Tutakuwa humu kwa muda mrefu!

Tutakuwa humu kwa muda mrefu!

tubalayya

Senior Member
Joined
Apr 16, 2010
Posts
110
Reaction score
174
Tutakuwa humu kwa muda mrefu!

Kuna wale wadhaniao kuwa hali tuliyonayo Watanzania ya kunyimwa uhuru wa kisiasa, kutishwa na kutishiwa, kutokuwa na uamuzi wowote juu ya serikali yetu, watu wachache kufaidi kupindukia, mtu kutokuwa na uhakika wa usalama wake.....yote haya yalianza vuuu tu, au mtawala mmoja au wawili ndiyo waliosababisha. La hasha!

Kila kitu au hali hapa Duniani huzaliwa, hukuwa na hatimaye hufa. Wale wanaofuatilia Dunia kwa karibu watalithibitisha hilo. Hali yetu ya kubanwa kwa uhuru na usalama, pia ilizaliwa, ikakuwa na labda SASA iko umri wa kijana au mzee! Acha niamini ni uzee.

Na, ili kuzaliwa, kukuwa, kuzeeka...kuna wanaohusika, wakiwemo wananchi wenyewe. Tulia! Sisi Watanzania tumechangia kuinyonyesha na kuilea hali hii. Simlaumu mtu, ila nazungumzia hali halisi ya jamii. Ndiyo, kulikuwa na majaribio ya hapa na pale dhidi yake, kama jaribio la jeshi 1964, Jaribio la akina Titi (kama ni kweli), Jaribio la kina Yasin Member... Ila yote haya hayakuwa ya wananchi wengi, hivyo hayakuwasumbua watawala.

Hali hii ilianza mwaka 1967 na Azimio la Arusha. Kwa nini nasema hivyo? Tazama nchi zooote zilizoingia tajriba ya Ukomunisti, au Usoshalisti (Ujamaa, Ishtirakiya), utaona msingi wa kufanikiwa mfumo huo ni utumiaji mabavu-violence. Tanzania tulikuwa na bahati kidogo vile aliyetuletea mfumo huo, Mwalimu, alikuwa ni mumini wa DINI hivyo akaweza kuduwaza kidogo mabavu hayo.

Lakini angalia Urusi kwenyewe: watu milioni 48 walipoteza maisha! China, zaidi ya milioni 150, Albania milioni 20, Ethiopia zaidi ya milioni 10, Somalia, Yemen, Misri, Iraq, Vietnam, Cambodia, Laos....kote huko stori ni hiyo hiyo! Naweza kusema ni Tanzania na Cuba pekee ndizo zilizopona na mauaji ya kutishwa. Tanzania kwa vile mwalimu alikuwa na dini, na Cuba kwa vile iko jirani ya Marekani, isingevumiliwa.

Na hii inaendana na mantiki: Ukomunisti kwa kweli unakwenda kinyume na hulka ya binadamu, hata kama Wana maneno ya asali. Hulka ya binadamu ya kawaida ni kuwa apambane maishani ale na wanawe. Wote sisi tuko tofauti katika ari, uchapa kazi, akili na hata talents tulizopewa. Haiwezekani wote tukadiriwe kipato kimoja. Hii haihalalishi ubepari hata kidogo. Ubepari ni wizi na kutwaa vya mwengine kwa ulaghai na ujanja nahatimaye kutwaa vyote- Ukoloni. Ila Wakomunisti wameturubuni kwa kusema juhudi za mtu binafsi pia ni ubepari na kwamba sawa ni wote tuwe maskini!

Turudi kwenye maudhui. Kwa hiyo utaona mtawala lazima atumie nguvu fulani ili mfumo huo utiiwe. Na ndivyo ilivyotoea Tanzania. Na ukisha 'introduce' utumiaji nguvu katika jamii, ndiyo basi.
Tanzania imekuwa nchi ya matumizi ya nguvu na kudharau rai ya mtu tangu 1967. Walio wakubwa Kati yenu mtakumbuka enzi za kura ya NDIYO na HAPANA. Ndiyo, yawekwa picha ya 'Mwalimu" na HAPANA kwawekwa punda, au jembe, walipochoka wakawa hawaweki kitu kabisaa-. Watu wakafasiri kuwa NDIYO ni mwalimu, HAPANA: yaani Hapana mwengine ila yeye!
Ama vitisho, nakumbuka mwaka 73 nami mdogo, nilithubutu kupinga kwa sauti hatua fulani ya serikali...nyanyaangu akaingiwa hofu kubwa akasema ;' Haa mwana wee, utakuja uchukuliwe tusikuone tenaa' Kauli hiyo imenikaa hadi leo!

Nasimamisha hoja kwamba hali tuliyonayo hivi sasa ni mwendelezo wa hali ile ile hadi kufika Magufuli. Hapo tayari matumizi ya nguvu yakawa yamezoeleka, tukaingia kwenye awamu ya mtoto kula ugali.

Marais wote Tanzania wameua, hata wale ambao hawakupenda, kama Mwinyi.
TWACHOMOKAJE?
Tazama hizo nchi nilizozitaja zilichomokaje?
Yatisha, lakini ndiyo ukweli!
 
Mfumo wa Ushoshalisti kwa Africa hauna manufaa japo viongozi wengi wanaongoza wanatoka kwenye familia duni hivo akiwa kiongozi haangalii maendeleo ya nchi anaangalia ugali wake, madaraka yake.
Viongozi wengi wa Afrika wana trauma za toka utotoni huko.
Lkn movement hizi Afrika haitakiwi kutawaliwa kimabavu sana kwa sababu muda huo ulishaisha enzi za 1960 huko.
 
Back
Top Bottom