Leo katika historia: Undani wa hayati Abeid Amani Karume (1905 - 1972)

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200

Leo katika historia April 7: Undani wa hayati abeid amani karume kuzaliwa mpaka kifo​

Bwana Abeid Amani Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa katika kitongoji cha Pongwe, Mudiria ya Mwera kisiwani Unguja tarehe 4 Agosti 1905. Karume ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watano ya Bwana Amani Karume na Bibi Amina binti Kadir (Amina Kadudu). Bwana Amani Karume na Bibi Amina Binti Kadudu walifunga ndoa huko Mwera.

Bwana Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu wanne wa baba mmoja na mama mmoja ambao ni wanaume wawili na wanawake wawili. Lakini wote walifariki kutokana na maradhi mbalimbali na kubaki yeye peke yake.

Kwa upande wa mama mmoja, Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu watatu, wanawake wawili na mwanaume mmoja ambao ni Asha, Shumbana na Othman. Baba yake mzazi Abeid Amani Karume alifariki dunia mwaka 1909 wakati Abeid Amani Karume akiwa na umri wa miaka minne.

Bwana Abeid Amani Karume alipata elimu ya Kurani na alianza masomo ya msingi katika skuli ya Mwera mwaka alofariki baba yake wa 1909, ambapo darasa lao lilikuwa la kwanza kuifungua skuli hiyo.

ka9.jpg

Hapa ndipo alipouwawa Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume miaka 44 iliyopita ndani ya ofisi za Makao Makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja, wakati akicheza bao na marafiki zake.

Matundu yanayoonekana ukutani ni ya risasi ambayo muuaji alimimina kabla na yeye kuuwawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa Hayati Karume. Sehemu hii imewekwa uzio maalumu ili kupahifadhi kama kumbukumbu, kwani kila kitu kipo vile vile kilivyokuwa siku hiyo.

Katika mwaka 1913 wakati akiwa na umri wa miaka 8 mama yake mzazi alimpeleka mjini Unguja kuendelea na masomo. Huko aliishi na mjomba wake aliyekuwa Sajenti katika jeshi la polisi la King African Rifle (KAR). Kwa bahati mbaya muda wake wote wa masomo ulikuwa miaka mitatu. Akiwa mjini Zanzibar Abeid Karume alipata marafiki kadhaa na kuvutiwa mno na harakati za bandari ya Zanzibar.

Kwa wakati huo, bandari ya Zanzibar ndiyo iliyokuwa kubwa Afrika mashariki. Pia Zanzibar, ilikuwa ndiyo kituo kikuu cha biashara katika eneo zima la Afrika mashariki na Maziwa Makuu.

Meli za mataifa ya nje hasa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Italia zilitia nanga bandarini Zanzibar kupakia na kupakua bidhaaa mbalimbali. Pia meli nyingi zilifika Zanzibar kuchukua maji safi ya kunywa yatokayo katika chemchem ya Mwanyanya. Meli hizo zilitoa ajira ya muda ya kusafisha mashine na kupangusa moshi. Mara nyingi mabaharia wa meli hizo waliajiri watoto kuwachukulia vikapu vya kununulia vyakula sokoni na kuwalipa ujira mdogo.

Kwa vile alipendelea kazi ya ubaharia, Abeid Amani Karume alifuatana na bwana mmoja aitwae Juma hadi bandarini. Alijumuika na watoto kadhaa waliofuata ajira ya muda huko bandarini. Ajira ya muda aliyoipata Karume huko bandarini ilimfanya akutane na mabaharia wa nchi mbalimbali na hivyo kuvutiwa na uzuri wa maisha ya ubaharia ya kusafiri na kuona nchi na watu mbalimbali. Hali hiyo ilimfanya Karume azidi hamu na ari ya kutafuta kazi ya ubaharia na kumuomba mama yake ruhusa ya kufanya kazi melini. Mwanzoni mama yake mzazi alikataa shauri hilo. Lakini baadaye alikubali ombi hilo baada ya kufahamishwa kuwa meli atakayofanyakazi mwanawe haitosafiri mbali na itatia nanga bandarini Zanzibar mara kwa mara.

Katika mwaka 1919 Abeid Amani Karume alipeleka barua ya kuomba kazi melini lakini alikataliwa kwa vile alikuwa na umri mdogo wa miaka 14. Hata hivyo hakuvunjika moyo na hakurudi Mwera kwa mama yake bali alimtembelea mara kwa mara. Alijiunga na timu za masumbwi na mpira wa miguu na kujuana na watu mbalimbali.

Kwa wakati huo timu za mpira wa miguu zilizojulikana Unguja zilikuwa ni timu ya skuli ya Kiungani iliyoanzishwa na Mwalimu Augostino Ramadhani na John Majaliwa. Mara nyingi timu hiyo ilishindana na timu ya watumishi serikalini. Baadaye kuliundwa timu nyengine za mpira wa miguu ambazo ni Vuga Boys, New Generation, United Service na New Kings. Karume alijiunga na timu ya New Generation na kucheza nafasi ya mstari wa mbele kushoto Inside left. Baadhi ya waanzilishi wa timu hiyo ni Bwana Malingumu, Shaaban Feruzi, Saad Shoka, Masoud Thani na Mzee wa Shangani.

Mara tu baada ya kujiunga na timu hiyo, Karume alichaguliwa kuwa msaidizi nahodha. Katika mwaka 1920 Abeid Amani Karume alikubaliwa kuwa baharia katika meli iliyoitwa Golden Crown (Taji la Dhahabu). Meli hiyo ilichukua abiria na mizigo kati ya bandari ya Zanzibar, Dar es Salaam, Pemba, Tanga, Mombasa na Mikindani huko Kilwa.

Baadaye alishuka katika meli hiyo na kufanya kazi katika meli nyengine iliyoitwa Cheko. Kwa bahati mbaya, meli hiyo iligonga mwamba na kuvunjika huko Kimbiji, nje kidogo ya Dar es Salaam lakini watu wote walinusurika.

Kazi ya ubaharia ilimpa tija Abeid Amani Karume kwani alinunua nyumba na viwanja kila alipopata nafasi ya kwenda nyumbani. Kwa muda wote huo Abeid Amani Karume alifanyakazi katika meli zilizopata leseni ya kufanyakazi katika mwambao wa Afrika Mashariki.

Katika mwaka 1922, akiwa na umri wa miaka kumi na saba, Abeid Amani Karume alipata kazi katika meli ya kampuni ya British Indian Steam Navigation Company ya Uingereza. Akiwa na kampuni hiyo Karume, alikaa nje miaka mitatu hadi 1925, aliporejea nyumbani kwa mapumziko.Tayari wakati huo, Karume alikwishatembelea nchi za Japan,Comoro,Madagascar, China,Singapore, New Zealand, Uingereza, Marekani, Canada, Ufaransa, Ubelgiji, India, Ureno, Hispania, Arabuni, Italia na Ugiriki.

Baada ya kupumzika kwa muda, Abeid Amani Karume alijiunga na kampuni ya Eastern Telegraph Company na kufanya kazi katika meli ya kampuni hiyo iitwayo Caranja. Meli hiyo ilikuwa ikitandika waya za simu baharini kati ya Zanzibar na Aden. Aliendelea na kazi ya ubaharia hadi mwaka 1938 alipoacha kazi hiyo kutokana na sababu mbalimbali. Karume alishauriwa na mama yake mzazi kuacha kazi hiyo. Vilevile aliacha kazi hiyo kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama duniani. Wakati huo, tayari vita vikuu vya pili vya dunia vilikaribia. Baadhi ya kazi alizofanya katika meli hizo ni Greaser, Fireman, Sailor na Headsailor.

Katika kipindi fulani cha kazi yake ya ubaharia, Abeid Amani Karume alifanyakazi chombo kimoja na Khamis Heri Ayemba kutoka Tanga. Wote wawili walirudi nyumbani wakati vita vya pili vya dunia vinakaribia. Baada ya kuacha kazi hiyo,Khamis Heri Ayemba alijihusisha na biashara huko kwao Tanga na kuwa tajiri mkubwa. Wakati wa kudai uhuru, Ayemba alishirikiana na Peter Muhando na Mwalimu Kihere kuunda tawi la TANU huko Tanga. Tarehe 23 Oktoba, 1955 wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua uongozi wa chama hicho. Katika uchaguzi huo, Khamis Heri Ayemba alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Peter Muhando alichaguliwa kuwa katibu.

Kutokana na kusafiri sehemu mbalimbali duniani, Abeid Amani Karume alijifunza mengi ya kimaisha na kuona jinsi gani mataifa ya ulaya na mabepari walivyotumia hila na ujanja kuzinyonya nchi za Afrika. Katika safari zake za ubaharia alikumbana na matatizo kadhaa. Tatizo kubwa zaidi alokumbana nalo ni dhoruba kali sana iliyoikumba meli yao wakati wakitokea Australia kwenda Lourenço Marques (Maputo -Msumbiji).

Katika miaka ya 1930, timu za mpira wa miguu Zanzibar zilikabiliwa na mgawanyiko. Kutokana na mgawanyiko huo, ndipo hapo mwaka 1931 timu zote za New Kings, Vuga Boys, United Service na New Generation zilipoungana na kuunda umoja wa michezo wa waafrika uloitwa “African Sports Club”. Timu hiyo ilikuwa na “A” na “B”, ambapo Karume alikuwa timu “A” iliyokuwa ya kwanza mwaka huo kwenda Tanganyika kucheza mechi ya kirafiki.

Umoja huo haukwishia hapo kwani katika mwaka 1934 uliundwa umoja wa Waafrika (African Association). Umoja huo wa Waafrika ndiyo ulogeuka kutoka kwenye michezo na kuwa umoja wa kisiasa.

Katika mwaka 1938 bandarini Zanzibar palikuwa na vijana wa Kiafrika walounda umoja uliyoitwa “Motorboats Association”. Vijana hao walikuwa wakivusha abiria kutoka bandarini hadi melini kwa kutumia mashua, kazi ambayo iliwasaidia kupata pesa chache za kuendeshea maisha. Lakini baadaye walijitokeza wafanyabiashara wajanja wenye asili ya Asia wenye uwezo na kununua boti za mashine na kuvusha abiria. Wafanyabiashara hao, walitumia mbinu ya kuungana na waafrika katika biashara hiyo.

Baada ya muda mfupi wafanyabiashara hao wenye asili ya Asia waliunda chama chao kilichoitwa Syndicate. Taratibu wafanyabiashara hao waliwaingiza ndugu zao na wale waafrika waanzilishi waligeuzwa vibarua na kulipwa ujira mdogo sana. Abeid Karume aliwakusanya waafrika hao kudai haki zao na kufanikiwa kufanya mapatano na waasia hao. Wamiliki wa maboti hao, walikubali kuwalipa waafrika asimilia 40% ya mapato yote na wao walichukua asilimia 60% na kugharamia uendeshaji na matengenezo ya boti hizo.

Baada ya mafanikio hayo Abeid Amani Karume alipata sifa nyingi na mwaka 1939 alianzisha harakati za kuunda chama cha mabaharia Zanzibar ili kupigania haki za wafanyakazi hao. Kwa wakati huo ilikuwa vigumu sana kuwashawishi watu wasojua mipango ya vyama vya wafanyakazi. Hivyo basi mwishoni mwa mwaka huo wa 1939 baadhi ya wafanyakazi waloshauriwa kuanzisha umoja huo walikataa kushiriki katika umoja huo. Karume hakusita na juhudi zake za kuanzisha umoja huo. Mwaka huohuo wa 1939, alionana na mzungu aitwae Bwana Douglas Basil Berber aliyekuwa Inspekta wa polisi kuomba kibali cha kuanzisha chama cha mabaharia wa Unguja na Pemba.

Mzungu huyo alimshauri Abeid Karume awakusanye wale wote wanaotaka kuanzisha chama hicho na wajiunge kwa mujibu wa sheria za India. Zanzibar kwa wakati huo haikuwa na sheria kuhusu vyama vya wafanyakazi Waafrika.

Baada ya kuwashauri wenzake, Abeid Karume alipata watu sita walokubali kujiunga na jumuiya hiyo. Watu hao ni Bakari Jabu, Miraji Mselem, Juma Maalim, Ismail Mbarouk, Mbarouk Salim na Kitwana Suwedi. Chama cha Mabaharia wa Unguja na Pemba kilipata usajili tarehe 30 Ogosti, 1949 na Makao Makuu yake yalikuwa Kisima Majongoo Zanzibar.

Sheria ya vyama vya wafanyakazi vya Zanzibar ilipitishwa mwaka 1931. Baadaye katika mwaka 1941, sheria hiyo ilifanyiwa mabadiliko na kuwa Sheria Nambari 3 ya vyama vya wafanyakazi.

Jumuiya za mwanzo za wafanyakazi kuanzishwa Zanzibar ni pamoja na Jumuiya ya Mabaharia, Jumuiya ya Wachukuzi na Umoja wa Watumishi wa Majumba ya Wazungu. Hadi kufika mwaka 1951 tayari chama cha mabaharia kilikuwa na wanachama 83. Tarehe 26 Oktoba 1959, Abeid Karume ambaye ni muasisi wa jumuiya ya mabaharia aliacha uongozi wa jumuiya hiyo na kujihusisha zaidi na siasa katika chama cha ASP ,lakini aliendelea kuwa mdhamini wa jumuiya hiyo. Kabla ya hapo katika mwaka 1942, Karume alikuwa katibu wa African Association na Rais wa Jumuiya hiyo hapo mwaka 1953. Baadaye nafasi hiyo ilishikiliwa na Bwana Herbert Barnabas.

Kwa mara ya kwanza Sheikh Abeid Karume alifunga ndoa na Bibi Pili binti Ahmed Ambari mwanzoni mwa miaka ya Arubaini. Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. Baada ya kutengana na wake hao wawili, Sheikh Karume alifunga ndoa na Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944 mwishoni mwa mwezi wa Novemba, harusi ambayo ilifanyika huko Bumbwini Misufini.

Bibi Fatma Gulamhussein Ismail alizaliwa Bumbwini mwaka 1929 akiwa ni mtoto wa Bwana Gulamhussein Ismail na Bibi Mwanasha Mbwana Ramadhani. Wazazi wa Bibi Fatma Karume ni wazaliwa wa Bumbwini. Bi Fatma Karume alipata elimu ya msingi katika skuli ya Bumbwini na kuolewa mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo hayo. Mara tu baada ya kufunga ndoa, Bibi Fatma Karume na Bwana Abeid Amani Karume walihamia mtaa wa Kisimamajongoo nyumba Nambari 18/22 mjini Unguja kwa Sheikh Karume. Nyumba nyengine mbili za Bwana Karume zilikuwa Gongoni na Michenzani.

Bi.Fatuma Karume alijifungua mtoto wa kwanza wa kike aliyeitwa Asha katika mwaka 1946, lakini mtoto huyo alifariki siku ya pili yake. Mtoto wa pili wa hayati Karume ni Amani Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 1 Novemba, 1948. Mtoto wake wa tatu ni Ali Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 24 Mei, 1950.

Mama yake mzazi Abeid Amani Karume, Bibi Amina binti Kadudu alifariki dunia 1963 na kuzikwa katika makaburi ya Michenzani. Wake wengine ambao waliolewa na Bwana Karume ni Bibi Nasra, Bibi Helemu na Bibi Fadya ambao kila mmoja alizaa nae mtoto mmoja wa kike.

Mbali ya kuanzisha chama cha mabaharia pia Abeid Amani Karume alikuwa muasisi wa Jumuiya ya Waafrika iliyoitwa African Dancing Club katika mwaka 1940. Jumuiya hiyo ilikuwa na lengo la kuwaunganisha pamoja vijana wa African Association.

Rais wa Jumuiya hiyo ya “African Dancing Club” alikuwa ni Bwana Pearcy Baraka, Abeid Karume alikuwa Katibu Mkuu na Mweka hazina ni Mtumwa Zaidi. Mbali ya kumiliki bendi ya muziki vilevile African Dancing Club ilinunua banda la zamani ambalo lilibomolewa na kujengwa makao makuu. Baadaye hapo tarehe 31 Januari, 1949 “African Dancing Club” ilibadilishwa jina na kuitwa “African Youth Union”.

Kuundwa kwa chama cha Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) mapema katika miaka ya 50 na kutolewa kwa mapendekezo ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Zanzibar katika mwaka 1957 yaliwafanya viongozi wa Jumuiya ya Waafrika African Association, na wale wa Shirazi Association waone umuhimu wa kushirikiana. Viongozi hao waliona ulazima wa kuungana kuwa kitu kimoja kupigania uhuru. Hivyo basi Jumuiya ya Shirazi Association ilimtuma Bwana Haji Khatibu aliyekuwa rafiki mkubwa wa Abeid Amani Karume apeleke shauri la kuunganishwa Jumuiya ya Waafrika na Jumuiya ya Washirazi.

Kabla ya kukutana, kila jumuiya ilifanya kikao cha faragha kujadili agenda ya mkutano. Shirazi Association walikubaliana kupendekeza jina la Abeid Karume kutoka African Association kuwa Rais wa chama kipya kitakachoundwa.

Nao African Association, walipanga kupendekeza jina la Sheikh Ameir Tajo kutoka Shirazi Association kuwa Rais wa chama kipya kitakachoundwa. Viongozi wa Jumuiya hizo walikubaliana kukutana kuanzia tarehe 1 hadi 5 Februari,1957. Mkutano ulifanyika kama ulivyopangwa hapo Mwembe Kisonge nyumbani kwa Abeid Amani Karume chini ya Mwenyekiti wake Muhidini Ali Omar. Kwa wakati huo, nyumba hiyo ya Abeid Karume alikuwa aliishi Hija Saleh na Haji Ali Mnoga.

Mkutano huo ulimalizika jioni ya tarehe 5 Februari, 1957 kwa viongozi hao kukubaliana kuunganisha Shirazi Association na African Association na kuunda chama kilichoitwa Afro – Shirazi Union.

Baadaye chama hicho kiliitwa Afro – Shirazi Party, jina ambalo lilitolewa na Ali Khamis kutoka Shirazi Association. Viongozi 18 wa African Association na Shirazi Association walikutana na kuunda Afro -Shirazi Party. Kumi ni kutoka African Association na Wanane kutoka Shirazi Association. Viongozi wa African Association walikuwa ni Abeid Amani Karume, Ibrahim Saadala, Abdalla Kassim Hanga, Bakari Jabu, Mtoro Rehani Kingo, Rajabu Swedi, Ali Juma Seif, Mtumwa Borafia, Saleh Juma na Saleh Mapete. Viongozi wa Shirazi Association ni Thabit Kombo Jecha, Muhidini Ali Omar, Ameir Tajo, Ali Khamis, Haji Khatibu, Mdungi Ussi, Ali Ameir na Othman Sharifu.

