Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni
10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri

Mkuu, kwakuwa uwezekano wa kuahirisha upo. Ni afadhari uahrishe kwanza na utulie, huenda biharus mpya tabia hiyo ni yake kweli ambapo naiman walau chembe za hyo tabia ulishaziona tangu mlipoanza kufahamiana(kufundshana kazi), kama hakuna mapungufu mengne yoyote, tulia na ufikiri upya, kwa huyo ulomwita biharuc mpya ninamashaka na nachelea kusema ye aliiona fursa na akaitumia ipasavyo. Sasa kazi kwako. La msingi. Usikulupuke.
 
Usifanye papara ya kuoa, tulia kwanza. Inawezekana mhemko wa kumuoa "Bi harusi mpya" ni kwa sababu umeudhiwa na mchumbwa wako. Ila kwa suala la kumuacha mchumba umeshaona taa nyekundu usingoje kupigiwa honi.

Usifanye papara, ndio ila Fanya haraka sana! Watu kama hao wachache afu wanatafutwa mbaya!
 
Uamuzi wako uko sahihi, tabia ya mtu ni kama ngozi ya mwili. Anaweza kujichubua akawa mweupe lakini badae itarudi vile vile na itakuwa mbaya za idi maana ameshaibreach.
 
Wakuu nawashukuru wote kwa mawazo yenu mazuri
Ingawa nipo chini ya shinikizo kutoka kwake na ndugu zake kuwa wameshafika mbali kwenye maandalizi ya send off na kwamba wanadai tuzungumze tuyamalize ila kwa kweli moyo wangu umegoma kabisa
Nawashukuru sana

wakafie mbali na mtoto wao.
wanawaza chereko tu hao na sio furaha na amani ya ndoa yako
 
Kwa sababu ni wachumba bado ni vizuri ujipe mda wa kutafakari, ki ukweli hapo mwanamke hakuna. Ninachojua wakati wa uchumba huwa mara nyingi upendo unakuwa ktk hali ya juu kiasi kwamba ambacho hamwezi kuchangia ni kifo tu. Kwa nini yeye kawa tofauti hafai atakusumbua.
Na kama utafunga ndoa ya kikiristo isiyo na kuachana utajuta, heri nusu shari kuliko shari kamili.
 
Uliponiudhi ni pale uliposema unaomba ushauri ningefurahi ungesema umemuacha totaly na maandalizi yanakwenda kasi kumuoa huyo aliyekusaidia pesa,sasa mkuu kama tu anashindwa kujua thamani ya mama mkwe wake unategemea nini.
Kwangu mimi mama ndiyo kila kitu hawa wake wapo tu kila siku lakini sio mama,huko mbeleni tunaomba mrejesho
 
Mkuu, kwakuwa uwezekano wa kuahirisha upo. Ni afadhari uahrishe kwanza na utulie, huenda biharus mpya tabia hiyo ni yake kweli ambapo naiman walau chembe za hyo tabia ulishaziona tangu mlipoanza kufahamiana(kufundshana kazi), kama hakuna mapungufu mengne yoyote, tulia na ufikiri upya, kwa huyo ulomwita biharuc mpya ninamashaka na nachelea kusema ye aliiona fursa na akaitumia ipasavyo. Sasa kazi kwako. La msingi. Usikulupuke.

we utakuwa ndugu ya bi harusi nini sina shaka na uliahidiwa udreva,
 
Kwanza napenda kukupa pole kwa maumivu yaliyokupata. Wanafalsafa husema moja ya vitu vinavyoweza kumsaidia mtu kuwa na Amani "peace in mind" ni kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ndani ya muda muafaka. Huu muda ni muafaka kwako kwa kumwoa "BIBI" harusi mpya na kama inawezekana hiyo tarehe ya harusi isogeze karibu zaidi na si mbali. Ukiendelea kujivuta vuta si ajabu ukaendewa kwa BABU kama sio mligotini au Bagamoyo. Wewe unafikiri hao wakwe zako hio aibu wapo tayari kuipokea? Kama hawapo si ajabu wakatafuta mpango mkakati wa kujitanzua. Hapo kuwa kama mtu asiekuwa na shule kwani akiamua jambo huwa habadiliki.
 
Hivi terms and conditions za kutumia JF zinawaruhusu JF wenyewe kupost thread ya mtu huko kwene ukurasa wa JF instagram na Facebook? Au wanaomba consent kwa alieomba ushauri kwanza kama wanaweza kufanya hivyo? Ipo maana ya mtu kuingia JF na mambo ya huku kuishia huku au huu ushauri tunaoombwa huku tunakua tunapoteza muda kushauri "hypothetical" cases?
 
Usioe huyo ana roho mbaya sana.Anawakilisha jamii ya wanawake wasio na upendo wapo kwa ajili ya kukuchuna tu chako chao chake ni chake.
Ukioa mwanamke wa aina hiyo hamtakuwa na ushirikiano kwenye masuala ya kiuchumi na usitegemee kuwa-treat vizuri ndugu zako wakija home kwako.
Wewe ni mwanaume fanya uamuzi mgumu,mwambie ukweli usiwe mnafiki na achana naye mara moja.Huyo ni muuaji kabisa.Tupa kule.
 
Huyo Mchumba hafai, nakuunga mkono kabisa piga chini ulete kitu kingine. Hivi angekua ni mzazi wake asingetoa?

Pili sikuungi mkono issue moja tu, ile mahari hakuna kuwaachia kumbafu zake, twende tukaidai ikiwezekana hata mahakamani. Kama hawana basi tukaandikishiane nao kua ikitokea akachumbiwa tena basi mahari unachukua wewe kufidia ile uliotoa mwanzo.

Na kama ofisini wewe ni Senior kwake muonyeshee undava kwa kumpangia kazi za kufa mtu awe anatoka saa nne usiku.

Mwishowe copy link ya huu Uzi umtumie aone tulivyokereka na u-roho mbaya wake shenx type zake!
 
hiyo siyo sababu ya kumwacha sema humpendi tu umepata sababu
Wewe utakua ni ndugu tu wa huyo Cha-roho mbaya.
Mwambie Dada yako aendelee na vikao vya sendoff na kitchen party kama kawaida, ila safari hii ataolewa na hiyo gari akishainunua!!
 
Huyo Kaka achana naye, lol, yatakuja kukukuta makubwa ujute, kwenye mahusiano kujaliana ni muhimu sana, huyo hakujali, hakuhurumii na hajui thamani ya binadamu mwenzake, achana naye, anataka ajulikane Mke wa mtu tu while anakuumiza, huyo hata Wewe ukiumwa hautokuwa na thamani kwake tena na ni mtu wa kuthamini mali kupita kiasi kuliko maisha ya binadamu mwenzake, oa mwingine unayeamini anakufaa
 
..Ameshindwa kukupa hela (kwa mkopo) ili umtibu mama yako, kwa kisingizio kuwa hana. Kumbuka huyo ni mama mkwe mtarajiwa.
...Ameshindwa hata kuja hospitali kumuona mama mkwe mtatajiwa kwa mda wa wiki mbili, sababu kuu ikiwa ubize wa kazi za ofisini.
..Wakati huo huo mpo katika vikao vya maandalizi ya arusi, ili aje kuwa sehemu ya familia yako.
Kiongozi una mtihani mkubwa, ninavyowajuwa wanawake walio wengi, angetumia mda huo kuonyesha kwako na familia yako kuwa yeye ni chaguo bora kuliko wote kwako. Yeye ameonyesha tofauti kabisa, tena si ndani ya ndoa. Huyo ana walakini tena mkubwa, wala sihitaji hadithi ya upande wa pili kufanya maamuzi. Kwa utafakari upya, uchumba unaweza kuvunjwa na hakuna atakayesema nyoko.

Mkuu umetoa kitu kimetulia uamuzi ubaki wake sasa mleta mada. Wewe boby- pitia hapa upate hii nondo.
 
Last edited by a moderator:
hiyo siyo sababu ya kumwacha sema humpendi tu umepata sababu
Awaeleze ndugu wa huyo Dada amecancel hiyo harusi na mtoto wao na sababu huyo dada anazijua mwenyewe, tena amwambie aziseme mwenyewe au yeye aziseme kwa wazazi wake, wajue wazi mtoto wao ndio kavuruga mwenyewe kwa kutoonyesha utu kwake na familia yake, ili asije akawaeleza ndugu zake uongo wamwone huyo Kaka hafai
 
Back
Top Bottom