Unaijua kanuni iliyosababisha mechi ya Azam FC na Kitayosce kuvunjika?

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
SURA: V MCHEZO
Kanuni: 17 Taratibu za Mchezo
(1) Michezo yote ya Ligi Kuu itachezwa kwa kufuata sheria kumi na saba za mpira wa miguu za FIFA (17 Laws of the Game).
(2) Kutakuwa na mkutano wa kitaalamu wa Maandalizi na Uratibu wa mchezo (MCM) utakaofanyika kabla ya mchezo, saa 4:00 (nne) asubuhi siku ya mchezo. Kwa sababu maalum, mkutano huu unaweza kupangiwa muda, siku na mahali pengine kama itakavyopendekezwa na FA(M) na kuidhinishwa na Kamishna wa mchezo au GC wa mchezo (kama ameteuliwa).
2.1 Wanaotakiwa kuhudhuria kikao cha MCM ni:
2.1.1 Wawakilishi wa Timu kwa mchezo husika (HoD, Meneja, Daktari, Afisa Vifaa, Afisa Usalama)
2.1.2 Kamishina wa Mchezo (atakuwa Mwenyekiti wa Kikao)
2.1.3 Mratibu wa mchezo (GC)
2.1.4 Waamuzi wa mchezo (wanaweza wasiwepo endapo kuna Mtathimini wa waamuzi)
2.1.5 Mamlaka ya Uwanja
2.1.6 Msimamizi wa Vijana wa Mipira (ballkids)
2.1.7 Huduma ya Kwanza
2.1.8 Afisa Usalama wa TFF/Kituo
2.1.9 Mamlaka ya Polisi ya Eneo husika
2.1.10 Mamlaka ya Zimamoto
2.1.11 Daktari wa Mchezo
2.2 Timu inawajibika kufika kwenye kikao cha kitaalamu cha maandaliziya mchezo bila kukosa kwa wakati ikiwakilishwa na viongozi waliotajwa (kanuni 17:2 (2.1) wakiwa kamili na vifaa tajwa (kanuni 17.2 (2.3) kwa idadi na nafasi na si mwingine yeyote asiyetajwa.
2.3 Kila timu inatakiwa kufika na vifaa vyake, jezi, bukta na soksi watakavyotumia kwa mchezo husika kwa mpangilio ufuatao:
2.3.1 Sare ya Vifaa kwa Wachezaji wa Ndani (Field players)
2.3.2 Sare ya Vifaa kwa Walinda Mlango (Goalkeepers)
2.3.3 Timu Ngeni ifike na Sare za Nyumbani na Ugenini/ya ziada
2.3.4 Sare ya Vifaa vya Mazoezi mchezoni (warming Up kit)
2.3.5 Kitambaa cha Alama ya Nahodha (Captain ArmBand)
2.3.6 Sare ya Maofisa wa Benchi la Ufundi (Technical Officials)
2.3.7 Msimamizi ahusike na Sare za Vijana wa mipira (BallKids)
2.4 Ni sare zilizoamuliwa kwenye MCM tu kwa wachezaji na viongozi ndizo zitazoruhusiwa kuvaliwa wakati wa mchezo.
2.5 Kila jezi inatakiwa kuwa na namba kubwa zinazosomeka vizuri zilizo kati ya namba 1 (moja) hadi 70 (sabini).
2.6 Endapo rangi katika sare za timu mbili zitafanana, timu ngeni italazimika kubadili sare yake na endapo moja ya timu sare zake zitafanana na sare za waamuzi, waamuzi watalazimika kubadili.
Taratibu za mabadiliko lazima zijulikane kwenye kikao cha MCM
2.7 Sare ya mlinda mlango isifanane rangi na sare (jezi) za wachezaji wa ndani na mlinda mlango wa timu pinzani.
2.8 Kikao cha maandalizi ya mchezo (MCM) kinaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa mazingatio ya Kanuni 17:2 .
