Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

aiseee....pole kwanza......

ingawa ni story ya upande mmoja.....bora ingekuwa unataka pesa ukafanye starehe lakini swala.la ugonjwa na bado mtu mgumu......


hairisha harusi......inawezekana kuna mengi unaweza kuyajua kuhusu huyu bibi harusi........jipe muda kabla ya kuamua kuoa tena huyu mpya uliyempata.......
 
Mpwa wangu asante sana ila hebu some hii signature yako mwenyewe, nadhani inabeba ujumbe tosha wa ku-support nilichokiongea mimi:
  • To every successful man, there is a very complicated woman who is causing a headache behind!. Bobi Wine
    ​
Mpwa complicated woman siyo huyo anayefurahia mimi kupotelewa na mzazi??? She can not be a Complicated Woman anayethamini Magari kuliko uhai wa mzaa chema? Unless otherwise Jamaa aliforce huo uchumba..

Narudia tena Complicated Woman hawezi kuwa huyo ambaye hathamini Afya ya Mama yangu au Baba yangu au Eti Kisa aqkanunue Vitz au Ist au Passo.

SHE IS STUPITY TO INFINITY NA ATAKUJA KUJUTA KAMA KWELI AKIACHWA HAYO SIYO YAKUZUNGUMZWA NA UPANDE WA FAMILIA YAKE GHARAMA WALIYOPOTEZA YA KUANDAA SENDOFF HAILINGANI NA UHAI WA MTU WAENDELEE WAMFANYIE SENDOFF ATAOLEWA NA HIYO GARI
 
Unaona sasa!

wanafikiria harus sio alichokifanya ndugu yao!
nilifikir watasema airishen kwanza had mambo yakae sawa? wanasema wafika mbali what a nonsense?
kiongozi ndoa nizaidi ya uijuavyo!

sisemi ili kukuforce umuoe mpya ila naanza kukuonea huruma ghafla kabla hata hujaanza kurud hapa na kuanzisha uzi baadae!
kwa binti hakuna raha kama kujipendekeza kwa wakwe!!
ukutane na mama asiye na makuu, mbona utasema ulikuwa wapi hapo mtu hata vikao havijaanza (huna uhakika kama atakuoa au laaah) sembuse vikao tayar, jaman si mahala pake pa kumuonesha mama kuwa mwanao hajakosea!!!!!!!!
duuuuuuuuuuh!

hapo hamna mke aiseeee.........aanze upya.
 
yaan mtu hata vikao vinaendelea amekunyima pesa huyo ni hatari na ndio tabia yake asikudanganye atabadilika oa
aliekusaidia huyo mwingine hafai kama upo anafanya hivyo ukiwa haupo si ataacha afe mchaga nn huyo dada
 
I beg to differ with you, usimpotoshe mwenzio. Endapo weweunamvumilia easy-taker wako ni vile tu
Hukupata bahati aliyoipata Bobby- kuona rangi mapemaaaa.Hivyo wote wana kazi? Kesho mume kalost…si atakula jeuri yake mpakaashangaeeee..


Ushauri wangu kwamhusika bora ukosee kujenga nyumba utabomoa kuliko kuoa….speaking fromexperience mambo ya kuja kuachana kwenye ndoa yana athari nyingi mno kulikomaelezo!


Mkuu....umeongea jambo la mbolea sana....Nyota njema huonekana Asubuhi km mwanamke kamuonyesha namna hiyo sasa hv je,,wakishaishi muda mrefu itakuwaje.....
 
Last edited by a moderator:
tupa kulee!! msamaha wa uwongo huyo atakusumbua,atakua anaishi na wewe kwa kupretend,lakini inner cole ni ana roho mbaya,nahisi atakua mzuri smart hicho labda ndio kinakuvuta,hivyo mfanye loose ball wako,muoe huyo mwingine
 
