Hivi udini wa Samia Suluhu uko wapi? Tuzungumze ukweli

Hivi udini wa Samia Suluhu uko wapi? Tuzungumze ukweli

Humu jukwaa kuna tuhuma ambazo Samia Suluhu anatupiwa ya kwamba ni mdini na amejaza waislamu katika wateule wake sasa najiuliza udini wa Samia uko wapi? Au udini wa Samia anaufanyia wapi?

Mbona nikiangalia kati wateule wake kati ya wakristo na Waislamu naona wakristo ni wengi sana kwa maana kuna idadi kubwa ya wakristo Kati wateule wake kuliko waislamu?

Je, udini wa Samia uko wapi? Na mbona kiongozi akiwa muislamu hizi kelele za udini ni nyingi sana kuliko akiwa wa dini nyingine?

Mimi nauliza tu wala sina maana mbaya uzi uachwe.
Kufungia Makanisa, kuteka kushambulia na kuumiza viongozi wa Kanisa mfano hai ni jaribio la kumuua Father Kitima hadi leo hakuna mtu aliyekamatwa kwa vile ni Samia aliyeagiza shambulio hilo. Hata hotuba yake kwa wale aliowaita wazee wa Dar es Salaam ilijaa vitisho na kejeli nyingi kwa Kanisa Katoliki, baada ya siku chache toka atoe hotuba hiyo aliwatuma mashehe kumshambulia Makamu wa Rais kuwa ni kibaraka wa TEC na anapokea maagizo toka kwa Father Kitima.
 
Zanzibar sio South Africa ukiipa Zanzibar mamlaka kamili inakuwa kama umoja wa kiarabu ambao leo ndio wafadhili wakubwa wa tz
Amini usiamini, Zanzibar ikijitenga na kua huru baada ya mwaka itakua kama Sudan, waZanzibar wapo waarabu na wabara-bantu, watagawanjika, Oman wanaweza kuingia hapo, na ISIS, hii ni kufuatana na historia ya hapo mahali. Hii ndiyo Tatatizo tutakalopata Tanganyika, maana wata-export terrorism Tanganyika.
 
Uibiwe kura ulipiga?.. ufanye uhalifu,utake kuangusha serikali utazamwe tu?!
Umechanganyikiwa nini? Kuangusha serikali maana yake ni nini? Fikra dhaifu na zisizo na maana. Haiwezekani serikali iangushwe majumbani kwa watu wakiwa wamelala then mnawaua, halafu unakuja hapa na utahaira wako wa kusingizia eti wanataka kuiangusha serikali. Shut the hole, tumepoteza ndugu zetu. Wacha kuongelea vitu usivyojua.
 
Amini usiamini, Zanzibar ikijitenga na kua huru baada ya mwaka itakua kama Sudan, waZanzibar wapo waarabu na wabara-bantu, watagawanjika, Oman wanaweza kuingia hapo, na ISIS, hii ni kufuatana na historia ya hapo mahali. Hii ndiyo Tatatizo tutakalopata Tanganyika, maana wata-export terrorism Tanganyika.
Unaishi fikra za Nyerere na ndio zilizofanya akainjinia mapinduzi ya Zanzibar

Wazanzibari sio wapuuzi kiasi hicho
 
Hivi unajua maana ya udini keeli au unaropoka tu ...shekh au padri kukas ndani diyo hoja kuna maladri hadi sasa wapo jela kwa ubakaji nk .....tatizo la waislamu kuwaelimisha ni kazi sawa na kumwelimisha nguruwe....
Mbona umepanik?

Ngoja ifike wakati wenu mje mvuruge kama kawaida yenu halafu tuone mkitoa matamko
 
Ni chuki tu dhidi ya Uislam na Waislam ukichanganya na husda.
Hachukiwi sababu ya uislam wake ,hayo mambo ya udini waliyaanzisha wenyewe ili kuwatoa wananchi katika reli najua huwezi kuelewa na hutaelewa kwa sasa ila siku moja yatakaa sawa utaelewa
 
Kwanza hongera kwa swali hili, pili jf ya sasa imebadilika sana, mtu unatoa hoja, badala ya watu kujibu hoja kwa hoja au kwa hoja mbadala, watu wanajibu hoja kwa viroja!.

