Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Kwa hiyo tuseme ingekuwa hana account hiyo bank usingejua kama muongo na ungemuoa ila mi pia binafsi ningeahirisha kama si kusogeza mbele niendelee kumpima!! Na si kuanzisha uhusiano mpya! Ukute na huyo ulishachungulia account yake! Vigezo vya siku hizi pesa le mbebez awe na pesa mbeleeez no money no wedding duh
 
Pole sana ndugu, inauma sana kumwacha mtu uliyempenda na mpaka umeanza mipango ya harusi.

Pole pia kwa kumuuguza mama yetu mpenzi, mama ambaye alikuleta hapa duniani. Pole kwa kuhangaika peke yako kumuuguza mama huku uliyempenda akiwa bize na kukusanya hela ya kununua gari na hivyo kushindwa hata kukusaidia na hata kufika hospitali kumuona mgonjwa.

Uamuzi wa mwisho uko kwako, ndoa sio mapenzi, angalia sana moyo (nafsi yako) wako unakwambia nini ufanye na nini usifanye.

Ukikurupuka kufanya maamuzi utakuja jutia na sijui kama utakuwa na nafasi ya kurekebisha.

MUOMBE MUNGU AKUONGOZE NA AKUPE UTULIVU WA HALI YA JUU ILI HATIMAYE UPATE MKE ATAKAYE KUWA FARAJA KWAKO PINDI UNAPOPITIA MAGUMU NAWE UWE FARAJA KWAKE KATIKA TAABU NA RAHA SIKU ZOTE ZA MAISHA YENU.
 
Red alarm, na msamaha wake ni kwa vile anaona harusi inayoyoma, uamuzi ni wako ila mi binafsi hapo nimeoneshwa sura kalimi, next time itaokea tuu akiwa na uhakika yuko ndani......binafsi ninge delete mazima siyo huyo maana umeoneshwa tayari
 
Mungu anajua njia mbalimbali za kukupa mke/ mume mwema katika maisha. Kaka Yangu umeomyeshwa Mke mwema, muoe kwani licha ya kujua wewe tayari una mchumba hivyo hakuwa na chance ya kukupata akakukopesha hizo hela/ Kwa kweli huyo mchumba wako wa mwanzo hafai kabisa! Maisha tena ya mama yako hapana hafai. Mwisho: Hata kama hutaamua kumuoa huyu aliyekuazima pesa usimuoe huyo aliyekukatalia pesa hata alie machozi ya damu!
 
hebu mshirikishe mzazi wako, ila mimi hapo zamaani ningepiga chini....
 
Mkuu piga chini chukua aliyekujali. Unaonekana mungu wako yupo karibu sana. Kwani maisha ni kufaana na sio kufaa. Ila waweza peleka harusi mbele na kufuata utaratibu unaofaa.
 
tunamshirikisha mungu kwa kila jambo pia yatupasa kuwasamehe waliotukosea huyu mchumba ajakukosea , kakuonyesha uhalisia wa tabia yake maamuzi ya kubeba gunia la misumali kichwan yako juu yako kesho usilalamike
 
Dah!!! Huyo dada ni ndugu yako nini? Haiji katika akili . Kama ameshindwa kwenda hospitali atakwenda kijijini kumuuguza kama mzazi wake kweli?
 
Nina wasisi kama hiyo gari angeweza hata kukupa siku umepata shida
 
Kweli huo mtihani ndugu yangu. Inawezekana kweli akawa amejutia na akawa amebadirika for good, lakini kwa ujumla lazima uchanganyikiwe. Huenda na huyo mpya alizidisha huduma baada ya kuona mwenzio amechezea bahati akaamua kuicheza game vizuri na ukute hana ukarimu wa kiasi hicho kama hana target fulani.

Juu ya yote pole na jipe muda wa kutafakari kwa kina, na je huyo mpya wampendea huduma zake au wampenda yeye binafsi? Ukijijibu vyema utakuwa na maamuzi sahihi!
 
mkuu kuna mengi sana ya kujifunzaa baada ya kukosea, naamini uyo mchumba wako wa kwanza yuko katika mateso na maumivu makari, anajua namna gani anaeenda kuaibika na kuwaaibisha wazazi wake na ndugu zake, amekwisha umia sana na atakua amekujua wewe ni mtu wa namna gani, na imani yangu ni kua amejifunza mengi sana, ni advantage kwako sasa, fanya kusogeza harusi mbele lakini muoe yule wa kwanza, huyu wa pili mfanyie kitu kikubwa as zawadi kuonesha ni mtu muhimu kwako kiasi gani, atakua na peace of mind tu, epusha laana zisizo na maana kila kitu kina happen for a reason na kila kitu kinacho cha kujifunza na kubadilisha....... adios amigo
 
Sitaki kuwa mtetezi wa kitu nisichokijua na kuhukumu upande mmoja, lakini wakati unakwenda kununua Plot ulimweleza? Na yeye ana access na account yako? Je mliwahi kukaa na kumweleza kuhusu situation ya kwenu kwamba wewe unategemewa kwenu? au ulitangaza utajiri? Huwa mnaznungmzia wapi mambo yenu? Bar? Au huwa baada ya kazi mnakwenda wapi? Unaaminije kuwa huyu alietoa Milioni mbili ni ili tu akupate na sio kwamba na yeye ni tofauti na huyo?

Mpwa tuliza kichwa, hizo ni ishu minor sana sana sana, kwenye ndoa hakutaki hasira kiasi hicho na maamuzi ya kitoto hivyo! Kaeni, zungumzini, nipo kwenye ndoa kwa muda mrefu sasa na nimeona mengi.

Kwa mfano, mke wangu huwa mgumu sana kumjulia Mama yangu hali ambaye ni mgonjwa, na huwa napiga simu kila jioni nikifika home tena mbele yake, lakini anaweza, nasema anaweza asikuulize anaendleaje, lakini nilikuja ku-study hio tabia nikajua ndio alivyo yaani yeye ni easy taker, watu wa namna hio wapo wengi sana. Kuna mtu hata ukimwambia kuwa sogea hapo utaungua moto, yeye atasema ngoja tu niungue si kuna dawa!!!!!


Kwahio, ushauri wangu kama Kaka yako wa JF endelea na mipango yako na jua kuwa pengine hio ndio tabia ya mkeo na pengine na wewe una tabia zako mbaya zaidi. Zungmzeni sometimes, mimi huwa namwambia mke wangu na hua sitaki tubishane, kwahio huwa namwambia tu na kupotezea.

Mpwa wangu, dont take life too serious Iasee utakufa uyaache hapa hapa maisha haya na bank kazi iishe.

Aaagghh niruhusu niishie hapa kama nimekukera, NISAMEHE

Acha kutetea ujinga huyo mwanamke hafai ingekuwa ni mimi ata mawasiliano yasingekuwepo. Am telling u jamaa akioa huyo roho mbaya kuna siku atakimbiwa akiwa kitandani amekata kauli kwa ugonjwa demu akiwa saloon anaset nywele. Ataikumbuka hii thread.

Kuna matukio sio km hili lipo wazi la kupigania maisha ya mzazi.
 
aise mkuu kweli uko njia panda maana nianzie wapi kukupa ushauri

cha kufanya umeshajua undani wa huyo mchumba wa zamani yukoje tabia yake
ni mwanamke ambaye hapendi nduguzo anajijali yeye nashida zake
cha kufanya wewe ongea naye kuwa ulikereka na tabia yake ya mwanzo
na vilevile hukupenda alivyofanya halafu mwambie uamuzi wako mpya wa sasa
ukoje juu yake

halafu nenda kwa huyo wa mchumba wa piili mshukuru sana kwani bila yeye
mama asingekuwepo ni kama Mungu alimtumia hyo dada kuponya uhai wa mama yako
mwambie umefurahishwa na tabia yake na anza kutangaza NIA kwake ya kuwa naye
kwani ana moyo wa upendo na kujali wengine hakujijali yeye alionesha utu wake

N.B:
CHA MWISHO NAOMBA TENDA YA KUWA MC WA HARUISI YAKO NA KUKUTENGENEZEA
KADI ZA MWALIKO WA HARUSI NA KEKI PIA MKUU USINITOSE BESTITO MWENZIO

 
nina hakika baada ya vikao viiingi vya familia na ofisini, bibiharusi atabaki kua yuleyule wa awali.
Kila la heri.

Wewe ndio umenena, bwana harusi nae anaonekana booya tu. Akili zimeshikwa upande wa mwanamke hii ishu anajadili na wakwe ila mama ajamwambia, ndio maana mwanamke analipelekapeleka ashalijua.

Eti wamesema nimsamehe kwa kuwa send off wameshaandaa kila kitu pumbaff ndugu wa mke unategemea wakushauri nini na wao wanataka kutua mzigo. Wanaume tumebaki wachache sana aisee mwanaume kauli yake ni moja.
 
Wakati wa matatizo ndio unaweza kujua rafiki yupi anakupenda/anakujali. katika hali ya kawaida huyu alitakiwa awe wa kwanza kukuonea huruma na kukusaidia kumtibu mkwewe na after all ungemrudishia. Huyu hafai kuwa mke
 
Back
Top Bottom