Human Nature

Human Nature

Haya leo ni mwendo wa masong tu

Welcome back mtoa mada
I'm back 🔥🔥🔥🔥
Ma song ya motoooo
Halafu ngoma zote ni vitu vyangu kabisa 🔥🔥🔥🔥
Say yeeeeeeeeee! Nice to hear that,karibu sana
Software hiyo ni dira yako ya kimaadili ama dhamira yako. Hii inatokana na malezi kuanzia ulipokuwa mdogo kabisa mpaka unapojitambua.

Ukitaka ujue malezi ni muhimu, binadamu waliolelewa na wanyama(feral humans) wanakosa kabisa hii dhamira.

Wengi watasema Mungu yupo, na ana mpango wake wa kuadhibu mabaya na kutukuza mema lakini mbona kuna mabaya mengi tu yanaachwa kama yalivyo, na kuna mema yanaadhibiwa? Nafikiri hayupo.

Suala dogo tu linalothibitisha kuwa maadili ni mtazamo ni suala la mahusiano ya jinsia moja. Ukienda magharibi mwa dunia, wengi wanaona ni sawa na kawaida. Ukienda mashariki, ni kinyume chake. Unafikiri ni kwanini?
Mimi bado nitakuwa na mtazamo tofauti na wewe

Bado nakuja pale pale kwenye ndani ya nafsi zetu,mfano binadamu wote tumeumbwa na nafsi ambayo inatuambia au kuhisi kuna nguvu zaidi yetu ambayo ndio kimbilio letu pale tunapotaka msaada au kutatua shida zetu

Wengine wanaita Mungu,wengine mizimu,wengine wanajua wanavyoita

Ndio maana kuna wanaobudu kwenye miti mikubwa,wengine kwenye mapango na wengine,jua na kadhalika,hii ni kuonyesha kwamba nafsi za binadamu zinatambua kuna nguvu ambayo ndio kimbilio lao

Sasa mazingira ndio huwa shape watu ama kubakia kwenye ile nafsi ya asili ambayo inatambua jema na baya au kuwapa kitu kipya ambacho kitawatoa kwenye uhasilia wao

Ndio ile mfano ulio toa sasa,binadamu sasa anatambulishwa kwenye system nyingine ya maisha ya kuwa na uhusiano wa jinsia moja,mazingira yana nafasi kubwa sana ya kubadilisha tabia na mienendo ya watu

Sasa kile ambacho ndio binadamu atakuwa anakutana nacho mara kwa mara ndio kitaamua awe ni mtu wa namna gani
 
Mkuu hivi unajua mnajiendekeza tu nyie?
Nani aliwadaganya wanaume eti nyie ndio mna tamani peke enu?

Mnajidanganya wenyewe na kutafuta kuhalalisha umalayer wenu tu

Niwe mkweli leo hata wanawake wanatamani kama mlivyo nyie
Na hii mtu aje ani prove wrong hapa

Issue ni kwamba nyie mmebebwa na hisia na kwa vile mlishahalalisha hilo jambo na kuliguza halali ndio hivyo kama unavyosema hapo

Mwishoni kwenye mada nimesema Issue sio kutamani kwa sababu ni hisia za gafla Issue ni maamzi yako baada ya hizo hisia za kibinadamu kukuvaa bila taarifa
Mdada to cut the story si unajua tuna vichwa viwili,sasa Saidi Kipara akifanya maamuzi ni ngumu kuyakwepa
20250818_222514.jpg
 
Nikichangia mada,naweza sema ni kweli kabisa hisia na baadhi ya mambo ambayo tunaishi nayo ni asili ya binadam

Yapo tu na hatuna namna ya kufanya tusiyahisi au Kuya experience

Lakini uwezo wa kuyadhibiti tunao,sawa ntahisi wivu labda juu ya maendeleo ya mtu fulani,na kupelekea kujisikia kumharibia michongo yake,lakini naweza kuchagua kutomharibia,naweza kuchagua kukaa kimya,huo uwezo upo ndani ya mamlaka yetu

Tunaweza hisi chuki ndani ya nafsi zetu juu ya watu fulani au mtu fulani,lakini tunaweza kuchagua kutofanya uamuzi wowote wa kutomdhuru huyo mtu au hao watu

Kwahiyo kama binadamu tumepewa uwezo mkubwa sana kutafakari mambo na kuyapima ndani nje

Je,hili ninalo taka kulifanya lina maslahi gani na mimi? Je mwisho wake utakuwaje

Sasa tukishawaza kwa namna hii,basi mwisho wa siku tutafanya yale ambayo yana maslahi na sisi
Hakika hakika
 
😅😅😅 nicheke kwanza et hakuna wema na ubaya

Unajua dunia inaenda kwa kanuni?
Kama unaamini dunia inaenda kwa kanuni basi kwenye kanuni hizo ndio unapatikana wema na ubaya

Kwa kanuni tu
Tumechagua kinachoumiza au kitu hasi basi ndio ubaya wenyewe

Kitu kizuri kisicholeta hisia za maumivu ndio wema wenyewe

Hayo yote ni kwa mkutadha unaokuwepo wakati huo
Sijui hata unaongelea nini hapa mkuu issu ni kua hakuna uhalali wa kuumiza mwingine ili wewe ufurahi

Ikiwa hivyo dunia hii itakua jehanamu
Na hata hivyo dunia baadhi ya sehemu zake mpaka sasa zimegeuka moto kwa sababu ya umimi uliopindukia
Akili zetu huchagua zaidi yale yaliyo mepesi na haraka kwetu. Hii inaweza kuwa kwa ajili ya kujilinda ama kupata faida flani.

Hizo "kanuni" tulizitunga sisi wenyewe wakati tunaanza kuishi kimakundi enzi hizo ili tusifarakane hovyo.

Lengo la kanuni sio kutubadilisha, ni kutudhibiti. Hatuwezi kubadilika, ila kuna wale ambao hupoteza utimamu wao, ama hushawishika kufanya mambo hatarishi sana mfano kuua watu. Kanuni/sheria zinasaidia kuwakabili hawa.
 
Hello Great thinkers 🫡

Mwanadamu ana baadhi ya mambo ambayo huwa yanatokea ndani yake bila yeye kuyapanga au kuyachagua kwa makusudi(Unakubaliana na mimi?)

Hayo tunaweza kuyaita Human Nature asili ya mwanadamu

Mfano:

Kupenda binadamu anaweza kujikuta anampenda mtu au kitu bila hata kupanga kukipenda
Hii ni sehemu ya nature ya mwanadamu

Kutamani kutamani mtu kitu, mafanikio maisha bora au kupata zaidi ni jambo ambalo linaweza kutokea naturally ndani ya mwanadamu

Kukosea kwa kawaida hua tunasema kwamba mwanadamu si perfect 💯
Ikiwa na maana kukosea haiepukiki

Kukosea ni sehemu ya maisha na ni sehemu ya asili ya mwanadamu
Mimi tangu nazaliwa nimekuta huo msemo

Kuhisi maumivu unapoumizwa, ni natural kuhisi maumivu
Huwezi kila wakati kuamua kwamba sitahisi au sitaumia ni ngumu kudhibiti hisia za maumivu kwa sababu huja natural

Huo ni upande mmoja wa Human Nature ambao tunaweza kuuita positive (chanya)

Lakini vipi 👇
Human Nature inaweza kuwa negative?

Kwa sababu kama binadamu anaweza kupenda anaweza pia kuchukia

Kwahiyo hapa tutasema chuki nayo ni sehemu ya human Nature?

Anaweza kuwa na wivu
MF: ameona mtu kamzidi kitu fulani akaingiwa na wivu gafla bila kupanga

Anaweza kutamani kitu vitu bila kupanga ni hisia tu zinamjia

Anaweza kukosea
Kuwa m binafsi

Najiuliza je, haya mambo nayo ni sehemu ya human nature?

Ikiwa baadhi ya hisia na impulses zinatokea naturally ndani ya mwanadamu je kuwa na hisia hizo kunamaanisha kwamba lazima uzifanyie kazi?

Yaani uwe selfish kwa wengine...

Uumize wengine pengine kwa sababu una history ya maumivu kwa kisingizio una hisia za maumivu

Uachonganishe watu...

Uchukie watu..

Uwe mtu anayefanya dunia isiwe salama kuishi kwa kisingizio kwamba hii ni human nature na kwamba hizo ni tabia zisizoepukika?

Utasikia kawaida binadamu sisi hatupendani hapo mtu anatafuta kuhalalisha mabaya anayofanya kwa watu wengine

Ex:👇

Kuna tabia moja ambayo sisi wanadamu tunayo
Mtu anakosea dhahiri, lakini anapofika kwenye kuomba msamaha hawezi kusema tu

JAMANI imekosea naomba nisamehewe

Badala yake anakimbilia kusema

Mimi ni binadamu, hakuna binadamu mkamilifu

Hii huwa naiona kama ina kiburi fulani ndani yake

Kwa nini usikubali tu kwamba umekosea na uombe radhi, bila kuambatanisha sababu ya kuhalalisha kosa lako?

Kwa maoni yangu binafsi, nakubali kabisa kwamba wakati mwingine kuna hisia zinaweza kukuingia bila hata kupanga

Labda ukapatwa na wivu

Labda ukakasirika

Labda ukahisi chuki

Lakini pamoja na yote hayo, huwezi kuendekeza hizo hisia zako kwa sababu tu zimekuja naturally

Wakati mwingine mtu ana uwezo wa kuzikataa hisia hasi zenye uharibifu, hasa zile ambazo hazina faida kwake wala kwa wengine

Naamini sio kila kitu unachohisi unapaswa kukiweka kwenye akili na kukifanyia kazi mara moja

Kuna tofauti kati ya kuhisi kitu na kuchagua kufanya kitu kwa sababu umehisi

Unaweza kuwa na wivu bila kumdhuru mtu

Unaweza kuwa na hasira bila kumtukana mtu

Unaweza kuumia bila kuamua kuwaumiza wengine

Unaweza kuhisi chuki bila kugeuza chuki hiyo kuwa tabia yako

Mwanadamu yeyote anaweza kuwa mtu mzuri sana bila kuwa kikwazo kwa wengine, pale tu anapojifunza ku.control hisia zake negative na kuchagua kwa busara jinsi ya kuzitendea kazi

Kwa sababu mwisho wa siku, hisia zinaweza kutokea naturally, lakini matendo ni choice

Dunia ingekuwa sehemu nzuri zaidi kama wote tungetumia Human Nature yetu kwa upande wa positive

Karibu kwenye mada
Blue Monday 💙

ShesRise_1 🤚
Mkuu karibu tena na Asante kwa maada mujarabu.

Binafsi nitatumia mtazamo wa kiimani ili kujibu hii hoja.

Mungu alipoumba dunia aliumba mambo mema na mabaya lakini pia alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua kati ya mema na mabaya. Kumbukumbu ya torati 30:15,19

Tukiongelea mambo mema na mambo mabaya hii inakua ni jambo la asili. Lakini binadamu kufanya jambo jema au baya hiyo siyo asili bali ni chaguo ambalo mtu ameamua kulitenda kwa akili zake.

Hivyo nahitimisha kwa kusema matendo yote mabaya au mema ni matokeo ya mtu kuchagua kuyatenda hayo wala sio human nature au sijui bahati mbaya. Hayo yote ni machaguo ya mtu mwenyewe.
 