Katika mkutano huo pia alikuwepo mgeni mwalikwa Rais wa TANU, Mwalimu J.K. Nyerere na Katibu Mkuu wa chama cha TANU, Bwana Zubeir Mtemvu. Pia alihudhuria Bibi Maida Springer Kemp ambaye ni Mmarekani mweusi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Viwanda wa Marekani American Federation of Labour Congress of Industrial Organization AFL – C 10. Bibi Springer alikuwa ziarani barani Afrika kuangalia harakati za ukombozi na alifuatana na Mwalimu Nyerere aliyepitia Zanzibar akielekea Tanga kuitangaza TANU.

Chama cha Afro – Shirazi Party kilimteuwa Abeid Amani Karume kuwa Rais, Mtoro Rehani Kingo kuwa Makamo na Thabit Kombo Jecha ni Katibu Mkuu. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ni Ibrahim Saadala, Ali Khamis, Ameir Tajo, Mtumwa Borafia na Muhidini Ali Omar. Baadaye wajumbe wa Shirazi Association kutoka Pemba ambao ni Muhamed Shamte, Ali Sharif Mussa, Issa Sharif, Suleiman Ameir na Hassan Ali waliitwa na kufahamishwa juu ya kuunganishwa vyama hivyo.

Katika mwaka 1947 kuliundwa serikali za mitaa (Local Government) na Baraza la Manispaa (Township Council) lilianzishwa 1954. Abeid Karume alichaguliwa kuwa diwani (Councillor). Katika mwezi wa Juni 1957, Bwana Karume alikwenda nchini Ghana kuhudhuria sherehe za uhuru wa taifa hilo. Safari hiyo ilikuwa ni mwaliko wa kiongozi wa nchi hiyo, Bwana Kwameh Nkrumah kwa vyama vyote vya kupigania uhuru barani Afrika.

Abeid Amani Karume alipendekezwa na chama cha ASP kuwa mgombea wa kiti cha baraza la kutunga sheria wa jimbo la Ng’ambo, katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Zanzibar wa 1957. Katika uchaguzi huo, Abeid Amani Karume alijiandikisha katika jimbo la Ng’ambo kituo Nambari 84 ambacho ni Old Shimoni School (Mao tse Tung) akiwa ni mfanyabiashara, mkaazi wa Kisima Majongoo nyumba Nambari 18/22. Kadi yake ya kupigia kura ilikuwa Nambari 5818. Karume alishinda kiti hicho kwa kura 3,328 dhidi ya wapinzani wake Ali bin Muhsin Barwan wa ZNP aliyepata kura 918 na Ibuni Saleh mgombea binafsi aliyepata kura 55.

Miaka 40 iliyopita hapo tarehe 7 Aprili, 1972 Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume aliuwawa kwa kupigwa risasi katika jengo la Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shirazi hapo Kisiwandui mjini Zanzibar. Katika mfululizo wa makala haya mwandishi Ali Shaaban Juma anaelezea historia ya maisha ya Mwanamapinduzi huyo.

Hapo tarehe 15 Januari, 1960 Abeid Karume alishtakiwa na mfanyabiashara aitwae Punja Kara Haji mkaazi wa Darajani mjini Unguja. Karume alishtakiwa kwa madai ya kuvunja mkataba wa kukodi bekari ya mfanyabiashara huyo.

Kesi hiyo Nambari 4 ya 1960 (Civil Case Number 4 of 1960) ilitayarishwa na wakili Dinshaw Karai kwa niaba ya Punja Kara Haji. Ilidaiwa mbele ya Jaji G.J. Horsfall wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kuwa hapo tarehe 17 Aprili,1958, Abeid Karume na Thabit Kombo waliingia mkataba na Punja Kara Haji wa kukodi bekari ya Mchangani, nyumba nambari 2759 mali ya Punja Kara Haji.

Mkataba huo ulieleza kuwa kodi hiyo itakuwa ni ya miaka mitatu kuanzia tarehe 1 Mei 1958 kwa malipo ya Shilingi 7,395/20. Abeid Karume alitakiwa alipe Shilingi 550/- kila mwezi. Waraka wa makubaliano hayo ulotayarishwa na Wakili Dinshaw Karai ulitiwa saini hapo tarehe 18 Novemba, 1959 na Punja Kara Haji kwa niaba yake na Abeid Karume kwa niaba yake na kwa niaba ya Thabit Kombo. Mkataba huo ulishuhudiwa na mawakili Dinshaw Karai na Hemed Said.

Akiwasilisha madai dhidi ya Karume hapo tarehe 27 Januari, 1960 Punja Kara Haji alidai kuwa tarehe 16 Novemba, 1959 Abeid Karume alifika nyumbani kwake na kumueleza kuwa yeye na Thabit Kombo wanataka kuiacha bekari hiyo kwa vile ilikuwa inawatia hasara.

Punja Kara Haji alieleza mahakama hiyo kuwa, baada ya kupata kauli hiyo ya Abeid Karume walifikia makubaliano na mlalamikiwa. Abeid Karume alitakiwa alipe Shilingi 7,395/20 kama ilivyo katika mkataba wao wa tarehe 17 Aprili, 1958. Pia Karume alitakiwa akabidhi jengo la bekari hiyo kwa mwenyewe hapo tarehe 31 Disemba, 1959. Akiendelea kutoa ushahidi wake Punja Kara Haji alidai mahakamani kuwa yeye na Karume walikubaliana fedha hizo Shilingi 7,395/20 zilipwe kwa awamu kwa udhibitisho wa maandishi.

Awamu ya kwanza ya Shilingi 2,000/- ziwe zimelipwa ifikapo Disemba, 1959. Fedha zilizobaki Shilingi 5,395/20 zilipwe kidogo kidogo kwa wastani wa Shilingi 500/- kila mwezi kuanzia tarehe 1 Januari, 1960. Fedha hizo zilitakiwa ziendelee kulipwa kwa utaratibu huo kila siku ya mwanzo ya kila mwezi. Punja Kara alidai kuwa Abeid Karume alishindwa kulipa Shilingi 2,000/- hapo tarehe 1 Disemba,1959 na hakulipa Shilingi 500/-ilipofika tarehe 1 Januari,1960 kama walivyokubaliana. Kutokana na madai yake hayo, Punja Kara Haji alidai mahakamani alipwe na Abeid Karume Shilingi 7,395/20, asilimia 9% ya riba ya mwaka kuanzia tarehe ya hukumu na alipwe gharama za kesi hiyo.

Waraka ulomtaka Abeid Karume kufika mahakamani tarehe 8 Februari, 1960 saa 3.00 asubuhi ulitiwa saini na Mrajisi wa mahakama Hussein A. Rahim tarehe 27 Januari, 1960.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo Abeid Karume aliambia mahakama hiyo kuwa hapo tarehe 20 Januari, 1960 alimlipa Punja Kara Haji Shilingi 1,000/-. Pia walikubaliana kuwa deni lililobaki lilipwe kwa wastani wa Shilingi 500/- kila mwezi. Karume alieleza kuwa licha ya makubaliano hayo, mlalamikaji alifungua mashtaka hapo tarehe 27 Januari,1960 bila kutoa stakabadhi ya malipo ya Shilingi 1000/- alizopewa. Baada ya kupokea waraka wa kumtaka afike mahakamani kujibu kesi hiyo,Karume alikwenda kwa Punja Kara Haji ambaye alimweleza Karume kuwa mashtaka dhidi yake yalifunguliwa na wakili wake aitwae Dinshaw Karai baada ya kutofahamiana na mteja wake .

Punja alimuhakikishia Abeid Karume kuwa atamwambia wakili huyo aifute kesi hiyo mara moja. Abeid Karume alieleza mahakama hiyo kuwa, kwa vile aliyaamini maneno ya Punja hakuona ulazima wa kufika mahakamani kujibu kesi hiyo. Inaelekea mlalamikaji (Punja Kara Haji) alitumia fursa ya kutofika Karume mahakamani na kupata upendeleo wa kisheria kwa vile kesi hiyo ilisikilizwa upande wa mlalamikaji pekee. Hivyo moja kwa moja Punja Kara alidanganya mahakama kuwa Abeid Karume alilipa Shilingi Elfu moja baada ya kufunguliwa mashtaka. Karume alieleza mahakama hiyo kuwa vile vile hapo tarehe 7 Machi, 1960 alitoa mahakamani amana ya Shilingi 2,000/- taslimu na kupatiwa stakabadhi ya malipo yenye Nambari 153/60. Lakini licha ya ukweli huo mlalamikaji aliomba mahakama hapo tarehe 11 Machi, 1960 itoe uwamuzi wa kesi hiyo. Hata hivyo Abeid Karume alishinda kesi hiyo na madai ya mlalamikaji yalitupiliwa mbali.

Katika mwezi wa Oktoba 1960, Sheikh Abeid Amani Karume alihudhuria mkutano mkuu wa chama cha Malawi Congress Party huko Nkhota Kota katika Wilaya ya kati ya Nyasaland (Malawi) akiwakilisha chama cha Afro- Shirazi. Katika mkutano huo wanasiasa wanane wa mwisho wa Malawi walokuwa kizuizini waliachiliwa huru. Wanasiasa hao walitiwa ndani kwa kupinga mpango wa wakoloni wa kiingereza wa kuanzisha Shirikisho la Rhodesia (Zimbabwe) na Nyasaland (Malawi). Baada ya kuachiliwa huru, walikabidhiwa kwa kiongozi wa chama cha Malawi Congress Party, Dr. Kamuzu Banda. Aliyewakabidhi wanasiasa hao kwa Dr.Banda ni Gavana wa mwisho wa Uingereza katika koloni la Nyasaland. Msamaha huo ulitolewa muda mfupi kabla ya nchi hiyo kupata uhuru.

Wanasiasa waloachiliwa ni pamoja na Masauko Chipembere, Matupi Mkandawire, Chimtambi na wengineo. Mkutano huo wa chama cha Malawi Congress Party ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Malawi. Viongozi kadhaa wa kisiasa wa Jumuiya ya PAFMECA (Pan African Freedom Movement for East and Central Africa) walialikwa ambapo viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo walihudhuria mkutano huo.

Mbali ya Abeid Karume na ujumbe wake wa chama cha Afro -Shirazi kutoka Zanzibar, pia walihudhuria Marton Malianga wa chama cha Southern Rhodesia African National Congress cha Rhodesia (Zimbabwe) kilichoongozwa na Joshua Nkhomo. Wengine ni Namilando Mundia wa chama cha Zambia National Congress kilichongozwa na Kenneth Kaunda, Sheikh Amri Abeid Kaluta na Austin Shaba wa chama cha Tanganyika African National Union, TANU cha Tanganyika.

Vilevile alihudhuria Abdulrahman Babu na ujumbe wake wa chama cha ZNP cha Zanzibar. Kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya chama cha ASP na chama cha Malawi Congress Party cha Malawi, Abeid Karume aliwaalika kuitembelea Zanzibar baadhi ya viongozi wa chama hicho cha Malawi mapema mwaka 1965. Viongozi walotembelea Zanzibar kutoka Malawi ni Orton Chingolo Chirwa, Yatuta Chisiza, Willie Chokani, Augustine Bwanausi na Kanyama Chiume.

Abeid Karume alichaguliwa tena kuwa mjumbe wa baraza la kutunga sheria katika uchaguzi wa pili wa Januari, 1961, katika jimbo la Jang’ombe kwa tiketi ya ASP.

Mara tu baada ya kumalizika uchaguzi huo wa 1961 ulokuwa na utatanishi Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Waziri wa Afya na Mambo ya Kienyeji katika serikali ya pamoja ya miezi sita. Uchaguzi Mkuu wa tatu wa Zanzibar ulifanyika tarehe 1 Juni, 1963.

Karume alichaguliwa tena kuwa Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria katika jimbo la Kwahani na Jang’ombe. Akiwa Waziri wa Afya, Karume alishughulikia Afya, Ajira, Ujenzi wa Nyumba, Serikali za Mitaa na Serikali za Wilaya.

Baada ya kuundwa serikali ya Waziri Mkuu Muhammed Shamte kufuatia uchaguzi wa 1963, Abeid Amani Karume aliteuliwa kuwa kiongozi wa upinzani katika baraza la kutunga sheria.

Wakati wa matayarisho ya Mapinduzi ya 1964 Abeid Karume alikuwa mwenyekiti wa kamati ya watu kumi na nne walotayarisha Mapinduzi hayo kwa siri. Akiwa na umri wa miaka 59, Karume aliongoza Mapinduzi ya 1964 na alitangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na vilevile kubaki na wadhifa wake wa Rais wa Afro- Shirazi Party.

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliungana hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 27 Aprili, 1964.

Akiwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Abeid Amani Karume aliongoza ujumbe wa watu kumi na tisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutembelea mikoa ya Musoma, Mwanza na Bukoba kuanzia tarehe 5 -15 Septemba,1965. Lengo la ziara hiyo ni kuonana na wananchi wa mikoa hiyo na kuwahamasisha kuhusu uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Septemba, 1965.

Mheshimiwa Karume aliteuliwa kuwa mbunge wa bunge la Tanzania kupitia viti maalum vya kuteuliwa na Rais wa Tanzania. Karume alikuwa ni mmoja kati ya wabunge 23 wa kuteuliwa kutoka Zanzibar kama ilivyokuwa katiba ya wakati huo. Aliapishwa rasmi kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania katika ukumbi wa Arnatoghly mjini Dar es Salaam hapo tarehe 30 Septemba, 1965'

Tokeo la picha la Abeid Amani Karume

Katika mwezi wa Aprili 1967, Mzee Karume akifuatana na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere na wajumbe kadhaa wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Tanzania walikwenda nchini Misri kuhudhuria mkutano wa siku nne wa nchi tano za Afrika. Mkutano huo, uliandaliwa na Rais Gamal Abdel Nasser wa Misri. Katika ziara hiyo Mwalimu Nyerere na Mheshimiwa Abeid Karume walitunukiwa uraia wa jiji la Alexandria la nchini Misri. Baadhi ya viongozi mashuhuri walotembelea Zanzibar wakati wa uhai wa Abeid Amani Karume ni pamoja na Waziri Mkuu wa Hungary, Bwana Gyula Ka’llai, Makamo wa Rais wa Zambia Reuben Kamanga na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Korea Bwana Kang Ryang. Wengine ni Rais Gamal Abdel Nasser wa Misri, Rais Modibo Keite wa Mali , Rais askofu Makarios wa Cyprus na Rais marshal Josip Broz almaaruf kama Tito wa Yugoslavia.

Wengine ni Rais wa Hungary Bwana Pal Losonczi, Waziri Mkuu wa Guyana Bwana Burham na Waziri Mkuu wa Swaziland, Prince Makhosini Dlamini.

Mheshimiwa Abeid Amani Karume, kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar, na mmoja wa waasisi wa Chama cha Afro-Shirazi na Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania aliuwawa akiwa na umri wa miaka 67. Mauwaji hayo yalitokea siku ya Ijumaa ya tarehe 4 Aprili, 1972 saa 12.05 za jioni katika jengo la Makao Makuu ya ASP Kisiwandui Unguja Zanzibar.

Mara tu baada ya mauaji hayo hali ya hatari ilitangazwa na msako mkali wa wahalifu ulianza nchi nzima. Watuhumiwa kadhaa wakiwemo raia na maofisa wa vikosi vya ulinzi na usalama walitiwa mbaroni, ambapo mtuhumiwa mkuu akiwa ni profesa Abdulrahman Muhammed Babu aliyekamatwa huko Dar es Salaam.

Maziko ya Sheikh Abeid Amani Karume yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kutoka nchi mbalimbali duniani. Wengi wa wageni hao walianza kumiminika Zanzibar kuanzia saa tatu za asubuhi na kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu katika jumba la serikali Forodhani. Baada ya kutolewa heshima za mwisho,jeneza lilitolewa nje na kikosi cha wanajeshi ili kusaliwa katika uwanja wa Ikulu.

Baada ya marehemu kusaliwa hapo Ikulu, jeneza lilichukuliwa hadi Makao Makuu ya ASP Kisiwandui, kupitia barabara ya hospitali ya Mnazi Mmoja, Makumbusho, Mkunazini na kupindisha kuelekea barabara ya Michenzani hadi Makao Makuu ya Afro-Shirazi.

Hitma ya Abeid Karume ilisomwa katika ukumbi wa klabu ya wananchi tarehe 29 Julai, 1972 wakati wa jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kadhaa. Kwa vile miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni pamoja na kuwapatia makazi bora wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba, Mzee Abeid Amani Karume aliweka jiwe la msingi la jumba la kwanza la fleti 132 hapo Michenzani tarehe 4 Mei, 1970.

Baadhi ya taasisi ambazo zimepewa jina la Karume ni Chuo cha Ufundi cha Mbweni Zanzibar, Kiwanja cha Ndege cha Chake Chake Pemba, Viwanja vya mpira vya Musoma na Dar es Salaam na Kituo cha Televisheni ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa vile miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni pamoja na kuwapatia makazi bora wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba, Mzee Abeid Amani Karume aliweka jiwe la msingi la jumba la kwanza la fleti 132 hapo Michenzani tarehe 4 Mei, 1970. Jumba hilo la kwanza liligharimu jumla ya Shilingi milioni 4,752,000/-. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikusudia kujenga fleti 7000 katika mji wa Zanzibar na kutoa nafasi za makazi kwa wananchi 30 Elfu.

Kufuatia kuuwawa kwa Sheikh Abeid Amani Karume hapo tarehe 7 Aprili,1 972 watu 81 wakiwemo wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, raia na polisi walishtakiwa kwa makosa ya uhaini katika mahakama ya wananchi ya Zanzibar. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 14 Mei, 1973.

Kesi hiyo Nambari 292 ya 1973 iliendeshwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bwana Wolfgang Dourado akisaidiwa na Ussi Khamis Haji. Katika kesi hiyo mshtakiwa mkuu alitajwa kuwa ni Abdulrahman Muhammed Babu. Washtakiwa tisa walikiri makosa yao, washtakiwa 54 walikana makosa ambapo 18 akiwemo kiongozi wa njama hizo za uhaini na kutaka kuipindua serikali halali ya ASP, Abdulrahman Muhammed Babu walishtakiwa wakiwa hawapo kortini.