Mpwa naomba nirudie tena kuwa huu ni ushauri tu sina lengo la kumpotosha! Huwezi kuhukumu upande mmoja wa story na pia huwezi kuhukumu kwa event moja tena ya namna hio, kwa mfano mleta mada anaifahamu Account ya Mpenzi wake huyo, well and good, lakini wakati huo huo mpenzi wake huyo alimwambia kuwa kama haamini waende wote wakaangalie kwenye Account yake! Kwanini hakwenda? Kwanini hakuweza ku-print salio na kumuonyesha in a friendly way ili ku-resolve na kuja kutosa judgement ambayo sio emotional driven? Narudia silengi kumpotosha mtu ila ni ushauri na mtazamo wangu!
Tukubali kuwa kila mtu ana namna ya ku-handle issues zake hasa ambazo ziko kwenye hii field kwahio ni lazima kwa nyakati fulani tuwe different. Nakubali

kaka umeongea kwa hekima na busara sana!
ila mimi naweza kupa majibu ya kwa nini hawakwenda na ta wangeenda binti alishaandaa majibu!
wangefanya kabla mama hajatibiwa angemwambia dada ameomba niwekee kesho anzichukua ( yaan kuna story iliandaliwa trust me, wadada tukiwa wekwa kwenye kum na nane ni hatari)

kumbuka anakwambia alipo muuliza baadae binti alikiri kuwa kweli alikuwa anasave za kununulia gari
(na hapo kakiri baada ya kuona jamaa kachange mwelekeo ili aombe masamaha na baada ya kuona mgonjwa kapona)

vipi mgonjwa angepoteza maisha? msimamo wake ungekuwa hazikuwa zangu dada aliniombe nimuwekee!!!!

mkuu huyu jamaa kapewa bonge la indicator!!
ila ni yeye akae amuombee huyo binti abadilike au ...........!!!!!?
 
Mpwa naomba nirudie tena kuwa huu ni ushauri tu sina lengo la kumpotosha! Huwezi kuhukumu upande mmoja wa story na pia huwezi kuhukumu kwa event moja tena ya namna hio, kwa mfano mleta mada anaifahamu Account ya Mpenzi wake huyo, well and good, lakini wakati huo huo mpenzi wake huyo alimwambia kuwa kama haamini waende wote wakaangalie kwenye Account yake! Kwanini hakwenda? Kwanini hakuweza ku-print salio na kumuonyesha in a friendly way ili ku-resolve na kuja kutosa judgement ambayo sio emotional driven? Narudia silengi kumpotosha mtu ila ni ushauri na mtazamo wangu!
Tukubali kuwa kila mtu ana namna ya ku-handle issues zake hasa ambazo ziko kwenye hii field kwahio ni lazima kwa nyakati fulani tuwe different. Nakubali

Katika wote humu Wewe ndio umeonyesha kuwa na mtazamo tofauti

Ila nimegundua kitu kimoja kama ulivyosema kuwa wewe hupendi kuumiza kichwa na mke wako ni mtu ambaye anapuuzia vitu, hii inatokana kuwa umesha gundua Mke wako ni wa aina gani ndio maana huwa hupendi kuangalia mambo kwenye mapana Hivyo huwa unatafuta sababu za kujifariji Caz huna jinsi nyingine maana ndio ameshakuwa mke tayari.

Napenda tu kusema kuwa maisha yako na ya mleta uzi ni tofauti sana. Wewe umeshaoa ndio maana inabidi uwe na mitazamo chanya hata kama mke wako kakosea kosa kubwa kiasi gani, Lkn mleta uzi yeye hajaoa bado na Huu ndio Wakati wa yeye kufanya maamuzi sahihi hata kama maandalizi yamesha anza.

Kifupi hakuna kitu kibaya kama mtu kutokuwa na utu, there is no justification for that, wewe umesema mke wako huwa hamjulii hali mama yako wakati anaumwa Halafu unatupa justification kuwa ndivyo alivyo, Huko ni kijipa faraja tu ndugu jibu sahihi hapo ni kwamba mke wako hamjali mama yako na hana utu Sema huna cha kufanya caz umechelewa maana umesha muoa,

Baada ya kusema hayo ndugu boby- hongera kwa kujibiwa sara zako na Mungu, huyo piga chini halafu jipe muda wa kuangalia mambo yatakavyo enda na huyo aliye kusaidia
 
Last edited by a moderator:
Tatizo sio kila kitu kwenda kuchungulia chungulia..ona sasa.

Kabla ya hili la pesa, kulikuwa na vingine ulivyokuwa una issue naye?
 
Mi naona akae chini afikirie nini cha kufanya coz wanawake ni wagumu sana kuwaelewa. Huyo aliyemkopesha pesa anaweza kuwa ni shetani mara tatubya huyu wa sasa ukute yeye anataka ndoa tu na amuharibie mwenzake ila akishaingia kwa ndoa ndio atatoa makucha yake. Be careful kijana unaweza ukaruka majivu ukakanyaga moto!

hizi ni hadith za kufikilika, yaani mtu mtenda mema unamfikilia ubaya khaa!!
 
Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni
10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri

Ndugu pole kwa hilo. Binafsi nakushauri go for the second one maana alitanguliza utu na kujali uhai wa mtu. Huyu mwingine iko siku atakufanyia vituko vikubwa.
 
Mnachosahaugi ni kuwa ''WANAWAKE'' ni watu na wana maamuzi yao binafsi, pamoja na hadithi yako kuwa na uongo-uongo mwingi wa kutunga tunga ngoja nikupe ushauri wangu kama ulivyoomba.

Ipo hivi, hakuna kazi ngumu hapa duniani kama kupata MKE mwema, binafsi naamini kupata mke ni ngumu hata kuliko kupata mme, especially kwa vile vigezo vyetu vya kibinaadamu. Amini usiamini as long as hawa wake zetu hatuwaumbi wenyewe lazima utakuta mapungufu ambayo unatakiwa taratiiibu ujaribu kuyakubali na kuyabadilisha kama si wewe mwenyewe kubadilika.

Swali kwako: Kwa mfano umeshaoa, mkeo akakaa kupika siku hiyo akisema 'hajisikii' kufanya chochote ... utampiga, utamtukana au utapika mwenyewe?! Utafanyaje?? ... Now akili kichwani mwako ....

MWISHO: Kuoa si mchezo na mke hapimwi kwa kitu kimoja.

(Ni mtazamo binafsi)
 
Mkuu tafadhari sana hapa umeleta mada yako na watu wamekushauri, na tunategemea mrejesho toka kwako n nn kimeendelea baada ya watu kuku ushauri, isije kuwa watu wanapoteza muda wao bure! Ila kumbuka kuwa majuto n mjukuu, na ndoa ya kikristo haina supplementary! Ukioa umeoa,

Ushauri wangu
Uyo mkuu si mke bali unaoa balaa na ndo maana ndugu zake wanakubembeleza umuoe hope wanafaham tabia zake, wanataka kutua mzigo wa misumari na wakupe wewe.

Hii ishu haina tofauti na ya kaka yangu, b4 hajao wakiwa kwenye uchumba na mke wake, aliniambia kuwa huyu mchumba wake hana roho ya huruma na hapendi ndugu, kwa kuwa sikuwa na maamzi nilimshauri kaka achukue maamzi atakayoona yanafaa. Jamaa akafunga macho akamuoa, sasa nakwambia mpaka sasa huyu dada keshafukuza babake na mamake, mama yetu mm na kaka ndo alimfukuza kama mbwa! Sasa kubwa zaidi ni pale kaka aliposimamishwa kazi, hata chakula hapikiwi kisa hajaacha ela ya matumizi! Hapa tulipo tunamuuguza kakayetu uyo mama hata kumlipia bili ya hospital hataki,
Pamoja na kulazwa hospital bibie pale pale kitandani anamdai fedha ya matumizi,
Hapo kumbuka bbie kasomeshwa mpaka masters na kaka, miradi yote anasimamia yeye uyu mama na ana kazi nzuri tu!

Jamaa mpaka sasa anataka kufa na presha kwa matendo anayofanyiwa na mke wake!

Ila kaka angechukua maamuzi mapema baada ya kugundua kuwa mke wake hana roho ya huruma na hapendi ndugu hope mpaka sasa jamaa angekuwa na afya tele
 
Mtoa mada BOBY wewe mwenyewe kama ulivyoona wachangiaji karibia wote wamekushauri achana na huyo mchumba asiefaa. Kwa kukazia tu na mimi nasema chukua uamuzi wa maana tangaza ndoa rasmi na huyo dada aliekusaidia na achana kabisa huyo wa kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom