Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Wanabodi,
Kwani Hasara kafanya kitu gani ktk mada hii kiasi kwamba sio tena hoja inayotazamwa ila Hasara!...

Dr.WHO, haya ya popo bawa nayo yameingia vipi hapa badala ya sehemu za Udaku!
 
HIKI NDICHO SERIKALI YA AWAMU YA NNE INAVYOFANYA : duh wazee wanaenda kinyume na hugo chavez wa venezuela> Ndio maana nasema hawa jamaa yaani haina jinsi tena !

SERIKALI imetangaza rasmi kumnyang'anya mwekezaji wa ndani, Kampuni ya Africommerce, mradi mkubwa wa kujenga mabomba ya kusafirisha mafuta.


Pia imeionya kampuni hiyo kuacha kuitisha serikali kupitia vyombo vya habari, kwa sababu haitishwi wala kuyumbishwa na mtu yeyote katika kutekeleza azma yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.


Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana na Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Dar es Salaam.


Alisema serikali imeamua kuipa Kampuni ya Noor Oil and Industrial Technology Ltd (NOIT) mradi huo, baada ya kuridhika na mapendekezo yake ya awali ya kuwekeza kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.6 katika mradi huo.


"NOIT ina uwezo wa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta ghafi na kutandaza mabomba ya kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam hadi jijini Mwanza.


"Iwapo kiwanda hicho kitajengwa kitakuwa cha pili kwa ukubwa barani Afrika na uzalishaji wake unakadiriwa kuwa mapipa 120,000 hadi 200,000 kwa siku, kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na matumzi ya Tanzania ambayo hutumia mapipa 30,000 kwa siku," alisema Ngasongwa.


Waziri huyo aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake kutoa tamko la serikali kuhusu madai ya Kampuni ya Africommerce, ya kuipa siku 30 kutizama upya uamuzi wake wa kuinyang'anya mradi huo, vinginevyo iwe tayari kuburuzwa mahakamani.


Akizungumza kuhusu mradi huo na vitisho vya Mkurugenzi wa Africommerce, Elisante Muro, Waziri Ngasongwa alisema mradi ambao awali ilipewa kampuni hiyo, ni wa kusafirisha mafuta ghafi na kutandaza mabomba ya kusafirisha mafuta kutoka jijini Dar es Salaam hadi jijini Mwanza.


Alisema kati ya Februari 20 na 21, mwaka huu, Muro alitoa malalamiko kupitia vyombo vya habari na kutishia kuishitaki serikali kwa hatua yake ya kuipa Kampuni ya NOIT mradi huo kinyume cha makubaliano ya awali yaliyokuwa yamefikiwa kati yake na serikali.


Alivitaja vitisho hivyo kuwa, ni pamoja na kuitaka serikali iendelee kutambua kuwa mradi huo ni wa Africommerce pamoja na kuipa siku 90 ili kutazama upya uamuzi wake kabla ya kuiburuza mahakamani.


Waziri Ngasongwa alisema madai ya kampuni hiyo yanalenga kuueleza umma kuwa serikali imepora mradi huo na kwamba haiwajali wawekezaji wazalendo, inawavunja nguvu na haiwapi ushirikiano wa kuendeleza miradi yao.


"Kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu, mtu yeyote anayo haki ya kufikisha madai yake mahakamani pale atakapoona hajatendewa haki, hali kadhalika, serikali ina haki ya kujitetea pale itakapokuwa imeshtakiwa mahakamani.


"Kutokana na msingi huo wa kikatiba, kampuni ya Africommerce inayo haki ya kupeleka madai yake mahakamani ili haki itendeke," alisema Waziri Ngasongwa


Alisema Africommerce imekaa na mradi huo kwa muda wa miaka 24 bila kubainisha kuwa haina uwezo wa kifedha wa kuutekeleza na kwamba madai inayoyatoa ya kukwamishwa na serikali ni visingizio visivyo na msingi wowote.