F
Hello Great thinkers 🫡

Mwanadamu ana baadhi ya mambo ambayo huwa yanatokea ndani yake bila yeye kuyapanga au kuyachagua kwa makusudi(Unakubaliana na mimi?)

Hayo tunaweza kuyaita Human Nature asili ya mwanadamu

Mfano:

Kupenda : binadamu anaweza kujikuta anampenda mtu au kitu bila hata kupanga kukipenda
Hii ni sehemu ya nature ya mwanadamu

Kutamani: kutamani mtu au kitu, mafanikio maisha bora au kupata zaidi ni jambo ambalo linaweza kutokea naturally ndani ya mwanadamu

Kukosea kwa kawaida hua tunasema kwamba mwanadamu si perfect 💯
Ikiwa na maana kukosea haiepukiki

Kukosea ni sehemu ya maisha na ni sehemu ya asili ya mwanadamu
Mimi tangu nazaliwa nimekuta huo msemo

Kuhisi maumivu unapoumizwa, ni natural kuhisi maumivu
Huwezi kila wakati kuamua kwamba sitahisi au sitaumia ni ngumu kudhibiti hisia za maumivu kwa sababu huja natural

Huo ni upande mmoja wa Human Nature ambao tunaweza kuuita positive (chanya)

Lakini vipi 👇
Human Nature inaweza kuwa negative?

Kwa sababu kama binadamu anaweza kupenda anaweza pia kuchukia

Kwahiyo hapa tutasema chuki nayo ni sehemu ya human Nature?

Anaweza kuwa na wivu
MF: ameona mtu kamzidi kitu fulani akaingiwa na wivu gafla bila kupanga

Anaweza kutamani kitu vitu bila kupanga ni hisia tu zinamjia

Anaweza kukosea
Kuwa m binafsi

Najiuliza je, haya mambo nayo ni sehemu ya human nature?

Ikiwa baadhi ya hisia na impulses zinatokea naturally ndani ya mwanadamu je kuwa na hisia hizo kunamaanisha kwamba lazima uzifanyie kazi?

Yaani uwe selfish kwa wengine...

Uumize wengine pengine kwa sababu una history ya maumivu kwa kisingizio una hisia za maumivu

Uachonganishe watu...

Uchukie watu..

Uwe mtu anayefanya dunia isiwe salama kuishi kwa kisingizio kwamba hii ni human nature na kwamba hizo ni tabia zisizoepukika?

Utasikia kawaida binadamu sisi hatupendani hapo mtu anatafuta kuhalalisha mabaya anayofanya kwa watu wengine

Ex:👇

Kuna tabia moja ambayo sisi wanadamu tunayo
Mtu anakosea dhahiri, lakini anapofika kwenye kuomba msamaha hawezi kusema tu

JAMANI imekosea naomba nisamehewe

Badala yake anakimbilia kusema

Mimi ni binadamu, hakuna binadamu mkamilifu

Hii huwa naiona kama ina kiburi fulani ndani yake

Kwa nini usikubali tu kwamba umekosea na uombe radhi, bila kuambatanisha sababu ya kuhalalisha kosa lako?

Kwa maoni yangu binafsi, nakubali kabisa kwamba wakati mwingine kuna hisia zinaweza kukuingia bila hata kupanga

Labda ukapatwa na wivu

Labda ukakasirika

Labda ukahisi chuki

Lakini pamoja na yote hayo, huwezi kuendekeza hizo hisia zako kwa sababu tu zimekuja naturally

Wakati mwingine mtu ana uwezo wa kuzikataa hisia hasi zenye uharibifu, hasa zile ambazo hazina faida kwake wala kwa wengine

Naamini sio kila kitu unachohisi unapaswa kukiweka kwenye akili na kukifanyia kazi mara moja