(3) Endapo kutatokea kufanana sare za timu wakati wa ukaguzi kabla ya mchezo kuanza, timu ambayo haikufika kwenye kikao cha MCM itawajibika kubadili sare zake.
(4) Kamishna atahakikisha timu zinatumia sare kwa mujibu wa rangi za nyumbani, ugenini na ziada kama zilivyoandikishwa na klabu kwa TFF.
(5) Timu zitaheshimu uchaguzi wao wa rangi za sare zao kwa michezo ya nyumbani na ugenini/ya ziada (katika mazingira ya mgongano wa rangi), na endapo itatokea timu ya nyumbani kukosa uzingativu wa kuwasilisha rangi sahihi kwa sare zake kwa mechi za nyumbani katika kikao kitangulizi cha MCM timu ngeni itakuwa na haki ya kwanza ya kuchagua rangi ya sare katika mchezo husika.
(6) Timu zinazocheza mchezo husika zinatakiwa kuwasilisha kwa Kamishina/Mratibu (GC) wa mchezo Orodha ya Viongozi wasiozidi nane (8) na wasiopungua watano (5) na Wachezaji wasiozidi ishirini (20) kwa mchezo husika masaa mawili kabla ya muda wa kuanza mchezo (kickoff) kwa kutumia fomu maalum iliyojazwa kwa unadhifu na ukamilifu ikiwa imesainiwa na kila mmoja.
(7) Kila klabu ya Ligi Kuu ina wajibu wa kuhakikisha linakuwepo Gari la wagonjwa (ambulance) na vijana waokota mipira (ball kids) uwanjani katika kila mchezo wake wa nyumbani timu yake inapocheza. Iwapo huduma hizo hazitakuwepo, Kamishna atazuia mchezo kuchezwa, na timu mwenyeji itapoteza mchezo huo.
(8) Kocha Mkuu na Viongozi wa Benchi la Ufundi wanawajibika kuvaa sare maalum za timu yao kwa Benchi la Ufundi. Endapo Kocha Mkuu atahitaji kuvaa mavazi tofauti, anawajibika kuwa katika Mavazi Rasmi ambayo ni ya Heshima na Nadhifu. Uvaaji wa Kaptula ya aina yoyote hauruhusiwi kwa Kocha Mkuu. Ukiukwaji wowote utavutia adhabu kwa muhusika na/au kwa
timu husika.
(9) Mchezaji anayeruhusiwa kucheza ni yule tu aliye kwenye orodha ya timu iliyowasilishwa kwa Kamishna na kukaguliwa kabla ya kuanza mechi.
Mchezaji ambaye hakukaguliwa atahesabika kuwa batili (nonqualified).
(10) Michezo yote ya ligi itachezwa kwa vipindi viwili vya jumla ya dakika 90 (tisini) kila kipindi kikiwa na dakika 45 (arobaini na tano) na mapumziko ya dakika zisizopungua 5 (tano) na zisizozidi 15 (kumi na tano) kati ya vipindi hivyo. Mwamuzi wa mchezo ndio mtunza muda.
(11) Mchezaji atakayevaa jezi isiyokuwa na nambari mgongoni ama itakayobandikwa kwa plasta au katika utaratibu wowote ule usiokubalika hataruhusiwa kucheza.
(12) Manahodha wa timu zinazoshindana wanatakiwa kuvaa vitambulisho (arm- band) vya rangi tofauti na jezi zao kwenye mikono ya jezi zao.
(13) Kila mchezaji ni lazima avae kilinda ugoko (shinguard) kwenye miguu yote miwili, mchezaji asiyevaa hataruhusiwa kucheza mpaka avae.
(14) Wachezaji/viongozi wa kiufundi hawaruhusiwi kushangilia goli kwa kufanya ishara yoyote isiyokuwa ya kiuanamichezo au ya kashfa au matusi kwa timu pinzani au watazamaji.
(15) Timu zinatakiwa kufika uwanjani si chini ya dakika tisini kabla ya muda wa kuanza mchezo.
(16) Muda wa kuanza mchezo (kickoff) utapangwa katika mazingira ya kawaida na kwa mazingatio maalum ya hali kwa michezo inayoonyeshwa kwenye televisheni, viwanja na sababu nyingine yoyote muhimu. Mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa ishirini na nne (24) kabla ya muda wa awali
uliopangwa. TPLB/TFF inaweza kubadili muda wa kuanza mchezo (kickoff) kwa mazingatio maalum katika mazingira ya dharura na/au yaliyo nje ya uwezo wa pande zote kwa maana ya TPLB/TFF na Klabu husika.
(17) Ni marufuku kwa viongozi kuingia kiwanjani (pitch) bila sababu za msingi kinyume na taratibu za mchezo kabla, wakati au baada ya mchezo.
(18) Ni marufuku kwa mashabiki kuingia kiwanjani (pitch) kabla, wakati au baada ya mchezo.
(19) Timu zinapokaguliwa au kupeana mikono zenyewe na waamuzi zitalazimika kufanya hivyo kwa heshima zote zinazostahili.
(20) Baada ya kuwasili Uwanjani katika muda rasmi na muda wote kabla ya kuanza kwa mchezo na wakati wa mapumziko, timu zitalazimika kupumzika kwenye vyumba vyao vya kuvalia kwa kutumia milango rasmi kwa ajili hiyo na si vinginevyo.
(21) Timu yoyote hairuhusiwi kuruka ukuta wa nje ili kuingia uwanjani (Stadium) ama kuruka uzio wa ndani unaotenga watazamaji na kiwanja (pitch), ama kupita katika mlango wowote usio rasmi kwa kuingizia timu.
(22) Wachezaji wote watatambulika kwa kutumia Leseni zao zitakazotolewa na kuidhinishwa na TFF. Mchezaji yeyote ambaye hatakuwa na leseni hatoruhusiwa kucheza katika mchezo husika.
(22.1) Timu mwenyeji kwa kushirikiana na Msimamizi wa Kituo ina jukumu la kuandaa ukumbi kwa ajili ya Kikao Cha Maandalizi ya Michezo (MCM) wenye sifa na vigezo kama ilivyoelezwa na na Bodi ya Ligi/TFF
(23) Katika mazingira maalum ya kukosekana Leseni ya mchezaji, TFF inaweza kutoa utambulisho wa dharura/muda ili kukidhi mahitaji ya kikanuni kwa mchezaji kucheza mchezo husika.
(24) Iwapo itathibitika bila kujali kukatwa au kutokatwa Rufaa, kupitia taarifa za mchezo za Kamishna ama kwa njia yoyote kuwa timu imechezesha mchezaji ambaye usajili wake haujathibitishwa na TFF hivyo kuwa batili kiusajili (nonqualified) timu hiyo itapoteza mchezo na ushindi kupewa timu pinzani.
(25) Iwapo itathibitika bila kujali kukatwa au kutokatwa Rufaa, kupitia taarifa za mchezo za Kamishna ama kwa njia yoyote kuwa timu imechezesha mchezaji ambaye hajaorodheshwa kwenye fomu maalum ya Orodha ya wachezaji na viongozi kama mchezaji wa siku hiyo kwa mchezo husika na hivyo kushindwa kupitia mchakato wa ukaguzi wa wachezaji kabla ya
mchezo timu hiyo itapoteza mchezo na ushindi kupewa timu pinzani.
(26) Wanaoruhusiwa kukaa kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo ni wachezaji tisa (9) wa akiba na viongozi nane (8) ambao ni Mwalimu Mkuu (head coach) Walimu Wasaidizi (assistant coaches) wasiozidi watatu, Daktari, Mtaalamu wa tiba ya viungo, Meneja wa Timu na Afisa Vifaa wa Timu.
(27) Endapo timu iliyokiuka maelekezo ya Kanuni (17:26) itakataa kutii maelekezo ya mwamuzi ya kuwaondoa wasiohusika kwenye benchi la ufundi, mwamuzi anaweza kuomba msaada kwa GC/Kamishna/Msimamizi.
 
Back
Top Bottom