Waziri Ngasongwa alisema serikali isingeweza kuizuia kampuni hiyo, kujenga mradi huo kama ingekamilisha taratibu za kuuendesha, ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kifedha na kitaalamu unaohitajika kwa miradi mikubwa.


"Ni dhahiri kuwa, kushindwa kwa Africommerce kutekeleza mradi huo tangu mwaka 1983, hakuwezi kutokana na njama za serikali bali ni uthibitisho wa uwezo wake mdogo," alisisitiza Waziri Ngasongwa
 
Hapa kuna topic mbili zimechanganywa: hii ya Africommerce na hilyo kuu ya kumshauri Kikwete.

(a) Nadhani kama kweli hawa jamaa wa Africommerce walipewa mradi huu na kukaa nao kwa miaka 24 bila kuutekeleza, hilo litakuwa ni tatizo kubwa sana kwa serikali kwa vile inatakiwa kampuni hii ishitakiwe na ikiwezakana walazimishwe kulipa riba itokanayo na kuichelewesha serikali kupata mapato yake yaliyotegemewa kutokana na mradi huo. Ila kama serikali wanafanya mbinu za kuwanyang'anya wazawa mikataba na kuwapa wa kuja kwa nia ya kupata masurufu mazuri ya pasenti basi serikali inatakiwa kukemewa na kumrudishia bwana Maro mradi wake.
<= Nimerekebisha makosa yangu ya kupiga keyboard. natumia kidole kimoja kwa hiyo ninapokuwa kwenye haraka huwa najikuta napiga key zaidi ya moja bila kutegemea. Samahani sana kwa usumbufu


(b) Kikwete anatakiwa afanye mambo mengi sana ili kuinusuru nchi na serikali yake binasfi, hata hivyo mimi nitamshauri matatu makubwa kama ifuatavyo:

-(i) Kwanza awe mkali kidogo kwa wateule wake hata kama walimsaidia kumpigia kampeini. Serikali itamshinda kama yeye atakuwa mr soft kwa wateule wake eti kwa vile hataki kuwaudhi kutokana na mchango wao kwenye kampeini. Kipindi cha kampeini kimekwisha sasa watu wanataka matokeo. Kama wateule wake hawawezi kumsaidia kuonyesha matokeo anatakiwa awaambie outright you are fired! Akishafanikiwa kuwabadilisha mindset wafuasi wake na kuwafanya watambue tofauti ya kipindi hiki na kile cha October 2005 atakuwa amepiga plus kubwa. Sambamba na wateule wake, anatakiwa atambue kuwa kwa vile yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi, wajibu wake mkubwa na kutoa mwelekeo wa nchi hivyo ni lazima awe na lengo la kitaifa analotakiwa kulifikia kwa mafanikio baada ya miaka mitano na afanye jitahida kubwa sana kulifikia. Asione madaraka hayo kuwa yeye ni bwana kubwa ambaye atakaa na kula maraha tu akiwachia wafuasi wake watekeleze kazi zao. Safari zake za nje zisiwe zinakuwa ndefu kisi hicho cha karibu wiki tatu.

-(ii)Atafakari Ilani aliyotumia kwenye kampeini kama alivyonukuu Mzee Mkandara hapo juu. Tatizo ni kuwa Ilani hiyo iliandikwa na watu wengine na huenda yeye aliitumia kwenye kampeini bila kujua undani wake. Sasa ndio wakati wa kuitafakari na kuitekeleza kwa vitendo na dhati. Kwa kufanya hivyo ataiepusha serikali kutokumbutia wafanya biashar uchwara wote wa nchi nchi za nje, na atakuwa nkweli anatekeleza ahadi zake za uchaguzi.


-(iii) Asiwe mtu wa kuamini kirahisi kila analoambiwa. Awe anachambua kila jambo analoambiwa kwa mapama na marefu kabla ya kulitolea maamuzi. Kwa vile kuna mtandao mkubwa sana wa habari, awe anafanya utafiti kutumia mtando huu nje ya channel zake za kiserikali ili kuweza kupata mambo kwa dimension kubwa. Hii itamsaidia sana katika maamuzi yake. Ni dhahiri kuwa mikataba ya makampuni uchwara kama Richmond asgenews kuikubali kama angekuwa amefanya utafiti kidogo kuhusu kampouni hiyo.
 
