mjadala huu ni mrefu ni mtamu na wachangiaji nwameeleza vizuri,kama kiongozi JK amekuwa na mazuri yake na amekuwa na mapungufu yake,na wakati huo huo watendaji wa kawaida wa serikali wamekuwa na mapungufu yao ambayo kwa kiwango kikubwa yameshusha maendeleo hapa nchini. wengi mnachangia lakinia aidha hampo tanzania au hampo serikalini,kwetu sie tuliopo serikali za mitaa mawilayani tunaweza kuwapa picha kamili,ila kiukweli japo kidogo JK ameleta maendeleo tusiwe that much stereotyped,mfano idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa vyuoni imeongezeka sana ingawa watu mnalalamika uhaba wa wahadhiri sijui kama mlisoma bongo,ila kwa sie tuliosoma bongo tunafahamu ni kwa namna gani wahadhiri wenyewe wamechangia kupoteza watu kwa kuifanya elimu iwe ngumu wakati kiukweli haiko hivyo,
serikali kuu inajitahidi sana kuzisaidia local goverments maana local govts ndizo mhimili mkuu wa maisha ya kila siku ya watanzania kuanzia afya,maji,elimu,barabara,kilimo ambazo ndo sekta kuu zinazomgusa mwanachi directly. lakini ni ukweli usiopingika kuwa serikali za mitaa nyingi ni dhaifu,watendaji wake wengi ndio wala rushwa wakubwa,shule hazijengwi inavyostahili,zahanati hazijengwi ipasavyo,mfamo pesa za ujenzi wa zahanati na ukarabati za mpango wa afya ya msingi MMAM,wakati mwingine zinaliwa na wajanja wachache,zabuni za barabara zinatolewa hovyo na ujenzi wa barabara wenyewe ni usanii mtupu,zikiletwa pembejeo au mbolea watendaji wa vijiji/kata au maafisa ugani hao ndio wanaoziuza badala ya kufikisha kwa wakulima,je hapo bado wa kulaumiwa ni JK au ni sisi watendaji tusio na maadili kwenye kazi yetu?watanzania ni wanafiki wakubwa hamuachi kumsifia nyerere lakini kwenye failure zake mnasema sio yeye isipokuwa watendaji ndo walimwangusha,kwa nini msiseme pia hata JK anaangushwa na sie watendaji wenyewe? wote tunafahamu kuwa TRA wamekuwa wakilea wakwepa kodi,kiasi kwamba wao wanachangia mapato ya serikali kutokuwa juu,
mimi simfagilii JK nilimpinga tangia 2005, na kura sikumpigia by then nilikuwa chuoni,leo nipo serikalini naona picha kamili ilivyo, nafahamu kabisa watendaji wa serikali ndio vikwazo kwa maendeleo ya kweli
mtasema ni jukumu la serikali kuukemea uchafu wote huo lakini serikali ni nani?watu ndio wachafu so ni jukumu letu sisi watendaji tutimize/tuplay our parts hapo ndipo maendeleo ya kweli yatapatikana