Huwa mnapiga story gani siku ya kwanza kukutana na ndugu yako ambaye hujaongea nae zaidi ya mwaka

ninjajr

Senior Member
Sep 16, 2023
133
140
Za usiku wana JF na poleni na shughuli za kujenga taifa.

Nina ndugu yangu wa kiume upande wa maza mkubwa kidogo ila ni kama tunalingana na mimi pia ni kiume tulikuwa close saana kipindi cha nyuma karibia mwaka sasa hivi ule ukaribu ulikufa wote.

Kwa mara ya kwanza tulipingana kauli hadi kufikia hatua ya kutosemezeshana na kufungiana makufuli kila mtu na life lake hakuna cha kupigiana simu wala baba ake message kwa kipindi cha mwaka mzima.

Kuna siku alinikuta mahali akatoa salamu tu hata wakati anaondok hakuniaga ndo nikavunjika moyo wa kumtafuta though kabla ya hapo pia tulikuw hatutafutan sema zilipishana wiki kazaa since Tunisian kauli .

Natokea siku hio nilifunga kufuli la kujipendekeza nisije nikaonekan mnanka.

kiukweli hio siku sikudhamiria kujibishana nae sema kwenye maongezi yake na mimi hio siku nlijikuta napata hasira baada ya kuona maneno ya kibehi na utumwa Kutoka Kwa huyu Ndug yangu.

Nimekuwa nikimsikiliza yeye ni kumfuata kama kaka mkubwa. Na kiukweli amenisave saan Kwa baadhi ya shida zangu ambazo mostly ni vijiela, amenikopesha kopesha saan 😁tumesaidian sana,tumekuwa tukiishi kama familia moja kwa muda mrefu saan,akiwa na lake Ana nambia na mm yangu anayajua ,tumefichian siri nyingi saan ambazo hata wazazi na Ndug wengine wakijua ni balaa lingine

Kesho nataka nimpigie tusahau yaliyopita. Ila msamaha siwezi nikamuomba Kwa upande wangu nilikuw sahihi kabisa kutokana na value na standard nlizochagua kuishi.Na sina kinyongo nae sema yule mpuuzi anajiona matawi saan anaambia watu hana story za kupiga na mimi.

Nafahamu asilimia yetu nyingi tumepishana kauli saan na Hawa ndugu zetu hasa wa wa karibu ,nipeni experience wana jf siku ya kwanza kuongea mlipiga story gani?
 
Hapo ndio pombe inapoingia sasa. Pombe inauwezo wa kusuluhisha hilo jambo lenu once & for all na wote mkawa na amani milele. Ukikutana na binaadamu asiyetumia mvinyo kuwa naye makini sana kwa asilimia kubwa ni lazima awe na chembechembe za unafiki
 
Sioni dalili za mgogoro wenu kuisha ki uhalisia. Mnaweza mkaongea na kuchekeana kinafiki then kila mtu akabaki na duku duku lake. Ni bora tu hata usimpigie simu maana kwa jinsi ulivyoandika inaonekana bado nyote wawili mnataka ligi iendelee
Mkuu mm nataka nitoe dukuduku langu moyoni ili ajue mipaka yake sina ligi naye
 
Beer haipandi mkuu
Baba. Yangu aligombna na kaka ake ugomvi ulikuwa ni wa muda tu tena walikuwa hawaongei ata yani walikataana kabisa, sasa ktk mazishi ya babu wazee wa ukoo wakakaa zikaletwa bia nyama watu wakanywa wakalewa vizuri. Ugomvi wao. Ukasulihishwa simpleee adi kesho wanaongea vizuri bila unafki . Ndugu wa kweli lazima mgombane
 
story za kinafiki nafikiii ... hamna uwazi kiivo manake waogopa ogopa mwambia ama muuliza baadhi ya vitu
 
Bila mmoja wenu kujishusha hakuna suluhu itakayoweza kupatikana.

Kuna kipindi katika maisha ni bora kuwa ana amani ya nafsi kuliko kuwa sahihi. Ni wazi tofauti yenu inakuathiri hivyo kukukosesha amani ya nafsi.
Sio kila siku mtu anaweza pata mtu mwingine ambae anaweza kuwa wazi kwake na kupata msaada pia, iwe ndugu au rafiki. Hivyo ni mtu muhimu kwako huyo kama mliweza share mambo yenu.

Pa kuanzia tafakari yale mazuri baina yenu ulinganishe na hiyo hitilafu yenu, ikiwa mazuri ni mengi zaidi basi ni sawa kujishusha na kuanza upya nae.

Nina assume wewe pia ni mwanaume na kawaida suluhu za kiume hazina kuombana msamaha. Tafuta siku moja unayojua anakuwa free, mpigie simu na mualike sehemu. Mpigishe story kama vile hakuna tofauti baina yenu. Ikiwa na yeye ana roho ya kiume hasa hapo itakuwa tayari mshasuluhishana.

Sometimes all it takes is just one phone call to make things right. Pengine na yeye anawaza atakuanzaje, hivyo kuwa muungwana zaidi kwa kumuanza yeye ikizingatiwa ni mkubwa wako. SIku zote Mungu hufanya wepesi pale penye dhamira ya kutengeneza muafaka baina ya waliogombana.

Maisha ni mafupi mno kuishi na vinyongo, tujaribu kujifunza kuongea yale yaliyo mioyoni mwetu kwa watu ikiwa bado wapo hai kuliko kuja kulia kwa majuto pale watakapoondoka na dhana tofauti na ile tuliyonayo mioyoni mwetu juu yao.
 
Baba. Yangu aligombna na kaka ake ugomvi ulikuwa ni wa muda tu tena walikuwa hawaongei ata yani walikataana kabisa, sasa ktk mazishi ya babu wazee wa ukoo wakakaa zikaletwa bia nyama watu wakanywa wakalewa vizuri. Ugomvi wao. Ukasulihishwa simpleee adi kesho wanaongea vizuri bila unafki . Ndugu wa kweli lazima mgombane
Hio safi gambe inasahaulish ugomvi kumbe
 
Bila mmoja wenu kujishusha hakuna suluhu itakayoweza kupatikana.

Kuna kipindi katika maisha ni bora kuwa ana amani ya nafsi kuliko kuwa sahihi. Ni wazi tofauti yenu inakuathiri hivyo kukukosesha amani ya nafsi.
Sio kila siku mtu anaweza pata mtu mwingine ambae anaweza kuwa wazi kwake na kupata msaada pia, iwe ndugu au rafiki. Hivyo ni mtu muhimu kwako huyo kama mliweza share mambo yenu.

Pa kuanzia tafakari yale mazuri baina yenu ulinganishe na hiyo hitilafu yenu, ikiwa mazuri ni mengi zaidi basi ni sawa kujishusha na kuanza upya nae.

Nina assume wewe pia ni mwanaume na kawaida suluhu za kiume hazina kuombana msamaha. Tafuta siku moja unayojua anakuwa free, mpigie simu na mualike sehemu. Mpigishe story kama vile hakuna tofauti baina yenu. Ikiwa na yeye ana roho ya kiume hasa hapo itakuwa tayari mshasuluhishana.

Sometimes all it takes is just one phone call to make things right. Pengine na yeye anawaza atakuanzaje, hivyo kuwa muungwana zaidi kwa kumuanza yeye ikizingatiwa ni mkubwa wako. SIku zote Mungu hufanya wepesi pale penye dhamira ya kutengeneza muafaka baina ya waliogombana.

Maisha ni mafupi mno kuishi na vinyongo, tujaribu kujifunza kuongea yale yaliyo mioyoni mwetu kwa watu ikiwa bado wapo hai kuliko kuja kulia kwa majuto pale watakapoondoka na dhana tofauti na ile tuliyonayo mioyoni mwetu juu yao.
Mkuu ushauri wako nimeupenda na ntaufanyia kazi ni wazi nahisi gape lake licha ya maneno yake yanayokera ila ananikubali saan ubarikiwe mkuu 🙏
 
Back
Top Bottom