Historia ya Wimbo wa Taifa wa Tanzania na mtunzi wake

ulidesiwa kutoka South Africa. Siupendi huo wa kudesiwa south. bora ule wa TanzaniaX2 nakupenda kwa moyo wote, nchi yangu Tanzania jina lako ni Tamu sana.

Sasa badilisha weka Tanganyika, hapo mpaka nasikia burudani juu ya ngozi.

teheteheh :) ... kazi ipo!!
 
Na ndipo hapo wazanzibari watakapotunga wimbo wao mwingine wenye mahadhi ya taarab...

Watunge wimbo wao wataifa mara ngapi, , Znz wana wimbo wao wa Taifa, wanabendera yao, labda tutarajia wawe na sarafu yao.
 
Huyo mtunzi wa South Afrika aliupata toka kwa Wazulu wa Tanzania a.ka Wangoni kina Njovu(Ndlovu).

Hivyo kwa kuwa Wangoni(Wazulu) wapo Tanzania, wimbo bado una nasaba ya Songea, Tanzania.
 
Mkuu Shani una hakika na hili? nafanya kuuliza tu sii ubishi, maanake nijuavyo ANC walikuwa infulenced na mwalimu ktk jitihada zake za Ukombozi wa Afrika.

Je, Ulitungwa lini na ulitafsiriwa na nani (kwa kiswahili) maanake nijuavyo hata Kenya nao wanautumia vile vile toka wapate Uhuru..hivyo nikitazama muda wa kutambuliwa ANC kwetu hasa ktk kupigania Uhuru ni baada yetu kuwa huru.

Hapa kidogo inanichanganya!
 
Mkandara said:
Mkuu Shani una hakika na hili?.. nafanya kuuliza tu sii ubishi, maanake nijuavyo ANC walikuwa infulenced na mwalimu ktk jitihada zake za Ukombozi wa Afrika..Je, Ulitungwa lini na ulitafsiriwa na nani (kwa kiswahili) maanake nijuavyo hata Kenya nao wanautumia vile vile toka wapate Uhuru..hivyo nikitazama muda wa kutambuliwa ANC kwetu hasa ktk kupigania Uhuru ni baada yetu kuwa huru..Hapa kidogo inanichanganya!

Mkandara,

..ANC kinakubalika kati ya vyama vikongwe vya siasa Afrika.

..i read somewhere kwamba ANC ilianzishwa mwaka 1912. hiyo ni takriban miaka 10 kabla ya Mwalimu kuzaliwa.

..mchango wa Tanzania/Mwalimu unaweza kuwa ktk kuwasaidia ANC kuanzisha tawi lao la Kijeshi ambalo lilikuwa likiitwa Umkhonto we Sizwe.
 
Hata kabla ya TANU (Tanganyika African National Union) kuanzishwa mwaka wa 1954, wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulikuwa unaimbwa Afrika Kusini.

Chama cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC), kilianzishwa miaka mingi kabla ya chama chetu cha TANU. Na kwenye mkutano wa kwanza uliofanyika Bloemfontein, South Africa, kuanzisha chama hicho mwaka wa 1912, waliimba Nkosi Sikelel' iAfrika. Nyerere alikuwa bado hajazaliwa. Na Hatukuwa na chama cha TANU miaka ile.

Chama cha kule Afrika Kusini kilichoanzishwa mwaka wa 1912 kiliitwa South African Native Congress chini ya uongozi wa John Dube, Mzulu, na Pixley ka I. Seme pia kutoka Natal kama Dube. Kikabadilishwa jina baadaye na kuitwa African National Congress (ANC).

Kuanzia mwaka wa 1925, wana ANC waliuchagua wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, kama wimbo wao wa taifa. Na bado unaimbwa leo.

Katika nyimbo za mataifa yetu ya Kiafrika, hakuna wimbo mwingine unaojulikana kama wimbo huo. Hata katika nchi za Afrika Magharibi, watu wengi wanajua Nkosi Sikelel' iAfrika ni wimbo gani na unamaanisha nini.

Watu wangapi nchi mbali mbali katika bara letu wanajua jina la wimbo wa taifa wa nchi ya Ghana ingawa ilikuwa ni nchi ya kwanza kupata uhuru miongoni mwa nchi zetu kusini ya jangwa la Sahara? Wangapi wanajua jina la wimbo wa taifa wa nchi ya Nigeria, nchi kubwa inayojulikana sana? Lakini ukienda huko, utawakuta wanaosema wanajua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika.