Kwenye hizi hoja za Udini, Tanzania tuna tatizo la mazoea ya kitu kinachoitwa Mfumo Kristu, unaoshikiliwa na Kanisa Katoliki Tanzania kupitia TEC, ambapo it's is systematic rais wa Tanzania akiwa Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki!. Hii haijaandikwa popote ila ndio hivyo!. Juliasi ni Mkatoliki, Benyamin ni Mkatoliki, Yohana ni Mkatoliki, anayefuata ni Emanueli!.

Hii imewafanya Wakatoliki kujisikia kuwa na an upper hand kwenye utawala wa nchi hii!.

Kwa sababu pia ni ukweli usiofichika, idadi ya wasomi Wakristo ni kubwa zaidi ya wasomi Waislamu, automatically kwenye teuzi nyingi lazima kutajaa Wakristo, hii ikapelekea Wakristo kujiona wao ni deserving kutawala idadi ya teuzi zote.

Tuhuma za Udini zikaanzia kwa Mwalimu Nyerere kuwa amejaza Wakatoliki kwenye serikali yake, Waislamu wakaanza kuita ni Mfumo Kristo, Father Sivalon ameandika kitabu kuhusu Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania.

Wakati wa Nyerere, kuwapata Waislamu wenye sifa za kuteuliwa ilikuwa ni wa kutafuta kwa tochi.

Mfano Benki Kuu ya Tanzania, ilihitaji kuwa na Naibu kutoka Zanzibar, sifa ni awe na Ph.D ya uchumi +10 years experience post Ph.D, mtu huyo hakuwapo, hivyo wa kwanza kupatikana ni enzi za JK.

Tanzania tuna ma CDF 8, kati ya hao mwenye jina la Kiislamu ni mmoja tuu, Abdullah Twalipo tena usikute ni jina tuu kama Jaji Mkuu Saidi au Jaji Ramadhani, majina ya Kiislamu, wenyewe Wakristo.

Samia akiteua CDF Muislamu sasa hivi utasikia kelele jeshini!, hii ndio mara ya kwanza Mnadhimu Mkuu ni kutoka Zanzibar!, kelele!.

Hakuna rais alukuwa na mkabila, mdini na nepotism kama JPM, kwa vile alikuwa Mkatoliki, hakuna kelele, sio tuu aliteua kabila lake tuu, ndugu zake, rafiki zake hadi something zake!, watu kimya.

Samia kateua tuu mtoto na mkwe, kelele!. Kiukweli Samia hana udini wowote, tatizo ni
1. Ni Mwanamke
2. Muislamu
3. Mzazibari mwenye nywele za singa

Enzi za Mwinyi hakukuwa na kelele hivi, hivyo huyu Mama wanamuonea tuu kwa uanamke wake!, dini yake na asili yake.

Tusiruhusu

P
Mzee Pasco, Umedhihirisha ukomavu ktk kipindi ambacho hisia hizi zimeshika nafasi.
 
Kwenye uongozi wa rais mwenye jina la kikristo, umewahi kuona kuna kundi likimtetea rais kwa misingi ya dini?

Nyerere, Nkapa, Magufuli!

Nani alitetetwa na wakristo kwasababu yeye ni mkristo?

Nakumbuka Magufuli alipigwa spana na TEC, kina Mwamakula na wengine...

Tazama tawala ya Samia...

Kuna kikundi kiliahidi kukata watu vichwa na bado kiko uraiani...

Makanisa yamefungwa bila sababu za kueleweka...

Viongozi wa dini moja kuwindwa wauwawe, (Kitima case...)

Ile sumu yetu inauwa zaidi wakristo kuliko waislamu (Ndugai vs Bashiru) kwa uchache...

Bashiru angekua na jina tofauti tusingekua nae...
Huwezi chukulia tukio la Dr Kitima kama ni jambo la viongozi wa dini moja kuwindwa! Hoja ya namna hio ni manipulation ya watu waovu wanaotaka tumia matatizo yetu dhidi ya taifa/utaifa wetu.

Kushambuliwa kwa Dr Kitima kuna uhusiano mkubwa na matamko yake ya kisiasa au kujihusisha kwake na siasa, na wala hakuna uhusiano na dini yake wala dhehebu lake. Mashambulizi ya namna hio si mageni Tanzania, baadhi ya wahanga ni pamoja na Sheikh Ponda, jopo la UAMSHO,

Hoja ya sumu, yaweza kuwa ni hisia inayo chochewa na udini vilevile, kwa watu wa aina yako huenda kifo cha Mwl Nyerere, Mzee Mkapa, kingetokea chini ya Rais muislam bado mngelisema kama hayo!.

Hoja ya kwanza ningependa kujibu kwa kutumia nukuu, nikiipata nitaweka hapa
 
..Udini wa Samia hauko ktk teuzi anazozifanya.

..Udini wa Samia uko katika mitizamo yake kwamba wanaokosoa maamuzi yake wanafanya hivyo kwasababu ya dini yake, na sio ubovu na madhaifu ya maamuzi yake.

..hakuna Rais amewahi kuhutubia taifa na kudai kuwa wanaomkosoa wanasukumwa na Udini, Samia ndiye wa kwanza kufanya hivyo.

View: https://www.threads.com/@muya51/post/DQ9prVWDKj5?xmt=AQF0kziQ8yWkJ4R3Nb7EQDxIcv-5UMFdhFyqLHjzBEku2xs6-pBunPoC0_byAYnCgtYsvEdi&source_surface=35&slof=1
 
-Udini
-Nepotism
-Uzanzibari
Just cut the hypocrisy hilo liko katika kila nyanja na humu JF lilishajadiliwa kwa kina na mifano halisi, muhimu hapa kwanza ni kuuvunja huu muungano unaofaidisha upande mmoja yanayobaki tutayamaliza wenyewe kama Watanganyika. Mizanzibari imejazana kila sekta na katika mambo hata yasiyohusu muungano, inamiliki ardhi everywhere ukijaribu kwao hawawezi kukukubalia hivyo tuunvunje huu muungano wa kikanjanja Samia akatawale kwao huko tuone kama watamkubali.
Mkuu mbona na watanganyika wapo wengi Zanzibar kule? Au nao watimuliwe?
 
Kumbe bado unautaka muungano 😹😹

Kama unautaka kuna haja gani ya kutimuana?
Siutaki kabisa lakini kuukataa kwangu kusiwe kigezo cha kunyima haki ya kusikiliza sauti za wengine, ipigwe kura na nina uhakika ikipigwa kura halali tunaoukataa tutashinda.
 
Ulikuwa umefunga maskio wakati kawatuma masheikh kuisema TEC? Ulikuwa umeweka pamba wakati anasema kaandikiwa nyaraka kadhaa na TEC? Samia anatumia dini kuficha udhaifu wake, anawalambisha asali masheikh ili wamtetee, mpaka inafika tunaambiwa tutakatwa vichwa, na mtu hakamatwi Wala nini, usichoelewa ni kipi? Sehemu nyeti zote zenye pesa kaweka waislam, bila kujali competence. Na kiukweli waislam wengi Tanzania hawana competence yeyote. Tunajuana bana
Kweli nimeamini kumbe mtu unaweza kuzungumza maneno yakapinduliwa maana yake halisi.

Ni wapi sheikh alisema tutakata vichwa wakristo?

Alichosema ni kwamba hao wanaochochea maandamano ya vurugu na kupora Mali za watu utakuta tumekatana vichwa huko barabarani.

Tunasema haya Wala hatutanii.

Nimenukuu.
 
Back
Top Bottom