ki2c
JF-Expert Member
- Jan 17, 2016
- 7,096
- 13,036
Umenena vyema.Mkuu nadhani wewe ndoa yako ni changa haijavuka miaka 10.
Ndoa za umri huo ndiyo zina mambo hayo mengi.
Nikwambie sasa, mwanamke hata kama ni mrembo kumzidi Cleopatra ukamuoa, kadri siku zinavyosonga ndivyo kwako anavyokuwa "garasa"!
Ajirembe ajirembueje, siku zinavyozidi kusonga ndivyo kwako anavyozidi kuwa "dada".
Na mkazaa watoto wa kutosha, mshajenga maisha yenu pamoja na kutimiza ndoto zenu zingine, mkeo anageuka kuwa ni ndugu!
Urembo na mvuto wake utaonwa na wengine, lakini siyo wewe mwandani wake!
Hakuna ulinganifu wa ndoa changa na ndoa kongwe, ni tofauti kubwa sana iliyopo!
Ninayaongea haya kwa uzoefu.
Ninakumbuka matendo ya miaka ya mwanzoni ya ndoa, namna mke alivyoninyanyasa kwa nyodo kabla sijamuoa, nikatumia nguvu na vitisho vingi mpaka nikampata!
Nilijiapiza kuwa huyu nikifunga naye ndoa nitamfanya mtumwa wa ngono kumkomesha anachoringia!
Kweli tulianza hivyo kwa kumuwashia moto mwingi, lakini leo baba ndoa ina zaidi ya miaka 30, natamani niishi chumba cha peke yangu tukutane asubuhi sebuleni.
Upendo uko pale pale, lakini 'muhu' na kihere here hupotea vyenyewe mnabakia tu kuangaliana!
Wadhani mchezo wewe!
Ndiyo maana ulivyoongea nikahisi kabisa kuwa wewe una ndoa mpya kabisa isiyozidi umri wa miaka 10.
Kwanza bado una "kisirani" cha kufunga magoli huku umemdhibiti kwa kumkunja golikipa asiweze kudaka mashuti yako, yaani ufunge hata magoli ya mkono na uyahalalishe, game gani la hivyo!
Sasa unadhani akikutosheleza kwa hayo uliyoyasema ndiyo utatulizana nyumbani, jambo ambalo haliwezekani.
Kwani ukitamani vya nje, shemeji ana wivu sana kukufuatilia kisogoni kila kona, embu mwache jinsi alivyojichagulia kuishi bhana.
Mambo hayo ya kinamama kubweteka baada ya kuolewa ni jambo la kawaida, si kwako tu, karibia %90 ya wanawake walioko kwenye ndoa ndiyo maisha yao hayo, asikudanganye mtu.
Ndiyo maana wananenepa sana, hata ukiwa barabarani ni rahisi sana kusoma haiba ya mke wa mtu kutokana na siha yake.
Mkuu mpende mkeo kutokana na alivyo.