Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Hii ndiyo kazi nzuri aliyo fanya JK tangia aingie madaraka kama ambavyo ES na mwenzake yule BBC London wamekuwa wakihubiri hapa . Sasa wache watueleze kwa nini inflation kubwa hii ?
 
I predict by budget time the inflation will have hit 10%.
 
Mimi nangoja wasemaji wa Serikali yule jamaa wa BBC sijui anaijiita majina gani humu na jina lake kamili pia liko na Mzee Es waje waseme kitu gani kinaendelea , maana Muungwana ni mchapa kazi lakini uchimi ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
someone is trying to be smart here/thinks that he/she smarter than others by culminating peoples idea, simply kwa kuweka his/her vague statements eti kwa kisingizio cha kutafuta mawazo ya wasomi, hii ndio tunaiita NONSENSE!

wee kama unataka anylysis be objective, what type of analysis you want, ya Kihasibu, kingwini, and on and on.

Hapa JF watu twawajua/wafahamu tokana na maandishi yao na wengine wachache wamejitaja kuwa wao ni nani, na watu wamekuwa wakishusha nondo hapa randomly wanapojisikia either kuelimisha au kufafanua jambo fulani.
 
Kwa mtu anayefuatilia kitimu timu cha kashfa ya Richmond, hakuna shaka kuwa ameishaona kuwa dalili zote zinaielekea serikali ya Jakaya Kikwete maarufu kama kasi mpya, nguvu na ari mpya.

Hakuna ubishi kuwa sasa kasi mpya,nguvu mpya na ari mpya tuliyoahidiwa haina maana nyingine bali kuelekea kuzimu. Pia hakuna shaka kuwa kwa taarifa iliyotoka mwezi jana kwenye gazeti la Rai linalomilkiwa na mshirika mkuu wa Kikwete na Lowassa, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, inaonyesha wazi Lowassa alivyo Richmond yenyewe.

Nilisoma makala moja kwenye gazeti la Tanzania Daima ambalo kwa sasa limekuwa adui namba moja ya ujambazi unaoendeshwa nchini mwetu. Makala ya mtu ajiitayo Mpayukaji, ilinivutia kuandika makala hii pamoja na kukaa kimya kwa muda mrefu.

Huyu Bwana ni mpayukaji kweli kweli. Yeye na Mbowe wamesababisha serikali ilione gazeti la Tanzania Daima mwiba kama ilivyokuwa mwaka jana kwa Habari Tanzania.

Sasa tukirejea kwenye taarifa ya kwenye gazeti B la CCM la Rai, kuna maswali yanajitokeza. Kwa mfano, ofisi ya waziri mkuu ilitoa tangazo la kupotosha kuwa kwa vile suala la Richmond liko mikononi mwa TAKURU haliwezi kujadiliwa na bunge. Kwanza ni mpumbavu gani anaweza kuiheshimu na kuiamini TAKURU ambayo inasifika kwa kuwasaka vidagaa wa rushwa huku ikiwakingia kifua mipapa?

Rejea kisa cha Mchungaji Christopher Mtikila alipomtuhumu waziri mkuu wa zamani Fredrick Sumaye kuwa ni mla rushwa nambari wani nchini.

Badala ya TAKURU kumhoji Sumaye ilimhoji Mtikila. Pia ukiachana na hilo ukaangalia wafanyakazi wa TAKURU, wana kila dalili za kuwa walarushwa sawa na waliwaajiri.

Hiyo tisa. Kumi ni pale ilipotoka barua nyingine toka kwa Waziri Mkuu kwenda kwa waziri wa zamani wa nishati Ibrahim Msabaha eti ikionyesha kuwa waziri mkuu, Lowassa alikuwa akimuonya Msabaha kuwa makini na dili la Richmond.

Ni utoto na kutapatapa kiasi gani! Kama waziri mkuu Lowassa kama anavyotaka tumuone mkweli, anashindwa nini kuonyesha nia hiyo ya kumtahadhalisha Msabaha ambapo imeishajulikana kuwa Richmond ni bomu na rushwa tupu? Je kwanini serikali inahangaikia Richmond hata kuliko wajibu wake mwingine? Inachoficha ni nini?

Hawa watawala majambazi wanataka kutufanya sisi mafala. Hawajui kuwa licha ya kuleta Richmond ambayo kimsingi haina lolote la maana zaidi ya kuwa uchochoro wa akina Lowassa kuibia pesa zetu, tunajua kuwa hata wakati wa mgao wa umeme mtoto wa Lowassa aliagiza majenereta toka Uchina akayapitisha bandarini bila kulipia ushuru na kuwalangua watanzania.

Pia hakuna ubishi kuwa jinsi bunge letu chovu la CCM na upinzani dhaifu ambao nao unaonekana kuanza kunogewa mashangingi,serikali imekuwa ikitoa majibu yenye mashaka na kuonyesha kuishiwa.

Akijibu swali la Mbunge wa Bububu, Cosmas Masolwa, waziri mdogo wa Uchumi, Mipango na Uwezeshaji, Gaudence Kayombo, kwa hila na jeuri alilidanganya bunge kuwa halina mamlaka kisheria kuangalia mikataba inayoingiwa na serikali.

Hii ni baada ya Masolwa alipotaka wabunge waletewe mikataba waangalie kulikoni.

Mwongo huyu anayeonekana kihiyo na chitalilo eti alisingizia dhana ya mgawanyo wa mamlaka (Separation of Powers).!

Dhana hii ilianzishwa ili kuzifanya nguzo tatu za dola yaani Utawala,Bunge na Mahakama kukaguana na kuheshimiana kimamlaka bila mmoja kumtumikisha mwenzake,kumdharau au kumuingilia. Hakuna anayeruhusiwa kujiona bora kuliko mwenzake wala mmoja kufanya kazi ya mwenzake.

Lakini chini ya utawala wa sheria ambao ndiyo mzizi wa dhana hii lazima vyombo hivi vitatu vikaguane.

Kwa ufupi ukiangalia waziri mdogo alivyojibu,unajua kabisa kuwa alitumwa na bosi wake.

Sasa Lowassa anaingiaje? Kwa taarifa za magazeti mengi ya Tanzania,kuna kila dalili kuwa kama Richmond si Lowassa ni Kikwete au wote. Kwa sababu jinsi wananchi walivyoshupalia uchafu huu, hakuna shaka wawili hawa wasingekuwa na ubia kwenye kampuni hili wangekuwa wameishachukua hatua.

Hapa ndipo maneno ya Baba wa taifa alipoonya kumtahadhali Lowassa yanatimia.
Hapa ndipo kukataliwa kwa Kikwete na Mwalimu kunaanza kuonyesha maana yake.

Hakuna ubishi kuwa Kikwete ameanza kuwa bomu kuliko hata Benjamin Mkapa ambaye wameunda urafiki wa kulindana na kufichiana madhambi. Rejea magazeti kutaka Mkapa ajieleze kuhusu dili la rada.

Kikwete akiwa Stokhlom alimkingia kifua kuwa Mkapa aachwe. Hiyo tisa. Sasa limefumka bomu la TANESCO. Nalo nyuma yake kuna Mkapa maana kwa wanaokumbuka Net Solution iliyoletwa na shemeji zake ilivyokingiwa kifua naye hawana wasi wasi kuwa alikuwa nyuma ya wizi huu.

Je tutakapomtaka Mkapa kwa mara ya pili atueleze ukweli, Jakaya ataruka na kusema tusimguse?

Kinachoendelea ni kuondoka kibaka mmoja na kuingia kibaka mwingine. Hapa ndipo hata siri ya mawaziri wezi na wachafu walioingia mikataba ya wizi kuteuliwa inapofichuka. Kimsingi kinachoendelea ni kiini macho kinachofanywa na bwana mazingaombwe wale wale.

Tuhitimishe. Jakaya na Lowassa hawawezi kuikomboa nchi yetu. Badala yake wanaizamisha kwenye Richmond na mambo mengine yatakayoibuka baadaye.

Leo uchumi wetu unaanza kuporomoka utadhani unaharisha. Matumizi yasiyo na nidhamu ndiyo hayo yamekuwa fasheni.

Rushwa inazidi kuongezeka. Au ndiyo kurejesha pesa walizotumia kwenye takrima.

Nchi yetu kwa sasa imevamiwa na genge sawa na lile la Marekani ambapo George Bush anaendeshwa na Dick Cheney nyuma ya pazia kama ambavyo Kikwete naye anaendeshwa na Lowassa na Mkapa nyuma ya pazi. Ni hatari kuwa na rais katuni.


Swali la leo. Je Lowassa na Rostam Aziz waliomfaidi Jakaya ndiyo wanaipiga mnada nchi yetu kurejesha takrima waliyowahonga wapiga kura wetu. Yangu macho.

Msisitizo. Kama Richmond siyo Lowassa basi ni Kikwete au Rostam Aziz au tuseme ndiyo utatu mtakakitu? Nuru tuliyoambiwa kumbe siyo bali kiza!
Kama Malecela, laana ya Mwalimu Nyerere na imtafune Lowassa milele na milele.

Source: HabariTanzania.com
http://www.habaritanzania.com/articles/3558/1
 
Shughuli pevu.... Tumekwisha! kule kwetu tuna msemo " Na litote, tugawane mbao!"
 
Habarileo,
Mimi nataka hata hiyo Vodafone itazamwe upya! hawa jamaa wezi wakubwa kwa kutoza wananchi hizo vocha ambazo hazina muda wa kuongea!
Itakuwaje Tsh 5000 ambayo ni kama dollar 4 huwezi kuongea hata dakika 5 hali nchi za wenzetu walioendelea unapata zaidi ya saa nzima?.. hiyo IPTL yenyewe mara hawana nyaya mara hawana simu, milingoti basi ili mradi wasiwepo ktk ushindani na makampuni ya wazee vigogo.
tazama TV cable ati ni laki moja karibu USd 80 kwa mwezi na kinachoonyeshwa zaidi ni mpira!... hapo pia kuna mguu wa mkubwa jamani JK nipe kazi mimi nimalizane nao hao kama wewe kweli waogopa kufa!... watapambana na Mkerewe mie tuone kama kweli wanaweza kuyakoga!

Upuuzi mtupu na nitawaibua wote!
 
Eee bwana Habarileo mimi nitarudi tena kusoma post yako; imesheheni ikasheheneka. Nimependa zaidi hitimisho, "laana ya mwalimu Nyerere na imtafune Lowasa milele na milele! Safi sana.
 
NB: Nimeruka salamu za mwanzo wa hotuba

Kwa vile ni hotuba ndefu, nimeona niwawekee kwenye attachment.
 

Attachments

Kaka tunashukuru! Tatizo ni kutafsiri hizi hotuba katika matendo!
 
Hongera Raisi, kwa kuona matatizo katika ajira, na kuweka ahadi ya kutetea na kulinda maslahi ya watanzania.

Hongera kwa Mfuko wa Akiba ya Uzeeni wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa. Hivi wakulima wanautaratibu gani wa mafao wanapozeeka??? Kama hakuna, taratibu gani zitumike ili waweze kujikimu uzeeni nguvu ya jembe inapoisha.

Hongera, kwa kuboresha mishahara ya wafanyakazi, ila epuka haya matume, pesa zinakwenda sana mzee.

Ni vyema umeongelea tatizo la wajiriwa katika sekta binafsi kuhusiana na mazingira ya kazi na mishahara yao, lakini, haujatoa bold statement nini hitima yao, umeishia kusema ni matumaini na matarajio yako ufumbuzi utapatikana kupitia ushirikiano kati ya bodi za kima cha chini, wafanyakazi na waajiri. Wewe, si ndio raisi, ulitakiwa kuwachapa tu na masentensi ya viwango.


Nimesikitishwa kimsingi kabisa kugundua kwamba mwekezaji wa nje naye amekuwa sehemu na umuhimu sawa katika nguvu kazi ya taifa hili. Inawezekana ni mimi tu, lakini inaniuma moyoni, mimi na mwekezaji wa nje kupewa hamasa sawa na raisi wangu, kwenye sikuku yangu ya taifa. Sikubali hata kidogo. Umesema (Kwa sababu hiyo, naomba kukumbusha wajibu wetu sote, viongozi, wafanyakazi, wakulima, wawekezaji na wananchi kwa ujumla wa kufanya kazi kwa bidii zaidi na maarifa katika kukuza na kuendeleza uchumi wetu).


Jamani jamani toka lini, toka lini, wawekezaji wakategemewa kuleta maendeleo kwa taifa?

Hii ni hatari kabisa, tunaongelea sikukuku ya wafanyakazi, lakini tunagundua kwamba na wawekezaji mumo kwa mumo, mama wee!

Hongera kwenye mikataba angalau kwa kujaribu kurekebisha mambo. Ila bado mzee, nionavyo mimi, tumeamua kula maembe, chungwa ama pera, lakini miti tumeiacha. Nionavyo mimi, hili linchi ni letu, letu kabisa, hatukuliokota, mungu kama yupo, ndio alisema hichi nikipande chetu, mimi nashidwa kuelewa tunashidwa vipi kufanya maamuzi yenye msimamo. Sikubaliani na hizo peanuts wanazotupa. Kama tumeingia nao mikataba tulikuwa ni sisi, na hili liardhi ni letu nitaendelea kukataa kusema hiyo mikataba haivunjiki. Kwani tukivunja watatufanyanini???

Hongera, lakini kazi bado ipo... tena pevu
 
kwa muda mrefu nimekuwa nikiamini kwamba Kikwete ni kilaza, lakini habari hii imenishawishi kuanza kumkubali. Hongera Jakaya Kikwete!!

source: www.majira.co.tz

Kikwete: Wingi wa vyuo vikuu si tiba

Na Joseph Lugendo

RAIS Jakaya Kikwete amechangisha sh. milioni 88 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sebastain Kolowa na akataja mbinu inayohitajika kuongeza idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji yake nchini.

Hafla hiyo ya kuchangia ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya Chuo hicho Kikuu Kishiriki cha Sebastian Kolowa cha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kinachojengwa Lushoto, Tanga ilifanyika Jijini Dar es Salaam juzi usiku.

Rais Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi alisema vyuo vikuu vinatakiwa kuongeza idadi ya wanafunzi ili kuongeza ufanisi
wa rasilimali watu kwenye vyuo hivyo.

Alisema kuwepo kwa vyuo vingi nchini lakini vinavyochukua wanafunzi wachache hakusaidii kumaliza tatizo la ongezeko la wanafunzi wanaohitaji kujiunga na elimu hiyo.

Badala yake, Rais alisema kunasababisha ongezeko kubwa la gharama ya uendeshaji kwa kila mwanafunzi atakayejiunga navyo.

"Sasa Tanzania ina zaidi ya wanafunzi 46,700 wanaochukua elimu ya juu ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi 10,000 kwa mwaka iliyokuwepo miaka michache iliyopita," alibainisha Rais Kikwete na kuongeza kuwa mafanikio hayo ni madogo ikilinganishwa na changamoto kubwa iliyopo mbele yao.

Alisema idadi hiyo ni jumla ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo 30 vya elimu ya juu nchini ambayo ni sawa na idadi ya wanafunzi waliopo kwenye chuo kikuu kimoja cha Havard cha Marekani.

"Kenya inachakua wanafunzi wa elimu ya juu 108,000 kwa mwaka na Uganda 88,000. Sidhani kama hawa wana vyuo vingi kiasi hicho," alisema na kuongeza Chuo Kikuu kipya cha Dodoma kitafikia uwezo wa kuwa na wanafunzi 40,000 kwa mwaka katika miaka michache ijayo.

Kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali watu, Rais alitoa mfano wa Mhadhiri mmoja kwenye chuo chenye wanafunzi 16,000 anavyoweza kutoa mhadhara kwa zaidi ya wanafunzi 500 kwa saa wakati kwenye chuo chenye wanafunzi 500 atajikuta akilazimika kutoa mhadhara huo huo kwa wanafunzi 40 tu.

"Hii kwenye lugha ya uchumi ya economics of scales (matokeo ya uchumi wa uzalishaji mkubwa) ni matumizi mabaya ya rasilimali watu," alisema Rais Kikwete.

Kuhusu mtazamo wa mwanzo wa chuo hicho kwenye ufundishaji walimu, utoaji huduma na utafiti kwenye elimu maalumu kwa jamii yenye mchanganyiko wa watu walemavu Rais Kikwete aliitaka jamii kwa ujumla kutoishia kutoa elimu maalumu tu, bali pia kutoa muangalizo maalumu kwa walemavu.

Aliwataka walimu wanafunzi wa sekondari kutilia mkazo masomo ya sayansi kwa kuwa uchumi wa nchi unahitaji watu wenye taaluma ya sayansi na tekinolojia ili yapatikane maendeleo ya kweli.

"Mwaka 2004 kati ya wahitimu wa zaidi ya 4,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam asilimia 21 tu walihitimu masomo ya sayansi," alisema na kulinganisha na Korea Kusini ambapo kati ya wanafunzi zaidi ya 600,000 kwenye vyuo vyao asilimia 39 walikuwa wakichukua fani za sayansi.

Chuo Kikuu Kishiriki cha Sebastian Kolowa kinatarajiwa kuanza na wanafunzi 200 wa fani ya ualimu na kuanzisha masomo fani za sheria, uchumi, uhandisi.

Tofauti ya chuo hicho na vyuo vingine ni mkazo kwenye mafunzo ya elimu maalumu kwa ajili ya kusaidia jamii ya watu wenye uelewa wa polepole na walemavu wa aina zote ambapo wanafunzi wote wa chuo hicho watatakiwa kujifunza.


Rais Kikwete alisema maendeleo ya nchi yataletwa kwa mapinduzi ya sayansi na teknolojia na kwa sababu hiyo ametoa wito maalum kwa vyuo vikuu vya umma na vya binafsi kutoa kipaumbele maalum kwa masomo hayo.

"Elimu ya sayansi lazima ipewe umuhimu wa pekee. Vijana wetu wengi hawapendi masomo ya sayansi na watoto wa kike wanakimbia masomo ya hesabu. Lakini ili nchi yetu iendelee lazima tutilie mkazo maalum masomo ya sayansi," alisisitiza.

Rais aliwaeleza washiriki wa hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Bw. Benjamin Mkapa na mkewe, Mama Anna Tanzania iko nafasi ya chini kwa uchache wa wanafunzi wanaochukua masomo ya sayansi.

Kwa mfano alisema, takwimu zinaonesha kuwa katika wanafunzi wote wanaosoma shule za sekondari ni chini ya asilimia 30 ndio wanaochukua masomo ya sayansi.

"Na ukilinganisha na vyuo vikuu vingine duniani, sisi hapa ndio wa mwisho katika masomo ya sayansi. Kwa hiyo lazima tuongeze nguvu katika kukuza na kuendeleza elimu. Lakini masomo ya sayansi yapewe umuhimu wa pekee," alisema.
Mbali ya kuvitaka vyuo vikuu vya umma na vile vya binafsi kutoa uzito maalum kwa masomo ya sayansi, pia aliwashauri wamiliki wa vyuo hivyo kufikiria mkakati wa kuvipanua vyuo vyao ili vichukue wanafunzi wengi zaidi kukidhi mahitaji.

"Napenda kutoa ushauri wangu kwa wamiliki wa vyuo vikuu vya umma na binafsi kwamba muanze kufikiria kuvipanua vyuo vyenu ili vichukue wanafunzi wengi zaidi.

Nalisema hili kwa sababu hofu yangu ni kuwa tunaweza kuwa na vyuo vingi lakini vinavyochukua wanafunzi wachache na tusipokuwa makini Tanzania itakuwa na sifa ya kuwa na vyuo vikuu vingi
lakini wanafunzi wachache" alisema.

Alisema lengo liwe kuwa na vyuo vikuu vikubwa na vinavyochukua wanafunzi wengi tofauti na ilivyo sasa ambapo tuna vyuo vikuu 30 vikiwamo vyuo vikuu vishiriki lakini vina wanafunzi 46,000 tu.

Alisema upanuzi wa vyuo vikuu vilivyopo utasaidia kukuza uwezo wake wa kuchukua wanafunzi wengi na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji wake.

Akizungumzia maendeleo ya jumla ya sekta ya elimu hapa nchini, Rais alisema Serikali imejitahidi na inaendelea na
kazi ya kuistawisha na kutoa kipaumbele maalum katika maendeleo ya sekta hiyo.

Alieleza kuwa ongezeko la bajeti katika sekta ya elimu kwa mwaka huu ni uthibitisho tosha wa namna Serikali inavyoweka mbele maendeleo ya elimu.

Hata hivyo alisema pamoja na mafanikio hayo, bado kuna kazi kubwa ya kupanua na kuimarisha elimu nchini na ndio maana Serikali imekuwa ikiwaomba wadau wengine yakiwamo mashirika ya dini, sekta binafsi na watu binafsi kuchangia katika maendeleo ya elimu hapa nchini.

Akizungumzia Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa ambacho kinatarajia kuanza kuchukua wanafunzi Septemba, Rais aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuamua kufundisha mitaala maalum itakayozingatia mahitaji ya walemavu.

Alisema watu wenye ulemavu mbalimbali na mahitaji maalum wanahitaji kutambuliwa na kuthaminiwa na jamii.

Aliwashukuru wadau wa elimu yakiwemo mashirika ya dini kwa mchango wao mkubwa kuendeleza elimu na kutambua jukumu la kuwapatia watoto waKitanzania elimu ni la viongozi wa Serikali, dini na sekta binafsi na wazazi.

Chakula hicho cha hisani kiliambatana na na mnada wa vitu mbalimbali ambapo sh. 83, 934,750 zilipatikana kati ya hizo sh. 18,711,000 zikiwa fedha taslimu na
sh. milioni 51.123,. 750 zikiwa ni ahadi.

Rais Jakaya Kikwete alichangia shilingi milioni tano huku Rais mstaafu, Bw. Mkapa na mkewe, Mama Anna wakitoa sh. milioni tatu. Bw. Mkapa pia alitoa saa yake iliyonadiwa kwenye halfla hiyo.

Lengo la makusanyo katika hafla hiyo lilikuwa sh. milioni 400. Tayari washarika wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya KKKT wamechangia sh.milioni 136 na hivyo kuwa sh. milioni 289. Hii ilikuwa ni harambee ya tatu kuchangia ujenzi huo.
 
JokaKuu,
Kwanini serikali ndo inaliona hili sasa! Kuna Vyuo Vikuu vingine vina wanafunzi 100!
Moi yeye alikuwa na matatizo yake- ila kwa investment in Higher Learning he was so strategic- alianzisha 4 large public Universities, (Moi, Ergaton n.k)- amnbavyo kwa pamoja sasa vina zaidi ya wanafunzi 80,000.
Sisi tumeruhusu kufungua mlolongo mkubwa wa Private Universities and converting existing colleges/ secondary schools into Universities- ila number of students so low!
JK angefungua tena 2 more Universities kama Dodoma then tungaenza kuongelea kuelekea ktk critical mass!
The problem is quality of products! This is a question of numbers- start quantitatively and improve the quality as you go alone!
 
Kikwete had a point mpaka alipoanza kuongelea ratio ya lectures to students. Ratio hiyo ikiwa kubwa sana inaweza kuathiri quality ya taaluma na wakufunzi.

All in all ameanzisha mjadala mzuri, na tumpe hongera zake.
 
....

Aliwataka walimu wanafunzi wa sekondari kutilia mkazo masomo ya sayansi kwa kuwa uchumi wa nchi unahitaji watu wenye taaluma ya sayansi na tekinolojia ili yapatikane maendeleo ya kweli.


“Elimu ya sayansi lazima ipewe umuhimu wa pekee. Vijana wetu wengi hawapendi masomo ya sayansi na watoto wa kike wanakimbia masomo ya hesabu. Lakini ili nchi yetu iendelee lazima tutilie mkazo maalum masomo ya sayansi,” alisisitiza.

...
“Na ukilinganisha na vyuo vikuu vingine duniani, sisi hapa ndio wa mwisho katika masomo ya sayansi. Kwa hiyo lazima tuongeze nguvu katika kukuza na kuendeleza elimu. Lakini masomo ya sayansi yapewe umuhimu wa pekee," alisema.

Hivi hawa wanaomuandikia hizi hotuba huwa wanafikiria? Mimi naona kuna kaukilaza ka aina fulani. Analalamikia wanafunzi wachache kuchukua masomo ya Sayansi wakati tuna wanafunzi karibu 20 wanaotaka kusomea udaktari, uhandisi kule Ukraine ambao serikali yake mwenyewe inataka kuwatumia tiketi warudi nyumbani? Mbona maneno hayaendani na vitendo? Mimi nimeanza kupatwa kidhungudhungu.

asante
 
Hivi hawa wanaomuandikia hizi hotuba huwa wanafikiria? Mimi naona kuna kaukilaza ka aina fulani. Analalamikia wanafunzi wachache kuchukua masomo ya Sayansi wakati tuna wanafunzi karibu 20 wanaotaka kusomea udaktari, uhandisi kule Ukraine ambao serikali yake mwenyewe inataka kuwatumia tiketi warudi nyumbani? Mbona maneno hayaendani na vitendo? Mimi nimeanza kupatwa kidhungudhungu.

asante

Take 5 Senti Fifty.

Wanafunzi huwa sio hohe hahe...utamshauri vipi mwanafunzi asome sayansi ili awe daktari (baada ya shule ya miaka 6) huku akiona madaktari wanatembeea kwa miguu na wenye Advance Diploma za Accounts wanaendesha Toyata Mark II na BMW's. Ukingangania kuwa mwasayansi Africa utakufa masikini; vijana wetu wanaona ukweli huo na wala hawadanganyiki.
Sana sana ukiwa mwanasayansi mashuhuri itakubidi utumie umaarufu wako kujiingiza kwenye siasa; kama wakina Prof Msolla na Prof Mwandosya ila huko nako utayumbushwa na wenye Advan Diploma mpaka na wewe mwenyewe utaonekana kilaza tu.

Zaidi ya hayo; mimi bado sijashawishika bado namuona huyu Mheshimiwa ana Mapungufu Mengi.
 
Back
Top Bottom