Historia ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na mtunzi wake

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Jana tumesherehekea miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika (sorry, Tanzania Bara). Kwa sisi tuliozaliwa baada ya uhuru tuna mambo mengi ya kujifunza juu ya historia ya taifa letu.

Moja ya mambo ambayo mimi binafsi napenda kujua ni kuhusu historia ya huu wimbo wetu wa Taifa. Naomba kwa yeyote aliye na taarifa za kuhusu historia ya huu wimbo anifahamishe, na kwa nini unafanana kwa namna fulani na nyimbo za taifa za Zambia na Afrika Kusini.

Pia kuna huu wimbo wa "Tanzania Nakupenda" kwa nini huwa unapendwa kuimbwa kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa wakati si wimbo wa taifa?

Tafadhari naomba kuelimishwa kwani hii sehemu ya historia ya nchi yetu.
View attachment 243307 Screenshot from 2015-04-14 16:57:55.png
Ulitungwa na Enoch Sontonga, Mkosa (a Xhosa), wa Afrika Kusini.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, yaani "God Bless Africa," ni wimbo wa taifa letu la Tanzania na la Zambia.

Pia ulikuwa ni "wimbo wa taifa" wa African National Congress (ANC) walipokuwa wanapambana na wakandamizaji wao Makaburu. Na bado unatumika katika nchi hiyo ya Afrika Kusini. Sehemu za wimbo huo pia ziko katika wimbo wa taifa wa nchi ya Afrika Kusini.

Kwahiyo ni wimbo wa taifa wa nchi tatu: Tanzania, Zambia, na South Africa.

Umeimbwa pia katika nchi zingine, kwa mfano Zimbabwe na Namibia, na labda hata Botswana, Lesotho Swaziland, na Malawi kwa miaka mingi.

It has been one of the most inspiring songs in the struggle for freedom on our continent. It's considered to be a classic.
Hata kabla ya TANU (Tanganyika African National Union) kuanzishwa mwaka wa 1954, wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulikuwa unaimbwa Afrika Kusini.

Chama cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC), kilianzishwa miaka mingi kabla ya chama chetu cha TANU. Na kwenye mkutano wa kwanza uliofanyika Bloemfontein, South Africa, kuanzisha chama hicho mwaka wa 1912, waliimba Nkosi Sikelel' iAfrika. Nyerere alikuwa bado hajazaliwa. Na Hatukuwa na chama cha TANU miaka ile.

Chama cha kule Afrika Kusini kilichoanzishwa mwaka wa 1912 kiliitwa South African Native Congress chini ya uongozi wa John Dube, Mzulu, na Pixley ka I. Seme pia kutoka Natal kama Dube. Kikabadilishwa jina baadaye na kuitwa African National Congress (ANC).

Kuanzia mwaka wa 1925, wana ANC waliuchagua wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, kama wimbo wao wa taifa. Na bado unaimbwa leo.

Katika nyimbo za mataifa yetu ya Kiafrika, hakuna wimbo mwingine unaojulikana kama wimbo huo. Hata katika nchi za Afrika Magharibi, watu wengi wanajua Nkosi Sikelel' iAfrika ni wimbo gani na unamaanisha nini.

Watu wangapi nchi mbali mbali katika bara letu wanajua jina la wimbo wa taifa wa nchi ya Ghana ingawa ilikuwa ni nchi ya kwanza kupata uhuru miongoni mwa nchi zetu kusini ya jangwa la Sahara? Wangapi wanajua jina la wimbo wa taifa wa nchi ya Nigeria, nchi kubwa inayojulikana sana? Lakini ukienda huko, utawakuta wanaosema wanajua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika.

Ndiyo maana hata Kenya wanaimba wimbo huo. Unaimbwa na unafahamika katika nchi nyingi katika bara letu hata kaskazini ya bara hili. Ukienda Egypt, Algeria na nchi zingine huko, utawakuta watu wengi wanaojua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika. Wangapi katika nchi zingine za Kiafrika wanajua kuhusu wimbo wa taifa wa Uganda, au Malawi, au Burkina Faso? Lakini waulize kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika. Utawapata wengi waliousikia wimbo huo.

Enoch Sontonga alitoka Eastern Cape Province, jimbo la Wakosa (Xhosa), ambako pia ni nyumbani kwa Mandela. Alitunga wimbo huo katika lugha yake ya Kikosa na alitunga kama wimbo wa kanisa.

