Historia ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na mtunzi wake

Wimbo wetu wa taifa tuliuchukua kutoka afrika ya kusini. Wimbo huo ulikuwa ukijulikana kama Nkosi Sikelel'i Afrika.

Wimbo huo ulikuwa umetungwa na enoch sontongo mnamo mwaka 1897.ulianza kutumika kama wimbo wa kanisani.

Kwa hisia zake zenye kuchoma mioyo ya watu ulipenya hadi mashuleni ambako ulijipatia umaarufu mkubwa kwenye shule za watu weusi.

Haukuishia hapo uliingia pia mitaani ambako uligusa mti wa kila aliyekuwa na rangi nyeusi ya ngozi ya mwili wake.

Baadae wimbo huu ulianza kutumika wakati wa kufunga vikao vya chama cha ANC.
Sio kweli..wimbo wa Taifa asa zile beti za Tanzania ulitokana na wimbo wa Bukoba Buhaya Union ..waliotaka kua na Taifa lao rasmi.
OMUKAMA ATUBELE EIHANGA LYAITU
OBELE ABANTU BAWE NA ABATWAZI BABO ...
Mtafute Bashiru Kakulwa
 
Tanzania nakupenda kwa moyo wote ni wimbo ambao una hisia kukiko wimbo wa taifa,wimbo huu wa TZ nakupenda ndiyo ulipaswa kua wimbo wetu wa Taifa,yamkini tuje tuusemee kwa nguvu
 
Na Tanzania Nakupenda si wimbo wa Taifa, lakini ni moja kati ya nyimbo zinazoheshimika sana nchini, kuufuatia wimbo wa Taifa. Nakumbuka pale uwanja wa Taifa wakati wa Maombolezo ya kitaifa ya Mwalimu wimbo huu uliwaliza asilimia kubwa ya viongozi pale jukwaani..Kuna wakati nilipata tetesi kuwa ulitungwa na aliyekuwa Mwanasanaa Mahsusi hapa nchini, Marehemu Kanali Moses Nnauye!
Tanzania ,Tanzania ulitungwa na babake Nape Brigedia Mosses Nnauye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom