ingawa ni picha ya kutengenezwa kwamba sio halisi ,lakini uhalisia upo hivyo katika jamii yetu.
ukosefu wa ajira sio hapa kwetu tu, sijawahi kutoka nje ya mipaka ya nchi hii lakini kazi yangu imenikutanisha na watu wengi wanaotoka kwenye mataifa makubwa yaliyoendelea huko Ulaya na Asia, kwa mujibu wao huko nako hakuna wepesi wa kupata ajira kwa kijana japo mazingira ya ukosefu wa ajira ni tofauti na sisi lakini hawana uafadhali kuliko sisi.
pia sio wakati huu tulio nao ndio ajira imekua ngumu hapana, tunaosoma hivi vitabu vya dini kuna mfalme mmoja alikua anahitaji vijana wanne wasomi hivyo akaagiza vijana karibu thelathini waingie darasani, walipo hitimu ni wanne tu walio pata ajira hao wengine hawakuhitajika kwa kua nafasi zao hazikuwepo.
ni swa na sasa hivi, elimu ya msingi ni lazima kwa kila mtoto anazaliwa katika taifa hili, kadhalika na elimu ya upili nayo imekua ya ulazima, ila kuna kuwa na mchujo kiasi, elimu ya juu nayo wanaendelea kuchuja kadhalika na elimu ya chuo nayo wanaoingia wamekua wamechujwa, mwisho kwenye ajira wanaotakiwa ni robo ya hao wote.
wanaanza elimu ya msingi 10, elimu ya upili 8 elimu ya juu 6 elimu ya chuo 4 na ajira 2.
kwa hio tunapoweka matajio 100% kwamba itapatikana ajira baada ya kuhitimu chuo ndio mwanzo wa makosa.
umuhimu wa elimu hautakuwa na mwisho hata kama matarajio ya faida ya hio Elimu yatakosena.
kwangu mimi naona sambamba na kugharamia elimu pia garamia baada ya elimu, ardhi yetu hapa Tanzania ni kubwa mno na yenye rutuba, tufanye miti, tupande mazao ya muda mrefu yanayostahimili ukame na maradhi ya mimea, tufuge wanyama kama mbuzi kuku na ngo'mbe, tujifunze ufundi , tufungue biashara ndogo ndogo na mengi mengi sana tunayoweza kufanya ili baada ya chuo isikosekane pa kuanzia.
tupunguze lawama kwa serikali japo kwa kiasi kikubwa serikali wameshindwa kuonyesha dira na mwelekeo kwa vinara wengi mwisho maumivu laumu na vilio vimekuwa vingi mno .
tusisahau pia kuzaa kwa mpangilio japo swala la uzazi ni la Mwenyezi Mungu .