Hello Great thinkers 🫡
Mwanadamu ana baadhi ya mambo ambayo huwa yanatokea ndani yake bila yeye kuyapanga au kuyachagua kwa makusudi(Unakubaliana na mimi?)
Hayo tunaweza kuyaita Human Nature asili ya mwanadamu
Mfano:
Kupenda : binadamu anaweza kujikuta anampenda mtu au kitu bila hata kupanga kukipenda
Hii ni sehemu ya nature ya mwanadamu
Kutamani: kutamani mtu au kitu, mafanikio maisha bora au kupata zaidi ni jambo ambalo linaweza kutokea naturally ndani ya mwanadamu
Kukosea kwa kawaida hua tunasema kwamba mwanadamu si perfect 💯
Ikiwa na maana kukosea haiepukiki
Kukosea ni sehemu ya maisha na ni sehemu ya asili ya mwanadamu
Mimi tangu nazaliwa nimekuta huo msemo
Kuhisi maumivu unapoumizwa, ni natural kuhisi maumivu
Huwezi kila wakati kuamua kwamba sitahisi au sitaumia ni ngumu kudhibiti hisia za maumivu kwa sababu huja natural
Huo ni upande mmoja wa Human Nature ambao tunaweza kuuita positive (chanya)
Lakini vipi 👇
Human Nature inaweza kuwa negative?
Kwa sababu kama binadamu anaweza kupenda anaweza pia kuchukia
Kwahiyo hapa tutasema chuki nayo ni sehemu ya human Nature?
Anaweza kuwa na wivu
MF: ameona mtu kamzidi kitu fulani akaingiwa na wivu gafla bila kupanga
Anaweza kutamani kitu vitu bila kupanga ni hisia tu zinamjia
Anaweza kukosea
Kuwa m binafsi
Najiuliza je, haya mambo nayo ni sehemu ya human nature?
Ikiwa baadhi ya hisia na impulses zinatokea naturally ndani ya mwanadamu je kuwa na hisia hizo kunamaanisha kwamba lazima uzifanyie kazi?
Yaani uwe selfish kwa wengine...
Uumize wengine pengine kwa sababu una history ya maumivu kwa kisingizio una hisia za maumivu
Uachonganishe watu...
Uchukie watu..
Uwe mtu anayefanya dunia isiwe salama kuishi kwa kisingizio kwamba hii ni human nature na kwamba hizo ni tabia zisizoepukika?
Utasikia kawaida binadamu sisi hatupendani hapo mtu anatafuta kuhalalisha mabaya anayofanya kwa watu wengine
Ex:👇
Kuna tabia moja ambayo sisi wanadamu tunayo
Mtu anakosea dhahiri, lakini anapofika kwenye kuomba msamaha hawezi kusema tu
JAMANI imekosea naomba nisamehewe
Badala yake anakimbilia kusema
Mimi ni binadamu, hakuna binadamu mkamilifu
Hii huwa naiona kama ina kiburi fulani ndani yake
Kwa nini usikubali tu kwamba umekosea na uombe radhi, bila kuambatanisha sababu ya kuhalalisha kosa lako?
Kwa maoni yangu binafsi, nakubali kabisa kwamba wakati mwingine kuna hisia zinaweza kukuingia bila hata kupanga
Labda ukapatwa na wivu
Labda ukakasirika
Labda ukahisi chuki
Lakini pamoja na yote hayo, huwezi kuendekeza hizo hisia zako kwa sababu tu zimekuja naturally
Wakati mwingine mtu ana uwezo wa kuzikataa hisia hasi zenye uharibifu, hasa zile ambazo hazina faida kwake wala kwa wengine
Naamini sio kila kitu unachohisi unapaswa kukiweka kwenye akili na kukifanyia kazi mara moja
Kuna tofauti kati ya kuhisi kitu na kuchagua kufanya kitu kwa sababu umehisi
Unaweza kuwa na wivu bila kumdhuru mtu
Unaweza kuwa na hasira bila kumtukana mtu
Unaweza kuumia bila kuamua kuwaumiza wengine
Unaweza kuhisi chuki bila kugeuza chuki hiyo kuwa tabia yako
Mwanadamu yeyote anaweza kuwa mtu mzuri sana bila kuwa kikwazo kwa wengine, pale tu anapojifunza ku.control hisia zake negative na kuchagua kwa busara jinsi ya kuzitendea kazi
Kwa sababu mwisho wa siku, hisia zinaweza kutokea naturally, lakini matendo ni choice
Dunia ingekuwa sehemu nzuri zaidi kama wote tungetumia Human Nature yetu kwa upande wa positive
Karibu kwenye mada
Blue Monday 💙
ShesRise_1 🤚