binafsi. Bado kuna kitu tutajifunza. Kwamba ni pumba au lah nadhani hiyo nimeweka kama changamoto tu kunogesha mjadala.

Tungoje wengine nao waseme.
 
mimi nadhani kuna point ya aina fulani:

Asilimia 70 hivi tunazotoa hapa ni pumba au hazivutii na labda kuna ukweli... kwani inaendana na asilimia 70 ya mbayuwayu au wale wanaofuata mkumbo. Lakini vile vile labda ipo haja ya kuangalia watu wengi zaidi na kuweza kuona kama the pattern can be analyzed kwa kuangalia fractal mathematics.

Haiwezekani kama at random shukrani zinatolewa katika posts zipatazo not more than 30 percent ya posts zote kwa zaidi ya mtu mmoja. Kama hii ni kweli kwenye wider net ya wachangiaji then there has to be a logical explanation kwa sababu kama hii pattern iko hivi kwa wakati huu yawezekana kabisa (I can't speak with absolute certainty) hata zile zilizofutwa ni hivyo hivyo. Hata hivyo tunaweza kupata picha nzuri kwa kuangalia forums nyingine nje ya JF kama control group ili tuweze kuona kama hii pattern ni ya JF tu au inajirudia rudia katika forums nyingine vile vile.
 
Hizi takwimu zinatuambia nini jamani? Wengine hatufanyi kitu bila kutathmini.

Kimaumbile ni binadamu wachache sana ambao wanatumia neno "Ahsante" jinsi linavyostahili. Neno "Ahsante" linatoka kwenye makuzi na siyo kwenye "vinasaba". Kama mtoto hajawahi kusikia neno "Ahsante" likitajwa na mzazi au mlezi tangia anazaliwa mpaka anafikia uwezo wa kujua kusoma na kuandika, ni vigumu sana yeye kulitumia katika maisha yake ya kila siku.
 
mimi nadhani kuna point ya aina fulani:

Asilimia 70 hivi tunazotoa hapa ni pumba au hazivutii na labda kuna ukweli... kwani inaendana na asilimia 70 ya mbayuwayu au wale wanaofuata mkumbo. Lakini vile vile labda ipo haja ya kuangalia watu wengi zaidi na kuweza kuona kama the pattern can be analyzed kwa kuangalia fractal mathematics.

Haiwezekani kama at random shukrani zinatolewa katika posts zipatazo not more than 30 percent ya posts zote kwa zaidi ya mtu mmoja. Kama hii ni kweli kwenye wider net ya wachangiaji then there has to be a logical explanation kwa sababu kama hii pattern iko hivi kwa wakati huu yawezekana kabisa (I can't speak with absolute certainty) hata zile zilizofutwa ni hivyo hivyo. Hata hivyo tunaweza kupata picha nzuri kwa kuangalia forums nyingine nje ya JF kama control group ili tuweze kuona kama hii pattern ni ya JF tu au inajirudia rudia katika forums nyingine vile vile.

Hili neno Mkuu...
 
Kimaumbile ni binadamu wachache sana ambao wanatumia neno "Ahsante" jinsi linavyostahili. Neno "Ahsante" linatoka kwenye makuzi na siyo kwenye "vinasaba". Kama mtoto hajawahi kusikia neno "Ahsante" likitajwa na mzazi au mlezi tangia anazaliwa mpaka anafikia uwezo wa kujua kusoma na kuandika, ni vigumu sana yeye kulitumia katika maisha yake ya kila siku.

Obuntu...nashukuru sana naona tunaanza kupata issues - this is what i wanted to see my comrade!!
Cultural dimension kwenye malezi.Ni kweli kabisa unavyosema kuna watu hawajalelewa kushukuru.
 
sasa unatakiwa kusema kwanini ni "too low" au kwanini ni "very unprofessional"..
mkuu,
i had feelings kwamba members are concerned on WHAT SOMEONE DELIVERS rather than hizo ''thanks''!huwezi kupima mashiko ya hoja za mtu kwa kuangalia ''thanks''!the way i see this forum ni kwamba kuna kitu muhimu zaidi ya hizo thanks!....

kuna wengine huwa tunatoa thanks kwa maana tofauti kabisa!.....
 
Asante BAK na Kichuguu kwa michango yenu - naweza nikakubaliana na maelezo yenu au pia kukataa.
Assuming kuwa thanks zilifutika wakati wa kurekebisha forum bado kuna hiyo trend.Iweje hata wageni kama siye bado tujikute tunapatikana na trend hii?
Kwamba thread haijengi nadhani ndugu Kichuguu hayo ni mawazo yako binafsi. Bado kuna kitu tutajifunza. Kwamba ni pumba au lah nadhani hiyo nimeweka kama changamoto tu kunogesha mjadala.
Tungoje wengine nao waseme.

Nadhani hukuniewelewa sawasawa.

(1) Kuhusu kufutwa kwa thanks, total posts ilibaki ile ile kwa hiyo denominator ya wakongwe ni kubwa mno: kwa mfano wewe leo ukiweka posts 15 na kupata thanks 10 leo utakuwa na total 77 na thanks 43 hivyo ratio ni zaidi ya 50%. BAK akiweka posts 15 na kupata thanks 20 leo, atakuwa posts 13,381, na thanks 1584 kwa ratio chini ya 10% ingawa kwa leo alikuwa na thanks nyingi zaid yako. Ndiyo maana nikasema metric yako siyo sahihi.

(2) Nilisema haijengi kwa vile sikuona kama thread hii ilikuwa inaongeza maarifa yoyote kwa msomaji; samahani kama tafsiri yangu haikuwa sahihi. Nimezowea kuwa ninaposoma thread mara nyingi zinakuwa na mafundisho fulani hata kama zimeandikwa hovyo hovyo tu; kwa mfano ulipotangaza hapa kumtafuta mwanamne mwenye sifa za aina fulani ulikuwa unatoa fundisho fulani ambalo niliona ni la maana na wala sikuandika lolote negative.
 
Nadhani Tausi Mzalendo ulikuwa unataka kuelezea ubora wa information na uchambuzi wa mada mbalimbali unaofanywa na wanaJF, lakini kwa kigezo cha kuangalia Thanks na idadi ya post ili kupata Percentage ya kujua MwanaJF ana ubora gani katika post zake sidhani kama uko sahihi sana, japo ukweli upo kwamba kuna pumba nyingi, lakini ukae ukijua sometimes utakuta kuna hoja ya maana inajadiliwa lakini katikati ya mada utaona chating ya Members ambayo haihusiani kabisa na Mada husika na hapo ndipo mzigo wa THANKS unapomwaga, kwa hiyo hizo thanks kila mtu anatoa anapojisikia, sometimes unaweza kuona Mdau kaweka bandiko lenye uzito lakini hakuna thanx kabisa,.

HIVYO UCHACHE WA THANX KULINGANISHA NA MABANDIKO YA MTU HAYAMAANISHI KUWA NI MTAALAAMU WA PUMBA
 
nadhani nilipomsoma TM sidhani kama suala ni content hasa ya postings.. nadhani ni suala la pattern inayoonekana. Kwangu mimi I'm more intrigued kwanini katika sample hii ndogo tu trend inayoonekana ni kuwa karibu watu wote wanaopewa thanks wanapewa thanks katika asilimia isiyozidi 30 hivi ya posts zao zote. Japo si sample ya kisayansi lakini kuonekana kwake kunazua maswali fulani fulani.. Yaani haijalishi mtu anaposti nyingi au kidogo trend iko pale pale... Don't you guys find this a little bit puzzling..?

Nina uhakika waliosoma mambo ya Fractal Maths wanaweza kutusaidia kwa sababu hata kitu kinachoonekana ni random kweli kumbe kina pattern yake ya aina fulani. Kwani hakuna kitu random sana hapa kama tunavyopeana thanks lakini at the end.. hakuna anayepewa thanks zaidi asilimia kama thelathini hivi ya posts zake zote.. Haijalishi kama anaposts nyingi au kidogo ndiyo assertion ya TM.
 
Hapa tumekutana watu wa aina mbalimbali. Na kamwe haitakuja tokea siku wote tufanane mawazo.

Kuna makundi ya watu wanafanana kitabia na kimawazo basi hujikuta 'wanaiva' na hilo kundi linajenga kama urafiki fulani. Na hizo thanks zinatolewa kwa kiushikaji mara nyingi na sio kwa ajili ya Points.

Kwa kusema hivo nina maana kupewa thanks au kutopewa haina maana post yako ni pumba au sio pumba.
We differ in perception and its Healthy!
 
Wengine hatujui hicho kitufe kiko wapi... au ni kwenye PC yangu tu??
 
Back
Top Bottom