Kikwete Afanye Nini Katika Utawala Wake ili aweze kujinusuru 2010, Wana JF tumezungumza mengi sana kuhusu utawala wa Rais Jakaya M.Kikwete sasa katika yale mapungufu tuliyo yaona katika safu ya Baraza la Mawaziri ,Ma DC, Ma RC, Katibu Wakuu, na Waziri Mkuu,Wakurugenzi, Safari za Nje, Mikataba,Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Mapanki, Ahadi za Kipindi Cha Kampeni, Madarasa, Umeme, Ajira kwa vijana, Wastaafu na Wazee,Kakina Mama na Watoto, Afya, Elimu, Richmond na Rada na mengine mnisaidie,

kiongozi wetu mpendwa, kipenzi cha wengi ,changuo la mungu, kisura,mpenda watu, afanye nini kulinusuru taifa letu.

Sasa tujadili hilikwa kina ninaomba kutoa hoja......

Heshima wanaJF
Hasara kaleta changamoto nzuri ambayo wengi walikuwa wanafikiria siku wakimuona JK watamuuliza au kumpa ushauri lakini kumuona ni vigumu kwa nafasi aliyo nayo ,

mimi binafisi na nina machache ya kuongea na mkuu huyu kama ingewezekana au tupate E-mail yake hapa JF au namba ya simu basi aweze kusikia sauti zetu,

rais wetu hana makosa au ajajulishwa kwamba tumefikia wapi kivitendo atakuwa anakaratasi mengi ofisini kwake yenye vitendo au kazi ambazo hazijafanyika ili kumpamba,

serikali ya JK imepoteza muelekeo pale alipo onyesha ukali baada ya kuingia madarakani,alikujaribu kuwa karibu na wapiga kura na kujenga uwadui na wasaidizi aliyo wateuwa , sasa hii nikama mke mwenye tabia baya alafu umegundua na amejua anachokifanya sasa anakuonyesha kile ambacho unakipenda,
wasaidizi wa Kikwete wanamuonyesha kile anachotaka akijue ,akuna kitu kibaya kama mtu kujua uzaifu wako, ndiyo sababu anapo safiri wote wako AIR PORT awabanduki kumpelekea umbeya, muungwana anapenda kusikia mambo kama hayo ; siyo ripoti za kazi,

jingine 80% ya wasaidizi wake wanamjua fika, awezi ku-act kwao wanamjua ilopia ni kosa kufanya kazi na watu ambao uwezi kuwakemea, kila waziri au hasara aliye wataja hapo juu kwa vyeo anahistoria ya kuwa na JK mahali fulani na kufurai pamoja, hapo kazi itafanyika kweli,

kwa sasa hivyi wako watu 600 wanatakiwa kusaidiwa na JK wanaokiri kumusaidia kwenye kampeni wengine tukiwa wamoja wapo, je muheshimiwa hutu atayaweza na kazi itafanyika na hizo nafasi za kuwasaidia zipo?

ninafikiri JK arudinjia panda aanze safari yake upya bado
mapema sana ili asome ramani upya akizidi kwenda mbele atapotea akija kurudi nyuma ni 2010 muda umeisha anala kutuambia wanaJF na watanzania kwaujumla,

jingene
changa kabisa wasaidizi wako wamepanga kukumaliza kisiasa wewe umekuwa mkali sana sasa wanakuwachia ufanye mwenyewe wao wanaendelea kutumia pesa za walipa kodi kufanya kampeni za kisiri wanajua siri ya wewe kushinda,

haiwezekani mwanasheria mkuu kupitisha mikataba mibovu na mikitu unakikemea kila siku RUSHWA na imefanywa mbele ya macho yako mkuu swali hilo pesa za hiyo mikata ndizo zitakazo kumaliza 2010,

muheshimiwa zamira yako ilikuwa nzuri sana kipindi chote cha kampeni tunajua wewe siyo mfanya biashara lakini wasaidizi wako wote ni wafanya biashara wanajua pesa wewe umezoea kutumikia wananchi nivitu viwili haviingiliani, ndiyo sababu wana sema wewe ni mtoto wa kiswahili unavuta raha tu na familia yako,

sasa mkuu ukuona kabisa watu wana weza kuwatumikia wananchi,wenye uchungu na hii nchi, umeishi na mwalimu nyerere, mbona yeye amekufa masikini kwa mwalimu alikuwa apendipesa, angalia watoto wake akuna ayeyoko kwenye serikali yako na mama nyerere amekufuata mara kibao kukusalimia mkuu hile akuwa salam alikuwa anakukumbushia umpe atamtoto wake mmoja nafasi ili ile heshima ya baba wa taifa isipotee na jina liwepo hewani,

huyo mwingine rose marry ameamua kuotesha mboga kwenye madoo ili na wewe ulione hilo, mimi siyo msemaji wa familia ya baba wa taifa, hivi nivitu ambayo vyakuangalia,

kama rais yeyote ni mtumishi wa umma, makamu wa rais na waziri mkuu ni lazima watumikie umma 100% kama wote ni wanya biashara wote wawe ni wafanya biashara kama wamarekani kama ni mafia basi wote wawe mafia.

hapa kwetu ni zigizaga rais ajui pesa, waziri mkuu anajua pesa, makamu wa rais ajui pesa, kuna viongozi wafanya biashara kama waziri mkuu rushwa haita isha mpaka yesu arudi,

muheshimiwa ujapotea sana unaweza kurudi njia panda na ukaanza tena na utamaliza vizuri, tuko pamoja na una suport kubwa sana kwa watanzania akuna mtuwakujilinganisha na wewe lakini usibweteke na hili,kuna ahadi ujakamilisha lakini tuna kupa muda wasaidizi wako wanatutia kichefu chefu sana haswa waziri mkuu na vitabia tabia vyake alivyo anzisha, japo kuwa kazi anafanya mwambie awache kabisa, msafishe la richmond na rada kwanza.
ili uwe safi,
 
Afanye aliyoaidi kuyafanya. Yaani atende aliyoyasema. Tatizo lake anafanya asiyoyasema na anayoyasema hafany!
 
Kikwete Afanye Nini Katika Utawala Wake ili aweze kujinusuru 2010, Wana JF tumezungumza mengi sana kuhusu utawala wa Rais Jakaya M.Kikwete sasa katika yale mapungufu tuliyo yaona katika safu ya Baraza la Mawaziri ,Ma DC, Ma RC, Katibu Wakuu, na Waziri Mkuu,Wakurugenzi, Safari za Nje, Mikataba,Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Mapanki, Ahadi za Kipindi Cha Kampeni, Madarasa, Umeme, Ajira kwa vijana, Wastaafu na Wazee,Kakina Mama na Watoto, Afya, Elimu, Richmond na Rada na mengine mnisaidie,

kiongozi wetu mpendwa, kipenzi cha wengi ,changuo la mungu, kisura,mpenda watu, afanye nini kulinusuru taifa letu.

Sasa tujadili hilikwa kina ninaomba kutoa hoja......

kwanza maliza kutoa hoja huku
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1704
 
Dr. Who.....mwanangu Hali Yako?

Nafikrii Unaendelea Vizuri.hofu Ilikuwa Katika Afya Yangu Lakini Mungu Amenijalia Uzima Namshukuru Sana Yeye Mungu Wa Babu Yangu Majebele 1.

Swali Lako Ni Zuri Hasa Ukiangalia Mambo Aliyonayo Huyu Mwanangu Jakaya.kwa Kweli Ninachoweza Sema Ni Kwamba Mitihani Ni Mingi Sana Na Hata Mambo Ya Kufanya Pia Ni Mengi Sana. Mie Nimekuwa Naangalia Nini Hasa Anachoweza Fanya, Kizuri Ni Kwamba Amewahi Kuja Mwanza Nikamwambia Nini Zuri La Kufanya.

Kwa Maneno Yangu Nafikri Jakaya Anaweza Kubaliana Nami. Nimeshawahi Kumkumbusha Kwamba Nchi Hii Ni Huru Na Kwamba Ina Watu Ambao Kwa Dhana Yao Wanajua Wako Huru Na Wanaipenda Sana. Wangependa Kuona Mambo Mazuri.

Mambo Anayofanya Kwa Sasa Ni Mazuri Sana Ninavyoyaaona Na Kwa Kweli Ni Mambo Ambayo Alituahidi Kwenye Uchaguzi Angetufanyia.kikwete Anatembea Nchi Za Akiomba Wahisani Na Marafiki Wetu Wa Karibu Waweze Tusaidia. Angalia Amekwenda Marekani, Norway Na Hata Uingereza. Matunda Yake Yameonekana. Tatizo Kubwa Watu Wengi Wanaangalia Mapungufu Na Kuyajengea Hoja. Hebu Tupate Muda Na Kufanya Mchanganuo Wa Yake Mazuri Anayo Yapata.

Labda Nitumie Muda Kuwakumbusha Machache. Kupunguza Tatizo Lililopo Sasa Katika Vyuo Vya Elimu Ya Juu , Mwanangu Huyu Anafanya Mipango Ya Kujenga Chuo Kikuu Pale Chamwino Dodoma. Na Hili Linafanyika Sambamba Kabisa Na Aliyeondoka Madarakani , Bwana Mkapa.na Pia Hivi Karibuni Amesema Wataanza Fanya Mjadala Wa Kuangalia Mfumo Wetu Wa Elimu.

Suala La Usafiri Wetu Kama Mlivyowahi Sikia,barabara Nyingi Zipo Kwenye Michakato Ya Mwisho Zikifanyiwa Niite Analysis Ili Ziweze Fanyiwa Kazi. Barabara Toka Dodoma Singida, Lindi Hadi Dar Es Salaam, Na Hata Pia Barabara Ya Kutoka Tabira Kwenbda Kigoma Na Nyengine Nyingi. Sio Hilo Tu Bali Pia Serikali Ya Ubelgiji Wameahidi Kutusaidia Reli Ya Umeme. Mnajameni, Mambo Haya Naomba Uzima Mwana Masanja.usafiri Wa Ndege Nao Unakwenda Vizuri Baada Ya Kubadilisha Board Ya Wakurugenzi Wa Atc. Haya Ni Machache Lakini Mengi Sana Anayafanya.

Kwa Kumaliza Na Kuondoa Kukuchosheni Kwa Kusoma Mazuri Haya Napenda Kusema. Kikwete Ni Mtoto Makini Ambaye Nafikiri Anahitaji Muda Aweze Fanya Mambo Ya Kweli. Tusiangalie Mapungufu Yaliyopo Na Kujaji Nini Akifanye. Yeye Aliahidi Pale Uwanja Wa Taifa Klwamba Atatimiza Yote Ambayo Watanzania Wanahitaji Kwa Lolote Lile Hata Kama Ikiwezekana Kuacha Kupata Usingizi. Kwa Maoni Yangu Kazi Anahifanya Na Hata Sisi Tunaona.naamini ,kwa Sasa Anahangahika Kwa Ajili Yetu Naamini. Ninachoweza Sema Ni Kwamba Bado Mapema Sana,ni Mwaka Mmoja Na Nusu Toka Achukue Madaraka.nafikiri Tusubiri Muda.

Nahene Getegete.......kwa Kiswahili Aksanteni Sana

Mimi Chief Masanja Wa Majebele
 
Pamoja na uozo wote huu majebele yeye anaona JK anajenga Nchi ama kweli chifu wa porini una shida sana .
 
Kichuguu,
Huyu waziri MUONGO sana, miaka 24 iliyopita tulikuwa bado WAJAMAA haiwezekani kuwa Nyerere aliwapa watu binafsi mradi mkubwa kama huo wa mafuta wakati tulikuwa na TIPPER!
 
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapaswa ajue - kati ya mengi ambayo waliotangulia wameyasema na watakaofuata watasema pia, kwamba nuru yake iliyokuwa inang'ara kabla ya 2005 October iliisha fifia na sasa inakaribia kuzimika kabisa.

Ili arudishe imani kwetu inabidi:

a). Abadili staili anavyokabili matatizo (hata majanga) yanayolikumba taifa. Mfano janga lililotukumba la umeme (mimi nililiona janga), alilichukulia kimzaha mno hadi taifa limeingia hasara kubwa itakayo zidi kudidimisha hali ya maisha ya Mtanzania wa kawaida. Tatizo likijitokeza na kama ni makosa ya utendaji ni SHART AWAWAJIBISHE NA KUCHUKUA HATUA ZA KINIDHAMU DHIDI YAO DAWA SI KUBADILISHA NYADHIFA ZAO!

b). Awakemee watendaji wake wakuu ambao wanajiona miungu watu.

c). Ni wakati mwafaka kuthamini mawazo na maelekezo ya wataalamu wazalendo. Ni ujinga kuwaona wageni ndio wanaweza. NET GROUP SOLUTION imetuachia nini TANESCO?

d). Aiangalie Ikulu kwa Uikulu wake. Anajishusha mno hadhi hapa nyumbani na ugenini kwa kufanya ama kuhhdhuria mambo ambayo wangeweza watendaji wake! Rais gani kila msiba anakwenda?

e) Atafakari: KASI MPYA, ARI MPYA NA NGUVU MPYA KWA TANZANIA YENYE NEEMA KILA JAMBO LINAWEZEKANA Kilichowezekana hapa ni watenndaji wake wakuu kuingia mikataba ya ajabu ajabu, wizi kila wizara hadi majuzi ofisi ya Waziri Mkuu ina skendo ya Lexus mbili kwa US$ 400,000
 
Kichuguu,
Huyu waziri MUONGO sana, miaka 24 iliyopita tulikuwa bado WAJAMAA haiwezekani kuwa Nyerere aliwapa watu binafsi mradi mkubwa kama huo wa mafuta wakati tulikuwa na TIPPER!

Mkandara na wanabodi wengine,

Samahani sana kwa makosa yangu ya kutaipu, ile post yangu ya kwanza ilikuwa na makosa mengi sana hadi nilipoiona tena leo asubuhi hii.

Inawezekana kweli kulikuwa na nia ya kuwapa mradi huo wakati huo kwa vile kati ya mwaka 1980 hadi 1984 hivi Tanzania pale kulikuwa na miradi mingi sana ya ujenzi wa barabara, viwanda na mabwawa. Kiwanda cha bia cha Mwanza kilianza kujengwa katika kipindi hicho, na miradi mingi ya viwanda pale Morogoro ilijengwa kipindi hicho. Kumbuka barabara ya morogoro Dodoma na ile ya Mwanza Musoma zote zilijengwa kipindi hicho, kwa hiyo pamoja na uchumi mgumu wakati huo, serikali ilikuwa inatoa contract za infrastructure.

Kitu nashindwa kukubaliana na waziri ni kuwa isingewezekana mradi huu uwepo kwa miaka yote hiyo bila kujulikana na wakaguzi hasa wale wa World Bank na IMF. Inawezekana kuwa kulikuwa na plani ya kumpa mradi huo wakati huo lakini hakupewa ingawa dokument za kuonyesha nia ya kumpa zilibaki. Kwa hiyo waziri anataka kutumia zile dokument za zamani ili kuhalalisha kumnyang'anya mradi huyu bwana Maro; nadhani ugonvi unaweza kuwa uko kwenye pasenti
 
Kichuguu,

Hivyo viwanda vya miradi ya kitaifa ulivyovitaja vilivyojengwa vilikuwa vikimilikiwa na watu binafsi?

