Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Huyu ndiye ‘the real’ Kikwete!

Tanzania yetu hususan viongozi wetu hutmia mass media kama kitendea kazi chao na kufichia ukweli wa mambo kupita kiasi!!!!! na baadhi ya vyombo vya habari vinakuwa vinashindwa kusema ukweli hasa pale unapoitajika? ila mpaka jambo liwahusu wao!

Mifano: timu yetu ya taifa imepigwa bao na ilisemekana ni timu nzuri kutokana na comments na assesments za wandishi wa habari

Raisi wetu pia, kwanza anajitahidi kutuongoza vizuri lakini he is too much a manipulator!!! and you know what he is using to manipulate us with......ofcoz the the mass media he is really working hard with media,,,trying to hide the real situation!!!! Mr. President we believe in you and we respect sometime you got to tell us the truth,,, be transparent.......''Changing your cabinet in less than a year??? come on man,,,thats very big"

Tatizo la umeme!!!! hilo sisemi..........................

`come on let us all do our job!!!!!from the truth we can all learn and move on!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kikwete avunja ukimya

2007-04-01 10:59:55
Na Mwandishi wetu


Rais Jakaya Kikwete, katika hali ya kuvunja ukimya, sasa ametoa wito kwa wananchi kila mmoja pale alipo kuhakikisha anachukua tahadhari zote muhimu kukabiliana na Homa ya Bonde la Ufa, ambayo hadi sasa imeua watu 33 na wengine 119 kuambukizwa.

Rais Kikwete alitoa wito huo jana alipohutubia Taifa kupitia redio na televisheni katika uratatibu wake aliojiwekea kila mwisho wa mwezi.

Alisema Mikoa ambayo watu wameathirika na hata baadhi yao kufariki dunia ni Manyara, Tanga, Dodoma na Morogoro na kwamba mikoa ya Dar es Salaam na Singida, pia inao wagonjwa wachache wenye kuonyesha dalili za maradhi hayo ambao wanaendelea kuchunguzwa.

Kwa upande wa mifugo, Rais Kikwete alisema mikoa iliyokumbwa na ugonjwa huo ni Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Iringa, Singida na Mbeya.

Hata hivyo, alisema Serikali inatambua uzito wa tatizo hilo na inafanya kila iwezalo kuutokomeza ugonjwa huo.

Rais Kikwete alisema hadi sasa, serikali imechukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huo ambao binadamu huupata kwa kula nyama ya mnyama aliyeathirika.

Aliitaja baadhi ya mikakati na hatua hizo kuwa ni kuzuia kufanyika kwa minada ya mifugo kote nchini, lengo likiwa ni kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo na kwamba minada itaruhusiwa tena kufanya kazi pindi hali itakaporejea kuwa nzuri.

Pia alisema serikali imeimarisha utoaji wa chanjo za mifugo dhidi ya ugonjwa huo kwenye maeneo yote yenye mifugo ambapo hadi sasa imetumia Sh. bilioni 1.7 kununulia chanjo na vifaa vingine vya kukabiliana na ugonjwa.

``Tayari tumeagiza dozi milioni mbili za chanjo ya RVF. Kati ya hizo, dozi 736,600 zimeshapokelewa na kusambazwa kwenye wilaya zilizoathirika na zile zilizo katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa,`` alifafanua.

Kadhalika, alisema serikali imeandaa chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu, mpango wa dharura wa kitaifa wa kudhibiti ugonjwa huo ambapo utagharimu dola za Kimarekani takriban milioni 12.3.

``Tunaendelea kuwasiliana na marafiki zetu wa nje kuhusu uwezekano wa kutusaidia kugharamia mpango huu mapema iwezekanavyo ili kunusuru mifugo yetu na maisha ya watu,`` aliongeza.

Aidha, alifafaunua kuwa, mnyama na mwanadamu wanaweza kupata ugonjwa huo kwa kuumwa na mbu wa aina ya Aedes mwenye wadudu wa maradhi hayo.

Alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha kwamba, mifugo yote inapata chanjo kwa kuwa hiyo ndiyo kinga ya kwanza ya kupambana na ugonjwa huo.

Rais Kikwete alisema kwa upande wake, Serikali inafanya jitihada ili kuhakikisha kwamba dozi za kutosha za chanjo zinapatikana na kuwahimiza wana wote kupeleka mifugo yao ikachanjwe mapema iwezekanavyo.

