Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

hapana naona Mr. Clean amepitiwa tu hapo... Rais asipokuwapo Tanzania, Makamu ndiye anaye Kaimu, na kama naye hayupo basi Waziri Mkuu ndiye anakaimu. Hivyo kwa vile Rais alikuwa nje ya nchi (siyo nje ya Dar) basi Makamu wa Rais ndiye aliyekaimu kiti hicho.
 
MKJJ,
Mapendekezo mazito hayo na yanahitaji tafakuri. Kadri ninavyofikiria naona TUNAHITAJI KATIBA MPYA!

Nadhani wizara nyingi (kama si kila wizara) zina wanasheria/kitengo chake cha sheria. Kwa kiasi gani wamekuwa wa msaada ni suala la kujadiliwa. Kama wapo, wanakwazwa na mfumo? Mathalani, kwenye RDC/Dowans, wanasheria wa wizara walihusika vipi? Au suala zima la kisheria waliachiwa ofisi ya AG peke yao? TANESCO nao waliangalia masuala ya kisheria kadri wanavyohusika?

Kwamba kuwe na Mwanasheria Mkuu wa Ikulu, una maana Mwanasheria Mkuu wa Ofisi ya Rais (kwa ajili ya ofisi zote zilizo chini ya Ofisi ya Rais-kwa sasa Menejimenti ya Utumishi w Umma, Usalama, Utawala Bora nk?)

BTW, sijawahi kusikia mshauri wa rais kwenye masuala ya sheria! Huwa nasikia waandishi na wapiga picha, washauri wa uchumi na siku hizi uhusiano wa jamii!

Kwa mwendo (mdundo!) huu labda tuweke utaratibu kuwa rais LAZIMA afundishwe sheria (kama hatakuwa Mwanasheria wakati anachaguliwa) na kupewa cheti (Certificate in Law ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) ndani ya miezi sita katika madaraka yake!
 
Wana JF, tuendelee kupiga kelele hapa,kumbe wanasikia tena kwa kasi ile ile waliyoianzisha. Mimi sijali chama, najali maendeleo.

Na pia natoa ari kuwa wana JF tuendelee kuwahimiza waTZ wenzetu wengine kupitia hapa JF japo once a week kwa nia ya kujihabarisha kuhusu yanayojiri nchini kwetu na kuchukua hatu pale inapowezekana.

HakiElimu, kama hapo baadaye viunzi toka serikalini bado vitakuwepo basi msisite kutumwagia wateja wenu hizo habari hapa JF.
 
source :http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=2278

HakiElimu yafurahia kulegezewa kitanzi

Habari Zinazoshabihiana
• Kikwete aiweka kiporo HakiElimu 02.02.2007 [Soma]
• Serikali yake yaisambaratisha HakiElimu 31.01.2007 [Soma]
• Mbunge Cheyo atiwa 'kitanzi' 07.07.2006 [Soma]

*Yampongeza Lowassa kwa kutanguliza busara

Na Mwandishi Wetu

ASASI isiyo ya kiserikali ya HakiElimu, imefurahia kulegezewa kitanzi na Serikali na kuahidi kushirikiana na wananchi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuimarisha maendeleo na demokrasia nchini.

Hayo yamo katika taarifa ya asasi hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Bibi Elieshi Lema na kusambazwa kwa vyombo vya habari jana, siku moja baada ya viongozi wa asasi hiyo kukutana na Serikali chini ya Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Dodoma juzi.

Katika taarifa hiyo, asasi hiyo ilisema ina imani makubaliano yaliyofikiwa juzi, yatafungua ukurasa mpya wa uhusiano baina yake na Serikali na mashirika huru ya kiraia.

Ilimshukuru Bw. Lowassa kwa kuongoza mkutano huo kwa hali ya uwazi na udugu, na kwa kutambua dhima ya mashirika huru ya kiraia na kwa msisitizo wake, kwamba Serikali na HakiElimu wana malengo yanayofanana ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.

