Human Nature

Human Nature

Attachments

  • Michael Jackson - Human Nature (Official Audio).mp4
    4.3 MB
Struggle for Existence and survival of the fittest! Mambo mengi anayofanya binadamu yamefumwa katika kanuni hii; na karibu kila kitu anachofanya kwa namna moja au nyingine kimelengwa katika kumnufaisha yeye. Na kwa vile ulimwengu umefinyangwa kwa kufuata kanuni ya hasi na chanya kama pande mbili za kitu kile kile (matter vs. antimatter), wema na ubaya unakwenda pamoja katika harakati zake za struggle for Existence and survival of the fittest. Hata anapopambana kupunguza makali ya entropy ili aendelee kuishi kwa raha na kwa muda mrefu inavyowezekana, hawezi kuepuka kanuni ya hasi na chanya maana ndiyo inaendesha mfumo mama wa maisha yake.

Huyu ndiye Homo Sapiens! Mnyama mtata, hatari na changamano kuliko wote!
 
Mikono inawasha kuandika bro 🙌🏼
Welcome back ShesRise_1

Kama hatuchagui kila hisia inayotokea ndani yetu, lakini tunachagua namna ya kuitendea kazi je, tunapaswa kumhukumu mtu kwa hisia aliyonayo, au kwa maamuzi anayofanya akiwa na hisia hiyo? Na kama tunajua impulse fulani inaweza kuwa destructive, ni wakati gani responsibility yetu inaanza pale tunapoihisi, au pale tunapoamua kuifuata? 🤔
Hisia acha zituvae kwa gafla lakini
Muhimu ni kuchagua nini tufanye baada ya kuvamiwa na hizo hisia
 
Sio rahisi hivyo.

Hatuwezi kudhibiti hisia muda wote. Kuna muda hatuna taarifa za kutosha kufanya maamuzi sahihi. Na hakuna ajuaye kesho.

Mzazi mwenye upendo wa dhati kwa mwanaye, anaweza kuiba ili mwanaye apate chakula. Anajua si sahihi, lakini upendo unamsukuma. Hajui anamuumiza kiasi gani anayemuibia.
 
Hakuna namna utalemba huo wizi wa mzazi kijana kwa sababu yeye anamuokoa mwanae kwa kuumiza mtu mwingine unaona ni sawa

Huwezi kuhalalisha wizi kwa mtindo huo
 
Hakuna namna utalemba huo wizi wa mzazi kijana kwa sababu yeye anamuokoa mwanae kwa kuumiza mtu mwingine unaona ni sawa

Huwezi kuhalalisha wizi kwa mtindo huo
Simtetei mzazi, wewe vaa viatu vyake utauona uzito wa maamuzi yake.

Hatuchagui kutenda jambo kwasababu tu ni sahihi, yapo mengi sana yanayotusukuma.

Ndio maana watu wenye akili wakatunga sheria ili tusijiamulie sana mambo.
 
mshamba_hachekwi
Narudia hakuna namna utaumiza wengine kwa sababu wewe umeumizwa na ukataka watu waelewe

Vipi huyo uliemuibia tuseme labda ni kiasi cha pesa na kumbe alikua amepanga kumnunulia mtoto wake chakula na yeye

Kwahiyo umemnusuru mwanao kwa kuumiza mtoto wa mwingine hiyo ni sawa huoni ni ubinafsi tena unaoumiza wengine?

Kwa nini usichukue hatua ukaomba

NB : Wizi ni Wizi tu hata ukipakwa rangi kwa sababu huacha maamivu kwa wengine
 
Wema na ubaya ni mitazamo tu. Kimsingi kabisa hakuna jema wala baya, kila kiumbe kinapambania uhai wake.

Binadamu tumetunga dhana za wema na ubaya ili tuweze kuishi pamoja. Na sheria ndiyo inayotuchorea mstari kwamba ni wapi tusivuke.

Angalia suala la tamaduni. Kuna tamaduni ambazo watoto wa kike kuolewa ni sawa. Labda tamaduni hizo zinapendelea uzao mwingi hivyo wanawake huolewa mapema ili wazae zaidi.

Hisia, matamanio, maarifa na hali tunazopitia vinatufanya tuwe jinsi tulivyo.
 
Back
Top Bottom