Aliwataka pia watu kuacha tabia ya kuhamisha mifugo kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kiholela kwa kuwa kufanya hivyo kunachangia katika kueneza ugonjwa na kurudisha nyuma jitihada za kuudhibiti.

Rais Kikwete aliwaasa watu kuepuka kuchinja wanyama na kuchuna ngozi bila kuchukua tahadhari za kujikinga pamoja na kutoshika damu, majimaji na nyama ya mnyama anayehofiwa kuwa na ugonjwa huo.

Vile vile, aliwataka watu kutokula nyama ya mnyama aliyekufa kwa ugonjwa huo na kuelezea kushangazwa kwake na taarifa za baadhi ya wanaodiriki kufukua mizoga iliyozikwa na kula nyama yake.

``Ndugu zangu, ni uchu wa kiasi gani huo unaotufanya hata tupuuze tishio kubwa kwa maisha ya mwanadamu kama hili la ugonjwa huu. Nawasihi tusikilize ushauri. Wahenga wamesema, asiyesikia la mkuu huvunjika guu,`` alihoji na kutolea mfano huo.

Hali kadhalika, alisema ni vema siku zote watu kunywa maziwa yaliyochemshwa vizur na kuwataka wataalam na watendaji kwenye ngazi ya wilaya na vijiji, kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa Sheria ya Magonjwa ya Mifugo ili kudhibiti kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.

Pamoja na yote hayo, Rais Kikwete alihimiza matumizi ya vyandarua hasa vile vilivyowekwa dawa ili kujikinga na mbu kwa kuwa ugonjwa huo huenezwa pia na mbu aina ya Aedes na kuongeza juhudi za kudhibiti mbu ili kupunguza kushamiri kwao kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa kufukia mazalia yao na pale inapowezekana, kunyunyizia dawa.

Alivishukuru vyombo vya habari na kuvitaka kuendelea kushirikiana na kuwa na mawasiliano ya karibu na mamlaka husika na hasa wataalamu husika ili kuepuka kuandika au kutangaza habari ambazo hazijathibitika.

Alisema vyombo hivyo vinalo jukumu kubwa la kusaidia kuelimisha umma kuujua ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga nao.

SOURCE: Nipashe
 
Sina uhakika kama kilichoandikwa na Nipashe ndicho ambacho Rais alikiongelea peke yake au Nipashe imeamua kuandika kuhusu RVF peke yake.

Anyway nitachangia kana kwamba hichi ndicho alichoongelea; Haya ni mambo yale yale ya kujitakia umaarufu kama lilivyokuwa suala la upungufu wa chakula mwaka jana. Alipokuwa Arusha ambako ugonjwa ndipo ulipoanzia alipata fursa ya kuliongelea hilo huko ili kuweka msisitizo lakini akaja Dar na kuamua kupoteza muda wa TV na Radio.

Angelitumia hata nusu ya hotuba yake kuongelea RVF mimi ningeona sawa maana wananchi kadhaa wameshakufa kwa hiyo this is serious issue. Lakini hotuba nzima...that's low. Washauri wake lazima wajifunze huu usaanii hautawafikisha mbali ukizingatia bado miaka mingine 3 mizima to go.
 
Gigo ilikuwa nzuri kivipi tupe yaliyo kuwemo kwenye hotuba hiyo tafadhali
 
HIVI HUJUI LEO NI SIKU YA WAJINGA DUNIANI ? kwahiyo kama raisi akiongelea rvf peke yake ni haki yake watanzania wote wajinga ndio maana kila anachoongea raisi wanakikubali

mimi nilitegemea raisi aongelee yafyatayo

- MFANO MSIMAMO WAKE KUHUSU AFRIKA MASHARIKI , ATUELEZEE HALI HALISI MANAKE WASOMI SI NDIO WANAKUSANYA MAONI ? si angetuambia kinaga ubaga kinachoendelea ?

- kwa sababu nchi yetu inategemea zaidi kilimo na msimu wa mvua unakuja basi angeliambia taifa kwa ujumla serikali imejiandaa vipi kusaidia hawa wakulima ambao ndio wako wengi huko vijijini , naon ahii raisi haongelei kabisa.

KUNA PIA MAMBO MENGINE MENGI YA KUONGELEA SASA NIMEONA HIYO TU

AHSANTE
 
Nicheke mie Binti Abdala.

