Wizara ya Afya yasema kuna ongezeko la wagonjwa wa COVID-19 na Virusi vya Mafua

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Wizara ya Afya imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa taarifa za magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na tetesi za kuwepo kwa magonjwa hayo ndani na nje ya nchi. Katika kipindi cha kuanzia mwezi Novemba, 2023 kumekuwa na tetesi juu ya ongezeko la visa vya magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa sehemu mbalimbali duniani na ndani ya nchi hususani katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Ndugu Wananchi, Wizara kwa kutumia mifumo yake, imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa ya mfumo wa hewa ili kubaini mwenendo au ongezeko; kutambua kwa haraka uwezekano wa uwepo kirusi kipya. Virusi vinavyofuatiliwa kwa ukaribu na Wizara ni pamoja na virusi vinavyo sababisha UVIKO- 19, virusi vya mafua vya aina ya influenza na vimelea vingine kutokana na uhitaji.

Ndugu Wananchi, Magonjwa ya mumo wa njia ya hewa yamekuwepo hapa nchini wakati wote. Aidha, kumekuwapo na vipindi vya kuongezeka na kupungua kwa visa hivi kwa vipindi tofauti katika mwaka.

Ugonjwa wa UVIKO-19, umeendelea kuwepo kwa kiwango cha chini kama magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa ukiongezeka na kupungua kwa nyakati tofauti za majira ya mwaka. Aidha, virusi vya Influenza vilivyobainika hapa chini havina madhara makubwa ndio sababu iliyopelekea kuitwa ugonjwa wa majira (Seasonal Influenza).

Hata hivyo, takwimu za ufualitiliaji (surveilance) za wizara zinaonesha ongezeko la visa vya ugonjwa wa UVIKO-19 toka visa 37 mwezi Oktoba 2023 na hadi visa 65 mwezi Desemba 2023. Aidha, ongezeko hili ni sambamba na ongezeko la visa vya mafua yanayotokana na influenza kutoka visa 34 hadi 49 katika kipindi hicho hicho. Aidha, mwenendo huu wa ongezeko la visa vya magoniwa haya ulionekana pia katika kipindi.

kama hiki kwa mwaka 2022. Mwaka 2022, visa vya UVIKO-19 viliongezeka toka 15 (Oktoba) hadi kufikia 65 (Disemba), wakati Influenza vilikuwa visa 2 hadi 59 katika kipindi hicho hicho.

Ndugu Wananchi, Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa magonywa ya fumo wa njia ya hewa na inaelekeza wataalam katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya kuendelea kufanya utambuzi kwa njia ya vipimo vya maabara na kutoa matibabu stahiki. Vilevile, Wizara inashauri wananchi kuwahi kwenye Vituo vya kutolea huduma mara wapatapo dalili za magonjwa ya mumo wa njia ya hewa Zikiwemo mafua, kikohozi, kuwashwa koo, kupumua kwa shida, homa na kuumwa kichwa. Aidha, wizara inatoa rai kwa wananchi wote kuzingatia kanuni za afya ikiwa ni pamoja na:-
  • Kutoshikana mikono ikiwa si lazima kufanya hivyo.
  • Kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vipukusi mara kwa mara
  • Usafi binafsi na mazingira.
  • Kufunika pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya pamoja na kuvaa barakoa pale inapohitajika.
  • Kupata chanjo kamili ya UVIKO-19 kwa wote ambao hawajachanja au kukamilisha chanjo.
Ndugu Wananchi, Tuwatoe hofu, kwani Serikali ya Awamu ya sita kupitia Wizara ya Atya inaendelea kufuatilia na kudhibiti magonjwa ya milipuko kwa kupitia mifumo madhubuti iliyopo chini. Wizara itaendelea kutoa taarifa kwa
wananchi pale itakapohitajika kufanya hivyo.

20231213_204150.jpg
20231213_204143.jpg
 
Nitarudi....

Siku ya tatu Leo....Na ndiyo imekuwa na afadhali.

Ila Bado hamu ya chakula hakuna...Juice fresh ya embe na Grand malt ndiyo chakula changu.
 
Bado wanaogopa kusema Covid19 wanafikiri kuna mtu atafufuka na kuja kuwashushia msala?😆😂

Kama Covid 19 waseme tu ni yenyewe "ati changamoto ya kupumua"

Mahokaa...😂😂😂😂😂😂😂
 
Hawa majamaa kinawauma sana sisi kula Pesa yao na wala hatukukaa quarantine Wana tafuta namna ya kutuweka watanzania quarantine hivo tuwapuuze
GBNIbjvWsAAm8_Q.jpeg
 
Back
Top Bottom