KERO Hivi hii shida ya maji ni huku tu au nchi nzima?
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Foffana

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2022
Posts
2,687
Reaction score
4,383
Hello Wakuu

Hii mitaa yetu huku Dar es Salaam tunakabiliwa na changamoto ya maji karibia wiki nzima na sio kawaida kabisa

Naomba kuuliza ni viunga vyetu tu hivi vya kimaskini au nchi nzima hili tatizo lipo?

Hii hali ikiendelea hivi mbele kutakuwa kubaya sana
 
Daaah hali ni mbaya sana hata sisi hatuna maji kabisa

Na kinachoumiza zaidi mama walimpa tuzo ya maji mawiki kadhaa nyuma

Alieleta uchawa na kutengeneza propaganda za uongo kwa ajili ya kufurahisha watawala ametuharibia sana nchi
 
Nikajua ni huku kwetu tu migombani ambako nndo tunafurahiaga maji misimu yote lakini awamu hii sijawahi ona ukame mpaka ardhi inapasuka mabomba hamna maji🗿😟🗿
Mtihani sana aisee hali ni mbaya
 
Daaah hali ni mbaya sana hata sisi hatuna maji kabisa

Na kinachoumiza zaidi mama walimpa tuzo ya maji mawiki kadhaa nyuma

Alieleta uchawa na kutengeneza propaganda za uongo kwa ajili ya kufurahisha watawala ametuharibia sana nchi
Dahh tunapoelekea pabaya sana
 
Na tunayoelekea kwenye machafuko ya amani tunahitaji maji mengi sana ili kuisafisha amani yetu
 
Hii ni maalumu kwa December 9, itachaguliwa kwenda kutafuta maji ama kwenda kwenye maandamano.
 
Nikajua labda ni tatizo la home kumbe ni Dar yote
Yaani siku ya 5 no water
 
Back
Top Bottom