Kuna tofauti kati ya kuhisi kitu na kuchagua kufanya kitu kwa sababu umehisi

Unaweza kuwa na wivu bila kumdhuru mtu

Unaweza kuwa na hasira bila kumtukana mtu

Unaweza kuumia bila kuamua kuwaumiza wengine

Unaweza kuhisi chuki bila kugeuza chuki hiyo kuwa tabia yako

Mwanadamu yeyote anaweza kuwa mtu mzuri sana bila kuwa kikwazo kwa wengine, pale tu anapojifunza ku.control hisia zake negative na kuchagua kwa busara jinsi ya kuzitendea kazi

Kwa sababu mwisho wa siku, hisia zinaweza kutokea naturally, lakini matendo ni choice

Dunia ingekuwa sehemu nzuri zaidi kama wote tungetumia Human Nature yetu kwa upande wa positive

Karibu kwenye mada
Blue Monday 💙

ShesRise_1 🤚
Finally, somebody has resurfaced after disappearing misteriously for a short while.
 
Akili zetu huchagua zaidi yale yaliyo mepesi na haraka kwetu. Hii inaweza kuwa kwa ajili ya kujilinda ama kupata faida flani.

Hizo "kanuni" tulizitunga sisi wenyewe wakati tunaanza kuishi kimakundi enzi hizo ili tusifarakane hovyo.

Lengo la kanuni sio kutubadilisha, ni kutudhibiti. Hatuwezi kubadilika, ila kuna wale ambao hupoteza utimamu wao, ama hushawishika kufanya mambo hatarishi sana mfano kuua watu. Kanuni/sheria zinasaidia kuwakabili hawa.
Shukran sana
Kanuni tulizipanga wenyewe kwa utashi na kwa kuzingatia asili ya mwanadamu

Tumetunga kanuni ya adhabu kwa mtu aliemuua mwingine ili iwe fundisho watu wasichukulie kawaida kuuana

Kwahiyo dunia bila kanuni
Ingekua mbaya zaidi

Kama ulivyosema awali kua mzazi kuiba kwa ajili ya mwanae ni kukosa option
Na ukajaribu kuhalalisha kua hakua na chaguo

Na kumbe wakati huo huo ameiba chakula kilichohifadhiwa kwa ajili ya mtoto mwingine kwahiyo amepeleka maumivu kwa mwingine

Kitu ambacho sio sawa
Kwa sababu kinaponya hapa kinajeruhi kule kwa mantiki hiyo akibainika atawajibishwa hata kama atajitetea mwanae alikua na njaa wala hakuna huruma juu yake

Kwa sababu bado angeweza kuomba kuliko kuiba
 
Mkuu karibu tena na Asante kwa maada mujarabu.
Shukran sana mkuu nimekaribia
Binafsi nitatumia mtazamo wa kiimani ili kujibu hii hoja.

Mungu alipoumba dunia aliumba mambo mema na mabaya lakini pia alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua kati ya mema na mabaya. Kumbukumbu ya torati 30:15,19

Tukiongelea mambo mema na mambo mabaya hii inakua ni jambo la asili. Lakini binadamu kufanya jambo jema au baya hiyo siyo asili bali ni chaguo ambalo mtu ameamua kulitenda kwa akili zake.

Hivyo nahitimisha kwa kusema matendo yote mabaya au mema ni matokeo ya mtu kuchagua kuyatenda hayo wala sio human nature au sijui bahati mbaya. Hayo yote ni machaguo ya mtu mwenyewe.

Yaan huku ulipokuja tutahamisha mada mkuu yaani kulikua na mantiki ipi
Mungu aumbe mabaya?
Kwa faida ipi?
Kwa lengo gani?
 
