Je, wajua wimbo wa taifa wa nchi ya Hispania hauna maneno?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,731
10,035
Screenshot_20240318-231759.jpg


Wimbo wa taifa la hispania (The Marcha Real) ni moja ya nyimbo za taifa zisizo na maneno rasmi, hata hivyo kuna maneno (mashairi) yaliwahi kuandikwa huko nyuma.

Aina mojawapo ni utunzi wa maneno yaliyotungwa kipindi cha utawala wa Alfonso XIII's na mwingine katika utawala wa Francisco Franco, hata hivyo hakuna toleo hata moja lililoweza kufanywa rasmi.
Tangu mwaka 1978 wimbo wa Spain uliendelea kuchezwa bila maneno, utunzi alioruhusiwa na general Franco ulitupiliwa mbali.
La_Marcha_Granadera_(1761).jpg


Mwaka 2007, aliyekuwa rais (Alejandro Blanco) baada ya kushuhudia wimbo wa "You'll never walk alone" ukiimbwa katika dimba la Anfield, alisema "najihisi kuvutiwa sana kutafuta maneno ambayo yangeimbiwa kwenye La Marcha tutakapokuwa tuna-hosti michuano ya michezo ya Olimpiki 2016. Mwaka huo huo chombo cha habari kinachoitwa Telecinco, kilivutiwa na maoni ya rais, na kuandaa mashindano ya kitaifa na kuweka hewani maandiko ya mashairi 25 kwenye tovuti yao ambayo kwa maoni yap waliona yakishabihiana na matakwa ya raisi.

Mshindi alichaguliwa, hata hivyo ni kura 40,000 tu ndio zilipigwa. Maneno ya utunzi wa Enrique Hernández-Luike (mwandishi wa magazeti), yaliyoongelea Uhuru, amani na katiba ndiyo yalimuibua mshindi. Ushairi ulioshinda uliimbwa na kwaya ya the Ronda de Aranzueque choir huko Pastrana, huku ikirekodiwa na chombo cha habari cha Kijerumani.

Hata hivyo, raisi aliandaa shindano jipya la utunzi wa maneno ya wimbo wa taifa, ambayo shindano hili lilitoa matokeo kati ya 2,000 na 7,000 (kulingana na chanzo). Timu binafsi ya baraza maalum lilichagua ushairi wa Paulino Cubero (hakua na kazi). Maneno hayo mapya ya wimbo yalipokea upinzani mkubwa, kitendo kilichofanya ushairi huo kuzuiwa siku tano tu baadae, na baadae yakafutwa kabisa.

Jumuiya mbalimbali za watu wa uhispania ziliamua kutumia maneno yao binafsi ambayo huyatumia huko mikoani kuimbia wimbo wa taifa hadi leo hii.
images (22).jpeg
 
Nchi nyingine zenye zisizo na lyrics kwenye nyimbo zao za taifa ni

  • Bosnia
  • Herzegovina
  • San Marino
-Kosovo
 
Na sisi huku tungeichukua ile tune ya wimbo wa Tazama Ramani na kuweka mashairi yenye uzalendo kwa nchi yetu, na hivyo kuwa na wimbo mpya wa Taifa.

Huu wimbo wa sasa wa Taifa ni wa hovyo! Kwanza tumeudesa kutoka kwa Wasauzi, na pia unahamasisha kuwaombea viongozi mafisadi na wezi wabobevu wa kura! Na hii bila shaka ndiyo sababu kuu inayochangia nchi yetu kuendelea kubakia hapa ilipo.
 
Back
Top Bottom