Hizi Taarifa za Makahaba wengi Dar zinatuchosha mnataka Waondolewe hivi kwa Kero za Wake zetu tutakuwa tunajipoza wapi?

Mkuu nadhani wewe ndoa yako ni changa haijavuka miaka 10.

Ndoa za umri huo ndiyo zina mambo hayo mengi.

Nikwambie sasa, mwanamke hata kama ni mrembo kumzidi Cleopatra ukamuoa, kadri siku zinavyosonga ndivyo kwako anavyokuwa "garasa"!

Ajirembe ajirembueje, siku zinavyozidi kusonga ndivyo kwako anavyozidi kuwa "dada".

Na mkazaa watoto wa kutosha, mshajenga maisha yenu pamoja na kutimiza ndoto zenu zingine, mkeo anageuka kuwa ni ndugu!

Urembo na mvuto wake utaonwa na wengine, lakini siyo wewe mwandani wake!

Hakuna ulinganifu wa ndoa changa na ndoa kongwe, ni tofauti kubwa sana iliyopo!

Ninayaongea haya kwa uzoefu.

Ninakumbuka matendo ya miaka ya mwanzoni ya ndoa, namna mke alivyoninyanyasa kwa nyodo kabla sijamuoa, nikatumia nguvu na vitisho vingi mpaka nikampata!

Nilijiapiza kuwa huyu nikifunga naye ndoa nitamfanya mtumwa wa ngono kumkomesha anachoringia!

Kweli tulianza hivyo kwa kumuwashia moto mwingi, lakini leo baba ndoa ina zaidi ya miaka 30, natamani niishi chumba cha peke yangu tukutane asubuhi sebuleni.

Upendo uko pale pale, lakini 'muhu' na kihere here hupotea vyenyewe mnabakia tu kuangaliana!

Wadhani mchezo wewe!

Ndiyo maana ulivyoongea nikahisi kabisa kuwa wewe una ndoa mpya kabisa isiyozidi umri wa miaka 10.

Kwanza bado una "kisirani" cha kufunga magoli huku umemdhibiti kwa kumkunja golikipa asiweze kudaka mashuti yako, yaani ufunge hata magoli ya mkono na uyahalalishe, game gani la hivyo!

Sasa unadhani akikutosheleza kwa hayo uliyoyasema ndiyo utatulizana nyumbani, jambo ambalo haliwezekani.

Kwani ukitamani vya nje, shemeji ana wivu sana kukufuatilia kisogoni kila kona, embu mwache jinsi alivyojichagulia kuishi bhana.

Mambo hayo ya kinamama kubweteka baada ya kuolewa ni jambo la kawaida, si kwako tu, karibia %90 ya wanawake walioko kwenye ndoa ndiyo maisha yao hayo, asikudanganye mtu.

Ndiyo maana wananenepa sana, hata ukiwa barabarani ni rahisi sana kusoma haiba ya mke wa mtu kutokana na siha yake.

Mkuu mpende mkeo kutokana na alivyo.
Umenena vyema.
 
Wakuu,

Kuna Ela nilikua nidai Taasisi flan MDA mrefu Sana Bila kulipwa, baada makao makuu kuhamishiwa dodoma na boss husika niliefanya nae hiyo biashara kuhamishiwa wizara nyngn, Basi matumaini ya kulipwa tena Ela ile yakawa kama yameyeyuka kabsa.

Maana Boss aliepo anadai Ile biashara anaitambua ila haikufuata utaratibu rasmi wa ofisi,hawezi kuidhinisha hayo malipo kwa Sasa. Anashughulikia kwanza madeni aliyoyakuta yaliyo ktk utaratibu rasmi.

Basi Katika fatilia sn Deni Lile makao makuu, nikakutanishwa na jamaa wawili wa ofisi ile ile wakaahidi kunisaidia Hadi nilipwe, ila mkono mtupu haulambwi, wakifanikisha nikalipwa, 30% itakua ya kwao. Nikasema POA, Haina shida pambaneni nirudishe hata nusu hasara.

Jumatatu asbh wakanipigia kua muamala tayar,tutumie chetu,nikawaambia sijaona sms yoyote ya bank deposit, Wakasema check salio, kuangalia hamna kilichoongezeka. Pesa ilkuja kuingia usiku saa 3, nikawapigia nmeiona ntawatumia mgao wenu kwny Simu zenu kesho asbh na mapema Sana.
Wakasema POA.
 
