IGP Sirro: Jeshi la Polisi kukagua yanayofundishwa kwenye nyumba za Ibada

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,957
141,948
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
===
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
 
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa lintakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
 
Ndio aliyotokanayo Rwanda

1631354618452.png
1631354981453.png
1631355071000.png
 
Kuuzungusha mkono wa kulia kichwani kwa lengo la kushika sikio la kushoto ni kupoteza muda na nguvu wakati mwingine.
 
Tunajua nyumba za ibada wanazozilenga. Lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu anajifunzia ugaidi msikitini, sio Tanzania labda nchi nyingine huko.

Badala ya kutafuta sababu za msingi na vyanzo halisi vya ugaidi wao wanaanza kutafuta chuki na uhasama na dini fulani. Upumbavu nao ni kipaji.
 
Kwa mtaalam wa masuala ya usalama haswa ukusanyaji na uchakataji wa taarifa za kiintelejensia, hili tamko la IGP ni passive.

Intel inayofanyia kazi realtime situations na kupuuzia core concepts zinazothimilisha mwenendo wa kiuhalifu, inasababisha kushindwa kubaini chanzo na mizizi ya matukio yanayoshamiri

Kuna wahuni wamejificha ndani ya safe zones na hata wengine kushiriki mambo chanya ya kijamii huku in real ni sleeper agents. Wanasubiri muda wa kufanya matukio yaliyo kwenye mikakati yao.

Nafasi za wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji zikitumika vyema tutaweza kuepusha madhara mengi ndani ya jamii.

Siro, pambana na vibaka waliojaa mitaani, hawa unaodhamiria kuwamulika mara nyingi wapo steps ahead.

Security and Intelligent diplomacy inahitajika sana kutengeneza goal concepts za usalama wa nchi.
 
Back
Top Bottom