Mwanasheria Dourado aliiambia mahakama hiyo kwamba mkutano wa mwanzo wa siri ulifanywa Dar es Salaam wakati wa sherehe za Saba Saba za mwaka 1968. Babu alifanya karamu kubwa ya chakula cha mchana nyumbani kwake, ambapo washitakiwa kadhaa kutoka Zanzibar na Dar es Salaam walihudhuria karamu hiyo. Siku hiyo Babu ndiye aliyetoa shauri kuwa, kazi za wanachama wa Umma Party zipangwe vyengine na akatoa taarifa ya dhamira ya kutaka kuipindua serikali ya ASP. Baramia aliambiwa awe ni kiungo na mpelekaji habari baina ya Zanzibar na Dar es Salaam.

Kesi ya uhaini ilimalizika tarehe 15 Mei, 1974, ambapo washtakiwa 43 walihukumiwa adhabu ya kifo. Washtakiwa 11 walihukumiwa kwenda Chuo cha Mafunzo miaka 15 kila mmoja na wanne walipewa adhabu ya kifungo cha miaka 4 kila mmoja.

Washtakiwa 16 waliachiliwa kwa kukosekana ushahidi na wengine 6 walisamehewa kwa kukosa kesi ya kujibu. Mshtakiwa mmoja alifariki akiwa kizuizini kabla ya kumalizika kesi hiyo. Ingawa washitakiwa 43 walihukumiwa adhabu ya kifo, wakiwemo tisa walokiri kupanga njama za kumuua Sheikh Karume wote waliachiliwa huru siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Mei, 1974.

Kwa vyovyote vile, jina la Abeid Karume halitosahaulika katika historia ya ukombozi wa Zanzibar. Haiwezekani kuandika au kuzungumzia ukombozi na mafanikio ya maendeleo ya Zanzibar bila kujata jina la Abeid Karume.​

Pia soma
- Utata kifo cha hayati Abeid Karume
Source: leo katika historia April 7: Undani wa hayati abeid amani karume kuzaliwa mpaka kifo
 
Hao washtakiwa waliachiwa kisa nini au ni kweli Nyerere alihusika kummalizia Karume so wakaona nao hao kazi wamemalizwa?

Ibrahim Babu hivi yupo hai?
 
Leo katika historia April 7: Undani wa hayati abeid amani karume kuzaliwa mpaka kifo​

Abeid-Amani-Karume.jpg

Hayati Abeid Amani Karume

Katika mwaka 1922, akiwa na umri wa miaka kumi na saba, Abeid Amani Karume alipata kazi katika meli ya kampuni ya British Indian Steam Navigation Company ya Uingereza. Akiwa na kampuni hiyo Karume, alikaa nje miaka mitatu hadi 1925, aliporejea nyumbani kwa mapumziko.Tayari wakati huo, Karume alikwishatembelea nchi za Japan,Comoro,Madagascar,China,Singapore,New Zealand,Uingereza,Marekani, Canada,Ufaransa, Ubelgiji, India,Ureno,Hispania,Arabuni,Italia na Ugiriki.

Baada ya kupumzika kwa muda, Abeid Amani Karume alijiunga na kampuni ya Eastern Telegraph Company na kufanya kazi katika meli ya kampuni hiyo iitwayo Caranja. Meli hiyo ilikuwa ikitandika waya za simu baharini kati ya Zanzibar na Aden. Aliendelea na kazi ya ubaharia hadi mwaka 1938 alipoacha kazi hiyo kutokana na sababu mbalimbali. Karume alishauriwa na mama yake mzazi kuacha kazi hiyo. Vilevile aliacha kazi hiyo kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama duniani. Wakati huo, tayari vita vikuu vya pili vya dunia vilikaribia. Baadhi ya kazi alizofanya katika meli hizo ni Greaser, Fireman, Sailor na Headsailor.

Katika kipindi fulani cha kazi yake ya ubaharia, Abeid Amani Karume alifanyakazi chombo kimoja na Khamis Heri Ayemba kutoka Tanga. Wote wawili walirudi nyumbani wakati vita vya pili vya dunia vinakaribia. Baada ya kuacha kazi hiyo,Khamis Heri Ayemba alijihusisha na biashara huko kwao Tanga na kuwa tajiri mkubwa. Wakati wa kudai uhuru, Ayemba alishirikiana na Peter Muhando na Mwalimu Kihere kuunda tawi la TANU huko Tanga. Tarehe 23 Oktoba, 1955 wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua uongozi wa chama hicho. Katika uchaguzi huo, Khamis Heri Ayemba alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Peter Muhando alichaguliwa kuwa katibu.

Kutokana na kusafiri sehemu mbalimbali duniani, Abeid Amani Karume alijifunza mengi ya kimaisha na kuona jinsi gani mataifa ya ulaya na mabepari walivyotumia hila na ujanja kuzinyonya nchi za Afrika. Katika safari zake za ubaharia alikumbana na matatizo kadhaa. Tatizo kubwa zaidi alokumbana nalo ni dhoruba kali sana iliyoikumba meli yao wakati wakitokea Australia kwenda Lorence Marques (Msumbiji).

Katika miaka ya 1930, timu za mpira wa miguu Zanzibar zilikabiliwa na mgawanyiko. Kutokana na mgawanyiko huo, ndipo hapo mwaka 1931 timu zote za New Kings, Vuga Boys, United Service na New Generation zilipoungana na kuunda umoja wa michezo wa waafrika uloitwa “African Sports Club”. Timu hiyo ilikuwa na “A” na “B”, ambapo Karume alikuwa timu “A” iliyokuwa ya kwanza mwaka huo kwenda Tanganyika kucheza mechi ya kirafiki.

Umoja huo haukwishia hapo kwani katika mwaka 1934 uliundwa umoja wa Waafrika (African Association). Umoja huo wa Waafrika ndiyo ulogeuka kutoka kwenye michezo na kuwa umoja wa kisiasa.

Katika mwaka 1938 bandarini Zanzibar palikuwa na vijana wa Kiafrika walounda umoja uliyoitwa “Motorboats Association”. Vijana hao walikuwa wakivusha abiria kutoka bandarini hadi melini kwa kutumia mashua, kazi ambayo iliwasaidia kupata pesa chache za kuendeshea maisha. Lakini baadaye walijitokeza wafanyabiashara wajanja wenye asili ya Asia wenye uwezo na kununua boti za mashine na kuvusha abiria. Wafanyabiashara hao, walitumia mbinu ya kuungana na waafrika katika biashara hiyo.

Baada ya muda mfupi wafanyabiashara hao wenye asili ya Asia waliunda chama chao kilichoitwa Syndicate. Taratibu wafanyabiashara hao waliwaingiza ndugu zao na wale waafrika waanzilishi waligeuzwa vibarua na kulipwa ujira mdogo sana. Abeid Karume aliwakusanya waafrika hao kudai haki zao na kufanikiwa kufanya mapatano na waasia hao. Wamiliki wa maboti hao, walikubali kuwalipa waafrika asimilia 40% ya mapato yote na wao walichukua asilimia 60% na kugharamia uendeshaji na matengenezo ya boti hizo.

Baada ya mafanikio hayo Abeid Amani Karume alipata sifa nyingi na mwaka 1939 alianzisha harakati za kuunda chama cha mabaharia Zanzibar ili kupigania haki za wafanyakazi hao. Kwa wakati huo ilikuwa vigumu sana kuwashawishi watu wasojua mipango ya vyama vya wafanyakazi. Hivyo basi mwishoni mwa mwaka huo wa 1939 baadhi ya wafanyakazi waloshauriwa kuanzisha umoja huo walikataa kushiriki katika umoja huo. Karume hakusita na juhudi zake za kuanzisha umoja huo. Mwaka huohuo wa 1939, alionana na mzungu aitwae Bwana Douglas Basil Berber aliyekuwa Inspekta wa polisi kuomba kibali cha kuanzisha chama cha mabaharia wa Unguja na Pemba.

Mzungu huyo alimshauri Abeid Karume awakusanye wale wote wanaotaka kuanzisha chama hicho na wajiunge kwa mujibu wa sheria za India. Zanzibar kwa wakati huo haikuwa na sheria kuhusu vyama vya wafanyakazi Waafrika.

Baada ya kuwashauri wenzake, Abeid Karume alipata watu sita walokubali kujiunga na jumuiya hiyo. Watu hao ni Bakari Jabu, Miraji Mselem, Juma Maalim, Ismail Mbarouk, Mbarouk Salim na Kitwana Suwedi. Chama cha Mabaharia wa Unguja na Pemba kilipata usajili tarehe 30 Ogosti, 1949 na Makao Makuu yake yalikuwa Kisima majongoo.

Katika mwezi wa Aprili 1967, Mzee Karume akifuatana na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere na wajumbe kadhaa wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Tanzania walikwenda nchini Misri kuhudhuria mkutano wa siku nne wa nchi tano za Afrika. Mkutano huo, uliandaliwa na Rais Jamal Abdul Nasser wa Misri. Katika ziara hiyo Mwalimu Nyerere na Mheshimiwa Abeid Karume walitunukiwa uraia wa jiji la Alexandria. Baadhi ya viongozi mashuhuri walotembelea Zanzibar wakati wa uhai wa Abeid Amani Karume ni pamoja na Waziri Mkuu wa Hungary, Bwana Gyula Ka’llai, Makamo wa Rais wa Zambia Reuben Kamanga na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Korea Bwana Kang Ryang. Wengine ni Rais Jamal Abdel Nasser wa Misri, Rais Modibo Keite wa Mali , Rais Makarios wa Cyprus na Rais Tito wa Yugoslavia.

Wengine ni Rais wa Hungary Bwana Pal Losonczi, Waziri Mkuu wa Guyana Bwana Burham na Waziri Mkuu wa Swaziland, Prince Makhosini Dlamini.

Mheshimiwa Abeid Amani Karume, kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar, na mmoja wa waasisi wa Chama cha Afro-Shirazi na Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania aliuwawa akiwa na umri wa miaka 67. Mauwaji hayo yalitokea siku ya Ijumaa ya tarehe 4 Aprili, 1972 saa 12.05 za jioni katika jengo la Makao Makuu ya ASP Kisiwandui.

Mara tu baada ya mauaji hayo hali ya hatari ilitangazwa na msako mkali wa wahalifu ulianza nchi nzima. Watuhumiwa kadhaa wakiwemo raia na maofisa wa vikosi vya ulinzi na usalama walitiwa mbaroni, ambapo mtuhumiwa mkuu akiwa ni Abdulrahman Muhammed Babu aliyekamatwa huko Dar es Salaam.

Maziko ya Sheikh Abeid Amani Karume yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kutoka nchi mbalimbali duniani. Wengi wa wageni hao walianza kumiminika Zanzibar kuanzia saa tatu za asubuhi na kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu katika jumba la serikali Forodhani. Baada ya kutolewa heshima za mwisho,jeneza lilitolewa nje na kikosi cha wanajeshi ili kusaliwa katika uwanja wa Ikulu.

Baada ya marehemu kusaliwa hapo Ikulu, jeneza lilichukuliwa hadi Makao Makuu ya ASP Kisiwandui, kupitia barabara ya hospitali ya Mnazi Mmoja, Makumbusho, Mkunazini na kupindisha kuelekea barabara ya Michenzani hadi Makao Makuu ya Afro-Shirazi.

Hitma ya Abeid Karume ilisomwa katika ukumbi wa klabu ya wananchi tarehe 29 Julai, 1972 wakati wa jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kadhaa. Kwa vile miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni pamoja na kuwapatia makazi bora wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba, Mzee Abeid Amani Karume aliweka jiwe la msingi la jumba la kwanza la fleti 132 hapo Michenzani tarehe 4 Mei, 1970.

Baadhi ya taasisi ambazo zimepewa jina la Karume ni Chuo cha Ufundi cha Mbweni Zanzibar, Kiwanja cha Ndege cha Chake Chake Pemba, Viwanja vya mpira vya Musoma na Dar es Salaam na Kituo cha Televisheni ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa vile miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni pamoja na kuwapatia makazi bora wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba, Mzee Abeid Amani Karume aliweka jiwe la msingi la jumba la kwanza la fleti 132 hapo Michenzani tarehe 4 Mei, 1970. Jumba hilo la kwanza liligharimu jumla ya Shilingi milioni 4,752,000/-. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikusudia kujenga fleti 7000 katika mji wa Zanzibar na kutoa nafasi za makazi kwa wananchi 30 Elfu.

Kufuatia kuuwawa kwa Sheikh Abeid Amani Karume hapo tarehe 7 Aprili,1 972 watu 81 wakiwemo wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, raia na polisi walishtakiwa kwa makosa ya uhaini katika mahakama ya wananchi ya Zanzibar. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 14 Mei, 1973.

Kesi hiyo Nambari 292 ya 1973 iliendeshwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bwana Wolfgang Dourado akisaidiwa na Ussi Khamis Haji. Katika kesi hiyo mshtakiwa mkuu alitajwa kuwa ni Abdulrahman Muhammed Babu. Washtakiwa tisa walikiri makosa yao, washtakiwa 54 walikana makosa ambapo 18 akiwemo kiongozi wa njama hizo za uhaini na kutaka kuipindua serikali halali ya ASP, Abdulrahman Muhammed Babu walishtakiwa wakiwa hawapo kortini.

Mwanasheria Dourado aliiambia mahakama hiyo kwamba mkutano wa mwanzo wa siri ulifanywa Dar es Salaam wakati wa sherehe za saba saba za mwaka 1968. Babu alifanya karamu kubwa ya chakula cha mchana nyumbani kwake, ambapo wasitakiwa kadhaa kutoka Zanzibar na Dar es Salaam walihudhuria karamu hiyo. Siku hiyo Babu ndiye aliyetoa shauri kuwa, kazi za wanachama wa Umma Party zipangwe vyengine na akatoa taarifa ya dhamira ya kutaka kuipindua serikali ya ASP. Baramia aliambiwa awe ni kiungo na mpelekaji habari baina ya Zanzibar na Dar es Salaam.

Kesi ya uhaini ilimalizika tarehe 15 Mei, 1974, ambapo washtakiwa 43 walihukumiwa adhabu ya kifo. Washtakiwa 11 walihukumiwa kwenda Chuo cha Mafunzo miaka 15 kila mmoja na wanne walipewa adhabu ya kifungo cha miaka 4 kila mmoja.

Washtakiwa 16 waliachiliwa kwa kukosekana ushahidi na wengine 6 walisamehewa kwa kukosa kesi ya kujibu. Mshtakiwa mmoja alifariki akiwa kizuizini kabla ya kumalizika kesi hiyo. Ingawa washitakiwa 43 walihukumiwa adhabu ya kifo, wakiwemo tisa walokiri kupanga njama za kumuua Sheikh Karume wote waliachiliwa huru siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Mei, 1974.

Kwa vyovyote vile, jina la Abeid Karume halitosahaulika katika historia ya ukombozi wa Zanzibar. Haiwezekani kuandika au kuzungumzia ukombozi na mafanikio ya maendeleo ya Zanzibar bila kujata jina la Abeid Karume.​

Source: leo katika historia April 7: Undani wa hayati abeid amani karume kuzaliwa mpaka kifo
Mbona hujaelezea alivyokuwa anaua watu kama kina Hanga
 
Source ndiyo walivyoandika nami nimenukuu tu baada ya kuona kuna kipande cha historia nzuri. Vipande vingine labda tutabahatika kuvipata na kuvitupia humu ikiwa wazee wetu hawa mababu waliokuwepo enzi hizo wataamua kufunguka na ku-'share' matukio waliyoyaona enzi zao
 
Takataka, umeanza kuchemka mapema sana, Karume hajazaliwa Unguja bali Alizaliwa Malawi
 
Hao washtakiwa waliachiwa kisa nini au ni kweli Nyerere alihusika kummalizia Karume so wakaona nao hao kazi wamemalizwa?

Ibrahim Babu hivi yupo hai?

Walakini, wote 34 waliopewa
hukumu ya kifo, hatimaye hukumu hiyo ilibatilishwa na mrithi wa Karume ambaye alikuwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi . Na Wale wote waliopatikana na hatia waliachiliwa mwaka 1978...

convicted of involvement in President Karume's assassination. However, all 34 death sentences were eventually commuted by the succeeding Zanzibar Source : Amnesty.org
 
Leo katika historia April 7: Undani wa hayati abeid amani karume kuzaliwa mpaka kifo​

Bwana Abeid Amani Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa katika kitongoji cha Pongwe, Mudiria ya Mwera kisiwani Unguja tarehe 4 Agosti 1905. Karume ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watano ya Bwana Amani Karume na Bibi Amina binti Kadir (Amina Kadudu). Bwana Amani Karume na Bibi Amina Binti Kadudu walifunga ndoa huko Mwera.

Bwana Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu wanne wa baba mmoja na mama mmoja ambao ni wanaume wawili na wanawake wawili. Lakini wote walifariki kutokana na maradhi mbalimbali na kubaki yeye peke yake.

Kwa upande wa mama mmoja, Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu watatu, wanawake wawili na mwanaume mmoja ambao ni Asha, Shumbana na Othman. Baba yake mzazi Abeid Amani Karume alifariki dunia mwaka 1909 wakati Abeid Amani Karume akiwa na umri wa miaka minne.

Bwana Abeid Amani Karume alipata elimu ya Kurani na alianza masomo ya msingi katika skuli ya Mwera mwaka alofariki baba yake wa 1909, ambapo darasa lao lilikuwa la kwanza kuifungua skuli hiyo.

ka9.jpg

Hapa ndipo alipouwawa Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume miaka 44 iliyopita ndani ya ofisi za Makao Makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja, wakati akicheza bao na marafiki zake.

Matundu yanayoonekana ukutani ni ya risasi ambayo muuaji alimimina kabla na yeye kuuwawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa Hayati Karume. Sehemu hii imewekwa uzio maalumu ili kupahifadhi kama kumbukumbu, kwani kila kitu kipo vile vile kilivyokuwa siku hiyo.

Katika mwaka 1913 wakati akiwa na umri wa miaka 8 mama yake mzazi alimpeleka mjini Unguja kuendelea na masomo. Huko aliishi na mjomba wake aliyekuwa Sajenti katika jeshi la polisi la King African Rifle (KAR). Kwa bahati mbaya muda wake wote wa masomo ulikuwa miaka mitatu. Akiwa mjini Zanzibar Abeid Karume alipata marafiki kadhaa na kuvutiwa mno na harakati za bandari ya Zanzibar.

