The Khoisan
Platinum Member
- Jun 5, 2007
- 18,258
- 17,454
Si mlitaka baby face!! Mlifikiri rais lazima awe mzuri?? Cheyo aliposema watu mkamponda leo baada ya mwaka mnajionea wenyewe uwezo wa mteule wetu. Je 2015 sijui itakuwaje??
Tusidanganyane hapa. Yebo Yebo kaeleza. Kinacho-determine taaluma siku hizi ni markatability. I can assure you, kama mtu angemaliza udaktari wake Muhi2..akaanza na mshahara wa Million 1.5/2 or so, au mwenye Bsc, ENG. NK anakuwa na mshahara wa kuishi na sio wa kulipa bill tuu.. na anayemaliza na Bcom akiingia BOT na TRA analipwa laki nne na nusu...Trust me..watu wangekesha wanasoma science. Hata mimi ningesoma science!..
Hivi jiulize mtu aliyesoma Bsc educ in Physics and Chemistry..anaishije katika Tanzania, kama sio mla rushwa? zaidi ya kuwa mwalimu wa sekondari? sasa utamwambia mtu akasome hiyo fani kweli..especially kama ni mtoto wako wakati unaona yanayowasibu waliosoma hayo masomo?
What happens siku hizi mtoto wa darasa la saba au o level wanaona the whole picture..kipato cha wazazi, kazi zao...kama baba ni hakimu na mambo yake ni super..I tell you utataka kuwa hakimu..kama baba/mama ni nesi, mwalimu..hali mbaya...utajitahidi kuavoid hizo fani. Si kama zamani..watu walikuwa wanasoma bila "mentorship" watoto wa siku hizi wanaambiwa na wazazi/walezi what to do wakiwa bado wadogo.
Ulimwengu wa leo, especially Tanzania, whether utaamua kuwa mwanasheria, daktari, muhandisi au vinginevyo..ni maslahi na wala si uzalendo. Kila mtu siku hizi anaingia siasa, why? ni kwamba wanapenda "kutumikia wananchi"? NOPE..ni maslahi..hiyo ya uzalendo ni secondary wishes.
Mzee Yebo Yebo,
Ukweli ni kwamba bila kuwa na mfumo mzuri wa kiuongozi katika nchi mengi yakiwemo elimu, uchumi nk hayawezi kwenda sawasawa.
Nakubaliana nawe kwamba hatuna zana bora za kufundishia kama maabara na uchumi wa soko una madhara makubwa kwa nchi zetu.
Mtazamo wangu ni kuwa tuna matatizo katika msingi (wananchi) na katika usimamizi (serikali).
Ninaweza kumuelewa mwanafunzi wa kidato cha sita aliyesoma PCB, PCM, nk kuamua kusoma Bcom au mhandisi aliyeamua kusoma MBA kwasababu mtazamo unakuwa wa soko la ajira.
Lakini inaniwia vigumu kumuelewa mwanafunzi wa O level asiyetaka kusoma hesabu. Matokeo ya somo la hesabu kwa waliofanya mtihani kidato nne mwaka jana ni aibu, 77% wamepata F. Kwa mwendo huu tunajenga Taifa la watu wa aina gani!
Ni katika hali kama hiyo ndio maana mwaka jana kuna wanafunzi wamechaguliwa A level kusoma HGE wakati wana F za hesabu kitu ambacho si utaratibu wa kawaida.
Kituko kimoja kinachotokea hapa nchini ni kuwa eti vijana waliosoma mfano HKL kidato cha sita (wengine wakiwa na F za hesabu O level) wanachaguliwa kusoma Accounting katika kiwango cha Advanced Diploma. Sijui tunatengeneza wahasibu wa aina gani.
Ni hapo ndio nakubaliana nawe kwamba kuna tatizo kwenye serikali yetu ila tusisahahau na ya sisi wananchi!
Tunahitaji msukumo toka serikalini na support (na juhudi) kutoka kwa wananchi. Wenzetu India walianza hivyo na kufanikiwa. Tunaweza tukiamua!
Mimi binafsi nilipokuwa olevel nikuwa napendasana masomo ya sayansi maana ilionekana kuwa ndio "vichwa" na wale vilaza walikuwa wanakwenda arts na biashara.Kwa hiyo form 2 nikaacha kabisa masomo ya biashara na kukimbilia kwa akina newton.
Nakumbuka siku moja ndugu yangu mmoja aliniuliza nachukua masomo gani nilimwambia PCM! jamaa alinicheka sana akanambia kama unataka uwe maskini basi soma masomo hayo,akaniambia utakuwa fundi bomba kijijini kwako kama huyu mzee.....(akamtaja fundi mmoja pale mtaani alivyokuwa na hali sii nzuri kimaisha na aliekata tamaa ya maisha)Niliachana nao nikachukua EGM.Ya waliowakuta wenzangu "wanasayansi" yanatia huruma sana.
Masomo ya sayansi hayana maslahi kwa nyumbani kuna jamaa mwingine namfahamu alimaliza udsm civil eng mwaka 1998 hakupata kazi mpaka mwaka 2004 alipoamua kujiunga na askari magereza,kakata tamaa.Kazi alizokuwa anapata ni party time tu na aliambiwa hajui kazi kama vijana wa dar tech.
Vijana wengi wanachanngamkia kozi za biashara ndio zinalipa,kama ukiwa na bahati ukaipata CPA(maana ni kama bahati kuipata) basi umeula au Proff nyingine kama ACCA na CA.
Mhe. Yebo Yebo hiyo 77% ya F za hesabu mwaka jana ni kwa nchi nzima kaka! Na hiyo 23% iliyobaki ndio vijana wamegawana A, B, C na D. Kama ulivyosema ni HATARI!!
Nchi zingine Waziri wa Elimu anajiuzulu kwa hili. Sijui ilikuwaje habari hizi zikanipita lakini 77% kupata F Hesabu tena O Level jamani kulikoni...!!!
- Ni mitihani migumu?
- Walimu hakuna?
- Walimu Wabovu?
- Silabasi ni mbovu?
Au maana yake nini, hawa wanafunzi kwanza walifikaje hiyo Form 4 kama hata wenye uwezo wa kupata A-D ni 23% peke yake?
Ina maana hakuna mitihani ya majaribio kabla ya kuvuka darasa au hiyo mitihani haina kiwango sawa na mtihani wa Taifa? Nina maswali mengi bila majibu...mwenye taarifa tafdhalini nielewesheni hapa.
Kutokana na hoja mbalimbali zilizotolewa hapa huoni kwamba kama hesabu haitaathiri maisha bora hapo baadae, ya nini kujihangaisha nayo. Tena imeshasemwa kwamba wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wanawashauri vijana kuachana na baadi ya masomo ili walenge kwenye yale yatakayowaletea maisha bora (rushwa ikiwemo) haraka sana.
Hivi hawa wanaomuandikia hizi hotuba huwa wanafikiria? Mimi naona kuna kaukilaza ka aina fulani. Analalamikia wanafunzi wachache kuchukua masomo ya Sayansi wakati tuna wanafunzi karibu 20 wanaotaka kusomea udaktari, uhandisi kule Ukraine ambao serikali yake mwenyewe inataka kuwatumia tiketi warudi nyumbani? Mbona maneno hayaendani na vitendo? Mimi nimeanza kupatwa kidhungudhungu.
asante