Alipotunga wimbo huo mwaka wa 1897, haukuimbwa hadharani mpaka mwaka wa 1899. Uliimbwa kanisani kwa mara ya kwanza mwaka huo. Halafu, baada ya miaka kumi na tatu, uliimbwa kwenye mkutano wa kwanza wa South African Native Congress mwaka wa 1912 uliofanyika Bloemfontein kuanzisha chama hicho kugombea haki za Wafrika.

Hata Watanganyika wengi waliokwenda kufanya kazi migodini Afrika Kusini miaka ya 1940s na 1950s waliujua wimbo huo. Walikuwa wanaimba Nkosi Sikelel' iAfrika pamoja na watu wa Afrika Kusini walipokuwa huko na waliporudi Tanganyika. Ninawafahamu wengi wao.

Na nina hakika kuna Watanganyika wengi, mara tu tulipopata uhuru, waliokuwa au walioziona music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika. Na ikiwa kuna ambao bado wanazo music sheets hizo, wanaweza kukuonyesha jina la Enoch Sontonga kama ndiyo mtungaji wa wimbo huo.

Nakumbuka sana nililiona jina lake kwenye music sheet hiyo kwa sababu hata mimi nilikuwa nayo. Na si mimi tu niliyekuwa nayo au niliyeiona music sheet hiyo ya wimbo huo. Ilikuwa katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza, na kichwa chake kilikuwa ni Mungu Ibariki Afrika, God Bless Africa, yaani Nkosi Sikelel' iAfrika.

Melody ya Nkosi Sikelel' iAfrika ilitungwa na Enoch Sontonga. Ukiisikiliza melody hiyo, hakuna tofauti hata kidogo na melody ya wimbo wetu wa taifa, Mungi Ibariki Afrika, au melody ya wimbo wa taifa kule Zambia. Sikiliza wimbo huo Youtube ambao mmoja wa waimbaji wake katika video ni Miriam Makeba. Pia lyrics za Nkosi Sikelel' iAfrika ziliandikwa na Enoch Sontonga, ingawa wimbo wetu una lyrics zake sehemu mbali mbali. Lakini chanzo chake ni wimbo uliotungwa na Enoch Sontonga: Nkosi Sikelel' iAfrika.

Kama nilivyosema kabla ya hapa, wimbo huo siyo wa watu wa Afrika Kusini tu. Enoch Sontonga aliandika na alitunga wimbo huo kama ni wimbo wa bara lote. Ndiyo maana alisema Nkosi Sikelel' iAfrika, God Bless Africa, na siyo God Bless South Africa.

Nyimbo zake nyingi zilikuwa ni nyimbo za huzuni kuhusu maisha magumu ya Wafrika chini ya utawala wa Wazungu waliokuwa wanawakandamiza Wafrika katika bara lote. Wimbo wake, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulitokana na maumivu hayo ya Wafrika ingawa pia ulikuwa ni wimbo wa kuwapa tumaini kwamba hawako peke yao. Mungu yuko nao, au yuko nasi, ingawa tunaumia na tunateswa na wanao tutawala kutoka nchi za Ulaya.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, uliwekwa kwenye sahani ya santuri kwa mara ya kwanza, London, mwaka wa 1923. Uliimbwa na Solomon Plaatje, mwimbaji maarafu wa Afrika Kusini ambaye pia alikuwa ni mmoja wa Wafrika walioanzisha chama cha South African Native Congress, Bloemfontein, South Africa, mwaka wa 1912.

Ni wimbo wetu pia kwa sababu Afrika ni moja. Ndiyo maana Enoch Sontonga alitunga wimbo unaosema Nkosi Sikelel' iAfrika - God Bless Africa.

Kwahiyo hatukuiba, na hatukuazima, wimbo huo. Ni wetu kama wao kule Afrika Kusini na nchi zingine. Na Enoch Sontonga alipewa full credit kwenye music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika, na baadayeTanzania, kama ndiyo mtungaji wa God Bless Africa.

Miaka yote hii, tangu nilipokuwa kijana mdogo miaka ya 1960s, nimejua kwamba wimbo huo ulitungwa na Enoch Sontonga kutoka Afrika Kusini. Kuna Watanzania wengine wanaojua ukweli huo. Si mimi tu.

