Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Pole boby. Hiyo nayo ni changamoto ya aina yake. Nahisi unahitaji ujipe muda, ni bora usogeze muda wa kuoa ili upate tafakuri njema zaidi. Ukikosea katika kuoa/kuolewa imekula kwako mkuu, labda huko ughaibuni kama kuna ndoa za mkataba. Tulia Mungu akuongoze
 
kaka mi ni mwanamke ila nakushauri oa huyu aliekusaidia kipindi una shida
huyo mchumba hamna kitu hapo
yaani kipindi hiki ye ndo alitakiwa ajipendekeze kwa wakwe zake ye ndo anaonyesha rangi halisi kabisa
yaani hajui ht kupretend duuh!!

tabia ni km ngozi na haibadiliki na huyo mchumba ndivyo alivyo hatobadilika mm sikushauri umuoe ng'odo
ht kuja hospitali....!!!
kkaaaaahhhhh
 
Sio kila baya huwa ni tatizo, mengine ni baraka. Naamini hili nalo ni baraka kwa uamuzi wa maisha.
 
Duh Jambo la busara ni kumsamehe kama kakiri makosa
Amsamehe kwa kuwa hakuwa na hela au kwa sababu hakuenda kumuona Mama Mkwe Mgonjwa, utasema alipitiwa na shetani.Acheni Kumdanganya huyu ndugu yetu maana kama vikao vya arusi vimeanza huyo ni zaid ya mchumba kufanya hivyo ni Majibu tosha kuwa sio type yake yuko pale ili kutimiza wajibu wa ndoa na hana upendo kwa mwanaume
 
Ushauri inalipa sana kuvunja uchumba kuliko ndoa. Maumivu ya kuvunja ndoa ni makali kuliko uchumba. Tulia piga mahesabu kisha fanya uamuzi sahihi. İla huyo sister hakufai. Kama ni mkristo funga na kuomba kama wiki au chini ya hapo kisha Mungu atakupa jibu sahihi lengo usikurupuke.
 
Leo amethamini hela kuliko uhai wa mama yako mzazi ambaye kimsingi atakuja kuwa mama yake pia, kesho hatashindwa kufanya hivyo kwa uhai wako wewe, huyo ni wa kumkimbia,

sio kidogo, kuhusu bibi harusi mpya, yeye hakukusaidia ili umuoe yeye, alifanya kwa ajili ya utu alionao, ukimuacha huyo utakuwa umeacha kitu cha thamani sana ambapo kila wakati kitakuumiza kila ukimuona mama
 
boby- Pole sana kwa mama na hongera kumtibu mama!!
ishu, hii ina hadithia mambo mengi...... hakuna wakulaumiwa! shukuru mungu mama hajambo, naufuate maamuzi yako.
Be blessed boby
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapo hakuna mke, chukua huyo no. 2 weka ndani, yaani mama aliyemzalia mume wake mtarajiwa badala ya kuonyesha compasion na ushirikiano kwenye kumtibu yeye anataka gari... ama kwa hakika yeye kwake mali ni bora kuliko utu, weka mbali na watoto huyo.
 
Dalili ya mvua ni mawingu,bora kuvunja uchumba kuliko ndoa huenda mungu amekuonesha ili ujue unaenda kuishi nae alivyo daima mtu mwema utamjua kipindi cha shida ss huyo hela ilikuwa ngumu kukukopa ht nguvu yake ya kwenda kumuuguza mm mkwe imemshinda muombe mungu wako atakupa jibu zur

Pole sana...Inauma mnooo aisee ....Ebu kaa chini waza na kuwazua....nduo ni kwikwi ...magizo ni mengi..bt kama mimi ningekuwa wewe...Wala siwaz mara mbili....napiga chini....akufae wakati wa dhiki ndo rafiki...
 
Aolewe na hiyo pesa yake tena mwambie bila mama usinge kuwepo
 
Ki ukweli ukiwa kwenye uchumba inabidi ujipendekeze kwa mama mkwe na upendo unakuwepo haswa. Nadhani huyo hajawa tayari kuolewa. Yupo kimaslahi zaidi. Muoe aliyekusaidia.
 
Mkuu fanya maamuzi yaliyo sahihi. Hakuthamini uhai wa mama means that hathamini furaha ya moyo wako. Kuna mwingine zaidi ya mama ndugu yangu?
Achana nae huyo.
 
boby- kwanza hongera sana kama haujafanya chochote na huyo unaemwita Bi harusi mpya. Kwa sababu alionyesha upendo wa hali ya juu sana, hilo tu linatosha hata mume aliye kwenye ndoa kuchepuka nae kuonyesha fadhila (Sitetei michepuko).

Kama umeshamwahidi Bi harusi mpya ndoa, usipotimiza nako huenda ukamuumiza kiasi cha kujutia hata uamuzi wake wa kukusaidia ulipokua na tatizo japo hakukusaidia ili umuoe.

Alichokionyesha huyo mpenzi na bibi harusi wa zamani kinakatisha tamaa na lazima uwe njia panda. Kwa upande mwingine naweza sema shukuru Mungu hili tukio limetokea huenda lilikua ni kukupa nafasi ya kuweza kumfaham huyo mkeo mtarajiwa.

Mimi mama watoto wangu aliwahi kunisaidia kwenye mazingira magum ambayo hata mimi sikutegemea na sikuamini. Pale ambapo hapakua na mtu wa kutegemea, alikua msaada mkubwa sana na sio mara moja. Wakati huo huo hapakua na mpango wa kufunga ndoa.

Kwa huo ukarim na upendo wake wa dhati, niliazimia moyoni kifo ndio kitakachotutenganisha, vinginevyo aniache yeye.

Tena hapo ukimwelezea mama yako huenda akatishia kukuachia radhi kama hautamuoa huyo binti aliyekusaidia.
Tahadhari, kuoa au kuishi na mtu kama mwenza ina jumuisha vitu vingi sana, kama ana tabia nzuri na unampenda na unaona anafaa kuishi nae ukiongezea na hili la msaada weka ndani ila usioe kwa sababu tu amekusaidia, utamuumiza sana kwa kuchepuka.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu nawashukuru wote kwa mawazo yenu mazuri
Ingawa nipo chini ya shinikizo kutoka kwake na ndugu zake kuwa wameshafika mbali kwenye maandalizi ya send off na kwamba wanadai tuzungumze tuyamalize ila kwa kweli moyo wangu umegoma kabisa
Nawashukuru sana
 
Uhai ni muhimu kwanza, hela baadaye, zaidi ya hayo hela ikipotea inatafutwa siyo uhai..
Kama jinsi unavyosema ndivyo ilivyotokea basi ni bahati mbaya sana, lakini inastaajabisha kama miaka 2 hukuwahi kujuwa tabia yake hii..
 
Back
Top Bottom