Kwa wakati huo, bandari ya Zanzibar ndiyo iliyokuwa kubwa Afrika mashariki. Pia Zanzibar, ilikuwa ndiyo kituo kikuu cha biashara katika eneo zima la Afrika mashariki na Maziwa Makuu.

Meli za mataifa ya nje hasa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Italia zilitia nanga bandarini Zanzibar kupakia na kupakua bidhaaa mbalimbali. Pia meli nyingi zilifika Zanzibar kuchukua maji safi ya kunywa yatokayo katika chemchem ya Mwanyanya. Meli hizo zilitoa ajira ya muda ya kusafisha mashine na kupangusa moshi. Mara nyingi mabaharia wa meli hizo waliajiri watoto kuwachukulia vikapu vya kununulia vyakula sokoni na kuwalipa ujira mdogo.

Kwa vile alipendelea kazi ya ubaharia, Abeid Amani Karume alifuatana na bwana mmoja aitwae Juma hadi bandarini. Alijumuika na watoto kadhaa waliofuata ajira ya muda huko bandarini. Ajira ya muda aliyoipata Karume huko bandarini ilimfanya akutane na mabaharia wa nchi mbalimbali na hivyo kuvutiwa na uzuri wa maisha ya ubaharia ya kusafiri na kuona nchi na watu mbalimbali. Hali hiyo ilimfanya Karume azidi hamu na ari ya kutafuta kazi ya ubaharia na kumuomba mama yake ruhusa ya kufanya kazi melini. Mwanzoni mama yake mzazi alikataa shauri hilo. Lakini baadaye alikubali ombi hilo baada ya kufahamishwa kuwa meli atakayofanyakazi mwanawe haitosafiri mbali na itatia nanga bandarini Zanzibar mara kwa mara.

Katika mwaka 1919 Abeid Amani Karume alipeleka barua ya kuomba kazi melini lakini alikataliwa kwa vile alikuwa na umri mdogo wa miaka 14. Hata hivyo hakuvunjika moyo na hakurudi Mwera kwa mama yake bali alimtembelea mara kwa mara. Alijiunga na timu za masumbwi na mpira wa miguu na kujuana na watu mbalimbali.

Kwa wakati huo timu za mpira wa miguu zilizojulikana Unguja zilikuwa ni timu ya skuli ya Kiungani iliyoanzishwa na Mwalimu Augostino Ramadhani na John Majaliwa. Mara nyingi timu hiyo ilishindana na timu ya watumishi serikalini. Baadaye kuliundwa timu nyengine za mpira wa miguu ambazo ni Vuga Boys, New Generation, United Service na New Kings. Karume alijiunga na timu ya New Generation na kucheza nafasi ya mstari wa mbele kushoto Inside left. Baadhi ya waanzilishi wa timu hiyo ni Bwana Malingumu, Shaaban Feruzi, Saad Shoka, Masoud Thani na Mzee wa Shangani.

Mara tu baada ya kujiunga na timu hiyo, Karume alichaguliwa kuwa msaidizi nahodha. Katika mwaka 1920 Abeid Amani Karume alikubaliwa kuwa baharia katika meli iliyoitwa Golden Crown (Taji la Dhahabu). Meli hiyo ilichukua abiria na mizigo kati ya bandari ya Zanzibar, Dar es Salaam, Pemba, Tanga, Mombasa na Mikindani huko Kilwa.

Baadaye alishuka katika meli hiyo na kufanya kazi katika meli nyengine iliyoitwa Cheko. Kwa bahati mbaya, meli hiyo iligonga mwamba na kuvunjika huko Kimbiji, nje kidogo ya Dar es Salaam lakini watu wote walinusurika.

Kazi ya ubaharia ilimpa tija Abeid Amani Karume kwani alinunua nyumba na viwanja kila alipopata nafasi ya kwenda nyumbani. Kwa muda wote huo Abeid Amani Karume alifanyakazi katika meli zilizopata leseni ya kufanyakazi katika mwambao wa Afrika Mashariki.

Katika mwaka 1922, akiwa na umri wa miaka kumi na saba, Abeid Amani Karume alipata kazi katika meli ya kampuni ya British Indian Steam Navigation Company ya Uingereza. Akiwa na kampuni hiyo Karume, alikaa nje miaka mitatu hadi 1925, aliporejea nyumbani kwa mapumziko.Tayari wakati huo, Karume alikwishatembelea nchi za Japan,Comoro,Madagascar, China,Singapore, New Zealand, Uingereza, Marekani, Canada, Ufaransa, Ubelgiji, India, Ureno, Hispania, Arabuni, Italia na Ugiriki.

Baada ya kupumzika kwa muda, Abeid Amani Karume alijiunga na kampuni ya Eastern Telegraph Company na kufanya kazi katika meli ya kampuni hiyo iitwayo Caranja. Meli hiyo ilikuwa ikitandika waya za simu baharini kati ya Zanzibar na Aden. Aliendelea na kazi ya ubaharia hadi mwaka 1938 alipoacha kazi hiyo kutokana na sababu mbalimbali. Karume alishauriwa na mama yake mzazi kuacha kazi hiyo. Vilevile aliacha kazi hiyo kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama duniani. Wakati huo, tayari vita vikuu vya pili vya dunia vilikaribia. Baadhi ya kazi alizofanya katika meli hizo ni Greaser, Fireman, Sailor na Headsailor.

Katika kipindi fulani cha kazi yake ya ubaharia, Abeid Amani Karume alifanyakazi chombo kimoja na Khamis Heri Ayemba kutoka Tanga. Wote wawili walirudi nyumbani wakati vita vya pili vya dunia vinakaribia. Baada ya kuacha kazi hiyo,Khamis Heri Ayemba alijihusisha na biashara huko kwao Tanga na kuwa tajiri mkubwa. Wakati wa kudai uhuru, Ayemba alishirikiana na Peter Muhando na Mwalimu Kihere kuunda tawi la TANU huko Tanga. Tarehe 23 Oktoba, 1955 wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua uongozi wa chama hicho. Katika uchaguzi huo, Khamis Heri Ayemba alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Peter Muhando alichaguliwa kuwa katibu.

Kutokana na kusafiri sehemu mbalimbali duniani, Abeid Amani Karume alijifunza mengi ya kimaisha na kuona jinsi gani mataifa ya ulaya na mabepari walivyotumia hila na ujanja kuzinyonya nchi za Afrika. Katika safari zake za ubaharia alikumbana na matatizo kadhaa. Tatizo kubwa zaidi alokumbana nalo ni dhoruba kali sana iliyoikumba meli yao wakati wakitokea Australia kwenda Lourenço Marques (Maputo -Msumbiji).

Katika miaka ya 1930, timu za mpira wa miguu Zanzibar zilikabiliwa na mgawanyiko. Kutokana na mgawanyiko huo, ndipo hapo mwaka 1931 timu zote za New Kings, Vuga Boys, United Service na New Generation zilipoungana na kuunda umoja wa michezo wa waafrika uloitwa “African Sports Club”. Timu hiyo ilikuwa na “A” na “B”, ambapo Karume alikuwa timu “A” iliyokuwa ya kwanza mwaka huo kwenda Tanganyika kucheza mechi ya kirafiki.

Umoja huo haukwishia hapo kwani katika mwaka 1934 uliundwa umoja wa Waafrika (African Association). Umoja huo wa Waafrika ndiyo ulogeuka kutoka kwenye michezo na kuwa umoja wa kisiasa.

Katika mwaka 1938 bandarini Zanzibar palikuwa na vijana wa Kiafrika walounda umoja uliyoitwa “Motorboats Association”. Vijana hao walikuwa wakivusha abiria kutoka bandarini hadi melini kwa kutumia mashua, kazi ambayo iliwasaidia kupata pesa chache za kuendeshea maisha. Lakini baadaye walijitokeza wafanyabiashara wajanja wenye asili ya Asia wenye uwezo na kununua boti za mashine na kuvusha abiria. Wafanyabiashara hao, walitumia mbinu ya kuungana na waafrika katika biashara hiyo.

Baada ya muda mfupi wafanyabiashara hao wenye asili ya Asia waliunda chama chao kilichoitwa Syndicate. Taratibu wafanyabiashara hao waliwaingiza ndugu zao na wale waafrika waanzilishi waligeuzwa vibarua na kulipwa ujira mdogo sana. Abeid Karume aliwakusanya waafrika hao kudai haki zao na kufanikiwa kufanya mapatano na waasia hao. Wamiliki wa maboti hao, walikubali kuwalipa waafrika asimilia 40% ya mapato yote na wao walichukua asilimia 60% na kugharamia uendeshaji na matengenezo ya boti hizo.

Baada ya mafanikio hayo Abeid Amani Karume alipata sifa nyingi na mwaka 1939 alianzisha harakati za kuunda chama cha mabaharia Zanzibar ili kupigania haki za wafanyakazi hao. Kwa wakati huo ilikuwa vigumu sana kuwashawishi watu wasojua mipango ya vyama vya wafanyakazi. Hivyo basi mwishoni mwa mwaka huo wa 1939 baadhi ya wafanyakazi waloshauriwa kuanzisha umoja huo walikataa kushiriki katika umoja huo. Karume hakusita na juhudi zake za kuanzisha umoja huo. Mwaka huohuo wa 1939, alionana na mzungu aitwae Bwana Douglas Basil Berber aliyekuwa Inspekta wa polisi kuomba kibali cha kuanzisha chama cha mabaharia wa Unguja na Pemba.

Mzungu huyo alimshauri Abeid Karume awakusanye wale wote wanaotaka kuanzisha chama hicho na wajiunge kwa mujibu wa sheria za India. Zanzibar kwa wakati huo haikuwa na sheria kuhusu vyama vya wafanyakazi Waafrika.

Baada ya kuwashauri wenzake, Abeid Karume alipata watu sita walokubali kujiunga na jumuiya hiyo. Watu hao ni Bakari Jabu, Miraji Mselem, Juma Maalim, Ismail Mbarouk, Mbarouk Salim na Kitwana Suwedi. Chama cha Mabaharia wa Unguja na Pemba kilipata usajili tarehe 30 Ogosti, 1949 na Makao Makuu yake yalikuwa Kisima Majongoo Zanzibar.

Sheria ya vyama vya wafanyakazi vya Zanzibar ilipitishwa mwaka 1931. Baadaye katika mwaka 1941, sheria hiyo ilifanyiwa mabadiliko na kuwa Sheria Nambari 3 ya vyama vya wafanyakazi.

Jumuiya za mwanzo za wafanyakazi kuanzishwa Zanzibar ni pamoja na Jumuiya ya Mabaharia, Jumuiya ya Wachukuzi na Umoja wa Watumishi wa Majumba ya Wazungu. Hadi kufika mwaka 1951 tayari chama cha mabaharia kilikuwa na wanachama 83. Tarehe 26 Oktoba 1959, Abeid Karume ambaye ni muasisi wa jumuiya ya mabaharia aliacha uongozi wa jumuiya hiyo na kujihusisha zaidi na siasa katika chama cha ASP ,lakini aliendelea kuwa mdhamini wa jumuiya hiyo. Kabla ya hapo katika mwaka 1942, Karume alikuwa katibu wa African Association na Rais wa Jumuiya hiyo hapo mwaka 1953. Baadaye nafasi hiyo ilishikiliwa na Bwana Herbert Barnabas.

Kwa mara ya kwanza Sheikh Abeid Karume alifunga ndoa na Bibi Pili binti Ahmed Ambari mwanzoni mwa miaka ya Arubaini. Mke wake wa pili ni Bibi Ashura binti Maisara. Baada ya kutengana na wake hao wawili, Sheikh Karume alifunga ndoa na Bibi Fatma binti Gulamhussein Ismail (Fatma Karume) katika mwaka 1944 mwishoni mwa mwezi wa Novemba, harusi ambayo ilifanyika huko Bumbwini Misufini.

Bibi Fatma Gulamhussein Ismail alizaliwa Bumbwini mwaka 1929 akiwa ni mtoto wa Bwana Gulamhussein Ismail na Bibi Mwanasha Mbwana Ramadhani. Wazazi wa Bibi Fatma Karume ni wazaliwa wa Bumbwini. Bi Fatma Karume alipata elimu ya msingi katika skuli ya Bumbwini na kuolewa mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo hayo. Mara tu baada ya kufunga ndoa, Bibi Fatma Karume na Bwana Abeid Amani Karume walihamia mtaa wa Kisimamajongoo nyumba Nambari 18/22 mjini Unguja kwa Sheikh Karume. Nyumba nyengine mbili za Bwana Karume zilikuwa Gongoni na Michenzani.

Bi.Fatuma Karume alijifungua mtoto wa kwanza wa kike aliyeitwa Asha katika mwaka 1946, lakini mtoto huyo alifariki siku ya pili yake. Mtoto wa pili wa hayati Karume ni Amani Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 1 Novemba, 1948. Mtoto wake wa tatu ni Ali Abeid Karume aliyezaliwa tarehe 24 Mei, 1950.

Mama yake mzazi Abeid Amani Karume, Bibi Amina binti Kadudu alifariki dunia 1963 na kuzikwa katika makaburi ya Michenzani. Wake wengine ambao waliolewa na Bwana Karume ni Bibi Nasra, Bibi Helemu na Bibi Fadya ambao kila mmoja alizaa nae mtoto mmoja wa kike.

Mbali ya kuanzisha chama cha mabaharia pia Abeid Amani Karume alikuwa muasisi wa Jumuiya ya Waafrika iliyoitwa African Dancing Club katika mwaka 1940. Jumuiya hiyo ilikuwa na lengo la kuwaunganisha pamoja vijana wa African Association.

Rais wa Jumuiya hiyo ya “African Dancing Club” alikuwa ni Bwana Pearcy Baraka, Abeid Karume alikuwa Katibu Mkuu na Mweka hazina ni Mtumwa Zaidi. Mbali ya kumiliki bendi ya muziki vilevile African Dancing Club ilinunua banda la zamani ambalo lilibomolewa na kujengwa makao makuu. Baadaye hapo tarehe 31 Januari, 1949 “African Dancing Club” ilibadilishwa jina na kuitwa “African Youth Union”.

Kuundwa kwa chama cha Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) mapema katika miaka ya 50 na kutolewa kwa mapendekezo ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Zanzibar katika mwaka 1957 yaliwafanya viongozi wa Jumuiya ya Waafrika African Association, na wale wa Shirazi Association waone umuhimu wa kushirikiana. Viongozi hao waliona ulazima wa kuungana kuwa kitu kimoja kupigania uhuru. Hivyo basi Jumuiya ya Shirazi Association ilimtuma Bwana Haji Khatibu aliyekuwa rafiki mkubwa wa Abeid Amani Karume apeleke shauri la kuunganishwa Jumuiya ya Waafrika na Jumuiya ya Washirazi.

Kabla ya kukutana, kila jumuiya ilifanya kikao cha faragha kujadili agenda ya mkutano. Shirazi Association walikubaliana kupendekeza jina la Abeid Karume kutoka African Association kuwa Rais wa chama kipya kitakachoundwa.

Nao African Association, walipanga kupendekeza jina la Sheikh Ameir Tajo kutoka Shirazi Association kuwa Rais wa chama kipya kitakachoundwa. Viongozi wa Jumuiya hizo walikubaliana kukutana kuanzia tarehe 1 hadi 5 Februari,1957. Mkutano ulifanyika kama ulivyopangwa hapo Mwembe Kisonge nyumbani kwa Abeid Amani Karume chini ya Mwenyekiti wake Muhidini Ali Omar. Kwa wakati huo, nyumba hiyo ya Abeid Karume alikuwa aliishi Hija Saleh na Haji Ali Mnoga.

Mkutano huo ulimalizika jioni ya tarehe 5 Februari, 1957 kwa viongozi hao kukubaliana kuunganisha Shirazi Association na African Association na kuunda chama kilichoitwa Afro – Shirazi Union.

Baadaye chama hicho kiliitwa Afro – Shirazi Party, jina ambalo lilitolewa na Ali Khamis kutoka Shirazi Association. Viongozi 18 wa African Association na Shirazi Association walikutana na kuunda Afro -Shirazi Party. Kumi ni kutoka African Association na Wanane kutoka Shirazi Association. Viongozi wa African Association walikuwa ni Abeid Amani Karume, Ibrahim Saadala, Abdalla Kassim Hanga, Bakari Jabu, Mtoro Rehani Kingo, Rajabu Swedi, Ali Juma Seif, Mtumwa Borafia, Saleh Juma na Saleh Mapete. Viongozi wa Shirazi Association ni Thabit Kombo Jecha, Muhidini Ali Omar, Ameir Tajo, Ali Khamis, Haji Khatibu, Mdungi Ussi, Ali Ameir na Othman Sharifu.

Katika mkutano huo pia alikuwepo mgeni mwalikwa Rais wa TANU, Mwalimu J.K. Nyerere na Katibu Mkuu wa chama cha TANU, Bwana Zubeir Mtemvu. Pia alihudhuria Bibi Maida Springer Kemp ambaye ni Mmarekani mweusi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Viwanda wa Marekani American Federation of Labour Congress of Industrial Organization AFL – C 10. Bibi Springer alikuwa ziarani barani Afrika kuangalia harakati za ukombozi na alifuatana na Mwalimu Nyerere aliyepitia Zanzibar akielekea Tanga kuitangaza TANU.

Chama cha Afro – Shirazi Party kilimteuwa Abeid Amani Karume kuwa Rais, Mtoro Rehani Kingo kuwa Makamo na Thabit Kombo Jecha ni Katibu Mkuu. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ni Ibrahim Saadala, Ali Khamis, Ameir Tajo, Mtumwa Borafia na Muhidini Ali Omar. Baadaye wajumbe wa Shirazi Association kutoka Pemba ambao ni Muhamed Shamte, Ali Sharif Mussa, Issa Sharif, Suleiman Ameir na Hassan Ali waliitwa na kufahamishwa juu ya kuunganishwa vyama hivyo.

Katika mwaka 1947 kuliundwa serikali za mitaa (Local Government) na Baraza la Manispaa (Township Council) lilianzishwa 1954. Abeid Karume alichaguliwa kuwa diwani (Councillor). Katika mwezi wa Juni 1957, Bwana Karume alikwenda nchini Ghana kuhudhuria sherehe za uhuru wa taifa hilo. Safari hiyo ilikuwa ni mwaliko wa kiongozi wa nchi hiyo, Bwana Kwameh Nkrumah kwa vyama vyote vya kupigania uhuru barani Afrika.

