Human Nature

Human Nature

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
19,850
Reaction score
46,605
Hello Great thinkers 🫡

Mwanadamu ana baadhi ya mambo ambayo huwa yanatokea ndani yake bila yeye kuyapanga au kuyachagua kwa makusudi(Unakubaliana na mimi?)

Hayo tunaweza kuyaita Human Nature asili ya mwanadamu

Mfano:

Kupenda : binadamu anaweza kujikuta anampenda mtu au kitu bila hata kupanga kukipenda
Hii ni sehemu ya nature ya mwanadamu

Kutamani: kutamani mtu au kitu, mafanikio maisha bora au kupata zaidi ni jambo ambalo linaweza kutokea naturally ndani ya mwanadamu

Kukosea kwa kawaida hua tunasema kwamba mwanadamu si perfect 💯
Ikiwa na maana kukosea haiepukiki

Kukosea ni sehemu ya maisha na ni sehemu ya asili ya mwanadamu
Mimi tangu nazaliwa nimekuta huo msemo


Kuhisi maumivu unapoumizwa, ni natural kuhisi maumivu
Huwezi kila wakati kuamua kwamba sitahisi au sitaumia ni ngumu kudhibiti hisia za maumivu kwa sababu huja natural

Huo ni upande mmoja wa Human Nature ambao tunaweza kuuita positive (chanya)

Lakini vipi 👇
Human Nature inaweza kuwa negative?

Kwa sababu kama binadamu anaweza kupenda anaweza pia kuchukia

Kwahiyo hapa tutasema chuki nayo ni sehemu ya human Nature?

Anaweza kuwa na wivu
MF: ameona mtu kamzidi kitu fulani akaingiwa na wivu gafla bila kupanga

Anaweza kutamani kitu vitu bila kupanga ni hisia tu zinamjia

Anaweza kukosea
Kuwa m binafsi

Najiuliza je, haya mambo nayo ni sehemu ya human nature?

Ikiwa baadhi ya hisia na impulses zinatokea naturally ndani ya mwanadamu je kuwa na hisia hizo kunamaanisha kwamba lazima uzifanyie kazi?

Yaani uwe selfish kwa wengine...

Uumize wengine pengine kwa sababu una history ya maumivu kwa kisingizio una hisia za maumivu

Uachonganishe watu...

Uchukie watu..

Uwe mtu anayefanya dunia isiwe salama kuishi kwa kisingizio kwamba hii ni human nature na kwamba hizo ni tabia zisizoepukika?

Utasikia kawaida binadamu sisi hatupendani hapo mtu anatafuta kuhalalisha mabaya anayofanya kwa watu wengine

Ex:👇

Kuna tabia moja ambayo sisi wanadamu tunayo
Mtu anakosea dhahiri, lakini anapofika kwenye kuomba msamaha hawezi kusema tu

JAMANI imekosea naomba nisamehewe

Badala yake anakimbilia kusema

Mimi ni binadamu, hakuna binadamu mkamilifu

Hii huwa naiona kama ina kiburi fulani ndani yake

Kwa nini usikubali tu kwamba umekosea na uombe radhi, bila kuambatanisha sababu ya kuhalalisha kosa lako?

Kwa maoni yangu binafsi, nakubali kabisa kwamba wakati mwingine kuna hisia zinaweza kukuingia bila hata kupanga

Labda ukapatwa na wivu

Labda ukakasirika

Labda ukahisi chuki

Lakini pamoja na yote hayo, huwezi kuendekeza hizo hisia zako kwa sababu tu zimekuja naturally

Wakati mwingine mtu ana uwezo wa kuzikataa hisia hasi zenye uharibifu, hasa zile ambazo hazina faida kwake wala kwa wengine

Naamini sio kila kitu unachohisi unapaswa kukiweka kwenye akili na kukifanyia kazi mara moja

Kuna tofauti kati ya kuhisi kitu na kuchagua kufanya kitu kwa sababu umehisi

Unaweza kuwa na wivu bila kumdhuru mtu

Unaweza kuwa na hasira bila kumtukana mtu

Unaweza kuumia bila kuamua kuwaumiza wengine

Unaweza kuhisi chuki bila kugeuza chuki hiyo kuwa tabia yako

Mwanadamu yeyote anaweza kuwa mtu mzuri sana bila kuwa kikwazo kwa wengine, pale tu anapojifunza ku.control hisia zake negative na kuchagua kwa busara jinsi ya kuzitendea kazi

Kwa sababu mwisho wa siku, hisia zinaweza kutokea naturally, lakini matendo ni choice

Dunia ingekuwa sehemu nzuri zaidi kama wote tungetumia Human Nature yetu kwa upande wa positive

Karibu kwenye mada
Blue Monday 💙

ShesRise_1 🤚
 
Welcome back ShesRise_1

Hili ni swali zuri sana, kwa sababu linatugusa kwenye mpaka kati ya kile tunachohisi naturally na kile tunachochagua kuwa

Nakubaliana na msingi wa hoja yako, sio kila hisia tunayoipata ni matokeo ya uamuzi wetu, Kuna emotions na impulses ambazo hujitokeza ndani yetu kabla hata hatujapata muda wa kuzipangilia, let's say wivu, hasira, attraction, hofu, maumivu, hata chuki.

Human Nature inaweza kueleza kwa nini tunahisi kitu, lakini haiwezi kuwa justification ya kila kitu tunachofanya kwa sababu ya hisia hiyo

Hisia inaweza kuwa natural; matendo bado yanahitaji uchaguzi. Kwa kiasi kikubwa

Na labda hapa ndipo swali kubwa zaidi linapoanzia:

Kama hatuchagui kila hisia inayotokea ndani yetu, lakini tunachagua namna ya kuitendea kazi je, tunapaswa kumhukumu mtu kwa hisia aliyonayo, au kwa maamuzi anayofanya akiwa na hisia hiyo? Na kama tunajua impulse fulani inaweza kuwa destructive, ni wakati gani responsibility yetu inaanza pale tunapoihisi, au pale tunapoamua kuifuata? 🤔
 
Kila mtu ni mbinafsi, Ila kuna wenye ubinafsi wa kushikilia vyao huku wakitamani na chako kiwe chao
Hakika kwa asili binadamu ni mbinafsi
Lakini kutaka vya wengine viwe miliki yako pia huo sio ubinafsi wa kawaida
Hii ni roho mbaya
Wengi ni wazuri wa sura na tabasamu pana ila moyoni hawatotamani uitwe mwamba
Watu wote tungeweza kua na kiasi kufanya mambo dunia ingekua nzuriii😊
 
Wanafalsafa ya ustoa tunajua njisi ya kucontrol human nature hatuwezi kuumizwa na yeyote wala hatuwezi kumuonea wivu yeyote, hatujitetei kama nyeupe, nyeupe kama nyeusi, nyeusi.
Hatumuumizi mtu. Wala hatuna tamaa.
Misingi yetu ni HAKI/USAWA, HEKIMA/AKILI,UJASIRI, UADILIFU, NIDHAMU, na UKWELI.
 
Back
Top Bottom