Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Muungwana mie nilikua na Imani nae kama kaja kutuokoa watanzania lakini sasa hivi naona kama vile ni njama imefanywa Awekwe ili aje kuvuruga kila kitu kama yeye havurugi wanaovuruga ni wa chini yake si awaondoe tu aweke wengine kwani wao ni muingu watu?
 
Kuna nafasi hazipaswi kufanyiwa majaribio,mojawapo ni ya Urais.

Kama alivyosema Mwalimu, urais sio nafasi ya mchezo, unapita mitaani na kuona namna wananchi wako walivyo hohehahe, unasoma magazeti na kuona namna watu wanavyoteketea na magonjwa yanayoweza kuzuilika, unaangalia kwenye runinga na kuona namna wananchi wa nchi nyingine zenye nafuu wanavyofaidika na ustawi wa nchi zao. Urais wa nchi masikini ni kazi ya wito…..

Japo bado wapo wabishi sugu wanaoendelea kuamini kuwa JK ni chaguo la Mungu na atapunguza kama sio kumaliza matatizo ya Tanzania, binafsi sioni dalili zozote za kunifanya niamini hivyo. Hakuna udhati kwenye dhamira za JK. Maisha bora kwa kila Mtanzania…..

Pia nilipomsikia JK akitamka bila uoga kuwa anawajua wala rushwa lakini anawapa muda wajirekebishe nikatambua wazi kuwa huyu jamaa hayuko serious na ahadi zake.

Rushwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo, sasa kwa kuwapa muda wala rushwa wajirekebishe inamaanisha kuwapa idhini wamalizie kula rushwa kabla hawajachukuliwa hatua.

Mwaka umepita sasa tangu JK atoe tamko hilo na hajatupa feedback iwapo hao wala rushwa wameshajirekebisha lakini haihitaji certificate ya uchumi kutambua kuwa nchi yetu inatafunwa vibaya mno.

Kasi, ari na nguvu mpya imeshaonekana: kwenye matumizi yanayozidi mapato. Utabiri wangu ni kuwa JK ataamua kutogombea 2010 baada ya kugundua kuwa urais sio jambo la majaribio. Hopefully,and good for him, atayemrithi atakuwa ni chaguo lake la sivyo atakuwa kiongozi wa kwanza TZ kwenda kunyea ndoo Segerea.


Ama kweli wewe Mlalahoi! Unawajua walalahoi wenzako wanachotaka. Inashangaza nafasi hii kubwa katika nchi yetu ikishikwa na mtu ambaye hayuko serious na matatizo yanayoikumba jamii yake. JK kishawatembelea watanzania walio wengi na kujionea ugumu wa maisha walio nao na kujionea namna walivyobandika picha zake kwenye kuta za nyumba zao za udongo huku picha zenyewe zikiwa ni zile za 2005 zenye kuambatana na maneno Tutahakikisha maisha bora kwa kila mtanzania, Tutahakikisha watanzania wote wenye uwezo wa kusoma wanasoma, Tutahakikisha tunapunguza kodi ambazo ni kero kwa wananchi n.k

Wanaoamini kuwa JK ni chaguo la Mungu basi Miungu ni wao waliomchagua kwani Mungu siku ya kupiga kura hakuchagua na kwa mawazo yangu madogo sana ni kuwa asilimia kubwa ya wanadamu ni wadhambi wakubwa na wanafiki, basi JK ni chaguo la wadhambi na wanafiki kwakuwa ndio wengi? No, not at all! Ni kuwa maneno yake matamu wakati wa kampeni na tabasamu lilioambatana na ahadi ya KUENDELEZA mazuri yote aliyoyakuta na vilichangia kumpa credit mbele ya walalahoi walio wengi! Laiti wangelijua kuwa uwezekano wa yasemwayo ni mgumu kiasi hiki.

Aliibuka Amina Chifupa wa Mpakanjia na mbinu ya kujitengenezea jina huku akidai kuwa na majina ya wazungu wa Unga; sijui imekuwakuwaje hadi imefifia na kutusahaulisha. Kama alidanganya anatakiwa AWAJIBISHWE! Same for JK, baadae kwenye vyombo vya habari akasema kuwa majina amewapa PCB na wanayafanyia kazi. Hivi mbona kesi ya Dito ilikimbizwa harakaharaka ili kumnusuru mwenzenu? Ina maana hawa wanaoliibia taifa mnawapa nafasi ya kuendelea kuiba?

Mlalahoi, JK kutogombea mwaka 2010 unakuwa umekosea, labda humjui huyu! Nakuhakikishia hata 2015 anaweza kutamani kuongeza kipindi cha miaka walau 5 afikie 2020! Yangu mie macho.


Kama Mtume alivyo shushiwa maandiko matakatifu ndivyo pia sisi Watanzania Mungu ametuletea Mtume na Mwokozi wa Watanzania JK au mnasemaje ?


Haha, Hussein now you made me laugh japo sikutarajia. Haya ndiyo anayoimba mwanamama mmoja (Vick Kamata) anayemfananisha JK na Nabii Suleiman. What a joke? Tena Televisheni ya Taifa umekuwa kama ndo wimbo wa taifa! JK naye nadhani kwa kufananishwa na Suleiman ameridhia kuwa anastahili. Hizi sifa nyingine zinakuwa beyond the expectations.


Mlalahoi,
Hilo dua lako naona umekosa pa kulielekeza. Yaani JK aachie hatamu za utamu thubutu! Nakuhakikishia hata 2015 kutakuwa na watu wanapendekeza abadilishe katiba ili aendelee tena.
Ninachoweza kubashiri hapa ni kuwa 2010 atakuja na maneno haya "nipeni tena miaka mitano niweze kumalizia kazi niliyoianzisha"
Wanaoweza kumfanya asigombee ni watoto wake ambao wanafika hapa jambo JF, Tafadhali mwelezeni Pops aitendee haki Tanzania kwa kuachia ngazi 2010. Kama ni hamu ya Urais si imeshaisha?


Tabasamu, nadhani kama kuna mmoja wa watu wanaohisi kitakachofuata na kupatia ni wewe. Hizo hisia ziko kwa wengi na wengine wanajiuliza ilikuwaje wakampa jamaa kura siku ile? Lakini yote yanabaki kuwa ni trial number 1! 2nd & 3rd will follow. Nadhani watoto wake hata wakija JF na kuchangia ama kusoma hawataweza kubadili msimamo wa baba; siwezi kuwalaumu watoto kwa kushindwa kumshauri baba lakini nitawalaumu wasipomfikishia ujumbe kuwa watanzania hawafurahishwi na mambo kadha wa kadha ambayo kama wameyasoma kwenye jamvi hili watakuwa wanaona wazi kuwa si kuwa watanzania wanalalamika tu bali wamechoshwa na usanii unaoendelea. Kifupi wanataka kuona ahadi zinazotekelezeka!


bajeti ya mwaka ujao wa pesa TRILLION 5.2 ..hiyoo inakuja ,sijui hii deficit ya mwaka huu 1.3 trillion projected till june wamejumlishia huko?


PM, hiyo 5.2 bado ni ndogo. Mwenyewe niliposoma gazeti nikaona wamesahau yaliyowakuta budget ya mwaka huu. Wangefanya 8 kamili inge-boost up mambo mengi yakiwemo ya vikao vya dharura na safari zisizotarajiwa na nyingine Bilioni kadhaa ziitwe Mabilioni ya JK ili watanzania wasije wakamsahau kabla ya 2010!


Kuna wengi humu Jambo Forums walishangilia sana JK alipoibuka mshindi Dodoma.

JK alipoanza vibaya sana kwa kutangaza baraza la mawaziri 60, nilitabiri kwamba kabla hajamaliza miaka 2 madarakani, kasi ya mfumuko wa bei itazidi 10% kwa mwaka. Nilitabiri vile kwamba kabla hajamaliza miaka 5 ya kwanza, tutafikia kasi ya mfumuko wa bei ya karibu 20% kwa mwaka.

Takwimu alizotoa Waziri wa Fedha wakati huu ni kwamba kasi ya mfumuko wa bei imeshafikia 7.3% (Ilikuwa 4.5% JK alipochukua nchi). Kasi ya kukua kwa pato la taifa ilikuwa 7.2% JK alipochukua nchi na tayari imeshuka hadi 5.8%. This 1.4% decline in GDP growth rate translates into a decline in the rate of growth of the national wealth by some 56bn/- each year.

Tutasingizia njaa na mafuta mpaka lini?

Augustine Moshi


Mwalimu wangu uko sahihi; siku JK amechaguliwa mimi sikushangilia bali nipigwa bumbuwazi. Yani nilibaki kama nimeganda vile! Wakashangilia wengi weee lakini mimi akili ilikuwa mbaali, nikitafakari kura zitakazofuatia wakati wa uchaguzi mkuu. That’s what happened buddy!

Mfumuko wa bei… kwa asiye Tanzania anaweza asielewe lakini hali ya maisha inazidi kudorora kila kukicha. Mishahara ya watanzania wengi haikidhi tena maisha yao. Rushwa lazima itaendelea kwa namna hii. Mshahara wa 58,000/= wa wafanyakazi wengi wa sekta binafsi ni almost NOTHING. Just imagine mtu na degree yake na anapewa u-Manager na mwajiri wake kasha analipwa mshahara Gross Tshs 150,000/= na fikiria kwa kina anakatwa PAYE na kuibuka na kama Tshs 105,000/= kisha kumbuka kuwa nauli ya daladala kwenda na kurudi anapanda magari mawili @ safari hivyo kutumia 1,200/- kila siku kwa nauli tu, halafu huyo huyo anakatwa NSSF na huyohuyo analipa kodi ya vyumba viwili (kama ameoa) kwa Tshs 50,000/= kwa mwezi, kumbuka gharama za maji kila mwezi walau 10,000/= halafu kumbuka gharama za umeme walau 25,000/= kwa mwezi, huyohuyo anasomesha mtoto, huyo huyo anauguliwa n.k; hapa unatarajia aone MAISHA BORA? Inakera sana hii!


Viongozi wa dini ni watu wa ajabu sana. Ndio walishawishi waumini wao kuwa JK ni chaguo la mungu! Hawakutaka kungalia sera wala uwezo wa mgombea.Matokeo yake wamewatumbukiza waumini wao katika umaskini wa kutisha.



Eric, mimi si kiongozi wa dini flani lakini nawatetea… Si wote! Na waliothubutu kutamka maneno haya wamedhalilisha viongozi wanzao na wote wakaonekana wanafiki wakubwa. Hukumu yao ipo na wajue ni dhambi kubwa walitenda. Mungu hajalala, na waumini nao wana makosa kwa kuziamini kila roho bila kuzipima!

Safari ni ndefu lakini… Tutafika tu!
 
Nakubaliana na hoja yako kuwa mtindo wa kila kitu kukimbilia kwa Kikwete siyo mzuri na hauna maana yoyote ila nilichogundua ni kwamba wananchi wengi wamekosa imani na viongozi wao ndiyo maana hali hiyo inajotokeza. Hebu angalia baadhi ya viongozi hawafanyi kazi ipasavyo mpaka wasikie Kikwete ama Lowassa kaongea au viongozi hao wazuru mahal fulani, je kwa hali hiyo je tutafika?
 
Mh,

Hapo mi sitii neno. Nakazana na maisha na Inshallah Mungu atajaalia nitafanikiwa ikishindikana naikimbia nchi!
 
mmmh kazi kweli kweli. Binafsi hakuna wimbo unaonitia kichefuchefu kama wa vicky kamata anathubutu kumfananisha rais na nabii suleiman LAhhh ama kweli tumekwisha. Hata tukipigwa,tuburuzwe, tufanywe watumwa badooo kuna wanaomuona ni nabii. Kweli maisha hoi kwa kila mtanzania.
 