Abeid Amani Karume alipendekezwa na chama cha ASP kuwa mgombea wa kiti cha baraza la kutunga sheria wa jimbo la Ng’ambo, katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa Zanzibar wa 1957. Katika uchaguzi huo, Abeid Amani Karume alijiandikisha katika jimbo la Ng’ambo kituo Nambari 84 ambacho ni Old Shimoni School (Mao tse Tung) akiwa ni mfanyabiashara, mkaazi wa Kisima Majongoo nyumba Nambari 18/22. Kadi yake ya kupigia kura ilikuwa Nambari 5818. Karume alishinda kiti hicho kwa kura 3,328 dhidi ya wapinzani wake Ali bin Muhsin Barwan wa ZNP aliyepata kura 918 na Ibuni Saleh mgombea binafsi aliyepata kura 55.

Miaka 40 iliyopita hapo tarehe 7 Aprili, 1972 Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume aliuwawa kwa kupigwa risasi katika jengo la Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shirazi hapo Kisiwandui mjini Zanzibar. Katika mfululizo wa makala haya mwandishi Ali Shaaban Juma anaelezea historia ya maisha ya Mwanamapinduzi huyo.

Hapo tarehe 15 Januari, 1960 Abeid Karume alishtakiwa na mfanyabiashara aitwae Punja Kara Haji mkaazi wa Darajani mjini Unguja. Karume alishtakiwa kwa madai ya kuvunja mkataba wa kukodi bekari ya mfanyabiashara huyo.

Kesi hiyo Nambari 4 ya 1960 (Civil Case Number 4 of 1960) ilitayarishwa na wakili Dinshaw Karai kwa niaba ya Punja Kara Haji. Ilidaiwa mbele ya Jaji G.J. Horsfall wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kuwa hapo tarehe 17 Aprili,1958, Abeid Karume na Thabit Kombo waliingia mkataba na Punja Kara Haji wa kukodi bekari ya Mchangani, nyumba nambari 2759 mali ya Punja Kara Haji.

Mkataba huo ulieleza kuwa kodi hiyo itakuwa ni ya miaka mitatu kuanzia tarehe 1 Mei 1958 kwa malipo ya Shilingi 7,395/20. Abeid Karume alitakiwa alipe Shilingi 550/- kila mwezi. Waraka wa makubaliano hayo ulotayarishwa na Wakili Dinshaw Karai ulitiwa saini hapo tarehe 18 Novemba, 1959 na Punja Kara Haji kwa niaba yake na Abeid Karume kwa niaba yake na kwa niaba ya Thabit Kombo. Mkataba huo ulishuhudiwa na mawakili Dinshaw Karai na Hemed Said.

Akiwasilisha madai dhidi ya Karume hapo tarehe 27 Januari, 1960 Punja Kara Haji alidai kuwa tarehe 16 Novemba, 1959 Abeid Karume alifika nyumbani kwake na kumueleza kuwa yeye na Thabit Kombo wanataka kuiacha bekari hiyo kwa vile ilikuwa inawatia hasara.

Punja Kara Haji alieleza mahakama hiyo kuwa, baada ya kupata kauli hiyo ya Abeid Karume walifikia makubaliano na mlalamikiwa. Abeid Karume alitakiwa alipe Shilingi 7,395/20 kama ilivyo katika mkataba wao wa tarehe 17 Aprili, 1958. Pia Karume alitakiwa akabidhi jengo la bekari hiyo kwa mwenyewe hapo tarehe 31 Disemba, 1959. Akiendelea kutoa ushahidi wake Punja Kara Haji alidai mahakamani kuwa yeye na Karume walikubaliana fedha hizo Shilingi 7,395/20 zilipwe kwa awamu kwa udhibitisho wa maandishi.

Awamu ya kwanza ya Shilingi 2,000/- ziwe zimelipwa ifikapo Disemba, 1959. Fedha zilizobaki Shilingi 5,395/20 zilipwe kidogo kidogo kwa wastani wa Shilingi 500/- kila mwezi kuanzia tarehe 1 Januari, 1960. Fedha hizo zilitakiwa ziendelee kulipwa kwa utaratibu huo kila siku ya mwanzo ya kila mwezi. Punja Kara alidai kuwa Abeid Karume alishindwa kulipa Shilingi 2,000/- hapo tarehe 1 Disemba,1959 na hakulipa Shilingi 500/-ilipofika tarehe 1 Januari,1960 kama walivyokubaliana. Kutokana na madai yake hayo, Punja Kara Haji alidai mahakamani alipwe na Abeid Karume Shilingi 7,395/20, asilimia 9% ya riba ya mwaka kuanzia tarehe ya hukumu na alipwe gharama za kesi hiyo.

Waraka ulomtaka Abeid Karume kufika mahakamani tarehe 8 Februari, 1960 saa 3.00 asubuhi ulitiwa saini na Mrajisi wa mahakama Hussein A. Rahim tarehe 27 Januari, 1960.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo Abeid Karume aliambia mahakama hiyo kuwa hapo tarehe 20 Januari, 1960 alimlipa Punja Kara Haji Shilingi 1,000/-. Pia walikubaliana kuwa deni lililobaki lilipwe kwa wastani wa Shilingi 500/- kila mwezi. Karume alieleza kuwa licha ya makubaliano hayo, mlalamikaji alifungua mashtaka hapo tarehe 27 Januari,1960 bila kutoa stakabadhi ya malipo ya Shilingi 1000/- alizopewa. Baada ya kupokea waraka wa kumtaka afike mahakamani kujibu kesi hiyo,Karume alikwenda kwa Punja Kara Haji ambaye alimweleza Karume kuwa mashtaka dhidi yake yalifunguliwa na wakili wake aitwae Dinshaw Karai baada ya kutofahamiana na mteja wake .

Punja alimuhakikishia Abeid Karume kuwa atamwambia wakili huyo aifute kesi hiyo mara moja. Abeid Karume alieleza mahakama hiyo kuwa, kwa vile aliyaamini maneno ya Punja hakuona ulazima wa kufika mahakamani kujibu kesi hiyo. Inaelekea mlalamikaji (Punja Kara Haji) alitumia fursa ya kutofika Karume mahakamani na kupata upendeleo wa kisheria kwa vile kesi hiyo ilisikilizwa upande wa mlalamikaji pekee. Hivyo moja kwa moja Punja Kara alidanganya mahakama kuwa Abeid Karume alilipa Shilingi Elfu moja baada ya kufunguliwa mashtaka. Karume alieleza mahakama hiyo kuwa vile vile hapo tarehe 7 Machi, 1960 alitoa mahakamani amana ya Shilingi 2,000/- taslimu na kupatiwa stakabadhi ya malipo yenye Nambari 153/60. Lakini licha ya ukweli huo mlalamikaji aliomba mahakama hapo tarehe 11 Machi, 1960 itoe uwamuzi wa kesi hiyo. Hata hivyo Abeid Karume alishinda kesi hiyo na madai ya mlalamikaji yalitupiliwa mbali.

Katika mwezi wa Oktoba 1960, Sheikh Abeid Amani Karume alihudhuria mkutano mkuu wa chama cha Malawi Congress Party huko Nkhota Kota katika Wilaya ya kati ya Nyasaland (Malawi) akiwakilisha chama cha Afro- Shirazi. Katika mkutano huo wanasiasa wanane wa mwisho wa Malawi walokuwa kizuizini waliachiliwa huru. Wanasiasa hao walitiwa ndani kwa kupinga mpango wa wakoloni wa kiingereza wa kuanzisha Shirikisho la Rhodesia (Zimbabwe) na Nyasaland (Malawi). Baada ya kuachiliwa huru, walikabidhiwa kwa kiongozi wa chama cha Malawi Congress Party, Dr. Kamuzu Banda. Aliyewakabidhi wanasiasa hao kwa Dr.Banda ni Gavana wa mwisho wa Uingereza katika koloni la Nyasaland. Msamaha huo ulitolewa muda mfupi kabla ya nchi hiyo kupata uhuru.

Wanasiasa waloachiliwa ni pamoja na Masauko Chipembere, Matupi Mkandawire, Chimtambi na wengineo. Mkutano huo wa chama cha Malawi Congress Party ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Malawi. Viongozi kadhaa wa kisiasa wa Jumuiya ya PAFMECA (Pan African Freedom Movement for East and Central Africa) walialikwa ambapo viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo walihudhuria mkutano huo.

Mbali ya Abeid Karume na ujumbe wake wa chama cha Afro -Shirazi kutoka Zanzibar, pia walihudhuria Marton Malianga wa chama cha Southern Rhodesia African National Congress cha Rhodesia (Zimbabwe) kilichoongozwa na Joshua Nkhomo. Wengine ni Namilando Mundia wa chama cha Zambia National Congress kilichongozwa na Kenneth Kaunda, Sheikh Amri Abeid Kaluta na Austin Shaba wa chama cha Tanganyika African National Union, TANU cha Tanganyika.

Vilevile alihudhuria Abdulrahman Babu na ujumbe wake wa chama cha ZNP cha Zanzibar. Kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya chama cha ASP na chama cha Malawi Congress Party cha Malawi, Abeid Karume aliwaalika kuitembelea Zanzibar baadhi ya viongozi wa chama hicho cha Malawi mapema mwaka 1965. Viongozi walotembelea Zanzibar kutoka Malawi ni Orton Chingolo Chirwa, Yatuta Chisiza, Willie Chokani, Augustine Bwanausi na Kanyama Chiume.

Abeid Karume alichaguliwa tena kuwa mjumbe wa baraza la kutunga sheria katika uchaguzi wa pili wa Januari, 1961, katika jimbo la Jang’ombe kwa tiketi ya ASP.

Mara tu baada ya kumalizika uchaguzi huo wa 1961 ulokuwa na utatanishi Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Waziri wa Afya na Mambo ya Kienyeji katika serikali ya pamoja ya miezi sita. Uchaguzi Mkuu wa tatu wa Zanzibar ulifanyika tarehe 1 Juni, 1963.

Karume alichaguliwa tena kuwa Mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria katika jimbo la Kwahani na Jang’ombe. Akiwa Waziri wa Afya, Karume alishughulikia Afya, Ajira, Ujenzi wa Nyumba, Serikali za Mitaa na Serikali za Wilaya.

Baada ya kuundwa serikali ya Waziri Mkuu Muhammed Shamte kufuatia uchaguzi wa 1963, Abeid Amani Karume aliteuliwa kuwa kiongozi wa upinzani katika baraza la kutunga sheria.

Wakati wa matayarisho ya Mapinduzi ya 1964 Abeid Karume alikuwa mwenyekiti wa kamati ya watu kumi na nne walotayarisha Mapinduzi hayo kwa siri. Akiwa na umri wa miaka 59, Karume aliongoza Mapinduzi ya 1964 na alitangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na vilevile kubaki na wadhifa wake wa Rais wa Afro- Shirazi Party.

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliungana hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 27 Aprili, 1964.

Akiwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Abeid Amani Karume aliongoza ujumbe wa watu kumi na tisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutembelea mikoa ya Musoma, Mwanza na Bukoba kuanzia tarehe 5 -15 Septemba,1965. Lengo la ziara hiyo ni kuonana na wananchi wa mikoa hiyo na kuwahamasisha kuhusu uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Septemba, 1965.

Mheshimiwa Karume aliteuliwa kuwa mbunge wa bunge la Tanzania kupitia viti maalum vya kuteuliwa na Rais wa Tanzania. Karume alikuwa ni mmoja kati ya wabunge 23 wa kuteuliwa kutoka Zanzibar kama ilivyokuwa katiba ya wakati huo. Aliapishwa rasmi kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania katika ukumbi wa Arnatoghly mjini Dar es Salaam hapo tarehe 30 Septemba, 1965'

Tokeo la picha la Abeid Amani Karume

Katika mwezi wa Aprili 1967, Mzee Karume akifuatana na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere na wajumbe kadhaa wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Tanzania walikwenda nchini Misri kuhudhuria mkutano wa siku nne wa nchi tano za Afrika. Mkutano huo, uliandaliwa na Rais Gamal Abdel Nasser wa Misri. Katika ziara hiyo Mwalimu Nyerere na Mheshimiwa Abeid Karume walitunukiwa uraia wa jiji la Alexandria la nchini Misri. Baadhi ya viongozi mashuhuri walotembelea Zanzibar wakati wa uhai wa Abeid Amani Karume ni pamoja na Waziri Mkuu wa Hungary, Bwana Gyula Ka’llai, Makamo wa Rais wa Zambia Reuben Kamanga na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Korea Bwana Kang Ryang. Wengine ni Rais Gamal Abdel Nasser wa Misri, Rais Modibo Keite wa Mali , Rais askofu Makarios wa Cyprus na Rais marshal Josip Broz almaaruf kama Tito wa Yugoslavia.

Wengine ni Rais wa Hungary Bwana Pal Losonczi, Waziri Mkuu wa Guyana Bwana Burham na Waziri Mkuu wa Swaziland, Prince Makhosini Dlamini.

Mheshimiwa Abeid Amani Karume, kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar, na mmoja wa waasisi wa Chama cha Afro-Shirazi na Makamo wa kwanza wa Rais wa Tanzania aliuwawa akiwa na umri wa miaka 67. Mauwaji hayo yalitokea siku ya Ijumaa ya tarehe 4 Aprili, 1972 saa 12.05 za jioni katika jengo la Makao Makuu ya ASP Kisiwandui Unguja Zanzibar.

Mara tu baada ya mauaji hayo hali ya hatari ilitangazwa na msako mkali wa wahalifu ulianza nchi nzima. Watuhumiwa kadhaa wakiwemo raia na maofisa wa vikosi vya ulinzi na usalama walitiwa mbaroni, ambapo mtuhumiwa mkuu akiwa ni profesa Abdulrahman Muhammed Babu aliyekamatwa huko Dar es Salaam.

Maziko ya Sheikh Abeid Amani Karume yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kutoka nchi mbalimbali duniani. Wengi wa wageni hao walianza kumiminika Zanzibar kuanzia saa tatu za asubuhi na kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu katika jumba la serikali Forodhani. Baada ya kutolewa heshima za mwisho,jeneza lilitolewa nje na kikosi cha wanajeshi ili kusaliwa katika uwanja wa Ikulu.

Baada ya marehemu kusaliwa hapo Ikulu, jeneza lilichukuliwa hadi Makao Makuu ya ASP Kisiwandui, kupitia barabara ya hospitali ya Mnazi Mmoja, Makumbusho, Mkunazini na kupindisha kuelekea barabara ya Michenzani hadi Makao Makuu ya Afro-Shirazi.

Hitma ya Abeid Karume ilisomwa katika ukumbi wa klabu ya wananchi tarehe 29 Julai, 1972 wakati wa jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kadhaa. Kwa vile miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni pamoja na kuwapatia makazi bora wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba, Mzee Abeid Amani Karume aliweka jiwe la msingi la jumba la kwanza la fleti 132 hapo Michenzani tarehe 4 Mei, 1970.

Baadhi ya taasisi ambazo zimepewa jina la Karume ni Chuo cha Ufundi cha Mbweni Zanzibar, Kiwanja cha Ndege cha Chake Chake Pemba, Viwanja vya mpira vya Musoma na Dar es Salaam na Kituo cha Televisheni ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa vile miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya 1964 yalikuwa ni pamoja na kuwapatia makazi bora wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba, Mzee Abeid Amani Karume aliweka jiwe la msingi la jumba la kwanza la fleti 132 hapo Michenzani tarehe 4 Mei, 1970. Jumba hilo la kwanza liligharimu jumla ya Shilingi milioni 4,752,000/-. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikusudia kujenga fleti 7000 katika mji wa Zanzibar na kutoa nafasi za makazi kwa wananchi 30 Elfu.

Kufuatia kuuwawa kwa Sheikh Abeid Amani Karume hapo tarehe 7 Aprili,1 972 watu 81 wakiwemo wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, raia na polisi walishtakiwa kwa makosa ya uhaini katika mahakama ya wananchi ya Zanzibar. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 14 Mei, 1973.

Kesi hiyo Nambari 292 ya 1973 iliendeshwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Bwana Wolfgang Dourado akisaidiwa na Ussi Khamis Haji. Katika kesi hiyo mshtakiwa mkuu alitajwa kuwa ni Abdulrahman Muhammed Babu. Washtakiwa tisa walikiri makosa yao, washtakiwa 54 walikana makosa ambapo 18 akiwemo kiongozi wa njama hizo za uhaini na kutaka kuipindua serikali halali ya ASP, Abdulrahman Muhammed Babu walishtakiwa wakiwa hawapo kortini.

Mwanasheria Dourado aliiambia mahakama hiyo kwamba mkutano wa mwanzo wa siri ulifanywa Dar es Salaam wakati wa sherehe za Saba Saba za mwaka 1968. Babu alifanya karamu kubwa ya chakula cha mchana nyumbani kwake, ambapo washitakiwa kadhaa kutoka Zanzibar na Dar es Salaam walihudhuria karamu hiyo. Siku hiyo Babu ndiye aliyetoa shauri kuwa, kazi za wanachama wa Umma Party zipangwe vyengine na akatoa taarifa ya dhamira ya kutaka kuipindua serikali ya ASP. Baramia aliambiwa awe ni kiungo na mpelekaji habari baina ya Zanzibar na Dar es Salaam.

Kesi ya uhaini ilimalizika tarehe 15 Mei, 1974, ambapo washtakiwa 43 walihukumiwa adhabu ya kifo. Washtakiwa 11 walihukumiwa kwenda Chuo cha Mafunzo miaka 15 kila mmoja na wanne walipewa adhabu ya kifungo cha miaka 4 kila mmoja.

Washtakiwa 16 waliachiliwa kwa kukosekana ushahidi na wengine 6 walisamehewa kwa kukosa kesi ya kujibu. Mshtakiwa mmoja alifariki akiwa kizuizini kabla ya kumalizika kesi hiyo. Ingawa washitakiwa 43 walihukumiwa adhabu ya kifo, wakiwemo tisa walokiri kupanga njama za kumuua Sheikh Karume wote waliachiliwa huru siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Mei, 1974.

Kwa vyovyote vile, jina la Abeid Karume halitosahaulika katika historia ya ukombozi wa Zanzibar. Haiwezekani kuandika au kuzungumzia ukombozi na mafanikio ya maendeleo ya Zanzibar bila kujata jina la Abeid Karume.​

Source: leo katika historia April 7: Undani wa hayati abeid amani karume kuzaliwa mpaka kifo

Hatujaona sababu (motive) ya kuuliwa na waliomuua ni kina nani?
 