"HakiElimu inaamini kuwa zuio la Septemba 8, 2005 kwa waraka wa Serikali namba 373 wa Novemba 2005 litaondolewa, ili ifanye kazi kwa uhuru katika ngazi za jamii na shule," ilisema taarifa.

HakiElimu ilieleza kufurahia, kuwa utawala wa sheria na kanuni za kidemokrasia vilisisitizwa wakati wote wa mkutano wake na Waziri Mkuu.

"Pamoja na sheria nyingine, hii inamaanisha kwamba haki ya kikatiba ya uhuru wa habari na wa kujieleza (Ibara ya 18) vitaendelea kuwa msingi wa kazi za HakiElimu na kuongeza uhusiano wetu na Serikali," ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa makubaliano, sasa HakiElimu itafanya utafiti shuleni na kuutangaza, lakini kwa mawasiliano na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi; itachapisha na kusambaza machapisho yake nchini, lakini kwa yale yatakayopelekwa shuleni, yatatakiwa kupata idhini ya Ofisa Elimu Kiongozi.

Pia HakiElimu itatakiwa kutumia busara kuandaa na kurusha vipindi redioni na katika televisheni, lakini ikizingatia kuwa kilichomo ni cha ukweli na itawakilisha mashirika ya kiraia katika michakato inayofanywa na Serikali bila vikwazo.

Makubaliano mengine ni pia kwamba maofisa wa HakiElimu na wale wa Serikali, watapeana taarifa na kudumisha mawasiliano ya kutosha.
 
MKJJ,
Mapendekezo mazito hayo na yanahitaji tafakuri. Kadri ninavyofikiria naona TUNAHITAJI KATIBA MPYA!

Nadhani wizara nyingi (kama si kila wizara) zina wanasheria/kitengo chake cha sheria. Kwa kiasi gani wamekuwa wa msaada ni suala la kujadiliwa. Kama wapo, wanakwazwa na mfumo? Mathalani, kwenye RDC/Dowans, wanasheria wa wizara walihusika vipi? Au suala zima la kisheria waliachiwa ofisi ya AG peke yao? TANESCO nao waliangalia masuala ya kisheria kadri wanavyohusika?

Kwamba kuwe na Mwanasheria Mkuu wa Ikulu, una maana Mwanasheria Mkuu wa Ofisi ya Rais (kwa ajili ya ofisi zote zilizo chini ya Ofisi ya Rais-kwa sasa Menejimenti ya Utumishi w Umma, Usalama, Utawala Bora nk?)

BTW, sijawahi kusikia mshauri wa rais kwenye masuala ya sheria! Huwa nasikia waandishi na wapiga picha, washauri wa uchumi na siku hizi uhusiano wa jamii!

Kwa mwendo (mdundo!) huu labda tuweke utaratibu kuwa rais LAZIMA afundishwe sheria (kama hatakuwa Mwanasheria wakati anachaguliwa) na kupewa cheti (Certificate in Law ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) ndani ya miezi sita katika madaraka yake!

hapana naona Mr. Clean amepitiwa tu hapo... Rais asipokuwapo Tanzania, Makamu ndiye anaye Kaimu, na kama naye hayupo basi Waziri Mkuu ndiye anakaimu. Hivyo kwa vile Rais alikuwa nje ya nchi (siyo nje ya Dar) basi Makamu wa Rais ndiye aliyekaimu kiti hicho.

Nafikiri upo sawa kwenye Makamu wa rais ,lakini waziri mkuu hapana .kwani kama Rais na makamu wake hawapo basi spika wa BUNGE la jamhuri ya muungano wa TANZANIA ndiye anachukuwa jukumu.Katika kumbukumbu zangu kama bado zipo makini ilishawahi tokea katika serikali ya awamu ya tatu kwa spika kuachiwa ukaimu wakati Rais BWM alipoenda kutibiwa uswisi.
 
KNKCU, Katiba ilibadilishwa, sasa hivi chain of succession ni Rais, Makamu, Waziri Mkuu.... Spika au Jaji Mkuu hawaruhusiwi tena kukaimu kiti cha Rais kwani wanatoka katika mihimili mingine...
 