Utumizi wetu wa wimbo huo, ambao pia ni wimbo wa taifa, Zambia, unaonyesha pia umoja na undugu wetu kama Wafrika. Ndiyo maana kulikuwa hata vyama vilivyopigania uhuru ambavyo majina yao yalifanana au yalikuwa karibu sana. Kwa mfano, African National Congress (ANC) iliyoundwa Tanganyika na kuongozwa na Zuberi Mtemvu na katibu wake mkuu John Chipaka ilikuwa na jina sawa na la chama cha Africa Kusini cha akina Mandela na wenzake. Pia chama cha kwanza kupigania uhuru Northern Rhodesia kilicho ongozwa na Harry Nkumbula kilikuwa kinaitwa African National Congress, na kiliendelea kuitwa hivyo hata baada ya wanachama wengine waliondoka na kuunda chama kingine, United National Independence Party (UNIP), chini ya uongozi wa Kenneth Kaunda.

Kenya kulikuwa na Kenya African Union (KAU) kabla ya Tanganyika African National Union. Baadaye KAU ikabadili jina kidogo na kuitwa KANU. Na ndugu zetu Zimbabwe waliunda chama kinachoitwa ZANU baada ya baadhi yao, pamoja na Robert Mugabe, kuondoka na kuachana na ZAPU.

Majina hayo, katika nchi zetu mbali mbali, yanafanana kwa sababu tunajiona kama ni ndugu, na ni kweli sisi sote ni ndugu. Pia inaonyesha ushirikiano wetu. Hata Uganda, jeshi lao ni Uganda People's Defence Forces (UPDF), jina linalotokana na jina la jeshi letu: Tanzania People's Defence Forces (TPDF).

Ni sawa na wimbo wa Nkosi Sikelel' iAfrika kuwa wimbo wa taifa Tanzania, Zambia, na South Africa.

Africa ni moja. Sisi sote ni ndugu bila kujali ukabila, rangi, dini, au asili.

Mungi Ibariki Afrika. Nkosi Sikelel' iAfrika.
 
Wimbo wetu wa taifa tuliuchukua kutoka afrika ya kusini. Wimbo huo ulikuwa ukijulikana kama Nkosi Sikelel'i Afrika.

Wimbo huo ulikuwa umetungwa na enoch sontongo mnamo mwaka 1897.ulianza kutumika kama wimbo wa kanisani.

Kwa hisia zake zenye kuchoma mioyo ya watu ulipenya hadi mashuleni ambako ulijipatia umaarufu mkubwa kwenye shule za watu weusi.

Haukuishia hapo uliingia pia mitaani ambako uligusa mti wa kila aliyekuwa na rangi nyeusi ya ngozi ya mwili wake.

Baadae wimbo huu ulianza kutumika wakati wa kufunga vikao vya chama cha ANC.
 
Na Tanzania Nakupenda si wimbo wa Taifa, lakini ni moja kati ya nyimbo zinazoheshimika sana nchini, kuufuatia wimbo wa Taifa.

Nakumbuka pale uwanja wa Taifa wakati wa Maombolezo ya kitaifa ya Mwalimu wimbo huu uliwaliza asilimia kubwa ya viongozi pale jukwaani..Kuna wakati nilipata tetesi kuwa ulitungwa na aliyekuwa Mwanasanaa Mahsusi hapa nchini, Marehemu Kanali Moses Nnauye!
 
Na Tanzania Nakupenda si wimbo wa Taifa, lakini ni moja kati ya nyimbo zinazoheshimika sana nchini, kuufuatia wimbo wa Taifa. ..Nakumbuka pale uwanja wa Taifa wakati wa Maombolezo ya kitaifa ya Mwalimu wimbo huu uliwaliza asilimia kubwa ya viongozi pale jukwaani..Kuna wakati nilipata tetesi kuwa ulitungwa na aliyekuwa Mwanasanaa Mahsusi hapa nchini, Marehemu Kanali Moses Nnauye!
Huu wimbo ni mzuri sana na una ujumbe mzuri pia!
 
..naomba kama kuna anayemfahamu mwananchi aliyetunga wimbo wa Taifa wa Tanganyika na baadaye Tanzania atueleze.

..nadhani mataifa mengine wanawajua watunzi wa nyimbo zao za Taifa lakini kwa hapa Tanzania sijapata kumsikia popote pale.


NB:

..wimbo wa Taifa wa Zanzibar nao umetungwa na nani?
 