Vita kubwa hapa sio ujenzi wa mradi mzima ila contract inavyosema ni:- Kusafirisha mafuta ghafi na kutandaza mabomba ya kusafirisha mafuta kutoka jijini Dar es Salaam hadi jijini Mwanza.
 
Kichuguu,

Hivyo viwanda vya miradi ya kitaifa ulivyovitaja vilivyojengwa vilikuwa vikimilikiwa na watu binafsi?

Vita kubwa hapa sio ujenzi wa mradi mzima ila contract inavyosema ni:- Kusafirisha mafuta ghafi na kutandaza mabomba ya kusafirisha mafuta kutoka jijini Dar es Salaam hadi jijini Mwanza.

Hapo nimekupata, na hiyo si kweli. Mwanzoni nilidhani kuwa Maro alikuwa mkandarasi wa kujenga bomba hilo kwa ajili ya serikali.
 
kwa mawazo ya masanja wa majebele kweli tutarudi zama za mawe. mwenzetu anaona reli za umeme zaja, air tanzania imerekebika usafiri wa anga unaenda vizuri, vyuo vikuu vinaongezeka laaah mpaka naumwa kichwa.
 
Habari Ndugu Wanaforum,

Leo nimesoma hii habari kutoka katika gazeti 'letu' la Uhuru, inasema CUF wanaimani na kweli, kwasababu ya mpasuko wa Kisiasa huko Zanzibar, Lakini naona kama si kweli!! au wewe unasemaje??? Soma Hapo Chini

CUF: Tuna imani na Kikwete

lipumba_80x120.gif

Ndugu Ibrahim Lipumba.​

<-> Ni kuhusu mazungumzo kuondoa mpasuko Z’bar

Kutoka gazeti 'letu' la Uhuru,
NA Gabriel John


MWENYEKITI wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa jitihada anazofanya kuhakikisha mpasuko wa kisiasa Zanzibar unapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Dar es Salaam wakati wa majumuisho ya mkutano wa baraza kuu la uongozi la CUF, uliofanyika kwa siku mbili, makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini.

Lipumba alisema kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa kwa mara ya kwanza bungeni, mjini Dodoma, Desemba 30, 2005 iliwapa moyo na kuamua kukaa pamoja na Chama Cha Mapinduzi kujadili hali ya mpasuko wa kisiasa Visiwani.

Alisema CUF inawakilishwa katika mazungumzo na viongozi wake wanaotoa ushirikiano wa hali ya juu, ili kuhakikisha kwamba mazungumzo hayo yanafanikiwa kwa manufaa ya taifa.

Kwa mujibu wa Lipumba, CUF imepokea kwa moyo mkunjufu na “kubariki taarifa zilizowasilishwa kwake kuhusu mwenendo wa mazungumzo hayo”.
 
Itabidi tuamini yale waliyoyasema kuliko yale ambayo hawajayasema maana hatuyajui ambayo hawajasema!
 
Mwanasiasa,

Unajua ndugu yangu Demokrasia ni utamaduni mgeni sana kwetu na hata siku moja hauwezi kusimama kwa sababu ya kijimila kimoja kiitwacho SIRI.
Leo hii na matangazo yote ya Kipumba hakuna hata mwananchi mmoja Zanzibar anayefahamu kinachoendelea.
UWAZI ni neno lilobaki katika kamusi.. I hope yanayozungumzwa ni kwa faida ya wananchi wote wa Bara na Visiwani sio maelewano kati ya CCM na CUF.
 
Itabidi tuamini yale waliyoyasema kuliko yale ambayo hawajayasema maana hatuyajui ambayo hawajasema!

Ambayo hayakusemwa inawezekana ndiyo ya maana zaidi. Kulikuwa na fununu kuwa JK alikuwa akisukumiza Zanzibar waunde serikali ya mseto kama alivyokuwa amependekeza Mwalimu. Nadhani sasa hivi wanaelekea huko.

Tusubiri tuone mwisho wake nini.

Yetu macho (Our eyes!)
 
Back
Top Bottom