Jumanne ile Simu tunayowasiliana nao wale jamaa ikawa imeisahaulika nyumbn, namba ya Simu nlotembea nayo ikawa hawana. Na kwasababu namba ile Haina Watu wengi sn,naitumia kwa Mambo yngu binafs na maalum na Ina vibration tu Haina mlio. sikujishughulisha hata kurud nyumbn kuifata Mana Najua haitamsumbua mtu ikiita. Ntaikuta jion nkirud.

Usiku sn nmerud nyumban nakuta missed call kibao za hao jamaa, akili ikanambia Hawa wanakumbushia pesa Yao,na sijawatumia,hata nikiwapigia usku ushaenda san washalala, Ntawatumia kesho asbh tumalizane. Nikazima Simu na nikalala.

Jumatano nmeamka nmebeba Simu zot Kwenda kazin, madukan hamna aliefungua, nmetoka kwa mguu na washkaji tumeenda kwa mkutanoni kumskiliza waziri mkuu, Kile kisimu kdg nmekisahau kwny Gari. Na Ela ya jamaa nmesahau kutuma, Basi kumbe ikawa wakipiga Simu inaita ila sipokei.

Nmekuja kupokea namba ngeni Simu hii Nlkua nayo mfukoni ni saa12 kasoro jioni,kupokea Ni wale jamaa wa dodoma wanajitambulisha na wanalaumu sn uhuni nnaowafanyia kua baada ya kuingiziwa pesa zangu hata Simu zao sizipokei, hii Ni jeuri, nikajitetea sn hawakunielewa.
 
Wakahitimisha kua wako dar sahv na wamefata pesa Yao na wamefika sinza,hotel flan. Niwapelekee pesa zao cash, kesho asbh wanatakiwa kurud kazini dodoma. Nikasema POA. Nawaletea.

Bahat nzur pesa Yao cash dukan ilkuepo kias, nyngn nikaazima kwa mtu kujazia nikawapelekea uko uko hotelin nilikoelekezwa. Nmefika mida ya saa 1 kasoro nawapigia wakanambia nije bar flan kubwa sn na maarufu sn,niwafate uko wameenda kula.

Kweli nmejongea mmewakuta wanapiga nyama na bia,kabla sijaeleza chochote wakaomba niwakabidhi chao kwanza hawataki siasa maana nimewakera sn mpk wameifata pesa wenyewe dar,nikawakabidhi Chao, nmejieleza wamenielewa na kunikaribisha nijumuike nao tupate kilaji. Kweli tukaanza kuzikata bia na nyama.

Story za Hapa na pale tukapata kufahamiana nao zaidi, mmoja akajitambulisha asili Yake ni mhaya wa bukoba,mwingine akajitambulisha Ni mnyakyusa wa mbozi. Zimeletwa round 3 ,ya nne nikaona aibu nikataka kuilipia Mimi, mhaya akanambia wee bado Ni bwana mdg sn kutulipia sisi Kaka zako bill, Tuko serikalini zaidi ya miaka 20 na tunapesa kuliko wewe, unapaswa kukaa kwa kutulia.
 
Ungetuzingua kutulipa pesa yetu tungekufanyia kitu mbaya sn usingesahau maishani mwako na usifikiri tumefata Hii pesa sababu tuna njaa nayo Sana, Bali tulitaka tukufundishe adabu kuheshimu makubaliano tuliyokubaliana.

wakasema
"Bwana mdg ujue tumepanda ndege Dom to dar kufata Hii pesa yako ndogo, na tutarudi kwa ndege dodoma. Pia unapaswa ujue hatujafikia sehemu za hovyo, pale hotel tumefikia, tunalipa laki usiku mmoja. Hii pesa uliyotulipa kwetu Ni pesa ndogo Sana,tunaweza kuinywa yote Hapa dar ikaisha, tukarudi dodoma Kama tulivyo, kwaiyo usituchukulie POA POA kijana". Nikaitikia "sawa wakuu, nmewaelewa sn maboss Wang,mniwie radhi sn, zilikua Changamoto TU za kimawasiliano,nisieleweke tofauti" Basi wakaelewa na nikaendelea kula kilaji free na maboss wangu Bila kuchangia chochote kile.

Sasa Meza ya mbele yetu kdg akaja mdada mmoja,kavalia kigauni kifupi kakaa akaagiza castle light Moja anakunywa uku anachezea simu Yake.

Uku meza yetu baada ya kumuona yule mdada,nikamchomekea mhaya kua inakuaje unalala chumba Cha laki usiku mzima peke yako na Mtoto mzuri kama yule pale mbele kakaa peke ake TU anashangaa,kiukweli haya Ni matumizi mabaya ya rasilimali fedha. Mhaya akacheka na mnyakyusa nae akasapoti wazo Lile.
 
Baadae mhaya akauliza nampataje Sasa uyo binti?, mnyakyusa akasema "KAZI ndogo sn iyo" akamwita mhudumu na kumwambia apeleke castle light 2 Ile meza ya binti, amwambie aliemnunulia Ni huyu mzee mwenye shati la kitenge (mhaya). Mhudumu kafanya vile, jibu limerudi dada kasema Asante. Basi tukaendelea kula pombe.

MDA umeenda bia zinatembea kasi ila mhaya Hana amani kabisa,MDA wote macho kwa mdada, tukawa tunamcheka,akasema msinicheke,huyu binti kweli nmemuelewa, mnisaidieni nampataje.

Nikamwambia mhaya anipe Simu yako nikusaidie kukuchukulia namba wkt naenda chooni, akasema POA.
Nmetoka chooni nikastop meza ya mdada na kumwambia yule mzee mwny kitenge kasema umuandike Hapa namba yako hapa, kweli mdada Kaandika namba Nikarudisha Simu kwa mhaya, hatujakaa Sana kumbe mhaya anamchatisha binti, ghafla binti kahama na kiti chake kaja meza yetu tuliyokaa na kuendeleza kilaji.

Baada ya kunywa bia Sana, mnyakyusa akasema bia za dar hata hazipandi, Bora Pombe Kali, akaagiza k-vant kubwa, nami nikasema bia nmezikinai, nikaagiza Konyagi bapa kubwa na mhaya nae akasema ataendelea kunywa bia.
 
Sasa baada ya MDA flan binti nae akasema bia kazichoka,nae anataka k-vant, mhaya akaagiza k-vant kubwa wakawa wanashea anamix kdg na bia.
Baada ya MDA mhaya akaachana na bia kabisa na kuanza kuikata k-vant kavu kavu Kama anavyofanya mnyakyusa na uyo binti. Bia zikabaki Kama 4 hivi mezani zimedoda hazina wanywaji.

Kuna MDA binti kaenda chooni na kurudi meza yetu akamnong'oneza mhaya kua Kuna Rafk zake pale meza ya mbele wanaomba bia Moja, mhaya kasema kwasababu hazina wanywaji, chukua mpelekee TU. Binti kachukua bia Mbili kapeleka kule na kukaa kidg km dkk 2 hivi wanaongea.

Uku alipotuacha tukaanza kumsimanga mhaya kua kakosea sn,anapelekaje bia mbali uko wkt sisi tupo Hapa single? Hao mabinti wanataka bia zetu, wazifate Hapa hapa tulipo sio kuwapelekea uko walipo. Katukosea Sana.

Inapaswa nasi tufurahie uumbaji wa mola, sio Yeye tu ndie anaenjoy peke ake na mtoto mzuri pale. Mhaya akaomba radhi na kusema Basi binti akirud atamwambia awaambie hao rafk zake wawili wanaotaka bia zetu waje wakae meza yetu. Tukasema POA.

Punde SI punde marafiki zake binti wakafika, Basi ikawa Ni wanaume 3 na wanawake 3, mezani kumebalance. Basi Pombe zikaongezwa na nyama zikawa Ni mwendo wa bandika bandua mpk MDA flani nimeimaliza bapa ya 2,nmeianza bapa ya 3 nainuka Kwenda chooni haja ndogo, nikaanza kujihisi Kama network kichwani hazisomi vizur, najhs kizunguzungu.
 
