tatizo mkuu wanaume ukiwapa hela kwa makubaliano yakurudisha ujue umetafuta njia yakuachana maana ukimkumbusha maswali haya yatakuhuau.
1. ina maana huwez saidia mimi?
2. nikikuoa wewe cjui utakuwaje.
3. halafu kama hii ndo tabia yako sidhan kama tutawezana! kama huna hela ya kula sema mi nmekupa vingapi?
nakushauri usimwache kama mabo mengine yuko poa kwani yaweza ashampaga mtu akamrusha.
mimi nliwahi mpa mtu hela alikuwa anasoma japo ana kazi alipe hela ya semister nzima afanye mtihan huwez amin nlirusishiwa elfu ishirin tu tena kwa matusi . na hiyo hela tulikuwa tunacheza kibati nlilazimika kuilipa kwa machungu sana. yaan nliapa mwanaume sikopeshi hela maisha labda mume wa ndoa najua tuko pamoja.
pole kwa machungu tafuta mda uongee naye