Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Kaka angalao haya yangefanyika na gazeti ambalo halina uhusiano na CHADEMA. Lakini ukweli sio tu ni gazeti lenye uhusiano wa karibu na CHADEMA lakini hata waandishi wake na hata wa makala wengi wao ni wanachama hai na wapapmbe wa karibu sana wa Mwenyekiti wake.

Sasa inakuwa vigumu sana kutenganisha haya na CHADEMA kama chama lakini pia nia na uhusika wa Mwenyekiti wa CHADEMA katika siasa chafu hizi zinazoendelea katika gazeti hilo, katika magazaeti ya mfadhili mkuu wa CHADEMA, hapa jf, na kwengineko ambako kampeni chafu hii inaendeshwa dhidi ya Zitto.

omarilyas
 

Good observation....

omarilyas
 
Wanao msakama Zitto wako kazini ila nadhani sasa Zitto kaamua vyema kwamba asome na akae kimya ajibu ikibidi na si JF atajibu mahali anapo pataka yeye .Zitto endelea na mambo mengine haya waachie hawa waendelee nayo uongozi ni gharama sana na uvumilivu .
 
Wote ni wana agenda zao hapa hivyo katika kipindi hiki sio watu makini kuhama na kwenda huko na huko ni busara kubaki katika vyama vyao
 
 
Last time niona sehemu imeainishwa kuwa zitto amejitole magari matatu kwa ajili ya ku facilitate ziara ya kafulila huko kigoma.

Lakini pia nimeshtuka sana kusoma gazeti la jana la Tanzania Daima kuhusu Kafulila na Zitto.

Please naombeni na nyie mcheki below kama ilivyo;

na Irene Mark

DAVID Kafulila, mwanachama mpya wa NCCR-Mageuzi, ambaye amekuwa akitumia uhusiano wake binafsi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kama kete ya kisiasa katika ugomvi wake na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema Zitto ni mzushi.

Kafulila, ambaye alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA kabla hajavuliwa cheo hicho na kukimbilia NCCR-Mageuzi, alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akijibu taarifa kuwa mbunge huyo amekanusha kumsaidia magari matatu ya kufanyia harakati za kujijenga kisiasa mkoani Kigoma baada ya kujiunga na NCCR-Mageuzi.

Msukumo wa Kafulila kumshutumu Zitto umetokana na tetesi kwamba amekuwa anatumia barua pepe ya mbunge huyo kusambaza taarifa zinazoleta chokochoko katika CHADEMA, kwa kuwa anajua neno siri la anuani ya barua pepe ya mbunge huyo ambaye amekuwa anamtumia kama msaidizi wake katika masuala mengi walipokuwa CHADEMA.

Taarifa hizo zilitokana na mawasiliano ya Zitto na watu walio karibu naye ambao juzi waliliambia gazeti hili wanachokiita ukweli wa madai ya mbunge huyo kumuunga mkono Kafulila katika harakati zake mpya akiwa NCCR-Mageuzi, kiasi cha kumpatia magari matatu kwa ajili ya kuzunguka maeneo kadhaa ya Jimbo la Kigoma Kusini katika siku chache zijazo.

Jana Kafulila aliiambia Tanzania Daima kuwa kama ni hivyo, Zitto ni mzushi, kwani hajawahi kumpa neno la siri la kufungua anuani ya barua pepe yake, wala hafahamu lolote kuhusu anuani hiyo.

Katika toleo la jana, gazeti hili lilkuwa na habari kuwa Zitto alimkana Kafulila, na kwamba mbunge huyo amekiandikia barua chama chake (CHADEMA) kukijulisha msimamo wake binafsi, kwa maelezo kuwa wanaomhusisha na kauli za Kafulila wana nia ya kumchonganisha (Zitto) na uongozi wa CHADEMA.

Kauli kama hii ilitolewa na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto, katika mahojiano yake na gazeti la MwanaHALISI wiki mbili zilizopita, akisema mwanawe anatumiwa na watu wenye lengo la kuvuruga chama na kumgombanisha mwanawe na uongozi wa chama chao.

Katika kauli yake ya juzi, Zitto alinukuliwa akiwaeleza watu walio karibu naye kuwa hata taarifa zinazoandikwa na vyombo vya habari kuhusu yeye ‘kumbeba’ Kafulila zinamnukuu bila kumhoji yeye.

Lakini jana Kafulila alisema: “Huo ni uzushi unaotengenezwa…password (neno siri) ni kitu muhimu, tena ni siri ya mhusika, sasa iweje Zitto anipe password yake? Hayo ni maneno ya uzushi.”

“Nimefukuzwa bila kufuata sheria. Sijaridhishwa kabisa na maamuzi yale, ndiyo maana nikaona nitafute tumaini jingine ambalo ni NCCR-Mageuzi,” alisema

Sasa tuamini yupi?
 

We nawe jana ulikuwa wapi?hii hoja imeshajadiliwa sana jana ndugu yangu...pole uwe unapitia kwanza thread za wenzako and then unatuma ya kwako.
 
Jamani nimeona article inayosema Zitto yuko mbioni kujiuzulu Chadema katika Mwananchi! Cha kushangazwa article hiyo wameitoa ghafla! Sasa najiuliza kulikoni?
 
Pia nimeiona lakini ghafla nimerudi siioni sijui vp au ilikuwa ni tetesi???
 
Si unajua gazeti la RA nathani Mh Zitto amewakoromea!
 
Guys,why don't you give Zitto a break!!!!!!,this Zitto issue imekuwa too much sasa,kila kukicha Zitto Zitto aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaargh,inaboa sasa!!
 
Ambacho nakijua , taarifa toka ndani ya chumba fulani cha habari katika haya magazeti ya mafisadi , ni kwamba habari ya kujiuzuru zito Imeisha pewa kichwa cha habari, wanasubiri huyo jamaa aamue kujiuzulu waijazie jazie maneno tu basi.
 
Guys,why don't you give Zitto a break!!!!!!,this Zitto issue imekuwa too much sasa,kila kukicha Zitto Zitto aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaargh,inaboa sasa!!
Yani mpaka inakera sasa, Nahisi hawa jamaa journalists wa TZ wamekosa habari. Maana za Ufisadi sijui zimechakaa?
 
Ukiangalia kwa makima yawezekana Mwanainchi imeishanunuliwa na mafisadi kwa ajili ya kufanya operation ya Zitto, wahahakishe wana disturbise na anaacha koconcentratre kwenye shule. Kisha ajiuzuru uanachama CHADEMA. Si unajua CHEDEMA ndo kinaipeleka puta CCM? mpaka Raisi anaona afadhari akabembeee.
 
 
Kuna Habari kupitia gazeti la Mwananchi kuwa Zitto ameweka bayana kuwa anataka kujivua nafasi zote kupitia Chadema kutokana na hali ya kisiasa kupitia Chadema na kudai kuwa anataka kuendelea na maisha yake ya kawaida na pia amesema kuwa ataendelea kumuunga mkono mgombea wa NCCR MAGEUZI Kigoma Kusini hata kama CHADEMA wakiweka mgombea wao. Je Ndugu zangu wadau wanasemaje huu ya hali ya mambo ndani ya CHADEMA. Hali kama hii inakatisha sana tamaa na kuona badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma.
 

Mkuu umeshathibitisha? ukituthibitishia tutajadili kwa lugha zote. Hatuwezi tukajadili hali ya Chadema mpaka tuone nini kinaendelea ndani.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…