Nmerudi toka chooni nmekaa, story zinaendelea, binti niliekaa nae akachukua mkono wangu wa kushoto na kuubana na mapaja yake. Akili ya kishetani ikaanza kunijia na kunifanya nianze kumpapasa mapajani chini ya meza(alivalia sketi kimini), Nae Bila aibu akachukua mkono wake mmoja akaupachika juu ya zipu na kuanza kuminya minya mdudu.

Akili ya haraka haraka ikanambia kua Hawa mabinti wote tuliokaa nao Ni Makahaba pure,hamna binti wa kawaida anaweza pata ujasiri Kama huu kwa mtu baki Asiyemjua mmekutana tu bar kwenye ulevi.

Hapa nikizubaa ntajikuta nishalala na kahaba na Hizi Pombe nilizonazo kichwani itakua balaa. Maamuz yaliyonijia Ni nitoroke kimya kimya Kama naenda chooni afu nipitilize uko uko niende zangu nyumbani. Hiyo Ni saa 5 na madakika kadhaa usiku.

Nmetoka nje Moja Kwa Moja parking,sikulemba Moja kwa Moja mpaka nyumbani, nmepakuliwa hata sikula, nmeoga, nmezima Simu na nmelala Moja kwa Moja Mpk kesho yake alhamis asbh naamshwa na wife saa 3 ninywe chai.

Nmewasha Simu wkt nakunywa chai. Nakutana na sms za jamaa zangu wananiuliza nn kimenipata uko chooni,vp Mbona sipatikani? Ikabd nimpigie mnyakyusa.
 
Mnyakyusa anasema walipata hofu Sana,ila walivogundua na gar haipo nje akajiongeza kua nmekimbia ligi ya pombe, akasema wengi wanaoogopa kulewa huwa hawaagi bar, nikamwambia Ni kweli aisee maana niliona hizi pombe zinakonipeleka Ni pabaya,nikiaga mtanizuia na nikiendelea kulewa itakua fedhea.

Akanambia mimi nna kichwa Cha togwa,yeye Alkua bado Yuko fit Japo ndo alikunywa pombe nyng Sana na Jana walipofunga pale bar ya pale Sinza, wakahamia TABATA na warembo wao kuendeleza kilaji. Ametoka tabata pale saa 8 usiku na Uber kurudi hotel kulala na mrembo wake baada ya mhaya kuondoka na yule binti wanakokotana wamelewa wakawaachia meza.

Nikamuuliza kwaiyo mhaya Yuko wapi sahv,atakua na Hali gani, akasema Bila shaka watakua walienda kulalana wale maana walitoka wamelewa Sana, watakua uko chumban kwake na mwanamke wake.

Akasema alivorudi usiku hata hajajisumbua kuwagongea. Punde SI punde akanipa nimsalimie uyo mrembo wake tulokua wote Jana usku, tukapeana hai na Kisha nikawaachia waendelee na mambo Yao.
 
Nmekata Simu ya mnyakyusa ikabd nimpigie mhaya, Simu Yake ikawa haipatkani,Basi nikapuuza nikajiandaa na nikaondoka nyumban kwnd kazin kwangu.

Nmekuja kupokea Simu ya mnyakyusa mida ya saa 10 jion kua mhaya amepata matatizo, nikauliza matatizo gan, akasema ya Jana usku,nikauliza yapi ayo, akasema nisihoji Sana Kama naweza nije police kituo flan ntamkuta. Nikasema POA,chap natokea hapo. Kweli nikaelekea apo polisi.

Nafika polisi namuona mhaya counter anaandika maelezo,nikamvuta mnyakyusa pembeni anijuze Nini kimejiri, ndo akaanza kunisimulia kua punde baada ya kukata ile Simu, kamkatia Elfu 50 binti alienae keshaenda zake, ameagiza supu ya kuku yuko anakunywa,akaskia anagongewa mlango na mhaya.

Kufungua anamuona mhaya kavalia suruali jeans njiwa (haimtoshi) na vest na miguuni kavalia kandambili za gesti (zile zimekatwa kdg kwa mbele na nyuma). Anamuulza vp Mbona uko hivi. Anasema Kwanza naomba elfu 10 nikalipe Ela ya bajaji, anampatia anaenda kulipa na kurudi na kuanza kumwambia ameibiwa wallet,simu na pesa zote alizokua nazo.