Nampenda Kikwete. anujua mambo gani yanatugusa sisi. Ndio maana hotuba nzima ya mwezi huu amezungumzia mambo mawili tu: "Mikopo ya Bilioni moja" na "RVF". Huyu ndio Rais wa watu, wala hakupoteza muda kuzungumzia EAC, Muswada wa Rushwa, Muswada wa Habari, Vita kati ya wananchi wa Msalala na Barick. Wala hakuzungumzia kwamba hazina imeanza kukauka. Bilioni moja amehakikisha tutazipata na RVF itatokomezwa kwa Ari mpya, Kasi Mpya Nguvu Mpya. Na tayari ameahidi madawa ya chanjo(chanzo?) yameanza kuingizwa. Kingine tu, hotuba hii hakuwa na tabasamu kubwa nilililizoea. Jakaya usitunyime tabasamu lakooooooooooooooooooo!!!!!
 
DrWHO Mkataba wa RICHMOND ni mkubwa sana,haiwezekani rais asijue mkataba wa Mamia ya Mabilioni, na kama hajui basi ni dalili za uzembe? Fedha zote hizo haziwezi kutolewa na waziri pekee ni lazima baraza zima la mawaziri lijadiliane! hivyo rais anajua! Kama kuongeza bilioni 48 kwa ajili ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu baraza lilikaa itawezekanaje bilioni 172 baraza lisikae?
JK is behind all these together with his cabinate!
 
Asha una mambo wewe na lugha ilojaa tasfida
tabasamu lake lazidi kufifia siku hadi siku kwa sababu anajua hotuba yake hailengi kwenye aliyoahidi "maisha bora kwa kila mtanzania" bali zinazidi kutuchosha.
 
Gigo ilikuwa nzuri kivipi tupe yaliyo kuwemo kwenye hotuba hiyo tafadhali

Mikopo!-Kwa sisi masikini-!!! , RVF!!!!!

Inafurahisha sana , Kuona na kusikia Raisi akiongea na watu wake mambo yanayo wahusu!! Kuwiana na wakati!!

Mimi Binafsi Ilinifurahisha sana!!.... alielweka ....
(Time)...
 
kuna watu wana mambo huyu Asha naye Mhhh?!!

Tabasamu linapungua siku hadi siku khali mbaya si kama ilivyotegemewa ndiyo maana hata kwenye uchanguzi TUNDURU kikosi kizima kilizama kule mpaka wazee wasiojiweza jamani...Mzee wetu KAWAWA amechoka sasa wamwache apumzike. Lakini wanajua kuwa sasa hivi hakuna cha tabasamu ndiyo maana wakaja na mbinu mpya mtazijua baadaye.
 
Asha Abdala

Mbona ukiulizwa maswali hujibu?
 
Nicheke mie Binti Abdala.

Nampenda Kikwete. anujua mambo gani yanatugusa sisi. Ndio maana hotuba nzima ya mwezi huu amezungumzia mambo mawili tu: "Mikopo ya Bilioni moja" na "RVF". Huyu ndio Rais wa watu, wala hakupoteza muda kuzungumzia EAC, Muswada wa Rushwa, Muswada wa Habari, Vita kati ya wananchi wa Msalala na Barick. Wala hakuzungumzia kwamba hazina imeanza kukauka. Bilioni moja amehakikisha tutazipata na RVF itatokomezwa kwa Ari mpya, Kasi Mpya Nguvu Mpya. Na tayari ameahidi madawa ya chanjo(chanzo?) yameanza kuingizwa. Kingine tu, hotuba hii hakuwa na tabasamu kubwa nilililizoea. Jakaya usitunyime tabasamu lakooooooooooooooooooo!!!!!

Asha wataka tabasamu heeee! shauri yako!

Nasikia siku hizi wanaikimbia kauli yao ya maisha bora kwa kila mtanzania

Walahi Kikwete atauona muda wa urais ni mrefu mno!
 
....Walahi Kikwete atauona muda wa urais ni mrefu mno!

..kama Waziri Mkuu wa Iraki ambaye hana hamu tena, anaomba tu muda wake uishe haraka!

Kuhusu Kawawa, Simba wa Vita ameamua kuji-assert , kuonyesha kuwa, yeye kama mmoja wa waasisi wa taifa hili, habaki nyuma, au hawi kimya sana katika siasa za nchi hii. Ieleweke kuwa kwa ujumla afya yake imekuwa si nzuri muda mrefu na ndiyo maana ilikuwa ni busara "apumzike" zaidi.