..naomba kama kuna anayemfahamu mwananchi aliyetunga wimbo wa Taifa wa Tanganyika na baadaye Tanzania atueleze....

Ulitungwa na Enoch Sontonga, Mkosa (a Xhosa), wa Afrika Kusini.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, yaani "God Bless Africa," ni wimbo wa taifa letu la Tanzania na la Zambia.

Pia ulikuwa ni "wimbo wa taifa" wa African National Congress (ANC) walipokuwa wanapambana na wakandamizaji wao Makaburu. Na bado unatumika katika nchi hiyo ya Afrika Kusini. Sehemu za wimbo huo pia ziko katika wimbo wa taifa wa nchi ya Afrika Kusini.

Kwahiyo ni wimbo wa taifa wa nchi tatu: Tanzania, Zambia, na South Africa.

Umeimbwa pia katika nchi zingine, kwa mfano Zimbabwe na Namibia, na labda hata Botswana, Lesotho Swaziland, na Malawi kwa miaka mingi.

It has been one of the most inspiring songs in the struggle for freedom on our continent. It's considered to be a classic.
 
kwa haopa tanzania hatuna mtunzi wa wimbo wa taifa bali ungetutaka tukusaidie aliye uomba utumike kwetu
 
kwa haopa tanzania hatuna mtunzi wa wimbo wa taifa bali ungetutaka tukusaidie aliye uomba utumike kwetu

Labda ni Nyerere au mmoja wa viongozi wenzake tulipokuwa tunakaribia kupata uhuru aliyekuwa na wazo hilo kwamba tutumie wimbo huo kama wimbo wetu wa taifa.

Ni Nyerere, Kawawa, Kambona au kiongozi mwingine aliyekuwa wa kwanza kuwa na wazo hilo? Mimi sijui lakini nadhani ni Nyerere.

Nasema hivyo kwa sababu ya nia yake kubwa kuwasaidia ndugu zetu Afrika Kusini walipokuwa wanakandamizwa na Makaburu. Hata kabla ya nchi yetu kupata uhuru, Nyerere alikuwa mbele kupigania uhuru wa Wafrika wenzetu kule Afrika kusini. Soma hotuba yake, London, Uingereza, tarehe ishirini na sita mwezi wa Juni mwaka 1959 kwenye mkutano uliohutubiwa pia na Father Trevor Heddleston. Mkutano huo ulikuwa ni mwanzo wa Boycott South Africa Movement ambayo baadaye ilibadili jina mwaka wa 1960 na kuitwa Anti-Apartheid Movement.

Tanganyika ilikuwa ni nchi ya kwanza kuutumia wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika - Mungu Ibariki Afrika - kama wimbo wa taifa ingawa ulitungwa Afrika Kusini miaka mingi sana kabla ya uhuru wetu. Halafu Northern Rhodesia ilipopata uhuru mwezi wa Oktoba mwaka wa 1964 na kubadili jina lake kuitwa Zambia, ikawa nchi ya pili, baada ya Tanganyika, kuutumia wimbo huo kama wimbo wa taifa.

Na nchi ambako wimbo huo ulitoka, nchi ya Afrika Kusini, ikawa nchi ya mwisho kuutumia wimbo huo kama wimbo wa taifa baada ya nchi hiyo kukombolewa kutoka kwa Makaburu.
 
Ulitungwa na Enoch Sontonga, Mkosa (a Xhosa), wa Afrika Kusini.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, yaani "God Bless Africa," ni wimbo wa taifa letu la Tanzania na la Zambia...

Kwa hiyo mkuu kutokana na maelezo yako ni kwamba hatuna wimbo wa Taifa kwa maana mwimbo siyo uniquely Tanzania bali ni mwimbo tu ulioimbwa kwa Kiswahili.

Kama that is the case mimi naona kuna haja ya kuangalia hili swala la mwimbo wa taifa upya. Kwa nini tuige au kuazima wakati watunzi wazuri tunao tu? BTW asante sana kwa info.
 
Ni kweli wimbo huo siyo wa Kitanzania, au kama ulivyosema, siyo "uniquely Tanzanian."

Lakini bila shaka ulichaguliwa na viongozi wetu kuwa wimbo wetu wa taifa in a spirit of Pan-African solidarity ambayo haitambui mipaka ya nchi zetu; mipaka iliyochorwa na wakoloni kwenye ramani ya bara letu.

Kabla ya hapo, Wafrika walikuwa huru kwenda na kuhamia mahali popote katika bara letu. Ndiyo maana, kwa mfano, asili ya makabila yetu huku Afrika Mashariki pamoja na ya kati na kusini ya bara letu ni Afrika Magharibi - sehemu za Nigeria na Cameroon karne nyingi sana zilizopita. Na hivi karibuni, asili ya Wangoni ni Afrika kusini; Wamasai (Maasai) kutoka Sudan na kadhalika.

Tulikuwa huru kwenda na kuhamia mahali popote katika bara letu mpaka wakoloni walipokuja na kuanza kutuzuia kufanya hivyo.

Kwahiyo, ikiwa moyoni viongozi wetu waliamini kwamba Wafrika ni ndugu moja, na bara letu ni moja, ni rahisi kuelewa kwa nini walichagua wimbo uliotungwa na ndugu yetu wa Afrika Kusini bila kumaanisha kwamba hatuna watungaji wa nyimbo katika nchi yetu iliyokuwa inaitwa Tanganyika miaka ile.

Mara nyingi, Nyerere alisema tufungue mipaka yetu kuwawezesha Wafrika wenzetu kuhamia nchi zingine kwa urahisi; kwa mfano wale ambao wanateswa, wanaouawa katika vita na ambao hawana ardhi ya kutosha kama Rwanda na Burundi. Alisema pia nchi zetu za Afrika Mashariki - Kenya, Uganda na Tanzania - zikiungana, zisiwasahau jirani zetu huko Rwanda na Burundi kuwakaribisha katika muungano huo. Ni kati ya masuala aliyoyajadili pia katika hotuba yake ya mwisho pale Mlimani, Chuo Kikuu (UDSM), Novemba 1997, miaka miwili kabla hajatuondoka.

Sababu ni kwamba aliamini Afrika ni moja na sisi sote ni ndugu bila kujali ukabila, rangi, asili au mipaka liyowekwa na wakoloni kutugawanya.

Ukiangalia hivyo, na kutokana na msimamo huo wa Nyerere na viongozi wenzake kama Kawawa na wengineo, utaona kwa nini Nyerere na viongozi wenzake waliuona wimbo huo pia kama ni wimbo wetu sisi Watanganyika (baadaye Watanzania); wimbo ambao kichwa chake ni Nkosi Sikelel' iAfrika - Mungu Ibariki Afrika.

Hata mtungaji wa wimbo huo kule Afrika Kusini hakusema Mungu Ibariki Afrika Kusini tu. Alisema Mungu Ibariki Afrika.

Alitunga wimbo huo mwaka wa 1897. Alifariki 1905.
 
Tukiamua kurudia mada za zamani ni vizuri tuziunganishe. Hili ya wimbo wa taifa limewahi kujadiliwa kwenye thread nyingine niliyounganisha kwenye linki hii hapa. Sidhani kama kweli wimbo wa taifa ni ishu kubwa sana kwa sababu, kama ilivyo bendera, ni alama tu ya kurepresent taifa, siyo taifa lenyewe. Kuwa na wimbo wa taifa uliotungwa na mtu ambaye siyo raia wetu hakupunguzi lolote katika utaifa wetu. Kuna mataifa mengi tena mengine yenye nguvu sana ambayo yanatumia nyimbo za taifa ambazo hazikutungwa na raia wake; iweje kwetu iwe nongwa?

Ikulu yetu yenyewe haikusanifiwa wala kujengwa na raia wetu, je mnataka tufanye mabadiliko ili tujenge Ikulu mpya iliyosanifiwa na kujengwa na watanzania? Bunge letu pia ni hivyo hivyo, na hata uamuzi wa kumfanya twiga kuwa mnyama wa taifa haukufanywa na watanzania.

Mwenge unaotumiwa kwenye nembo ya JWTZ haukutengezwa na watanzania, huu ulitokana na wagiriki wa kale sana.
 
Ulitungwa na Enoch Sontonga, Mkosa (a Xhosa), wa Afrika Kusini.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, yaani "God Bless Africa," ni wimbo wa taifa letu la Tanzania na la Zambia...

Je Enock ni mtunzi wa melody na lyrics au vipi?

Je alitutungia sisi Watanzania au kama kawaida yetu tulinukuu bila kulipa hata hati miliki?

Je tulipopata Uhuru tuliimba wimbo gani kabla ya Muungano na Zanzibar?
 
Enoch Sontonga alitunga lyrics na melody za wimbo huo. Alikuwa ni choirmaster. Wimbo huo ulitukuka sana na ulianza kuimbwa na watu mbali mbali katika nchi hiyo ya Afrika Kusini. Halafu viongozi weusi walipoanzisha chama chao kugombea haki za Wafrika mwaka wa 1912, walianza kuutumia wimbo huo.

Wakati wa maisha yake, hakukuwa na nchi iliyokuwa inaitwa Tanzania. Wimbo huo ulitungwa mwaka wa 1897 nchi yetu ilipokuwa inatawaliwa na Wajerumani.

Kulikuwa na nchi iliyokuwa inaitwa Deutsch Ostafrika, yaani German East Africa. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza, ikagawanywa katika colonies mbili: Tanganyika iliyotawaliwa na Waingereza, na Ruanda-Urundi iliyotawaliwa na Wabeligiji.

It was really three countries which collectively constituted German East Africa: Tanganyika, and what later became the separate countries of Rwanda and Burundi.

Kwahiyo Enoch Sontonga hakututungia wimbo huo kama Watanzania. Alilitungia bara lote la Afrika. Ndiyo maana unaitwa, Nkosi Sikelel' iAfrika - God Bless Africa, au katika lugha yetu, Mungu Ibariki Afrika.

Tulipopata uhuru, wimbo wa taifa tulioimba ulikuwa ndiyo huo, Mungu Ibariki Afrika, uliotungwa na Enoch Sontonga. Nakumbuka sana. Nilikuwepo miaka ile ingawa nilikuwa kijana mdogo.

Kabla ya Muungano wetu na Zanzibar, tuliendelea kuimba wimbo huo. Verse ya kwanza ilisema Mungu Ibariki Afrika; ya pili ilisema Mungu Ibariki Tanganyika. Baada ya Muungano, verse ya kwanza ilibaki ilivyo, na ya pili tukabadili kidogo tu. Badala ya kuimba, "Mungu Ibariki Tanganyika," tukaanza kuimba, "Mungu Ibariki Tanzania."

Muungano ukivunjika, sisi Wabara tutaanza kuimba tena: "Mungu Ibariki Tanganyika"; pia "Tanganyika, Tanganyika, nakupenda kwa moyo wote...jina lako ni tamu sana."
 
Licha ya kuwa haukutungwa na Mtanzania lakini wimbo bado unawakilisha utaifa wetu.
 
Swali la JokaKuu bado lipo pale pale. Sontonga hakututungia lyrics. Ni lazima kuna mtu au watu ambao waliozitunga au kubadilisha za Sontonga ili ziendane na taifa changa la Tanganyika. Hawa ni muhimu kuwafahamu kama ilivyo kwa walioibuni bendera ili tuenzi mchango wao.

Tatizo nchini kwetu ni kuwa tulidhani kuwa chechote kisichomhusu Nyerere hakina maana. Ni lazima tubadilike na kuwatafuta wale wote waliochangia taifa hili kwa hali yeyote. Wote hao ni sehemu ya historia yetu.

Amandla.......
 
Nakumbuka kulikuwa na sheets za wimbo huo zilizochapishwa tulipopata uhuru. Na kwenye music sheets hizo, kulikuwa na jina la Enoch Sontonga aliyetajwa kama ni mtungaji wa wimbo huo.

Nilikuwa na sheet moja hiyo kwa miaka mingi lakini imepotea. Kuna Watanganyika (baadaye Watanzania)wengine waliokuwa na music sheets hizo na walioliona jina hilo la Enoch Sontonga.
 
..naomba kama kuna anayemfahamu mwananchi aliyetunga wimbo wa Taifa wa Tanganyika na baadaye Tanzania atueleze.

..nadhani mataifa mengine wanawajua watunzi wa nyimbo zao za Taifa lakini kwa hapa Tanzania sijapata kumsikia popote pale...

ulidesiwa kutoka South Africa. Siupendi huo wa kudesiwa south. bora ule wa TanzaniaX2 nakupenda kwa moyo wote, nchi yangu Tanzania jina lako ni Tamu sana.

Sasa badilisha weka Tanganyika, hapo mpaka nasikia burudani juu ya ngozi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom