Hii picha inaongea nini?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,859
18,282
Hii picha inaongea mambo mengi sana. Wazungu wanasema a picture speaks louder than words. Nikiiona hii picha nahudhunika mno, hasa kwa ajili ya vijana wa kitanzania wanaohitimu vyuoni makumi kwa maelfu kila mwaka.

Maisha ya kiafrika ni magumu sana. Unaweza ukute hata elimu yenyewe aliyoipata haiwezi kumpa uwezo wa kurudisha alichokitoa ama kubadilisha hayo maisha ya nyumbani kwao. Kibaya zaidi familia zetu pia zinaamini kuwa ukishapata degree basi wewe ndio tegemeo la ukoo , ndio maana vijana wengi huwa wanakimbia nyumbani.
1702627209579.png
 
Duh! Hukoo mzima unamwangalia akawakomboe! Alafu unaambiwa akajiajiri!
Hapo sasa. Sijui atajiajirije wakati mtaji wote ameuacha chuoni. Kuna kijana wetu mmoja tumemsomesha pale UDSM digrii ya BA Kiswahili. Baada ya kuhitimu akapata ajira ya kuolewa na kuzalishwa mtoto. Hadithi ikawa imeishia hapo.

Wewe fikiria familia yenyewe ya kimasikini tumejipinda kumsomesha kwa miaka yote 3 halafu ajira anayopata ni kuolewa kwa mahari ya Tsh laki 8. Na bado anadaiwa mkopo na serikali. Ama kweli jehanamu ni hapa hapa Tanganyika.
 
Ila huyu naye alizidi, utasomeaje Shahaha ya Kiswahili hapa Tanzania?? Shahada ya namna hii itakusaidia nini ktk maisha yako kwa hapa Tanzania??? Ni vyema vijana hawa wakatafuta taarifa sahihi mapema ktk safari zao za maisha ya kuisaka elimu, wafanye utafiti wa kina mapema juu ya masomo yanayofaa zaidi kusoma kuanzia wakati wanapokuwa kwenye Shule za Sekondari.
Wafanye uchaguzi sahihi wa masomo ya kusomea tangu wakiwa Sekondari na wakiwa Vyuo Vikuu, wasikurupuke au kufuata mkumbo.
Kwa maoni yangu, ni vyema wakachagua au kupendelea kusoma masomo ya Sayansi zaidi kuliko masomo ya Sanaa ambayo kwa kiasi kikubwa soko lake kwa sasa linaonekana kuwa gumu sana hapa duniani.
Sayansi asili (yaàni Sayansi na Teknolojia) ndio inayotawala dunia kwa sasa, whether you like it or not.
 
Katika kipindi hiki cha graduation kwenye taasisi nyingi za elimu nadhani ni wakati wahitimu na wahitimu watarajiwa wajiweke sawa kifikra wajue kabisa wanapomaliza wajue jamii ya mtaani si lelemama. Wanapokuja huku wasije na mentality za kichuo huku maisha ni mkanda ukilegeza unaadhirika. Kila la kheri kwa wote
 
Ila huyu naye alizidi, utasomeaje Shahaha ya Kiswahili hapa Tanzania?? Shahada ya namna hii itakusaidia nini ktk maisha yako kwa hapa Tanzania??? Ni vyema vijana hawa wakatafuta taarifa sahihi mapema ktk safari zao za maisha ya kuisaka elimu, wafanye utafiti wa kina mapema juu ya masomo yanayofaa zaidi kusoma kuanzia wakati wanapokuwa kwenye Shule za Sekondari.
Wafanye uchaguzi sahihi wa masomo ya kusomea tangu wakiwa Sekondari na wakiwa Vyuo Vikuu, wasikurupuke au kufuata mkumbo.
Kwa maoni yangu, ni vyema wakachagua au kupendelea kusoma masomo ya Sayansi zaidi kuliko masomo ya Sanaa ambayo kwa kiasi kikubwa soko lake kwa sasa linaonekana kuwa gumu sana hapa duniani.
Vijana wengine wanajisomea tu ilmradi wapate digrii wakidhani kitaeleweka mbele kwa mbele. Nawaona vijana wengi waliohitimu Bachelors za Education wapo vijiweni wanaendesha bodaboda.

Kusema kweli kuna haja ya serikali kubadili mtaala wa elimu na kuondoa masomo ya kipumbavu kama vile Kiswahili, Civics, History na masome mengine ya kipuuzi ili kuwapa wanafunzi nafasi ya kujikita kwenye masomo ya maana.
 
Wewe unaongea Kwa kutumia hisia wala sio akili

Je ninani kafanikiwa Kwa kusoma science na nani kashindwa Kwa kusoma arts ,kufanikiwa maisha kuna involve mambo mengi Sana. Ni mtu mjinga pekee anaweza kutoa lawama Kama hizo.
 
Ila huyu naye alizidi, utasomeaje Shahaha ya Kiswahili hapa Tanzania?? Shahada ya namna hii itakusaidia nini ktk maisha yako kwa hapa Tanzania??? Ni vyema vijana hawa wakatafuta taarifa sahihi mapema ktk safari zao za maisha ya kuisaka elimu, wafanye utafiti wa kina mapema juu ya masomo yanayofaa zaidi kusoma kuanzia wakati wanapokuwa kwenye Shule za Sekondari.
Wafanye uchaguzi sahihi wa masomo ya kusomea tangu wakiwa Sekondari na wakiwa Vyuo Vikuu, wasikurupuke au kufuata mkumbo.
Kwa maoni yangu, ni vyema wakachagua au kupendelea kusoma masomo ya Sayansi zaidi kuliko masomo ya Sanaa ambayo kwa kiasi kikubwa soko lake kwa sasa linaonekana kuwa gumu sana hapa duniani.
Sayansi asili (yaàni Sayansi na Teknolojia) ndio inayotawala dunia kwa sasa, whether you like it or not.
Kiswahili kinafundishwa sehemu nyingi huko duniani ni swala la kupata exposure tu huyo utamuonea wivu.
 
Back
Top Bottom