Mnyakyusa akauliza Kivipi, mhaya anasimulia kwamba anachokumbuka Mara ya mwisho Ni kwamba Alikua na mnyakyusa pale bar tabata na wanawake wao wanakunywa pombe, mi nishaondoka maana niliawaacha sinza, ila kilichoendelea hakumbuki Ten,mpk alipozinduka saa 4 asbh Yuko uchi wa mnyama kitandani peke ake na mwanamke aliekua nae usiku Kucha hayupo.
 
pesa zote alizokua nazo,zile million 2.5 nilizompatia ,wallet na Simu Yake havioni. Katafuta nguo za kuvaa hazioni ndipo kuingia chooni kakuta zote zimelowekwa kwenye ndoo ya maji. Kajifunika shuka na kwenda kaunta kujieleza kwa mhudumu.

Mhudumu akasema binti kweli alitoka alimuona ila hamkumbuki sura na yeye usiku ule wa manane ndo Alikuja nae na binti ndo aliekodi chumba na kukilipia.

Pale pale Zimepigwa namba zske hazipatikani, namba za binti alizoandika Kwny kitabu Cha wageni nazo hazipatikani, ndipo ikabd aombe nguo ya kujisitiri aondoke pale,ndo akapatiwa suruali ya jeans njiwa iliyochakaa iliyokua inatumika Kama kanyagio.

Mhaya Akaenda kukamua nguo zile na kuzianika, vest akaikamua Sana na kuikung'uta sana kisha kuivaa MDA ule ule na kuita bajaji impeleke hotelin kwao walikofikia sinza na kukutana na mnyakyusa Rafk yake kumueleza yaliyojiri.

Apo hapo hotelin mnyakyusa akajaribu kuipigia namba ya mhaya haipatkani,namba ya binti alielala nae namba aliyopewa hapatkani, akahitimisha wale mabinti wanajuana,lao Moja. Ikabd mnyakyusa ampe nguo zake nzuri na sendoz rafiki Yake mhaya avae ili waende wote kuripoti tukio hilo polisi.
 
Ila hapo Moja kwa moja mnyakyusa akahitimisha kua wale mabinti wote lao ni Moja,Ni wezi na pia huenda na yeye angepigwa tukio maana walipofika alikabidhi pesa zote nilizompa mil.2 5 pale counter,akabakiwa na pesa zake elfu 80 tu na kisha walipoingia TU chumbani, akafunga mlango na kuweka funguo mfukoni, binti akataka mnyakyusa ndie akatangulie yeye kuoga. Wakabishana kdg,ila binti ndo akatangulia kuoga.

Binti Alivoingia tu kuoga, mnyakyusa akasogeza kitanda hadi mlangoni,akaitoa funguo ya mlango mfukoni na kuibana na biggy G vizur nyuma ya kioo Cha Cha kujitizama cha plastic kilichoning'inizwa kwny msumari jiran na meza walikoweka vitu vyao.

Kisha binti alipomaliza kuoga,karudi katahamaki kitanda kilivokaa, mnyakyusa akamwambia kitanda akiache hivo hivo kilivyo,kaoga kamaliza, wamefanya Yao wamelala mpk asbh binti ndo anamwamsha kua kushakucha, apewe ujira wake anahitaj kuondoka. Wamelipana vzur kamfungulia binti kaondoka zake.

Mnyakyusa kamaliza kunisimulia hayo,mhaya nae ndo anatoka kuandika maelezo,namuuliza vipi, mhaya kawa mpole Hana hata Cha kusema,nkaona Bora nisimsemeshe.
Ngoja tuache polisi Kwanza wafanye kazi yao.

SEMA WAKUU,
Baada ya hiki kisa Naomba mnijuze,
hivi Hawa Makahaba wengine huwa Ni walozi, washirikina sana au vipi ?

Au Kuna vitu huwa wanawachanganyia kwenye vilevi mpk mtu anazima na kupoteza kumbukumbu KABISA anaibiwa?

Yaan yule binti namkumbuka KABISA,ukimuangalia mwonekano wake,ana aibu na sio mwongeaji huwez mdhania KABISA km anaweza fanya kitendo kile

Nawasilisha wakuu
 
2487627f-5376-408c-aab2-c96271e0f94a.jpg
 
Back
Top Bottom