Status
Not open for further replies.
Habar wana JF,

Nimepita mtaani kwetu huku nikiwa napiga mishe za hapa na pale,

Nimegundua kuwa kila mfanya biashara kaweka maji na sanitizer kwenye eneo lake kwa ajili ya wateja wake kunawa mikono kwa kujikinga na hili janga la Corona.

Lakini cha kusikitisha ni pale watu/wateja wanayapita maji hayo bila kunawa na wengine wakihimizwa kunawa wanakataa kabisa.

Iki ndo tunakiita KIBURI au ndo tamaduni zetu Watanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
oscar classic, Wakati mimi naenda kunawa nikifungua ile koki ya maji kama nina corona si nawaacha hapo kwenye koki ?

Na nikifunga koki baada ya kunawa nawachukua tena corona wangu na wengine nawaacha ?

Anaekuja kunawa atasalimika vipi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nini na nini boss?
Usafi wa salon unajulikana..
Sterilizer, Spirit, usafi wa vitendea kazi naofisi kwa ujumla..

Hivi bado havitoshi kukukinga kwa korona ila magonjwa ya ngozi ambayo ndio hatarishi kwa salon.

Cha ziada kwa korona kwenye ma salon..
Ni maji ya kunawia/sanitizer/sabuni, ambavyo popote sasahv n muhimu.

Mask nazo pia, japo kiutaratibu Kinyozi anatakiwa avae mask, kwaio sio suala geni, na hata anae nyolewa salon inashauliwa avae mask.

Sasa sijajua ni kipi unazungumzia boss.
 
Naangalia chanel 5 hapa kipindi cha Friday Night Live. Ni kipindi kizuri ila kwa mzaha huu juu ya huu ugonjwa kwa kweli mnatuangusha.

Waandaaji hamjajipanga na hamna plan yoyote ya kupambana na corona. Mnaacha washiriki wanashirikiana mike, wanashikana, wanasogeleana, n.k.

Hakika kama kuna mwenye ugonjwa hapo utasambaa kijinga sana na kituo chenu msishangae kikawekwa karantini. Ni hayo tu kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom