Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Huyo demu ni mpare nini? mteme mazima akifika 30yrs atakuwa used, expired na kuanza kutafuta visharo vya kumkuna.
cc. mshana jr.
 
hiyo siyo sababu ya kumwacha sema humpendi tu umepata sababu

unatetea ujinga . mwanamke anathamini gari kuliko uhai . Siku mumewe ataumwa atashindwa hata kumpeleka hospital kisa anataka kununua meri
 
piga chini ndugu- TABIA NI KAMA NGOZI huyo demu sio! anafanya hivyo kabla hujamuoa-ukimuoa si itakuwa balaa!! huyo anaweza akamtimua hata mama yako eti
 
Mkuu tuliza boli kwanza. Ahirisha ndoa hiyo ili ujipe muda wa kutosha kumsoma tena huyu mpya ambaye unamfahamu tokea zamani kama friend tu. Usikute naye alikuwa desperate kuolewa (the second one) ili ampate mtu. Time will tell. Give yourself a year or so then utapata majibu. Ila huyo binti hakika ni kiboko ya njia, unakuwa mchoyo kiasi hicho. Bora angetoa hata laki tano ili hizo tano usake kwa washikaji.

Kuna issue moja ya ukweli bwana mmoja anaishi na mwanamke kwa miaka zaidi ya kumi ila hawajafunga ndoa kwa kuwa jamaa si mtu wa kueleweka na alimtesa sana huyo mwanamke kiasi kwamba alikataa kuolewa. Ninafikiri anajipanga kuondoka. Unajua unapokuwa na hela au utajiri halafu ukautumia vibaya na kudhalilisha nao hasa wake zetu siku ukifilisika unakosa wa kukusaidia. Basi jamaa alipata msiba wa kufiwa na mwanaye wa kwanza alizaa miaka hiyo akawa hana senti mfukoni. Pamoja na mateso na manyanyaso ya kifedha aliyomfanyia huyo mwanamke lakini mwanamke alimpa shilingi laki tano na zaidi kwenda kijijiji kumzika mwanae. Sasa ona mwanamke kama huyu ambaye pamoja na mateso na manyanyaso alikuwa na huruma je huyu mchumba ambaye hajapitia haya ila ni mchoyo anafaa kuwa mke huyo? kwa kifupi hafai na atakutesa sana pindi hali ya maish ikishuka kwa bahati mbaya.
 
Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni
10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri

tatizo mkuu wanaume ukiwapa hela kwa makubaliano yakurudisha ujue umetafuta njia yakuachana maana ukimkumbusha maswali haya yatakuhuau.
1. ina maana huwez saidia mimi?
2. nikikuoa wewe cjui utakuwaje.
3. halafu kama hii ndo tabia yako sidhan kama tutawezana! kama huna hela ya kula sema mi nmekupa vingapi?
nakushauri usimwache kama mabo mengine yuko poa kwani yaweza ashampaga mtu akamrusha.

mimi nliwahi mpa mtu hela alikuwa anasoma japo ana kazi alipe hela ya semister nzima afanye mtihan huwez amin nlirusishiwa elfu ishirin tu tena kwa matusi . na hiyo hela tulikuwa tunacheza kibati nlilazimika kuilipa kwa machungu sana. yaan nliapa mwanaume sikopeshi hela maisha labda mume wa ndoa najua tuko pamoja.

pole kwa machungu tafuta mda uongee naye
 
kama ulikuwa umemshirikisha Mungu kupata mke mwema hakika hilo ndo amekupa jibu huyo sio mke kabisa,mm binafsi sijamuelewa ni mchoyo kupitiliza mama yako ni mama yake je angekuwa mama yake hizo hela asingetoa?

aisee yamkini huyo aliyekusaidia ndie mtu sahihi ,sasa usichukue maamuzi haraka ww endelea kumsihi Mungu,sasa hivi tulia hicho kikao peleka mbele

I hate these kind of comments!.Iko vipi kama na yule mchumba wake alikuwa anamshirikisha mungu kuhakikisha anayunza ile milioni 4 ili atimize azma yake ya kununua gar?.

Acheni kuendekeza umaskini wa mawazo!,Ukishindwa kupambanua akili yako na kuwaza nini cha kufanya ili utoke kimaisha na kusema kwamba mungu atakusaidia ww utakuwa wa ajabu sana.

Ni ajabu sana kuona kuna watu katika karne hii ya 21 wana mawazo kama hayo.
 
Hakuna mke hapo mkuu! Utajuta ukiona mwanamke mwenye roho mbaya kiasi hicho.

Nakushauri hebu futa kwanza hayo mambo ya harusi ujipange upya kwa kumsoma kwa karibu huyo dafa aliyekusaidia na huku ukimlilia Mungu akuonyeshe njia sahihi.Ndoa ahirisha kabisa kwanza kwa mwaka huu.
 
Huyo wa kwanza achana naye kabisa hafai.
Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni
10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri
 
Uamuzi wako ni sahihi kabisa. Nakuunga mkono kwa asilimia mia. Achana na huyo mwanamke.Muoe aliye kusaidia.
Kweli mkuu, ubaya siku hizi unalipwa kwa ubaya, mpige chini.. Atakuja mlaza njaa mama yako atakapokuja kukutembelea, na hela ya kula umempa. Kumbe ana save hela ya kwenda saluni
 
..Ameshindwa kukupa hela (kwa mkopo) ili umtibu mama yako, kwa kisingizio kuwa hana. Kumbuka huyo ni mama mkwe mtarajiwa.
...Ameshindwa hata kuja hospitali kumuona mama mkwe mtatajiwa kwa mda wa wiki mbili, sababu kuu ikiwa ubize wa kazi za ofisini.
..Wakati huo huo mpo katika vikao vya maandalizi ya arusi, ili aje kuwa sehemu ya familia yako.
Kiongozi una mtihani mkubwa, ninavyowajuwa wanawake walio wengi, angetumia mda huo kuonyesha kwako na familia yako kuwa yeye ni chaguo bora kuliko wote kwako. Yeye ameonyesha tofauti kabisa, tena si ndani ya ndoa. Huyo ana walakini tena mkubwa, wala sihitaji hadithi ya upande wa pili kufanya maamuzi. Kwa utafakari upya, uchumba unaweza kuvunjwa na hakuna atakayesema nyoko.
 
Mkuu kwa ushauri wangu mimi.
1. Huyo mchumba achana naye kabisa. Maana ndoa ni ndoa haina ujanja na kama ni ya Kikristo ndio kabisa huna ujanja. Na ujue huyo utakae muoa utaishi nae miaka yako yote.

2. Huyo dada alie kukupesha hela unatakiwa kujipa muda. Muulize Mungu kama ni wakwako kweli maana unaweza ona kuwa anakufaa maana umesha umizwa halafu na yeye akaja kukuumiza. Mshukuru sana Mungu amekushtua mapema kwa huyo wakwanza kaa chini omba upate jibu.

3. Usitape msukumo toka kwa mtu maana mke unaishi nae wewe na wala sio sisi. Siku mambo yakiwa magumu ni yako yakiwa mazuri ni yako. Sisi hatutakuwepo huko tena.

Tumia muda wako vizuri kufanya maamuzi mazuri.
 
Mkuu mbona hapo wala haihitaji ushauri aisee...huyu siyo mwanamke ni shetan,piga window chini fastaaaa na asikuzoee kabisa,pumbavu sana...
 
Kwanza ulisha muacha kimoyo. Hayupo moyoni mwako ila unamuona tu asubuhi kwa kuwa mko ofisi moja. Angekuwa mji mwingine, hata humu jf usingali andika kuomba ushauri bali ungetangaza ndoa mpya mapema na mchumba mpya.
Sasa, kaka, usipoteze mda wako, mwambiye kuwa penzi lako lilikufa siku ile alipo kutosa ukiwa na hekaheka za kumsevu mama yako. Mwambiye ulidhani angekuambia kuwa wala sikukopeshi bali nakupa kamponye mama yetu. Kwa kuwa hakumwona ka mama yake, ndo maana hata kwenda kumwona hakuenda hospitalini, tena hakuwa na tyme naye hata kuulizia hali yake mpaka unamwambia kuwa karuhusiwa.
Hata kama alikuwa amesha agizia gari na kuwa lilikuwa tayari njiani, alitakiwa akueleze kuwa nina hela kwenye akaunti lakini tayari nimeagiza gari na kulipia nusu hivyo saa yeyote wataniita kumalizia, hapo ningekuambia, hana kosa. Lakini ka alisevu kwa ajili ya gari, GARI NA LIMUOE.
Chukua huyu aliye kufaa kwenye dhiki yako. Tena umesema alikuwa anaenda kumjulia hali mamako kule hospitali. Huyu ana moyo wa huruma, atakujali zaidi na hata haitakuwa shida kumweleza mamako kwani aliuona uso wake kule hospitali.
Oa anaye kufaa leo, kama anakupenda tena, umefunga kazi hapo. Achana na mwenye machozi ya mamba, leo amekukatalia kumsaidia mamako, je ukipoteza kazi si atakuacha ndani akalale ofisini?? Achana naye huyoo
 
Wakuu nawashukuru wote kwa mawazo yenu mazuri
Ingawa nipo chini ya shinikizo kutoka kwake na ndugu zake kuwa wameshafika mbali kwenye maandalizi ya send off na kwamba wanadai tuzungumze tuyamalize ila kwa kweli moyo wangu umegoma kabisa
Nawashukuru sana

Huu uzi sikutaka kuchangia coz yote ya maana wameshatangulia kusema wadau huko juu but hapa imenibidi..kataa kabisa hayo mashinikizo ya ndugu kwa manufaa ya maisha yako huyo bora ungemkuta ananyonywa mate uchochoroni ungejipa moyo kwamba baada ya harusi atabadilika ila kwa kushindwa kukusaidia ktk ugonjwa wa mama yako mzazi ameonyesha ni jinsi gani asivyojua ninini maana ya maisha ya ndoa,itatokea siku mama akaumwa tena akalala kitandani akawa ni wa kuogeshwa,kuveshwa na kulishwa unadhani huyu aliyeshindwa kwenda kumuona hospital ataweza kufanya haya,zaidi ukimwambia atakwambia nenda kamuogeshe wewe huku ame-log in Facebook ana-update profile yake,bora angeonyesha hata kujali kwa kukwambia chukua hii 300,000 nyingine fanya fanya donation hapa ofsini but macho makavu anakwambia hana hata cent???,sawa basi hela huna,jamani hata kwenda kumuona mgojwa aliefanyiwa operation na kulazwa umeshindwaa??!!(tena ni bi harusi mtarajiwa)ni wakati gani binadamu utaonyesha utu wako kama sio wakati wa matatizo hasa yahusuyo ugonjwa?mkuu boby- lawama hawakuumbiwa wanyama,tumembiwa sisi binadam unadhani hao ndugu wanaojaribu kukushinikiza kumuoa ndugu yao ingekuwa imetokea kwa mmoja wao wangekubali aingie kwenye mdomo wa mamba!ingekuwa familia inayojitambua wangekaa kimya kwa aibu hii,ni jinsi gani hawakumlea ktk maadili mema,achana nae huyo,hakuna mke hapo!!
 
Last edited by a moderator:
Hapo hakuna Mke kabsaaa. Waswahili husema dalili ya mvua ni mawingu na Siku njema huonekana asubuhi. Sasa wewe unasubiri ishara gani? Kwanza mshukuru Mungu kwa kukufungua macho kabla ya kujiingiza kwenye shiida za milele tena ndoa yenyewe ya kanisani? thubutu , huwezi kuachana naye kirahisi.Afadhali ndoa yenyewe ingekuwa ya kimila au ya kienyeji . Ndugu yangu usijaribu kabisa. RAFIKI WA KWELI NI YULE ANAYEKUSAIDIA WAKATI WA SHIDA YAANI A FRIEND IN NEED IS A FRIEND INDEED.
 
Napiga chini aisee! Naoa wa kunipa milioni 2, na siyo wa kujifanya bize na ofisi wakati bi. Mkubwa anaumwa!
 
Huyo alokusaidia kaonyesha upendo wa dhati , oa huyo atakufaa kama alivyofanya sasa. Huyo mchumba wa awali acha aolewe na hilo gari analotaka kununua
 
Back
Top Bottom