Ndiyo maana hata Kenya wanaimba wimbo huo. Unaimbwa na unafahamika katika nchi nyingi katika bara letu hata kaskazini ya bara hili. Ukienda Egypt, Algeria na nchi zingine huko, utawakuta watu wengi wanaojua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika. Wangapi katika nchi zingine za Kiafrika wanajua kuhusu wimbo wa taifa wa Uganda, au Malawi, au Burkina Faso? Lakini waulize kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika. Utawapata wengi waliousikia wimbo huo.

Enoch Sontonga alitoka Eastern Cape Province, jimbo la Wakosa (Xhosa), ambako pia ni nyumbani kwa Mandela. Alitunga wimbo huo katika lugha yake ya Kikosa na alitunga kama wimbo wa kanisa.

Alipotunga wimbo huo mwaka wa 1897, haukuimbwa hadharani mpaka mwaka wa 1899. Uliimbwa kanisani kwa mara ya kwanza mwaka huo. Halafu, baada ya miaka kumi na tatu, uliimbwa kwenye mkutano wa kwanza wa South African Native Congress mwaka wa 1912 uliofanyika Bloemfontein kuanzisha chama hicho kugombea haki za Wafrika.

Hata Watanganyika wengi waliokwenda kufanya kazi migodini Afrika Kusini miaka ya 1940s na 1950s waliujua wimbo huo. Walikuwa wanaimba Nkosi Sikelel' iAfrika pamoja na watu wa Afrika Kusini walipokuwa huko na waliporudi Tanganyika. Ninawafahamu wengi wao.

Na nina hakika kuna Watanganyika wengi, mara tu tulipopata uhuru, waliokuwa au walioziona music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika. Na ikiwa kuna ambao bado wanazo music sheets hizo, wanaweza kukuonyesha jina la Enoch Sontonga kama ndiyo mtungaji wa wimbo huo.

Nakumbuka sana nililiona jina lake kwenye music sheet hiyo kwa sababu hata mimi nilikuwa nayo. Na si mimi tu niliyekuwa nayo au niliyeiona music sheet hiyo ya wimbo huo. Ilikuwa katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza, na kichwa chake kilikuwa ni Mungu Ibariki Afrika, God Bless Africa, yaani Nkosi Sikelel' iAfrika.

Melody ya Nkosi Sikelel' iAfrika ilitungwa na Enoch Sontonga. Ukiisikiliza melody hiyo, hakuna tofauti hata kidogo na melody ya wimbo wetu wa taifa, Mungi Ibariki Afrika, au melody ya wimbo wa taifa kule Zambia. Sikiliza wimbo huo Youtube ambao mmoja wa waimbaji wake katika video ni Miriam Makeba. Pia lyrics za Nkosi Sikelel' iAfrika ziliandikwa na Enoch Sontonga, ingawa wimbo wetu una lyrics zake sehemu mbali mbali. Lakini chanzo chake ni wimbo uliotungwa na Enoch Sontonga: Nkosi Sikelel' iAfrika.

Kama nilivyosema kabla ya hapa, wimbo huo siyo wa watu wa Afrika Kusini tu. Enoch Sontonga aliandika na alitunga wimbo huo kama ni wimbo wa bara lote. Ndiyo maana alisema Nkosi Sikelel' iAfrika, God Bless Africa, na siyo God Bless South Africa.

Nyimbo zake nyingi zilikuwa ni nyimbo za huzuni kuhusu maisha magumu ya Wafrika chini ya utawala wa Wazungu waliokuwa wanawakandamiza Wafrika katika bara lote. Wimbo wake, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulitokana na maumivu hayo ya Wafrika ingawa pia ulikuwa ni wimbo wa kuwapa tumaini kwamba hawako peke yao. Mungu yuko nao, au yuko nasi, ingawa tunaumia na tunateswa na wanao tutawala kutoka nchi za Ulaya.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, uliwekwa kwenye sahani ya santuri kwa mara ya kwanza, London, mwaka wa 1923. Uliimbwa na Solomon Plaatje, mwimbaji maarafu wa Afrika Kusini ambaye pia alikuwa ni mmoja wa Wafrika walioanzisha chama cha South African Native Congress, Bloemfontein, South Africa, mwaka wa 1912.

Ni wimbo wetu pia kwa sababu Afrika ni moja. Ndiyo maana Enoch Sontonga alitunga wimbo unaosema Nkosi Sikelel' iAfrika - God Bless Africa.

Kwahiyo hatukuiba, na hatukuazima, wimbo huo. Ni wetu kama wao kule Afrika Kusini na nchi zingine. Na Enoch Sontonga alipewa full credit kwenye music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika, na baadayeTanzania, kama ndiyo mtungaji wa God Bless Africa.

Miaka yote hii, tangu nilipokuwa kijana mdogo miaka ya 1960s, nimejua kwamba wimbo huo ulitungwa na Enoch Sontonga kutoka Afrika Kusini. Kuna Watanzania wengine wanaojua ukweli huo. Si mimi tu.

Utumizi wetu wa wimbo huo, ambao pia ni wimbo wa taifa, Zambia, unaonyesha pia umoja na undugu wetu kama Wafrika. Ndiyo maana kulikuwa hata vyama vilivyopigania uhuru ambavyo majina yao yalifanana au yalikuwa karibu sana. Kwa mfano, African National Congress (ANC) iliyoundwa Tanganyika na kuongozwa na Zuberi Mtemvu na katibu wake mkuu John Chipaka ilikuwa na jina sawa na la chama cha Africa Kusini cha akina Mandela na wenzake. Pia chama cha kwanza kupigania uhuru Northern Rhodesia kilicho ongozwa na Harry Nkumbula kilikuwa kinaitwa African National Congress, na kiliendelea kuitwa hivyo hata baada ya wanachama wengine waliondoka na kuunda chama kingine, United National Independence Party (UNIP), chini ya uongozi wa Kenneth Kaunda.

Kenya kulikuwa na Kenya African Union (KAU) kabla ya Tanganyika African National Union. Baadaye KAU ikabadili jina kidogo na kuitwa KANU. Na ndugu zetu Zimbabwe waliunda chama kinachoitwa ZANU baada ya baadhi yao, pamoja na Robert Mugabe, kuondoka na kuachana na ZAPU.

Majina hayo, katika nchi zetu mbali mbali, yanafanana kwa sababu tunajiona kama ni ndugu, na ni kweli sisi sote ni ndugu. Pia inaonyesha ushirikiano wetu. Hata Uganda, jeshi lao ni Uganda People's Defence Force (UPDF), jina linalotokana na jina la jeshi letu: Tanzania People's Defence Forces (TPDF).

Ni sawa na wimbo wa Nkosi Sikelel' iAfrika kuwa wimbo wa taifa Tanzania, Zambia, na South Africa.

Africa ni moja. Sisi sote ni ndugu bila kujali ukabila, rangi, dini, au asili.

Mungi Ibariki Afrika. Nkosi Sikelel' iAfrika.
 
Taanzania, Tanzaniaaaaa!!
Nakupendaa kwa moyoo wooote!!
Iiinchi yaangu Tanzaniaaa!
Jina lakooo ni tamu sana...................

huu wimbo uliotungwa na askari wa KAR kutoka Tanganyika waliopigana vita kuu ya pili ya dunia kule India. walipokuwa wanapigana huko waliandaa harakati za kusaka uhuru wa tanganyika ila naamini waliporudi hawakufanya aproach mapema au walishindwa how to start ndo maana wanafikra wa amani walichukua usukani wa kudai uhuru bila kumwaga damu.... nadhani wimbo huu hakupendwa na waasisi wa taifa letu
 
Unaweza kutupatia link ya hiyo hotuba ya London, Uingereza, tarehe ishirini na sita mwezi wa Juni mwaka 1959 kwenye mkutano uliohutubiwa pia na Father Trevor Heddleston?
 
wanajf,
swali na jokakuu bado liko palepale. nimebahatika kusoma kitabu cha maisha ya chediel mgonja ambapo aliandika akidai kuwa kati ya wananchi walioshiriki katika shindano la kuandika wimbo wa taifa. pia alikuwa miongoni mwa wananchi waliopewa zawadi na kutambulishwa kwa ushiriki wao katika shindano hilo. according to mgonja, ilikubaliwa kuwa wimbo wa taifa wa tanganyika utakuwa na tune kama wimbo wa nkosi sekeleli wa afrika kusini ambao shwari ameutaja hapa.zaidi ya swali la jokakuu napenda kuwajua watanzania wote walioshiriki katika shindano hilo na vilevile kumjua ni nani alikuwa mshindi.
 
Asante Mkuu Shwari kwa ufafanuzi uliotulia na kujikamilisha. Kweli ni wimbo wa Afrika na hatukuuiba. Lakini swali la J.K. bado halijajibiwa. Nani alitafsiri hizo lyrics za Sontonga na kuongeza ubeti wa pili unaozungumzia Tanganyika/Tanzania? Na huo wimbo anaoulizia Msanii, " Tanzania, Tanzania...." nani aliutunga?

BTW, Mkuu Shwari, kuokana na taarifa yako wimbo huo uliimbwa kwenye mkutano wa A.N.C miaka 13 na sio 3, baada ya kuimbwa kanisani kwa mara ya kwanza. Hii haibadili shukrani zangu kwa shule uliyotupa.


Amandla.
 
Asante Mkuu Shwari kwa ufafanuzi uliotulia na kujikamilisha. Kweli ni wimbo wa Afrika na hatukuuiba. Lakini swali la J.K. bado halijajibiwa. Nani alitafsiri hizo lyrics za Sontonga na kuongeza ubeti wa pili unaozungumzia Tanganyika/Tanzania? Na huo wimbo anaoulizia Msanii, " Tanzania, Tanzania...." nani aliutunga?

BTW, Mkuu Shwari, kuokana na taarifa yako wimbo huo uliimbwa kwenye mkutano wa A.N.C miaka 13 na sio 3, baada ya kuimbwa kanisani kwa mara ya kwanza. Hii haibadili shukrani zangu kwa shule uliyotupa.

Amandla.......

Asante sana Fundi Mchundo. Nimesahihisha. Badala ya miaka mitatu, ni kumi na tatu wana ANC walipoanza kuimba wimbo huo mwaka wa 1912.

Sijui ni nani alitafsiri lyrics za Sontonga au ni nani aliyetunga ubeti wa pili kuhusu Tanganyika (baadaye Tanzania).

Pia sijui nani alitunga "Tanganyika, Tanganyika, nakupenda kwa moyo wote." Tulikuwa tunaimba sana wimbo huo.
 
Unaweza kutupatia link ya hiyo hotuba ya London, Uingereza, tarehe ishirini na sita mwezi wa Juni mwaka 1959 kwenye mkutano uliohutubiwa pia na Father Trevor Heddleston?

Nitakutafutia link hiyo, au hotuba yenyewe, lakini kwa sasa nitakupa yafwatayo hapa chini kuhusu suala hilo kutoka kitabu cha Godfrey Mwakikagile, Nyerere and Africa: End of an Era, ambacho naendelea kukisoma:

Julius Nyerere on the Boycott of South Africa
in a Letter to the Editor, Africa-South, October-December 1959


ON JUNE 26, 1959, Julius Nyerere was the principal speaker - along with Father Trevor Huddleston - at a meeting in London, which launched the Boycott South Africa Movement. It was re-named the Anti-Apartheid Movement in 1960.

That was at a time when most African leaders were only concerned about the independence struggle and problems in their own countries. Tanganyika itself was then not yet independent. But Nyerere still felt that it was necessary for the people of Tanganyika and others to get involved in the struggle for the liberation of South Africa from apartheid. An injustice to one is an injustice to all because humanity is one. As he stated in his letter to the editor of Africa-South, October-December 1959:

When I was a schoolboy, a friend of mine took me to the tailor one day and had me measured for a pair of shorts. We were great friends. His was mine and mine was his. He knew I needed a pair of shorts very badly. A few days later I got my pair of shorts, well made, fitting perfectly. I was proud of myself and proud of my friend. But it was not long before I discovered how my friend had obtained the money with which he had bought that pair of shorts for me. I returned it to him immediately. I could not disapprove of the manner in which the money had been obtained and still enjoy what the money had bought for me.

It is this same principle, which makes me now support the boycotting of South African goods. We in Africa hate the policies of the South African Government. We abhor the semi-slave conditions under which our brothers and sisters in South Africa live, work and produce the goods we buy. We pass resolutions against the hideous system and keep hoping that the United Nations and the governments of the whole world will one day put pressure on the South African Government to treat its non-European peoples as human beings.

But these resolutions and prayers to the United Nations are not enough in themselves. Governments and democratic organisations grind very slowly. Individuals do not have to. The question then is what an individual can do to influence the South African Government towards a human treatment of its non-white citizens.

Can we honestly condemn a system and at the same time employ it to produce goods, which we buy, and then enjoy with a clear conscience? Surely the customers of a business do more to keep it going than its shareholders. We who buy South African goods do more to support the system than the Nationalist Government or Nationalist industrialists.

Each one of us can remove his individual prop to the South African system by refusing to buy South African goods. There are millions of people in the world who support the South African Government in this way, and who can remove their support by the boycott. I feel it is only in this way that we can give meaning to our abhorrence of the system, and give encouragement to sympathetic governments of the world to act.

It is most fitting that Jamaica, that island which has solved its racial problems so well, should have taken the action it has in support of the boycott. It is equally fitting that the Trade Union Congress of Ghana should immediately have given its support. I was personally happy to participate in a meeting in London where the boycott was launched. Already the authors of apartheid are beginning to feel the sharp effect of the boycott. But they cannot feel it fully until every person in the whole world who disapproves of the South African system withdraws his support of it by withdrawing his contribution to its upkeep.

I must emphasise that the boycott is really a withdrawing of support, which each one of us gives to the racialists in South Africa by buying their goods. There is a very real sense in which we are part of the system we despise, because we patronise it, pay its running expenses.

We are not being called upon to make much of a sacrifice. We are not being called upon to go hungry and court imprisonment. That is the lot of our brothers and sisters inside South Africa. We are being asked to substitute other goods for South African goods, however much of a sacrifice this may mean to our suffering brethren in South Africa itself. We are not being called upon to support or not to support the oppressed in South Africa. We are being called upon to stop supporting those who oppress them.

The issue is as simple as that. Let every man and woman who disapproves of the South African system search his or her conscience, and decide to support or not to support the racialists of South Africa.

Source:

ANC Documents, African National Congress (ANC), South Africa. See also Voices, Africa Resource Center, On the Boycott of South Africa, by Julius Nyerere, then president of the Tanganyika African National Union (TANU), in a letter to the editor of Africa-South, October-December 1959.

Godfrey Mwakikagile: The principle enunciated here by Nyerere, and which he upheld throughout his life, was also reflected in his conduct when he was a student at Tabora. He was appointed a prefect, overseeing other students. Because of his status, he and the other prefects were entitled to double rations. Nyerere objected to that, saying all the students were equally entitled to the same amount of food. The double rations were dropped, and there was no more double-dipping for prefects, at least not as an entitlement. - (reproduced from Godfrey Mwakikagile, Nyerere and Africa: End of an Era, Fourth Edition, 2008, pp. 548 - 550).
 
una maanisha upi? huu



AU


AU



AU


Au


Sheet music



tz.gif

National Anthem of Tanzania
Mungu ibariki Afrika

  • Author: Author unknown
  • Composer: Enoch Mankayi Sontonga (1860-1904) -"South African"
  • Adopted: 1961
  • National Day: April 26 (1964) - Union Day (Tanganyika and Zanzibar)
    Formerly Tanganyika
Note: Tanzania's & Zambia's National Anthems have the same origin, but there are slight differences, the Composer is the same Enoch Mankayi Sontonga (1860-1904).
Same as Nkosi Sikelel' iAfrika for South Africa and also sound similra for Zimbabwe and Namibia.

Read more: http://www.joburg.org.za/content/view/240/52/#ixzz0e5vJpbfB

http://www.national-anthems.org/anthems/country/TANZANIA.
 
Last edited by a moderator:
Ongeza pia hapa kutoka Youtube Nkosi Sikelel' iAfrika, na wimbo wa taifa, Zambia, halafu linganisha nyimbo hizo na wimbo wetu wa taifa.

Zisikilize zote. Hakuna tofauti.
 
Shwari

Mimi huwa naangalia hata bendera yetu na ile ya Afrika Kusini, inaonekana kufanana fanana sana hasa mpangilio wa rangi zake. Huu uhusiano unazidi kupendeza.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom