Udini wake upo pale anapojaribu kujitetea tuhuma dhidi ya uongozi wake kuwa anachukiwa sababu ya dini yake.
Watu wanahoji matendo ya ukandamizwaji haki, utekaji na kuuwa watu hovyo 29/10 yeye hajibu hizo hoja analeta hoja ya dini yake.
Namheshimu Sana, na nimemtetea mwanawe kufanya biashara, nimekemea wanaomkosoa kwa kumtukana. Ila sitaacha kumkosoa kwa kutowadhibiti wabadhirifu wa mali za umma na wauwaji na watekaji. Pia nitamkosoa kwa uteuzi wake kwa baadhi ya watu inaonesha upendeleo(nepotism) kwa kujuana au undugu kuliko kuangalia sifa.