Walakini, wote 34 waliopewa
hukumu ya kifo, hatimaye hukumu hiyo ilibatilishwa na mrithi wa Karume ambaye alikuwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi . Na Wale wote waliopatikana na hatia waliachiliwa ilikapo mwaka 1978...

convicted of involvement in President Karume's assassination. However, all 34 death sentences were eventually commuted by the succeeding Zanzibar Source : Amnesty.org
Kwakweli sijaelewa kwanini watuhumiwa wote waliachiwa huru? Tena mapema mno
 
Hatujaona sababu (motive) ya kuuliwa na waliomuua ni kina nani?

Utata kifo cha Karume: Chuki binafsi au mapinduzi

I​

Miaka 40 iliyopita, Aprili 7, 1972; Rais wa Serikali ya awamu ya kwanza ya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Abeid Amani Karume, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mazingira na sababu za kutatanisha.

Risasi nane zilitolewa mwilini kwake mwili wake ulipofikishwa kwenye Hospitali ya V. I. Lemin, mjini Unguja kwa uchunguzi, sawa na idadi ya miaka minane ya utawala wake tangu 1964 hadi kifo chake.

Ilikuwa hivi: Rais Karume na Makomredi wenzake wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP) alikuwa na mazoea ya kucheza karata, damma au dhumuna kwenye ukumbi wa ofisi za makao makuu ya Chama hicho Kisiwandui, kila jioni kama sehemu ya mapumziko.

Siku hiyo alifika saa 11.00 jioni akiwa na walinzi wake, akaingia ndani nao wakabaki nje kulinda.
Ikafika zamu yake kucheza; akawa anacheza na Mzee Maalim Shaha Kombo ambaye alionekana kulemewa. Ndipo Karume akamwita Mzee Mtoro Rehani ajitayarishe baada ya Kombo, naye akaitikia kwa kuaga kwanza aende msalani kujisaidia.

Sekunde chache baada ya hapo na kabla Mzee Mtoro Rehani hajarejea kutoka msalani, ghafla watu wawili wenye silaha walivamia chumba alimokuwa Karume na wenzake na kumimina risasi wakimlenga; na kufumba na kufumbua, akawa katika dimbwi la damu kimya, amepoteza uhai. Hakuna mtu mwingine aliyeuawa mbali na kujeruhiwa tu, mmoja wao akiwa Katibu Mkuu wa ASP, (sasa) Hayati Thabit Kombo Jecha.

Risasi uaji (the fatal bullet), mbali ya risasi zote, iliyochukua uhai wa Karume ilitoka kwenye bunduki ya Luteni Hamoud Mohammed Hamoud wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT), ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa uvamizi huu na aliyefyatua risasi ya kwanza wakati Karume akicheza na wenzake. Inasemekana, Hamoud aliuawa papo hapo na mlinzi wa Karume.

Wauaji wengine waliofuatana na Hamoud katika uvamizi huo ni Kapteni Ahmada Mohamed, Koplo mmoja wa jeshi ambaye jina lake halijafahamika hadi leo, na raia mmoja aliyekwenda kwa jina la Ali Khatibu Chwaya, ambao inaelezwa wote hao waliuawa kwenye mapambano ya silaha nje ya eneo la tukio.

Dakika chache baada ya mauaji kutokea, alifika Kanali Ali Mahfoudhi na askari mwingine, Kapteni Makame Hamis, wakauchukua mwili wa Karume na kuukimbiza hospitali.
Itakumbukwa, Kanali Mahfoudhi ni mmoja wa vijana wa Umma Party (UP) cha Abdulrahman Mohamed Babu, kilichoungana na ASP baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kuunda Serikali ya mseto. Ni kati ya vijana waliopelekwa Cuba kwa mafunzo ya kijeshi, na ni mmoja wa wapiganaji walioendesha mapambano ya kisayansi usiku wa Mapinduzi na kukamata uwanja wa ndege mchana Aprili, 1972.

Ni mmoja wa wanaharakati wa siasa za mrengo wa Kikomunisti ambao hawakutakiwa Zanzibar wakati wa utawala wa Karume, hivi kwamba kufuatia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26, 1964, Karume alishinikiza kwa Nyerere wapewe kazi Tanzania Bara aweze “kupumua” ambapo Mahfoudhi alipewa cheo cha Mkurugenzi wa Operesheni katika JWTZ.

Wengine ambao hawakutakiwa ni pamoja na Babu mwenyewe aliyepewa Uwaziri wa Mipango ya Uchumi, na kama tulivyoona makala zilizopita, hasimu mwingine wa Karume, Othman Sharrif, ambaye alifanywa Afisa Mifugo wa Mkoa, Mtwara au Mbeya, na Balozi Salim Ahmed Salim wakati huo Balozi wa Zanzibar nchini Misri ikaridhiwa aendelee kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano nchini humo.

Tuache hayo, lakini hapa swali linazuka: Kwa kuwa Kanali Mahfoudh hakuwa kipenzi cha utawala wa Karume tangu mwaka 1964, ilikuwaje akawa Afisa wa kwanza kuwa kwenye tukio kabla ya maafisa wengine vipenzi, kama vile Kanali Seif Bakari ambaye alikuwa pia Mkuu wa Usalama wa Taifa Zanzibar ambalo halikuwa jambo la Muungano, na wengineo?

Je, alikuwa katika ziara ya kikazi wakati mkasa huu ukitokea au alijua kilichotarajiwa kutokea? Kwa nini alikuwa mmoja wa washitakiwa zaidi ya 100 kwa tuhuma za mauaji hayo, na mmoja wa watuhumiwa 18 miongoni mwa hao walioshitakiwa wakiwa Tanzania Bara, Abdulrahman Babu akiwa mmoja wao.

Kuna dhana mbili kinzani kuhusu jinsi Karume alivyouawa na hatima ya wauaji. Dhana moja inadai kwamba, watu wanne walivamia mahali alipokuwa Karume na wenzake, wakamimina risasi mara nne au mara tano hivi, risasi ya kifo ikampata Karume shingoni akafa, huku zingine zikiendelea kumiminwa kulenga meza walipokuwa.

Inadaiwa kuwa Hamoud aliuawa kwenye eneo la tukio, ambapo wawili waliuawa baadaye na vyombo vya usalama (kwa mapambano?) na mmoja alijiua.

Dhana ya pili inadai kwamba Hamoud alikufa kwenye eneo la tukio katika mazingira ya kutatanisha, ama kwa kujipiga risasi kuepuka kukamatwa hai na kuteswa baada ya kuona asingeweza kutoroka; au alijeruhiwa vibaya na walinzi wa Karume, kisha Ahmada akampiga risasi na kumuua kumwepusha kuteswa na kutoa siri kama angekamatwa hai, kisha (Ahmada) akaweza kutoroka kwenye eneo la tukio.

Juu ya utata huu kuhusu hatima ya wauaji, ni ukweli kwamba ni Luteni Hamoud pekee aliyeuawa kwenye eneo la tukio na washiriki wengine katika mauaji waliweza kutoroka eneo la tukio na baadaye kuuawa katika mazingira yasiyofahamika.

Kufuatia mauaji hayo, watu 1,100 walikamatwa na kuhojiwa juu ya kuhusika au kutohusika kwao na mauaji, wengi wakiwa viongozi na wanachama wa zamani wa Umma Party, chama cha Babu na wanachama mashuhuri wa ASP wenye siasa za mrengo wa kikomunisti.

Yote haya yanaturejesha kwenye swali letu la awali: je, kuuawa kwa Karume kulikuwa na lengo la kulipiza kisasi kwa chuki binafsi, kama baadhi ya watu wanavyodai, au lilikuwa jaribio la Mapinduzi lililoshindwa kwa Serikali ya Mapinduzi? Ni nani huyu Luteni Hamoud Hamoud aliyeongoza mauaji na kwa nini?
Je, lengo lilikuwa ni mauaji hayo pekee au kulikuwa na mpango mkubwa zaidi nyuma? Ukiongozwa na nani?

Kupata majibu ya maswali haya, hatuna budi kuiangalia hali ya kisiasa Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na baada ya Muungano na Tanganyika, Aprili 26, 1964.

Kama nilivyoeleza katika mfululizo wa makala nne hivi karibuni katika gazeti hili kuhusu jinsi “Field Marshal” John Okello alivyoongoza Mapinduzi ya 1964, na kuundwa kwa Serikali ya Mseto kati ya vyama vya ASP na Umma, lengo kuu la Karume lilikuwa ni kuzivunja nguvu za wanaharakati wa Umma Party na za wakomunisti wa ASP walioshabihiana kimawazo na kimtazamo wa kitaifa na wana-Umma Party na kumnyima Karume usingizi.

Lakini tofauti na matarajio ya Karume, hatua hiyo iliwaleta karibu zaidi wanamapinduzi hao na kumnyima zaidi usingizi kwa hofu ya kupinduliwa, wakimtuhumu kushindwa kuongoza na kusimamia madhumuni ya Mapinduzi Visiwani.
Mungu bariki kwa Karume, ukatokea Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika mwaka huo, akaona vyema awasambaratishe kwa kuwatafutia nafasi Tanzania Bara ambako wasingeweza kufurukuta.

Waliokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Abdulrahman Babu (Umma) na aliyepewa Uwaziri wa Mipango na Uchumi kwenye Serikali ya Muungano; Kassim Hanga (ASP) aliyeteuliwa Waziri katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri, Mambo ya Muungano; Salim Ahmed Salim (Umma) aliyeteuliwa Balozi nchini Misri.
Wengine ni Othman Sharrif (ASP) aliyeteuliwa Balozi nchini Marekani, lakini Karume akampinga Nyerere akidai hastahili, uteuzi ukafutwa; badala yake akateuliwa kuwa afisa mifugo katika moja ya mikoa ya Kusini Tanzania, Mbeya au Mtwara, na Kanali Ali Mahfoudh (Umma) aliyeteuliwa Mkurugenzi wa Operesheni katika Jeshi la Wananchi (JWT), na wengineo.

Kwa wale wenye maoni tofauti na ya kukosoa Serikali waliobaki Visiwani, hasira ya Karume aliyetawala kwa mkono wa damu iliwashukia, wengi walikamatwa na kutiwa kizuizini na pengine kupoteza au kuuwawa kikatili na katika mazingira ya kutatanisha.
Mmoja ya waliouawa kikatili kizuizini ni Mzee (mwanaharakati) Mohamed Hamoud, baba yake Luteni Hamoud Mohamed muuaji wa Karume. (Rejea video ya Mzee Aman Thani hapo juu)

Tangu Mapinduzi ya Januari 12, 1964, Zanzibar haikuwa na Katiba wala Sheria; iliongozwa kwa Amri za Rais (Presidential Decrees) kadri alivyoona inafaa. Na kwa mujibu wa Gazeti la “The Tanganyika Standard” la March 9, 1968, Karume aliapa kutofanya uchaguzi wala kuwa na Katiba Kisiwani kwa miaka 50 tangu 1964 – 2014 Kwa madai kwamba “chaguzi zote ni vyombo vya mabeberu kuwakandamiza wananchi”.

Na kadiri kalamu ya Karume ya wino wa damu ilipozidi kuandika historia ya ukatili, udikteta na umwagaji damu kwenye kurasa ngumu za kukwaruza ndivyo alivyojichongea na kujiongezea upinzani na uadui kwa jamii ya Kizanzibari.

Kufikia mwaka 1967 hofu ya Karume dhidi ya wenzake na kwa nafasi yake ilitia fora kiasi cha kuogopa kivuli chake mwenyewe. Na ili kuendelea kuwamaliza wenzake, mwaka huo zilitungwa tuhuma za uongo dhidi ya watu 14 makada wa ASP katika kumpindua, zikiwalenga hasa wenye fikra za kikomunisti.

Walioingizwa kwenye tuhuma hizo ni pamoja na mawaziri wa Serikali yake mabwana Abdallah Kassim Hanga, Salehe Saadallah Akida, Abdul Aziz Twala na makatibu wakuu wa wizara, Aboud Nadhif na Mdungi Ussi na baadaye Othman Sharrif.

Wote waliokuwa Visiwani walikamatwa, kisha Karume akamwomba Nyerere kuwarejesha Zanzibar kutoka Bara, Othman Sharrif na Hanga ili “wakahojiwe” lakini wote wakaishia kuuawa kikatili bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mmoja wa mashahidi wa uongo walioandaliwa dhidi ya “watuhumiwa” kwa vyombo vya Karume, alikuwa Ahmada ambaye kwa uongo wake, watu wanne akiwamo Hanga, Twala, Saadallah na Othman, walinyongwa mwaka 1969. (Rejea video ya Mzee Aman Thani hapo juu)

Kwa uongo huo, Ahmada alizawadiwa cheo cha kapteni jeshini. Ni Kapteni Ahmada huyu, aliyeshiriki kwenye mauaji ya Karume miaka mitatu baadaye.
Kwa hofu ya jamii ya Kizanzibari kufikiwa na fikra na mawazo mapya ya kimaendeleo, Karume alipiga marufuku vijana wa Kizanzibari kwenda nje kwa masomo ya juu ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam; alipiga marufuku pia ujenzi wa Chuo Kikuu Visiwani.

Mbali na kutokuwapo kwa utawala wa sheria enzi za Karume, unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi kwa misingi ya historia na kisiasa ulitia fora. Kwa mfano, mwaka 1966, alitoa amri (decree) kuwanyima wazazi haki ya kuwakataa wanaume walioposa binti zao kama njia ya kuondoa ubaguzi wa rangi.

Kwa sababu hii, wasichana, hasa wale wa Kiarabu walilazimishwa kwa nguvu ya Serikali kuolewa kwa nguvu. Karume mwenyewe, wakati huo akiwa na umri wa miaka 65, aliwania kuoa kwa nguvu, wasichana wanne wa Kiajemi, na alipokataliwa, aliamrisha wazazi wao watiwe kizuizini na kuchapwa viboko kwa kosa la kuzuia mpango wa ndoa mchanganyiko, na baadaye kutimuliwa Zanzibar.
Chini ya mpango huo, raia wa kigeni waliotaka kuchumbia wasichana wa Kizanzibari walitakiwa kuilipa Serikali Sh. 64,000,000, bila hivyo hawakuruhusiwa kuwaoa.

Karume alikuwa ameanza kuwa mwiba kwa Mwalimu Nyerere pia juu ya Muungano. Kwa mfano, alimkatalia Nyerere kwa lugha ya dharau na kejeli juu ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha kutumika Zanzibar.

Na kuhusu akiba ya fedha za kigeni ya Zanzibar iliyofikia dola milioni 80 mwaka 1972, alimuonya asithubutu kuitolea macho, akamwambia: “Fedha ya kichwa cha Malkia si yako na usiniulize, labda niulize juu ya hii (sh.) yenye picha ya kichwa chako”.
Na kuhusu Muungano, Karume alikuwa ameanza kuchoka nao. Siku moja alisema, “Muungano ni kama koti tu; likikubana unalivua”.
Ufa huu kati ya viongozi hao wawili juu ya Muungano, ndio uliosababisha kamati ya kupendekeza Katiba (Constitutional Committee) isiundwe na Bunge la Katiba (Constitutional assembly) lisiteuliwe ndani ya muda wa mwaka mmoja tangu Muungano, kama ilivyotakiwa chini ya Mkataba wa Muungano wa Sheria ya Muungano ya 1964.

Wadadisi wa mambo ya siasa wanakubaliana kuwa, kama Karume angeendelea kutawala miaka kadhaa baada ya 1972, Muungano ungefikia kikomo kwa njia ya kutisha na kusikitisha.

Kufikia mwaka 1972, upinzani kwa Serikali ya Karume ulikuwa umechukua harakati za uasi wa umma, chini kwa chini kwa mara ya kwanza tangu Hanga na wenzake wanyongwe mwaka 1969.
II
KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya toleo lililopita, tuliona jinsi Rais wa Serikali ya awamu ya kwanza Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Abeid Amani Karume, alivyouawa kikatili na wanajeshi wakati akicheza bao, Aprili 7, 1972 mjini Unguja.

Kwa kifupi, tuliona kwamba, kwa vigezo vyovyote vile vya utawala na uongozi, Karume alitawala kwa mkono wa chuma; alitawala kidikteta katika nyanja zote za maisha ya Wazanzibari kisiasa, kiuchumi na kijamii. Alikuwa kero pia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa Muungano.

Kwa kusema haya sina maana kwamba Karume hakutenda mema kwa Zanzibar na kwa Wazanzibari; bali najaribu kutafiti tu kuona ni mazingira na sababu zipi zilizochochea na kuharakisha kuuawa kwake; kati ya sababu hizi kuu za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimuungano. Kwa vyovyote vile, moja au zaidi ya mambo haya manne yalichangia.

Tunajua kwa mfano, kwa baadhi ya Wazanzibari, Karume alikuwa mtawala mkatili asiye na huruma wala hakujua kusamehe; lakini pia alikuwa na sifa za pekee nzuri kama kiongozi na binadamu; alikuwa mhimili na mtetezi wa Waafrika wa Kizanzibari na hakuyumbishwa na siasa za migogoro Visiwani.

Alikuwa mwenye fikra zenye kujitegemea, alifanya maamuzi yake bila woga wala kuhofia matokeo; alikuwa kiongozi mwenye kuthubutu na mwenye kujituma.

Mwisho tutaona jinsi mpango mzima wa mauaji ulivyoandaliwa kwa wasomaji kuona kama ilikuwa chuki binafsi au mapinduzi. Si madhumuni ya makala haya kumwona Karume kama dikteta mwema (benevolent dictator) au dikteta katili (ruthless tyrant), maana hilo ni jambo la maoni ya kila mtu binafsi.

Alitawala kwa mkono wa chuma
Tumeona jinsi Karume alivyoitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma, na namna alivyowaengua wote aliodhani hawakuwa upande wake, ama kwa kuwahamishia kwenye Serikali ya Muungano, ama kwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Sambamba na hatua hiyo, jamii ya Kiarabu wasio Wazanzibari, iliamriwa kuondoka, na wale Waarabu raia waliobaki waliishi chini ya jicho kali la Serikali; waliweza kukamatwa, kama Wazanzibari wengine na kutiwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka. Walifanyiwa jinsi serikali ilivyofikiri inafaa; mashamba na mali zao zilitaifishwa bila kufidiwa.

Wapo waliohukumiwa na “Mahakama ya wananchi” (tutaiona baadaye), kifungo na kuchapwa viboko kuonyesha kwamba Serikali ya Karume haikuwa ya mchezo; akaionya jamii ya Ki-Athnasheri wa Kiajemi kwamba kama wangeendelea kuleta “mgogoro”, wangefukuzwa wote Zanzibar licha ya kuwa raia.

Alitawala bila Sheria wala Katiba
Karume alitangaza utawala wa chama kimoja cha ASP na kuamrisha kila Mzanzibari mtu mzima, kuwa mwanachama. Kila familia ilitakiwa kutundika picha ya Karume nyumbani; kutofanya hivyo lilikuwa kosa la jinai lenye adhabu kali.
Kikosi cha Usalama wa Taifa chini ya Kanali Seif Bakari, kilichopewa jina la “Viwavi Jeshi”, na kufunzwa Ujerumani Mashariki kikaiva kwa mbinu za utesi na mauaji, kilipewa mamlaka ya kukamata, kutesa, kutia kizuizini na hata kuuwa bila mashitaka. Yeyote aliyelalamika, hata juu ya upungufu wa chakula tu, aliitwa “adui wa Mapinduzi” na hivyo mhaini. Enzi hizo, nduguyo akigongewa mlango usiku na kutakiwa kwa mahojiano na Serikali, usingemwona tena milele.

Wakati wa Karume hapakuwa na utawala wa Sheria wala Katiba; amri za rais (decrees) ndizo zilizotawala nchi. Mapema mwaka 1966, mfumo wa mahakama wa kawaida ulipigwa marufuku; na Oktoba 1966, rais alijipa madaraka ya kuteua mahakama maalumu za watu wasiozidi 14 wenye mamlaka ya kusikiliza kesi za makosa ya kisiasa kama vile uhaini, uhujumu uchumi na wizi wa mali ya umma.
Mahakama hizi hazikufungwa na kanuni zozote katika kusikiliza kesi; huduma za kisheria kwa watuhumiwa zilifutwa na mawakili kupigwa marufuku Zanzibar. Upande wa mashitaka ndio uliokuwa pia upande wa utetezi; kwa maana kwamba, mwendesha mashtaka wa serikali alipomaliza kuwasilisha mashtaka dhidi ya mtuhumiwa aligeuka kuwa mtetezi wa mtuhumiwa.

Mahakama hizi zilipewa uwezo wa kutoa hukumu za kifo. Mwaka huo huo (1966), Baraza la Mapinduzi lilipiga marufuku pia haki ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki [EACA] na rufaa zote zikawa kwa Rais Karume pekee.
Mwaka 1970, Karume alipitisha amri (decree) ya kuanzishwa mahakama (za kienyeji) za watu watatu.

“Mahakimu” wapya wa mahakama hizo waliteuliwa na Karume mwenyewe kutoka miongoni mwa makada wa ASP.

Moja ya sifa ya kuteuliwa hakimu ni kutokuwa msomi wa sheria, na ikiwezekana uwe hujui kusoma na kuandika. Adhabu ya kifo ilipanuliwa kuingiza makosa kama vile utoroshaji wa karafuu, uhaini na utoaji mimba. Matumizi ya vidonge vya uzazi wa majira lilikuwa kosa kubwa pia.

Karume alichochea hasira na chuki kubwa ya Wafanyabiashara wa Kiasia mwaka 1971, pale alipowapa notisi ya mwaka mmoja kufungasha virago kwa madai ya kuonekana kudhibiti uchumi wa Zanzibar. Hasira yao iliungana na ile ya Waarabu ugenini waliofukuzwa mwaka 1964 na kupokonywa mali na mashamba yao bila kulipwa fidia; achilia mbali wale ambao mabinti zao waliozwa kwa nguvu kwa Wazanzibari Waafrika.
Wakati huo huo, Karume aliendelea kuwaachisha kazi na kuwatimua Visiwani, watumishi wa serikali waliojulikana au ndugu zao kuwa wafuasi wa zamani wa vyama vilivyopigwa marufuku vya ZNP na ZPPP na nafasi zao kujazwa na “watiifu” kwake. Hata hivyo, kwa huruma ya Nyerere, walipewa utumishi serikalini Tanzania Bara.

Mapema mwezi Januari 1972, Waziri mdogo, Ahmed Badawi Qualletin, na afisa mwingine wa Serikali, Alli Sultani Issa, walifukuzwa kazi. Kisha, Februari 1972, ujumbe mzito wa watu sita ulitumwa kwa Nyerere kumwambia awarejeshe Zanzibar, Abdulrahman Babu na wenzake kadhaa wakahojiwe kwa tuhuma za kutaka kuiangusha Serikali.

Babu ambaye alikuwa bado mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa Zanzibar, na aliyeamua kutorejea Zanzibar ya Karume kwa kuhofia usalama wake, kivuli chake na mzimu wa wahanga wa ukatili vilimtisha na kumnyima usingizi Karume, mithili ya Macbeth kwa mzimu wa Mfalme Duncan na Banquo, aliowaua kwa upanga ili atawale.

Nyerere, kwa kuhofia yaliyompata Hanga, Twala, Othman Sharrif na wengine kutokea alipowarejesha Zanzibar mwaka 1967, safari hii alikataa kumrejesha Babu Zanzibar, ingawa alikubali shinikizo la Karume la kumwachisha uwaziri katika Serikali ya Muungano.

Karume aliwatimua pia wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufunga Kituo chao cha Utafiti na Udhibiti wa malaria Visiwani kwa madai kwamba, Wazanzibari walikuwa “malaria proof”, yaani hawaguswi wala kuugua malaria.
Kwa hatua hiyo, ugonjwa wa malaria uliongezeka kwa asilimia 45. Na ingawa Zanzibar ilikuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni, zaidi ya pauni za Uingereza milioni 14 kwenye Benki ya Urusi mjini London, (taarifa nyingine zinadai dola milioni 80), Karume hakuwa tayari kutumia fedha hizo kudhibiti malaria wala kuagiza chakula; badala yake akaona muhimu zaidi kuanzisha kituo cha televisheni ya rangi na ya pekee barani Afrika wakati huo.

Mwaka huo huo (1971), katikati ya mrindimo wa njaa Visiwani, Karume alipiga marufuku uagizaji wa chakula (mchele, sukari, unga wa ngano) kutoka nje, kama hatua ya kujitegemea kwa chakula.
Hatua hii ilizua tafrani na malalamiko na kusababisha biashara ya magendo ya chakula kushamiri; hapo, “Viwavi Jeshi” na mahakama za “kangaroo” zikapata wahanga kukamatwa, kushitakiwa na kunyongwa. Watu wengi wakaikimbia Zanzibar. Aprili 1972, ukosefu wa chakula ulikithiri. Ni wakati huo Rais Karume alipouawa ghafla.

Kwa yote hayo, pamoja na tabia yake ya kutoamini wasomi na kuchukia wataalamu, Karume hatimaye alianza kuchukiwa pia na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi wenye siasa za mrengo wa ki-Karl Marx.

Karume adha kwa Nyerere na Muungano
Nyerere alikuwa ameyatoa sadaka mengi ya Tanganyika kwa Zanzibar, ilimradi tu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ufikiwe. Kwa mfano, wakati Tanganyika ilipoteza hadhi ya kuwa nchi na baadaye jina lake, pale Muungano ulipobadili jina kutoka “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar”, kutwa “Jamhuri ya Muungano wa Tan-zan-ia”, Zanzibar ilibakia kuwa Zanzibar, na Karume akabakia Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania.

Si hivyo tu, Wazanzibari watano walipewa uwaziri kamili katika Baraza la Mawaziri 14 la Muungano. Na ingawa idadi ya Wazanzibari ilikuwa asilimia tatu tu ya Watanganyika, lakini Zanzibar iliruhusiwa kuwa na Wabunge 52 katika Bunge la Muungano, wakiwamo Wajumbe wote 32 wa Baraza la Mapinduzi.

Licha ya upendeleo huu, Nyerere hakufanikiwa kudhibiti mhimili wa kisiasa Zanzibar chini ya Karume. Mfano, Zanzibar chini ya Karume, ilikataa kuhamishia kwenye Muungano mambo mengi yaliyopaswa kuwa chini ya Serikali ya Muungano; kwa mfano, iliendelea kudhibiti jeshi lake la ulinzi na Idara ya Uhamiaji, Karume akiwa amiri jeshi wake Mkuu. Ndiyo kusema, aliuawa na wanajeshi wa jeshi lake la Zanzibar, si Wanajeshi wa JWTZ.

Karume alikataa Serikali ya Muungano kugusa akiba ya fedha za kigeni ya Zanzibar, japokuwa fedha lilikuwa jambo la Muungano. Aidha, Karume na Baraza lake la Mapinduzi walikiuka mara nyingi mapendekezo ya kisera kutoka Bara kiasi kwamba Nyerere hakuwa na kauli tena juu ya sera za kiserikali.

Karume akakataa pia mazungumzo zaidi ya kikatiba kwa hofu ya Zanzibar kupoteza hadhi na mamlaka yake. Karibu kila alichopendekeza Nyerere, alipata jibu la mkato kutoka kwa Karume: “Kama hivyo ndivyo, tuvunje Muungano”.

Mitazamo hasi ya viongozi hawa wawili juu ya Muungano, ndiyo iliyosababisha mchakato wa kupata Katiba ya Muungano ndani ya mwaka mmoja kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano usifanyike, na Muungano kuongozwa kwa Katiba ya Muda kwa miaka 13 hadi 1977 na baada ya Karume kufariki.

Nyerere alipowasilisha na kupitishwa kwenye Bunge la Muungano, Mpango wa kwanza wa Maendeleo wa miaka mitano, na kutangaza nia yake kuona unatumika pia Visiwani, Karume aliupinga; akaja na mpango wake tofauti wa miaka mitatu kwa Zanzibar ulioandaliwa na mchumi kutoka Ujerumani Mashariki.

Kwa yote hayo na mengine, Nyerere alianza kuonyesha dhahiri chuki yake kwa utawala wa kimabavu wa Karume. Naye (Karume) alipotambua hilo, alizuia mwingiliano huru wa watu kati ya Visiwani na Tanzania Bara kwa hofu na kwa sababu zinazofahamika.
Si mara moja, hofu na wasiwasi wa kimaasi vilipojionyesha Zanzibar, mamlaka za usalama zilimshauri Mwalimu kufuta ziara zake Visiwani. Hofu hizi zilijidhihirisha zaidi pale Othman Sharrif, baada ya uteuzi wake wa Ubalozi Marekani kufutwa kwa shinikizo la Karume na kurejea Zanzibar, alipokamatwa na kutiwa kizuizini bila kosa.

Ilibidi Nyerere aingilie kati na kumwita Karume Ikulu, kuonyesha jinsi alivyochukizwa na kitendo hicho; lakini Karume alimkatalia, kuonyesha kwamba Nyerere hakuwa na mamlaka kwake. Sharriff aliachiwa baadaye kwa hiari ya Karume, na Nyerere akamteua kuwa Afisa Mifugo Tanzania Bara.

Hata hivyo, Oktoba 1969, wakati Nyerere akiwa ziarani nchi za nje, Sharrif alikamatwa Tanzania Bara na kurejeshwa Zanzibar alikouawa.
Zipi adha nyingine kwa Nyerere? Ni nani huyu Luteni Hamoud Hamoud? Kwa nini aliongoza mauaji ya Karume?
KATIKA sehemu ya pili ya makala haya wiki iliyopita, tuliona jinsi Rais Abeid Amani Karume alivyotawala kwa mkono wa chuma bila kufuata katiba wala utawala wa sheria, na hivyo kujitengenezea maadui wengi katika jamii ya Kizanzibari na kwa makada wenzake wa ASP wenye siasa za mrengo wa kushoto ambao, alianza kuwatimua kazi au kuwahamishia kwenye Serikali ya Muungano.

Tulimaliza kwa kuona kwa sehemu tu, jinsi alivyogeuka kuwa adha na kero kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa Muungano wenyewe, kiasi cha kuuweka Muungano huo kwenye hati hati ya kuvunjika. Tuendelee na sehemu ya Tatu, kuona kilichofuata.
Karume alikuwa mwiba kwa Nyerere
Mbali ya Karume kuweka wazi kwa kusema kwamba, “Muungano ni kama koti tu; likikubana au kukuzidishia joto unalivua na kuendelea na safari yako”, pia alijipa ujasiri usio wa kawaida kwa kumkatalia Nyerere hadharani kila mara juu ya baadhi ya mambo ya Muungano akisema: “…..kama ni hivyo, sikubali, bora tuvunje Muungano”.

Ni ujasiri huu wa Karume usio wa kawaida juu ya jambo nyeti kama hili, uliofanya Nyerere atoe tamko lake maarufu juu ya hatima ya Muungano akisema: “Kama watu wa Zanzibar, bila ya ulaghai kutoka nje, wataona ni bora kuvunja Muungano, mimi siwezi hata kidogo kuwapiga mabomu na kuwaua wananchi wa Zanzibar. Kama waliingia katika Muungano kwa hiari yao, vivyo hivyo wanaweza pia kujitenga kwa hiari yao.
Hatukuishinda Zanzibar (kuwafanya mateka) vitani” (Soma: William Edgett Smith, “Mwalimu Julius K. Nyerere”, tafsiri ya Kiswahili na Paul Sozigwa, uk. 154).

Wakati Mwalimu alikuwa mstari wa mbele katika kupinga ubeberu wa Marekani wakati wa vita ya Vietnam, na kwa ukombozi wa nchi za dunia ya tatu kwa ujumla, Karume alimbeza na kutangaza adhabu kali Visiwani kwa yeyote aliyelaani na kupinga ubeberu, au kuimba nyimbo za kuikashifu Marekani.

Mwalimu alipokosana na Uingereza kwa nchi hiyo kuukingia kifua utawala wa kidhalimu, kibaguzi na wa mabavu (UDI) wa Ian Smith nchini Rhodesia Kusini (sasa Zimbabwe), na kwa sababu hiyo uhusiano wa Mwalimu na Balozi wa Uingereza nchini, Sir Horace Phillip kuingia mkwara, Karume alionyesha hadharani kila mara kusuhubiana na Balozi huyo kwa kicheko cha bashasha na uswahiba kwa chukizo kwa Nyerere.
Tunaweza kutua kidogo hapa kuangalia nyuma mazingira aliyokuwamo Karume, miezi michache kabla ya kifo chake; bila shaka tutabaini kuwa, kiongozi huyo alikuwa katikati ya uhasama na uadui wa kujitakia.

Kwanza alikuwa na uhasama mkubwa na jamii pana ya Kizanzibari kwa udikteta wake uliokithiri uliosababisha mauaji, watu kutiwa kizuizini au kuhamishiwa Bara. Pili, kulikuwa na tatizo la njaa na mlipuko wa malaria; mambo ambayo hakuonekana kujali.

Tatu, kulikuwa na uhasama mkubwa wa kisiasa kati yake na makada wenzake wenye siasa za Ki-Karl Marx ndani ya ASP waliomtuhumu kushindwa kuongoza, achilia mbali jamii ya Kiarabu aliyoitimua kikatili Zanzibar na iliyoendelea kutema laana kwake ughaibuni.

Nne, kulikuwa na Nyerere ambaye alianza kumuona kama mzigo na kero kwa Serikali ya Muungano na kwa siasa za kimataifa. Yote haya yalikuwa baruti tosha kuweza kulipuka na kumdhuru Karume kwa namna yoyote iwayo.

Ni nani huyu Luteni Hamoud?
Luteni Hamoud Mohamed Hamoud, alikuwa mtoto wa mzee Mohamed Hamoud ambaye alikamatwa na kutiwa kizuizini na Karume miezi kadhaa baada ya Mapinduzi ya Januari 1964, na hatimaye kufariki dunia akiwa kizuizini.

Miaka kadhaa baadaye, wakati Hamoud Hamoud akichukua mafunzo ya kijeshi huko Tashkent nchi iliyokuwa katika Shirikisho la Urusi ya zamani USSR, alifahamishwa na mmoja wa wanafunzi wenzake juu ya kuuawa kwa baba yake. Kwa uchungu mkubwa, aliapa sawia na baadaye, kwamba angemuua Karume kulipiza kifo cha baba yake.

Mfumo wa Usalama wa Zanzibar ulioenea kila mahali, ulijulishwa haraka na mmoja wa ma-ofisa usalama waliokuwa kwenye mafunzo pamoja na Hamoud, juu ya kusudio hilo la Hamoud.
Lakini cha kushangaza ni kwamba, Hamoud aliporejea Zanzibar baada ya mafunzo hakukamatwa wala kuwekwa kwenye uangalizi; badala yake alipandishwa cheo kuwa luteni usu, katika sherehe iliyohudhuriwa na Karume mwenyewe kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa, suala la Usalama wa Taifa halikuwa jambo la Muungano; liliongezwa kwenye orodha mwaka 1984 kufuatia kadhia ya Aboud Jumbe ya kuchafuka kwa hewa ya kisiasa Zanzibar, likaunganishwa kusomeka kwa pamoja na jambo la Ulinzi kuwa “Ulinzi na Usalama”.

Pale risasi ya Hamoud ilipochukua uhai wa Rais Karume miezi kadhaa baadaye, Serikali ilisisitiza kwamba, mauaji hayo yalikuwa sehemu ya njama kubwa ya kuangamiza Mapinduzi ya 1964, kutokana kwamba, Hamoud na wauaji wenzake walikuwa wanachama wa zamani wa Umma Party, kilichokiunga mkono ASP huko nyuma, na kukipa [ASP] mwelekeo bora wa kiitikadi [Ukomunisti] na kuheshimika kisiasa.

Kufuatia mauaji hayo, watu 1,100 walikamatwa na kuhojiwa. Babu alikamatwa na kutiwa kizuizini Tanzania Bara kwa tuhuma za kuongoza mpango mzima; nao maofisa wa ngazi za juu wa Kizanzibari Jeshini Bara, kama Ali Mahfoudh na wengine, nao walishukiwa na kuondolewa kwenye utumishi wa Jeshi Tanzania Bara bila kurejeshwa Zanzibar.

Mgongano dhana ya mauaji
Kuna dhana mbili zinazogongana, lakini zote zenye nguvu; juu ya sababu za kuuawa kwa Karume. Dhana ya kwanza ni hii ya Hamoud kulipiza kisasi.
Lakini suala la kulipiza kisasi linakoma pale tunapoona watu kama Kapteni Ahmada na raia Ali Chwaya ambao hawakuwa na uhusiano wa kifamilia na marehemu Mohamed Hamoud aliyeuawa, kujiingiza katika kulipiza kisasi.

Lakini, kama tutakavyoona baadaye, Kapteni Ahmada alijiingiza kama hatua tu ya kujisafisha kwa kujutia ushahidi wa uongo aliotoa dhidi ya Hanga na wenzake 18 waliouawa mwaka 1969, na yeye kuonekana kama adui na msaliti wa umma wa Kizanzibari. Inapofikia hapo, inakuwa dhahiri kwamba mpango huo ulibeba hasira za jamii pana ya Kizanzibari.

Dhana ya pili ambayo ndiyo msimamo wa Serikali ni kwamba, mauaji hayo yalikuwa mpango mpana wa kupindua Serikali. Dhana hii inapata nguvu kutokana na watu wengi kuhusishwa na tuhuma hizi, lakini kama tu tuhuma dhidi yao zilikuwa za kweli; vinginevyo dhana ya kwanza inashinda.

Mipango ilivyopangwa na kupangika
Chuki binafsi? Hapana, Hamoud hakuwa peke yake; ilikuwa ghadhabu ya umma kwenye jamii pana ya Kizanzibari, kila kundi au sehemu ya jamii na malalamiko yake.
Kwa mujibu wa taarifa za Usalama wa Taifa Zanzibar, mipango ya kupindua Serikali ya Karume ilianza kusukwa tangu 1967 – 1972 ndani ya Zanzibar na Tanzania Bara, ambako nyumba ya Abdulrahman Babu ilikuwa kituo cha mikutano ya Wazanzibari ya kupanga Mapinduzi hayo.

Kama hivi ndivyo, Karume alikuwa na sababu tosha kumtaka Nyerere kumrejesha Babu Zanzibar “kuhojiwa”, Februari 1972.
Mkutano wa mwisho ulifanyika Aprili 2, 1972, ambapo ilikubaliwa Mapinduzi yatekelezwe Aprili 7, 1972, yakihusisha makundi mawili: kundi la Wazanzibari kutoka Bara, wengi wao wakiwa wanajeshi, na kundi la Wazanzibari ndani ya Zanzibar, likihusisha raia na wanajeshi wachache.

Pamoja na uamuzi huo, kikao kilitoa majukumu mazito kwa baadhi ya washiriki, ikiwa ni pamoja na Hamoud na Ahmada kupewa jukumu la kuiba silaha kutoka kambi ya kijeshi, Bavuai.
Ilikubaliwa kuwa, Babu na wafuasi wake kutoka Bara wasafiri kwa mtumbwi kwenda Zanzibar Aprili 6 kuamkia alfajiri ya Aprili 7, na kufikia eneo lililopo kati ya mitambo mikuu ya mawasiliano [Cable and Wireless] na Klabu Starehe. Baada ya hapo, Babu abakie amejificha kwenye nyumba ya Hamoud Hamoud, iliyotizamana na Klabu Starehe eneo la Shangani, kusubiri saa ya mapambano kuwadia.

Kwa mujibu wa taarifa, Babu aliondoka Dar es Salaam kwa mtumbwi uliofungwa redio mbili za mawasiliano, jioni ya Aprili 6, safari iliyoelezwa kuwa ya “kuvua samaki”; wakati madhumuni halisi yalikuwa ni kuwafikisha Babu na wafuasi wake Visiwani usiku wa Aprili 6, kwa maandalizi kamili ya kupindua Serikali
Jioni hiyo, Aprili 6, Uongozi wa Jeshi uligundua upotevu wa silaha nyingi Kambini Bavuai. Na ingawa uongozi ulikuwa bado haujamhusisha mtu yeyote, lakini Hamoud, Hamada na askari wengine walianza kufuatiliwa kwa siri.

Yaelekea kufikia hapo, Babu alijulishwa na kuonywa kwa njia ya redio akiwa baharini, juu ya kugunduliwa kwa mpango mzima wa Mapinduzi; akakatiza safari na kurejea haraka Dar es Salaam hima. Haijulikani kama wafuasi wake walikuwa wamekwishafika Zanzibar au la; au kama nao walijulishwa na kurejea Dar es Salaam.

Lakini kuwapo Visiwani wanajeshi kama Kanali Mahfoudh (Mkurugenzi wa Operesheni JWTZ, Dar es Salaam) na Luteni Hashil Seif (Kikosi cha WanaAnga, Ukonga, Dar es Salaam) saa ya kuuawa Karume, kunaonyesha baadhi yao tayari walikuwa Zanzibar kusubiri wenzao.

Saa 12.00 asubuhi, Aprili 7; Ali Khatibu Chwaya (raia) alikwenda kwa Ali Mshangama Issa (afisa wa tatu, meli M.V. Afrika, mkazi wa Zizi la Ng’ombe, Zanzibar), kumweleza juu ya kutowasili kwa kundi la Dar es Salaam.
Baadaye asubuhi hiyo, Ali Mshangama, Chwaya, Miraji Mpatani (karani wa shirika moja, Zanzibar), Mohammed Abdullah Baramia (Mtunza Bohari, Idara ya Elimu), Ahmada na Hamoud, walikutana nyumbani kwa Hamoud na kuonyesha kukerwa na kusikitishwa kwa kutowasili kwa wapanga mapinduzi kutoka Dar es Salaam, hasa wakijua pia kwamba, silaha zilizoibwa bado zilikuwa nyumbani kwa Hamoud, na hatari ya kuweza kugunduliwa.

Ilipofika saa 6.00 adhuhuri siku hiyo, Mshangama, Hashil Seif, Amar Saad Salim, maarufu kama “Kuku” (afisa usafirishaji, Idara ya Siha, Zanzibar) na Chwaya, walikutana nyumbani kwa Amar Saad ambako Mshangama, Hashil Seif na Baramia walipendekeza mpango wa kupindua Serikali uahirishwe hadi watakapopata taarifa tofauti kutoka Dar es Salaam.
Kwa hiyo, saa 9.00 mchana siku hiyo, saa mbili tu kabla ya kuuawa kwa Karume, Baramia alikwenda nyumbani kwa Hamoud eneo la Shangani kuwasilisha pendekezo hilo. Alimkuta Miraji Mpatani nje ya nyumba na kumweleza Baramia kwamba, pamoja na kundi la Dar es Salaam kutowasili, Ahmada na Hamoud walishikilia Mapinduzi yafanyike tu siku hiyo, kwa sababu Ahmada alikuwa anatafutwa na maafisa wa Jeshi.

Je, ni kwa sababu hii Luteni Hamoud, Kapteni Ahmada na Chwaya waliamua kufanya Mapinduzi, licha ya wenzao kutaka yaahirishwe?.
VI
SEHEMU ya tatu ya makala haya toleo lililopita, tuliona jinsi na namna mipango ya kupindua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilivyoandaliwa kwa kuhusisha vikundi viwili; yaani kundi la Wazanzibari, wengi wao wakiwa wanajeshi, kutoka Dar es Salaam lililopanga kuwasili Zanzibar usiku wa manane kuamkia Aprili 7 na kundi la Wazanzibari ndani ya Zanzibar, lililojumuisha wanajeshi na raia.

Tuliona, baada ya kundi la Dar es Salaam kutowasili Zanzibar saa iliyopangwa, na Serikali ya Zanzibar kugundua kuibiwa kwa silaha Kambi ya Bavuai ambazo zingetumika katika Mapinduzi, na Luteni Hamoud na Kapteni Ahmada kuanza kufuatiliwa na wakuu wa Jeshi, wanajeshi hao waliamua kutekeleza zoezi hilo wenyewe kwa kumuua Rais Abeid Amani Karume dhidi ya ushauri wa washirika wao wa kuahirisha mapinduzi.

Tuseme, kwa mfano, kwamba kundi la Dar es Salaam lingewasili Zanzibar kwa kazi hiyo kama ilivyopangwa, Mapinduzi yangetekelezwaje?
Kwa mujibu wa mkakati wa Mapinduzi uliofikiwa Aprili 2, 1972, Suleiman Mohamed Abdullah Sisi (mwanajeshi wa JWTZ, mkazi wa Ilala Flats, Dar es Salaam) alipangwa kuongoza utekaji wa kambi ya Jeshi, Mtoni, ambapo Kapteni Ahmada, alitakiwa kuteka kambi ya Jeshi, Bavuai, Makao Makuu ya Jeshi na Chuo cha Jeshi cha mafunzo ya Redio, vyote hivi viko eneo la Migombani.

Kituo cha Polisi cha Malindi kingeshambuliwa na kutekwa na kikundi chenye silaha kikiongozwa na Luteni Hamoud ambacho kingeweza kuteka magari yenye Redio za mawasiliano.

Askari Yusufu Ramadhan angeongoza kikundi cha maafisa wa Polisi walioingizwa kwenye mpango huo na kuteka Kituo cha Polisi cha Ziwani.
Amour Dughesh (mwanajeshi; Zanzibar), yeye angeteka Ikulu na kumkamata Karume, kisha kumpeleka Kituo cha Redio kumlazimisha atangaze kupinduliwa kwa Serikali yake. Baada ya hapo, Kituo hicho kingeachwa chini ya udhibiti wa Badawi, Mpatani na Mohamed Said Mtendeni (mwandishi wa habari, gazeti la China, mkazi wa Vuga, Unguja).

Uwanja wa Ndege ungetekwa na kikosi cha wanajeshi na baada ya hapo kingeachwa chini ya udhibiti wa Ali Sultan Issa (meneja wa Shirika la Mafuta, Zanzibar).

Mpango huo ulilenga pia kuteka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa ASP, ambayo yalikuwa pia Makao Makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar, ikiongozwa na Kanali Seif Bakari na kuwekwa chini ya udhibiti wa Mohamed Abdullah Baramia, Kapteni Khamis Abdullah Ameir, wa Makao Makuu ya Jeshi, Zanzibar; yeye alipangwa kuzuia mashambulizi kutoka nje kama Mapinduzi yangefanikiwa.

Mapinduzi au mauaji ya Kisiasa?
Mapinduzi ni kitendo cha kutaka kubadili sawia hali, serikali au mfumo fulani wa kijamii kwa matumizi ya nguvu, ikiwa ni pamoja na kuondoa mhimili wa mfumo huo.

Mapinduzi yanaweza kuwa kwa njia ya jeshi kama jeshi limetumika au ya kiraia kama raia walitumika, kama yalivyokuwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Mauaji ya Karume hayawezi kuitwa mapinduzi ya kijeshi wala ya kiraia kwa sababu kifo chake hakikubadili mfumo wala muundo wa serikali. Haya yanaweza kuitwa mauaji ya kisiasa yenye lengo la kuondoa chanzo au mhimili wa kero katika jamii bila kubadili serikali.
Mwanazuoni mahiri Barani Afrika, Profesa Ali Mazrui, anatafsiri “mauaji ya kisiasa (political assassination) kuwa ni kitendo cha siri cha kutoa uhai wa mtu mashuhuri kisiasa, kinachofanywa na wakala asiye wa serikali; kwa sababu za kisiasa au zisizofahamika.

Naye Profesa William Gutteridge wa Chuo Kikuu cha Aston, anasema mauaji ya kisiasa kuwa ni kitendo cha kutoa uhai wa mtu mashuhuri katika jamii kwa sababu za kisiasa na kinajumuisha pia jaribio la mapinduzi lililoshindwa na watu wengi kuuawa katika kutekeleza kilichokusudiwa.
Kwa mantiki hii, mauaji ya Karume, kama yalivyokuwa mauaji ya Rais Anwar Sadat wa Misri, kwa kupigwa risasi wakati akiangalia gwaride la jeshi lake, yalikuwa na lengo la kuiondolea jamii kero bila umuhimu wa kubadili serikali. Katika mauaji kama hayo, mlengwa huwa mmoja tu kama chanzo au mhimili wa kero.

Karume aliuawa kwa sababu ya utawala wa kimabavu, ukatili na ukiukaji wa haki za binadamu kama tulivyoona hapo juu; wakati Sadat aliuawa kwa kuisaliti jamii ya Kimisri, kwa kusaini Mkataba wa suluhu kati ya Misri na Israeli uliojulikana kama “Camp David” ili kusitisha harakati za Waarabu dhidi ya Uzayuni wa Kiyahudi.

Sababu nyingine ilikuwa ni kukumbatia sera za kiuchumi za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), hatua iliyoathiri maisha ya Wamisri kiuchumi na matarajio ya kijamii ya Waislamu nchini humo na Jumuiya pana ya Kiarabu kwa ujumla.
Malengo ya mauaji ya Karume yanajidhihirisha kwa vielelezo kwa yale yaliyofuatia chini ya utawala wa mrithi wake, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, aliyechukua uongozi Aprili 11, 1972.

Baraza la Mapinduzi lililoketi Aprili 10 – 11, 1972, pamoja na kumthibitisha Jumbe kuanzia Aprili 7, 1972 kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza hilo, pia lilipitisha azimio la kudumisha, kulinda, kutetea na kuendeleza fikra, malengo ya kimapinduzi na sera alizoacha Karume.

Hata hivyo, Wazanzibari wengi walitaka Kanali Seif Bakari amrithi Karume kwa kuwa alikuwa mtu wa karibu zaidi kwa Karume kuliko Jumbe, kwamba ndiye pekee miongoni mwa Wazanzibari ambaye angeweza kuendeleza fikra za mwasisi huyo wa Taifa la Zanzibar.

Nyerere aliingilia kati akiwa na hoja kwamba, kwa kuwa Rais Karume aliuawa na mwanajeshi, kumteua Bakari ambaye alikuwa mwanajeshi kumrithi kiongozi wa kiraia, kungetafsiriwa kuwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoweka mwanajeshi madarakani. Hoja ya Nyerere ikashinda.

Kwa kuanzia, Jumbe alifuta Amri ya Karume ya kutoagiza chakula na bidhaa nyingine kutoka nje; akaruhusu akiba ya fedha za kigeni kutumika kuagiza chakula kumaliza tatizo la njaa na upungufu wa vitu, jambo lililokuwa mwiko wakati wa Karume.

Vivyo hivyo, kwa mara ya kwanza, Serikali ya Zanzibar iliruhusu wanafunzi 17 kutoka Zanzibar, kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuahidi kupeleka wengi zaidi.
Desemba 1972, ASP kilifanya Mkutano Mkuu wake wa kwanza tangu 1962 uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 900 kutoka Visiwani, Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wa TANU, pamoja na wageni wengine kutoka nchi 12 za Kiafrika, wakiwamo wawakilishi wa chama cha MPLA cha Angola.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Jumbe alilaani tawala za kimabavu na ubabe, ukandamizaji na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya raia, alisema: “Viongozi lazima wawatumikie watu, na si watu wawatumikie viongozi…..”
Kwa maneno hayo, alikuwa amefungua milango ya demokrasia Visiwani, utawala bora, uwajibikaji na kuongoza kwa mifano, tofauti na enzi za Karume.

Februari 5, 1977, Nyerere na Jumbe waliunganisha vyama vyao, TANU na ASP, kuunda Chama cha Mapinduzi – CCM, jambo ambalo lisingewezekana wakati wa Karume ambaye hata Muungano wenyewe aliweza kuusigina kwa kisigino cha nguvu. Vivyo hivyo, mwaka 1979, Zanzibar ilijipatia Katiba yake ya kwanza baada ya Katiba ya Uhuru ya 1963, chini ya Serikali ya Mseto wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP).

Ni wakati wa utawala wa Jumbe, Zanzibar ilipata Bunge (Baraza la Uwakilishi) lake la kwanza kwa njia ya uchaguzi, wakati kabla ya hapo, Karume aliapa pasingekuwa na uchaguzi Zanzibar kwa miaka 50, kuanzia 1964 hadi 2014.

Chini ya Jumbe, kwa mara ya kwanza tangu 1964, wanasheria waliruhusiwa kufanya kazi Zanzibar; watu hawakugongewa tena milango usiku na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Na tazama, yote yalifanywa kuwa mapya, ambapo isingewezekana chini ya utawala wa Rais Karume.

Imeandikwa na;
Joseph Mihangwa [Raia Mwema (raiamwema.co.tz) April 11, 2012
 
Hao washtakiwa waliachiwa kisa nini au ni kweli Nyerere alihusika kummalizia Karume so wakaona nao hao kazi wamemalizwa?

Ibrahim Babu hivi yupo hai?
Makomredi wa Chama cha Umma (UMMA PARTY)

Tarehe 26 April, 1978, wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 13 ya Muungano, hatimaye Mwalimu Julius Nyerere aliamuru kuachiwa kwa Abdulrahman Babu na wengine kumi na mbili waliokuwa kizuizini bara. Ijapokuwa wote waliokuwa kizuizini bara waliachiliwa, hukumu za kifo kwa wanne wao – Babu, Ali Mahfoudh, Tahir Ali Salim na Hamed Hilal – kamwe hazikufutwa.

14 June 2023
April 26, 1978 Mahojiano na aliyekua Waziri wa Uchumi na Maendeleo Tanzania, Abdul-Rahman Babu miaka sita baada ya kuachiwa kutoka kifungoni kwa tuhuma za kupanga mauwaji wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume.

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZYu1na4gcTo&

CLICK:
Source : TANZANIA: FORMER TANZANIAN MINISTER SPEAKS ON RELEASE AFTER SIX YEARS DETENTION ON CHARGES OF MASTERMINDING ASSASSINATION OF ZANZIBAR HEAD OF STATE.

Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu(Amnesty) lilifanya mpango wa kuwapatia hadhi ya ukimbizi Hamed na Hashil, na hatimaye waliondoka kwenda Denmark. Huko, Hamed aliniambia ‘baada ya uchunguzi wa kitabibu na tiba, ndipo tulipoweza kurudisha imani na ari yetu’. Ali Mahfoudh aliondoka Tanzania kwenda kuishi Msumbiji.
 
Nimejifunza mengi ambayo nilikuwa sikuyajua
 
APRIL 7 kila mwaka ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kiongozi wa Mapinduzi Matukufu na huadhimishwa kila mwaka tarehe 7 April

1712306871530.png

1712306971914.png
 
February 1966
Zanzibar

Maadhimisho ya miaka miwili ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mwaka 1966 mjini Unguja

View: https://m.youtube.com/watch?v=KJOZDp6psU0

Sherehe zilisogezwa mbele toka January 1966 hadi mwezi February 1966 kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhan

Footage of Tanzanian President attending a military parade in Zanzibar which celebrated the overthrow of the Zanzibar Sultanate. He watched the proceedings from a review stand alongside Vice President Abeid Karume.The event was watched by delegations from Cuba, East Germany, the USSR and China. Soviet and Chinese-made vehicles were on display.The parade was postponed from January 12th because of the festivities associated with the Moslem season of Ramadan
Source: Adeyinka Makinde
 
Back
Top Bottom