KNKCU, nitakupatia taarifa baadaye leo...

Serikali ya Tanzania imebatilisha uamuzi wake wa kuifungia Asasi ya Kiraia ya Haki Elimu na hivyo kuiruhusu Asasi hiyo iendelee na shughuli zake zikiwemo zile za kurusha matangazo yahusuyo masuala mbalimbali ya Elimu na pia kuiruhusu Asasi hiyo kuweza kufanya utafiti wa kielimu katika shule zetu. Jinsi Haki Elimu ilivyoweza kusimama kidete kutetea haki yake ya Kikatiba ni mfano wa kuigwa kwa asasi nyingine na kwa raia wa kawaida. Hata hivyo hatuna budi kujiuliza kama ruhusa hii ya Serikali ni ushindi wa haki ya mtu kutoa maoni au ni kitendo cha huruma ya serikali baada ya watu wengi kulalamika? Je, huko mbeleni asasi nyingine haitatakiwa kujipanga mstari na kucheza kila serikali inapopiga ngoma?

sikiliza: http://mwanakijiji.podomatic.com
 
KNKCU, hapa nilipo nashindwa kupata nakala ya Katiba toleo la 2005.... hiyo ndiyo nakala ambayo imefanyiwa mabadiliko yote...
 
Mwanakijiji,
Isije kuwa unasema katiba ya chama cha Mapinduzi (CCM).
Ni kweli kabisa kuna mabadiliko ambayo yalizungumziwa hata kabla ya uchaguzi huu kuanza mwaka jana kukihoji mabadiliko ndani ya Katiba ambayo yaliondoa madaraka ya Rais wa Zanzibar kuwa tena makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano nchini na pia mshauri mkuu wa Rais.
Kichekesho ni kwamba hata Shein mwenyewe ni title hana nguvu ya EL hata kidogo. Wote Shein au Karume - are NOOOOBODY bara.
 
KNKCU, hapa nilipo nashindwa kupata nakala ya Katiba toleo la 2005.... hiyo ndiyo nakala ambayo imefanyiwa mabadiliko yote...

MKJ,
Sawa mwaka jana nilitafuta Dar duka la vitabu vya serikali wakaniambia hawana mpaka Dom,nilibahatika kwenda huko nayo hawakuwa nayo maduka mengine mengi hawakuwa nayo.Labda ndiyo hiyo iliyokuwa na mabadiliko.
 
KNKCU, hapa nilipo nashindwa kupata nakala ya Katiba toleo la 2005.... hiyo ndiyo nakala ambayo imefanyiwa mabadiliko yote...

Mwanakijiji,
Isije kuwa unasema katiba ya chama cha Mapinduzi (CCM).
Ni kweli kabisa kuna mabadiliko ambayo yalizungumziwa hata kabla ya uchaguzi huu kuanza mwaka jana kukihoji mabadiliko ndani ya Katiba ambayo yaliondoa madaraka ya Rais wa Zanzibar kuwa tena makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano nchini na pia mshauri mkuu wa Rais.
Kichekesho ni kwamba hata Shein mwenyewe ni title hana nguvu ya EL hata kidogo. Wote Shein au Karume - are NOOOOBODY bara.
Mkandara,
Tutaendelea kutafuta ukweli wa hii katiba kwasababu hata kwenye web site ya bunge bado ipo hiyo ya 2000.sasa kwanini basi kama kuna mabadiliko ya 2005 wasiiweke.
 
Kikwete Afanye Nini Katika Utawala Wake ili aweze kujinusuru 2010, Wana JF tumezungumza mengi sana kuhusu utawala wa Rais Jakaya M.Kikwete sasa katika yale mapungufu tuliyo yaona katika safu ya Baraza la Mawaziri ,Ma DC, Ma RC, Katibu Wakuu, na Waziri Mkuu,Wakurugenzi, Safari za Nje, Mikataba,Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Mapanki, Ahadi za Kipindi Cha Kampeni, Madarasa, Umeme, Ajira kwa vijana, Wastaafu na Wazee,Kakina Mama na Watoto, Afya, Elimu, Richmond na Rada na mengine mnisaidie,

kiongozi wetu mpendwa, kipenzi cha wengi ,changuo la mungu, kisura,mpenda watu, afanye nini kulinusuru taifa letu.