Wanafalsafa ya ustoa tunajua njisi ya kucontrol human nature hatuwezi kuumizwa na yeyote wala hatuwezi kumuonea wivu yeyote, hatujitetei kama nyeupe, nyeupe kama nyeusi, nyeusi.
Hatumuumizi mtu. Wala hatuna tamaa.
Misingi yetu ni HAKI/USAWA, HEKIMA/AKILI,UJASIRI, UADILIFU, NIDHAMU, na UKWELI.
Ukiweza hivi maisha yanakua matamuu mnoo
 
Struggle for Existence and survival of the fittest! Mambo mengi anayofanya binadamu yamefumwa katika kanuni hii; na karibu kila kitu anachofanya kwa namna moja au nyingine kimelengwa katika kumnufaisha yeye. Na kwa vile ulimwengu umefinyangwa kwa kufuata kanuni ya hasi na chanya kama pande mbili za kitu kile kile (matter vs. antimatter), wema na ubaya unakwenda pamoja katika harakati zake za struggle for Existence and survival of the fittest. Hata anapopambana kupunguza makali ya entropy ili aendelee kuishi kwa raha na kwa muda mrefu inavyowezekana, hawezi kuepuka kanuni ya hasi na chanya maana ndiyo inaendesha mfumo mama wa maisha yake.

Huyu ndiye Homo Sapiens! Mnyama mtata, hatari na changamano kuliko wote!
Homo Sapiens big 🧠
 
Mimi bado nitakuwa na mtazamo tofauti na wewe

Bado nakuja pale pale kwenye ndani ya nafsi zetu,mfano binadamu wote tumeumbwa na nafsi ambayo inatuambia au kuhisi kuna nguvu zaidi yetu ambayo ndio kimbilio letu pale tunapotaka msaada au kutatua shida zetu

Wengine wanaita Mungu,wengine mizimu,wengine wanajua wanavyoita

Ndio maana kuna wanaobudu kwenye miti mikubwa,wengine kwenye mapango na wengine,jua na kadhalika,hii ni kuonyesha kwamba nafsi za binadamu zinatambua kuna nguvu ambayo ndio kimbilio lao

Sasa mazingira ndio huwa shape watu ama kubakia kwenye ile nafsi ya asili ambayo inatambua jema na baya au kuwapa kitu kipya ambacho kitawatoa kwenye uhasilia wao

Ndio ile mfano ulio toa sasa,binadamu sasa anatambulishwa kwenye system nyingine ya maisha ya kuwa na uhusiano wa jinsia moja,mazingira yana nafasi kubwa sana ya kubadilisha tabia na mienendo ya watu

Sasa kile ambacho ndio binadamu atakuwa anakutana nacho mara kwa mara ndio kitaamua awe ni mtu wa namna gani
Ujue hapa wewe na mshamba_hachekwi hamtaelewana
Maana hapa umeshaingiza dini na yeye sidhani kama ni vitu vyake
 
Ukiweza hivi maisha yanakua matamuu mnoo
siku ukiacha kutafsiri mambo au vitu kwamba hili baya au nzuri unaweza kuishi maisha ya raha sana binafsi siamini kama kuna mtu anaweza kuniumiza au kunipa furaha tofauti na mim.
DUNIANI hakuna jambo baya wala nzuri ni mtazamo wako tu unaomuumiza mtu mfano mzuri unakuja kuabiwa fulani alikuwa anakuogea vibaya unaumia kabla hujajua why hukuumia lakn ukichukulia kawaida kama unavyolichukulia jiwe huwezi kuumia.
 
Duniani hakuna jambo baya au zuri?
Ukimuibia mtu ni nini inakua ?

Ukimkata mkono mtu mwingine ni nini hiyo inakua?

Dunia ipi hiyo haina baya wala zuri nikaishi?
 
nikuulize swali jepesi tu kabla sijakujibu
Ni jambo lipi ambalo binadamu wote tunaamini ni nzuri au baya?.
Kwamba ili jambo ukifanya kila mtu anaamini ni nzuri?
 
Jambo lolote lile linaloacha hisia za maumivu tunaliita baya

Labda kama wewe una jina lingine
Haya ni nijib na mimi
 
Back
Top Bottom