Katch, hilo ndilo tatizo hasa na ndicho kitu kinachonisumbua. Hivi kweli viongozi wengine wako kama tv zinazoendeshwa kwa rimoti?
 
sasa Rais afanye nini, mimi naona yuko njia panda! Asipoingilia kati watu wata muona hawajali na hatimizi ahadi zake, akiingilia kati wengine watasema anaingilia kazi za watu wengine na anaweza "kususiwa". Sasa kama ungekuwa wewe ndiyo Kikwete ungefanya nini?

Mwanakijiji,
Katika mchango wangu wa kwanza kwenye mada hii,naamini nilikupatia jibu la swali unalouliza hapa kwamba "sasa Rais afanye nini."Jibu fupi,AJIUZULU KAMA AMESHINDWA.Jibu refu,APANGUE TIMU YAKE NA KUWEKA WATU WAWAJIBIKAJI AMBAO WATADILI NA ISHU ZA WANANCHI HUKO WALIKO BADALA YA KILA ISHU KUMSUBIRI RAIS.
 
huyo ni msanii, si keshamjua kuwa huyo ni mr misifa, kwa hiyo just ana.................
 
Mlalahoi, kujiuzulu is out of the question. Kupangua timu, inawezekana lakini itasaidia nini kama atakaowaweka hapo watamsubiri yeye ili wafanya kazi zao. Haiwezekani awe anapangua timu kila mwaka!! I think there should be a third option or more other options..
 
Hivi Hakuna ajira ya Uwaziri kwa mantiki ya kuomba kazi na kutizamwa sifa na kuitwa kwenye usaili na unapoonyesha uwezo ndipo unajiriwa ukitibua unaachishwa na si kwa mantiki ya kuteuliwa.
 
Mzee Moshi,

Aliyempa Muuungwana urais kwanza ni rais mwema na mtukufu wa zamani Mkapa, na baadaye sisi wananchi tukampigia kura, baada ya kuambiwa na mtukufu Mkapa kuwa anafaaa, au?
 
Mzee Moshi,

Aliyempa Muuungwana urais kwanza ni rais mwema na mtukufu wa zamani Mkapa, na baadaye sisi wananchi tukampigia kura, baada ya kuambiwa na mtukufu Mkapa kuwa anafaaa, au?


Yethu wangu! Hivi mi nilimpigia nani? Hata sikumbuki vema... I might have made the same mistake ES!
 
Mzee ES,

Aidha wewe, au mtu mwingine mwenye kufahamu mambo ya huko ndani, alituelezea kwenye hivi vijiwe vyetu kwamba Mkapa alishinikizwa na Mtandao kumpitisha JK.

Mkapa alifanya mazuri kwenye kujenga uchumi, lakini alikuwa na makosa yake mengi ya kisiasa. Moja ya makosa yake makubwa ni hili la kutuachia JK kama Rais. Ameacha mtu anayebomoa uchumi ambao yeye Mkapa aliujenga kwa uangalifu sana.

Uchumi aliojenga Mkapa kwa miaka 10 utabomolewa kikamilifu kabisa na Kikwete katika kipindi cha miaka 3 tu. JK akitawala miaka 10, atatuachia uchumi mbaya kuliko hata ule uliokuwepo wakati Mkapa anaingia madarakani.

Augustine Moshi
 
Naam mwalimu wangu,

I like the way you recall the past. Aidha nakuunga mkono kuwa kama JK hajaangalia mapema ni wazi kuwa ndani ya miaka 3 anaweza kutu-Mwinyi ghafla na ikawa si kama matarajio ya wengi.

Ama kweli matumizi ya serikali ya JK inahitaji kuangaliwa kwa mapana zaidi. Tena sio na wa-Norway bali watanzania wenyewe maana hii ni nji yao ati.

Oh yes, we need to keep the bell ringing hadi muungwana asikie hizo kengele
 
JK akitawala miaka 10, atatuachia uchumi mbaya kuliko hata ule uliokuwepo wakati Mkapa anaingia madarakani.

I agree with you Deni la taifa limeongezeka kwa asilimia zaidi ya 10 {10% more} na hii ni within a year. Kwa hiyo kama akikaa miaka 10 deni litakuwa more than 100% {zaidi ya mara mbili}.

Alipoingia alianza na ngonjera za ajira kwa WTZ lakini hadi sasa hajaliongelea hilo. Je, ni wafanyakazi wangapi wageni wameingizwa tangu JK achukue madaraka? Je, kazi wanazofanya haziwezi kufanywa na WTZ? Uhamiaji wanaweza kuweka data hapa.
 
Eh we mzee Dua,

Hilo limepigiwa kelele sana na wananchi lakini wamepuuzwa kuwa hawa ni wawekezaji. Nashangaa kwanini kusiwe na limitations za uwekezaji.

JK mwenyewe amewahi kugusia kuwa si kweli tena hakuongea kwa mapana. Lakini ukiangalia viwandani na kwenye kampuni zinazokuja Tz na wawekezaji wetu uchwara ni kuwa wanakuja nyakati nyingine na walinzi.

Ah, I love this!
 
Halafu kuna suala la kuuza vitu kwa dollar ndani ya nchi hii ambapo wanaoviuza wanafanya watanzania waamini dollar ndo hela na si shilingi ya kitanzania.

Kulikuwa na udhibiti juu ya hili lakini kwa sasa naona wamefumbiwa macho.

Yani kipindi hiki cha JK ndo wenye kutaka kufanya mambo yao wanafanya watakavyo. Kama wabunge wanatoa maoni juu ya EAF na wanaambiwa ni mawazo yao na si ya wananchi sasa unadhani nani atambadili JK kama hata maoni ya wawakilishi wetu anaona pumba tu?

Yani EL anaogopewa sana na si JK; implication yake nini?
 
The crucial role of leadership

Leadership with proper vision and decisive action is the most important driver of organizational change. This is true for any organization, from the micro level such as a firm or a committee, to the macro level such as a country or even the global community. Although some changes are realized through popular pressure or effort by middle-ranking technocrats, bold policy shifts or administrative reforms are usually accomplished under strong leadership.

We are particularly interested in the quality of the top leader of the state such as the president or the prime minister. In addition, effective leadership is desirable at any level, including ministers, committee chairs, department heads, etc. These leaders determine the effectiveness of organizations under their supervision.

There are many "strong" national leaders in the world, but only a few of them succeed in promoting development. This is because strong power is only a necessary, but not sufficient, condition for effective leadership. Good leaders are not just strong.

First and foremost, the personal character and ability of the top leader is crucial. A strong national leader must at the same time be economically literate. He or she must have the keen sense of what works and what does not in accelerating development. PhD in economics is not needed, but instinct to select right policies and good people is essential. When that instinct is combined with strong determination and quick action, development begins. In contrast, a strong leader who is economically illiterate only causes stagnation and confusion.

Second, a political regime that enables a leader to execute necessary policies and reforms is needed. However, this requirement is secondary, since a truly strong, economically literate leader can build such a regime if it does not already exist. In this sense, leadership is primary, since it can change all other conditions and relations, including the political regime

Kikwete anaweza kama atapanga timu yake vizuri bila kujali ushikaji ni rahisi hata kuwawajibisha wasiotimiza wajibu wao.
 
Tatizo kubwa unaloongelea la Rais kujiingiza kwenye petty problems za wananchi ni la kihistoria hapo kwetu. Linatokana zaidi na rais kuwabembeleza wasaidizi wake, na hivyo kuishndwa kushinikiza wafanye kazi alizowapa.

(1) Rais Nyerere alikuwa na tume ya kudumu ya rais iliyokuwa ikiongozwa na Chifu Erasto Mang'enya. Mojawapoa ya majukumu ya tume hii ilikuwa ni pamoja na kusikiliza shida mbalimbali za wananchi ambazo zilikuwa zimechukua muda mrefu kutatuliwa na serikali. Tume hii ilikuwa ni nzuri sana ila wakati huo wanachi wengi hawakuwa na shida nyingi zilizohitaji attantion ya serikali kuu kwa vile ndiyo taifa lilikuwa linaanza tu. Sielewei ile tume ya kudumu ya Rais ilishia wapi.

(2) Rais Mwinyi alikuja na utaratibu wa kuwasikiliza wananchi wa kawaida mara moja kwa mwezi pale ofisi za CCM Lumumba. Ilikuwa ni kichekesho sana kwa vile Tanzania wakati huo ilikuwa na raia wapatao milioni 32 ambao sidhani kama mikutano yake pale Lumbumbwa kwa miaka yote kumi ya utawala wake ilimwezeasha kusikiliza matatizo ya watu hata kama asilimia moja tu. Mwinyi pia alikuwa na bahati mbaya ya kuwa cornered na wasaidizi wake ili afute kodi au kutoa misamaha kwa watu mbalimbali hata ile ambayo ilikuwa ni kinyume na maadili ya kazi yake.

(3) Kwa bahati mabaya sina rekodi nzuri kuonyesha jinsi utawala wa Mkapa ulivyoshughulikia petty problems za wananchi. Najua kuwa huyu jamaa alikuwa ni kichwa ngumu ambaye inawezekana hakuwa na utaratibu wa aina hiyo kabisa. Kwanza hakuwa na rekodi nzuri ya kupendwa raia wa nchi; kumbuka kuwa mwaka 1995 nadhani alipta kama asilimia 60 hadi 65 tu.

(4) Kikwete amejikuta kwenye mlolongo ule wa mtu wa watu wa asilimia 80; anataka aonyeshe kusikilza shida za wanachi. Tatizo lake linaweza kuwa kama la Mwinyi. Atajikuta anaitwa kwenye kusuruhisha migogoro ya kindoa ya raia wake kwa vile hajaweka mpaka kati ya ofisi ya Rais na mambo ya kawaida ya raia wa nchi. Kitendo cha yeye kutembelea wagonjwa na kukifanya kuwa ni sehemu ya kazi za Rais ni kudhalilisha ofisi yake na ndicho kinachosababisha watu wadhani kuwa anaweza kufanya kila kitu. Nimesikia kuwa serikali yake imeanza tena misamaha ya kodi kama nilivyowahi kuonyesha wasiwasi pale yule kiongozi wa Bakwata aliposema kuwa ataomba kwa Rais wajenzi wa ule msikiti wa Qadaffi wasamehewe kodi; ni kama ilivyokuwa wakati wa Rais Mwinyi.


-------------------------To be continued.
 
2007-04-24 10:13:05
By Juma Thomas, Dodoma
Inflation has reached 7.3 per cent by February this year compared to 6.8 per cent in June, last year, the Minister for Finance Zakia Meghji said yesterday.

Meghji attributed the rise to increasing oil prices in the world market, famine and prolonged power woes that the country experienced last year, as some of the factors that triggered the escalation.

�The GDP was projected to grow to 5.9 per cent in 2006 and 7.3 per cent in 2007, while inflation was estimated to stand at 4 per cent by July 2007,� the minister said.

Presenting a report on implementation of the 2006/2007 budget to MPs at a meeting held here yesterday, Meghji said despite the existence of such problems, the first half of the financial year had seen implementation of the budget going well.

The minister said it was projected that revenue collection should be 14.5 per cent of the GDP in 2006/07 and 14.7 per cent in 2007/08.

Meghji said although indicators in the first four months of the budget showed improvement, increase of oil prices in the world market, famine and power problems that faced the country last year had frustrated the projection.

GDP in 2006 grew at 5.8 per cent compared to 6.8 per cent in 2005.

She said during the 2006/2007 financial year, the government planned to collect 4.850 trillion/- from internal and external sources, for development and recurrent expenditure.

The minister said expenditure in the first half of 2006/07 had reached 2.1 trillion/-, which was 61.5 per cent of the budget.

Out of the money, 1.8trillion is for recurrent expenditure, while 906.519 billion is for development expenditure.

She said revenue collection as of March had reached 259.9bn/- per month, being above the targeted amount.

The minister said it was projected that revenue collection would hit 2.5 trillion/- or above by June this year.

She said loans and grants for general budget support were also projected to meet the target as almost 90 per cent of the money had already been released.
 
Back
Top Bottom