Hivi wachezaji wanawezaje kuingia uwanjani bila utaratibu rasmi (kuruka ukuta) lakini mashabiki hawawezi?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,153
Kuna kitu huwa kinanishangaza sana katika karne hii ya 21 kila nikisikia kuwa wachezaji wa timu fulani (hususani Yanga na Simba) wamepigwa faini kwa kosa la kuingia uwanjani pasipo kupita kwenye geti rasmi la wachezaji (kuruka ukuta) na wakaingia uwanjani (pitch) na vyumbani.

Maswali ninayojiuliza ni haya;
1. Kwanini hili suala liwe jambo rahisi sana kwa wachezaji kiasi cha kujirudia rudia lakini lisiwezekane kwa mashabiki?

2. Kwanini mamlaka ya ulinzi na usalama haikubali kuwajibika kwa hili?
 
Tff wanaendekeza ulozi kwa sababu haya matukio yamekuwa yakijirudia rudia na mbaya zaidi anayeongoza kufanya vitendo hivi ni timu moja. Kama wangeweka adhabu Kali Kama kunyang'anya pointi na faini ikafika hata milioni 50 hivi vitendo vingeisha.
 
Hawaruki ukuta ila wanapita geti lisilo rasmi. Chakujiuliza nani anawapa ufunguo wa hilo geti?
Kwenye sentensi yako ya mwanzo, umepatia vizuri kabisa. Hiyo ya pili ndiyo umechanga madesa.

Maana yake kinachofanywa na hizo timu ni kupita milango isiyo rasmi kwa mujibu wa kanuni za ligi, na pia masharti ya wadhamini; wakiwemo Azam Media.

Na ukumbuke hiyo milango ya kupita kwa siku za mechi huwa inafunguliwa na kuachwa wazi, kwa ajili ya wahusika mbalimbali kuitumia. Hivyo hakuna anayewafungulia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom