#COVID19 China yaidhinisha Chanjo ya COVID-19 inayotolewa kupitia pua

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
Kwa mara ya kwanza duniani, nchi ya China imeidhinisha matumizi ya chanjo ya kupambana na ugonjwa wa COVID-19 inayotolewa kwa njia ya kuvuta kiasi kidogo cha dozi kupitia pua.

Chanjo hiyo iliyopewa jina la CaSino's Ad5-nCoV imetengenezwa kwa kutumia adenovirus, aina ya virusi waliopoozeshwa na kupewa vinasaba vyenye sifa ya kuufundisha mwili jinsi ya kujilinda.

Taarifa za majaribio ya kitabibu zinaielezea kuwa na ufanisi wa asilimia 66 katika kukinga maambukizi ya ugonjwa pamoja na kuzuia athari za kushambuliwa vikali na vimelea vya COVID-19 kwa asilimia 91.

CaSino's Ad5-nCoV itaondoa adha ya kutumia sindano, pia itatoa ahueni ya haraka kwa watu kwa kuwa uvutaji wa kiasi kidogo tu cha hewa yake unatosha kabisa kutoa kinga kusudiwa.

Bloomberg
 
Kwa mara ya kwanza duniani, nchi ya China imeidhinisha matumizi ya chanjo ya kupambana na ugonjwa wa COVID-19 inayotolewa kwa njia ya kuvuta kiasi kidogo cha dozi kupitia pua.
Huenda wametuiga, sisi si ndiyo tulikuwa wa kwanza kujivukiza halafu wakatucheka!?
 
Back
Top Bottom