Sasa tujadili hilikwa kina ninaomba kutoa hoja......
 
Hasara,
Hili swali gumu sana ktk kipindi alichonacho JK. Kuna majibu mengi sana ambayo ni rahisi kuyasema lakini hayawezi kutendeka kirahisi. mfano mdogo ni kusema AJIUZULU!..
Hii haikubaliki na yeye, chama wala wananchi walio wengi kwa sababu nyingi za kimsingi. Wala kujiuzulu kwake hakuwezi kuleta mabadiliko ya haraka isipokuwa labda la msingi hapa ni JK kufuata sera za msingi za chama ambazo zilimpa kura zaidi ktk kugombea URAIS!..
Mtakumbuka kuwa JK alipendwa na wengi kwa dhana kwamba yeye ndiye mkombozi wao hasa alipokuja na hiyo Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya wakitangaza kwa nguvu sera yenye nuru kubwa kwa kupitia Ujamaa na Kujitegemea. Sera hii inasema:-

Lengo la Ujamaa na kujitegemea ni kuhakikisha kwamba wananchi wenyewe wanamiliki na kuendesha uchumi wa nchi, mmoja mmoja, kwa kupitia vyama vyao huru vya ushirika wa aina mbalimbali, kwa kupitia makampuni ya wananchi na ya ubia ambamo maelfu ya wananchi watanunua hisa....Kwa mtazamo huu wa CCM, sehemu kubwa ya uchumi wa nchi inakusudiwa umilikiwe na wananchi wenyewe ili kuinua hali ya maisha yao na kutosheleza mahitaji yao ya msingi. Dola....itaendelea kushika nafasi ya muhimili wa uchumi wa Taifa.

Hii ni ahadi kubwa sana ya CCM kwa wananchi, ahadi ambayo JK kashindwa kabisa kuiwekea misingi zaidi ya kuendeleza yale ya Mkapa kwa kutafuta wageni kuja kumiliki uchumi wa Tanzania akitumia lugha nyepesi ambayo asingeweza kabisa kuitumia kuwaahidi wananchi wakati wa uchaguzi.
Lugha yenye kila excuse ya kusema kwamba nchi yetu ni maskini inahitaji bado nguvu na fedha za wageni kushika uchumi wetu hali baadhi ya watu wachache hasa viongozi wakitumia nafasi hiyo kujilimbikiza mali. Matokeo yake yamekuwa kinyume kabisa cha falsafa na sera zote zilizojengwa na CCM kimaandishi.

Tunamuomba arudishe usemi uliompa kura na kuanza kuufanyia kazi...
 
Hasara

hebu kwanza malizia huku maana uliacha minongono mingi tuu ili hali uliahidi ungekuja weka mambo sawa

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1704&page=4

popoz.jpg
 
huyu mtu mie nafikiri tumuache tu kama alivyo maana inawezekana akawa hajui anachokifanya: nimefikaje mpaka kusema hivi; huyu mtu anajua anachokifanya hakiwafurahishi wadanganyika na haonyeshi njia yoyote ya kubadilika, so nadhani suala la yeye kubadilika tusahau mpaka 2010 itakapofika ndipo atakapoanza kutia huruma ( lakini kwa huruma tuliyonao wabongo + ujinga, atachaguliwa tena ) !! we will see inshaallah, bwana akipenda !!

mie nadhani watu kutoka jambo nao waanze kujipanga safari ya 2015 kugombea urais mapema maana uozo mwingine utaletwa baada ya jk kuritaya !!

HAYA SASA TUANZE KUPATA LIST YA POTENTIAL CANDIDATES KUTOKA JAMBO ( ila sijui chama gani ) maana ugombea binafsi ndio hivyo tena !!
 
Back
Top Bottom