Lakini sasa ameamua kuwa "active" zaidi badala ya kusubiri kutembelewa pale Kiluvya na watu wenye nia ya "kujifunza" kukuza uyoga na kufuga nyuki, au kwenda kupokea tuzo iwe ya BASATA, BAKITA au Martin Luther King Jr.

Huenda Kamanda anataka kutoa ujumbe kwa wananchi na watawala, kuwa YUPO, na kwamba HARIDHIKI na mambo yanavyokwenda. Public appearances zake za karibuni:

1. Uchaguzi wa Tunduru

2. Kutembelea uwanja mpya wa michezo wa taifa Dar es Salaam

3. Mgeni rasmi katika baraza la Iddi Morogoro (ambapo awali ilikuwa VP ndiyo awe mgeni), na hapo akazungumzia zaidi masuala ya ushirika kama mkombozi

Usishangae sasa "akialikwa" na bunge kulihutubia mwezi huu, atoe somo kuhusu mustakabali wa nchi hii (na kufanya marejeo kwenye Azimio la Arusha!)
 
DUA


Maswali gani eti. Mi siingiagi hapa mara kwa mara labda yamenipita. Nkumbushe basi
 
Yaani Kawawa ? Jamani mna mamno Kawawa ahutubie Bunge ? Je anakumbuka anacho kisema baada ya dakika 5 ? yaani Kawawa na Kingunge ambaye toka Ikulu hadi Airport huwa kesha ota ndoto kibao ? Ama kweli CCM inajua namna ya kuwakumbuka wazee wa asisi . Lakini nauliza jamani Tanzania matatizo ni RVF pekee na mabilioni ? JK are you serious na hotuba zako ? Umetuchoka Watanzania ama hujui ufanyalo ? Rais kila akihutubia hakosi kutamka kuomba omba . Pesa wanazozitoa wafadhili kila siku zinaenda wapi ?
 
Asha wataka tabasamu heeee! shauri yako!

Nasikia siku hizi wanaikimbia kauli yao ya maisha bora kwa kila mtanzania

Walahi Kikwete atauona muda wa urais ni mrefu mno!

Nilishawahi kusema Anakuna kichwa,Mvi zimeanza kutoa na nywele zitaanza kunyonyoka kidogo kidogo na Uze utamjia haraka kuongoza Nchi si mchezo wa kuigiza kunahitaji umakini wa hali ya juu!
 
Asha Abdala

Uliandika hivi kwenye thread hii: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1930&page=2

Asha Abdala Nicheke mie Asha. wanavyoumbuka! Eti rushwa rushwa rushwa. Kama kweli mnakerwa na rushwa mbona hamchangii muswada wa RUSHWA? Au mna nongwa tu na RICHMONDULI?

Hii sheria mpya wazungu wenyewe wameikubali. Sio unaona Denmark wameturudishia misaada?

Ndio mambo ya Kaka JAKAYA hayo. He is the man..


Nilikuuuliza swali hili

Nicheke mie Asha. wanavyoumbuka! Eti rushwa rushwa rushwa. Kama kweli mnakerwa na rushwa mbona hamchangii muswada wa RUSHWA? Au mna nongwa tu na RICHMONDULI?

Naomba unisaidie mimi nina swali moja kwa mshikaji wako, alitoa pesa kwenye Harambee ya kiasi cha shillingi millioni 60. Swali langu ni je alilipa kodi kiasi gani kwa pesa hizo alizotoa? Ofisi ipi ilipokea malipo hayo?

Hii sheria mpya wazungu wenyewe wameikubali. Sio unaona Denmark wameturudishia misaada?

Sheria ikikubaliwa na wazungu wewe unaona inafaa? Au unawaabudu hao wazungu?

Gonga hapo chini utaenda kwenye hiyo thread unipe majibu............kwa hiyo usishangae swali.

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1930&page=3
 
CCM wanaingiza hata makontena ya vitabu utasikia wanatangaza misaada tu kujipa majina lakin kodi hata gharama za kusafirishia hawalipi na watu wanabaki kushangaa . Unauliza 60m kulipiwa kodi ? Unacheza wewe .Utasikia nayoa msaada wa vitabu kata fulani sijui jimboni kwangu lakini nyuma ya msaada huo kuna mengi .
 
Back
Top Bottom