Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Achana nae huyo 'mama ni mama tu' gari? Ndo nin? Ama kweli acha gari alilokua analitaka limuoe' ukiomuoa huyo ndo atakuonyesha jeuri ya ajabu. ACHANA NAE
 
Wee nae mgumu kuelewa kha! Ebu soma tena hiyo part

Unakuwa mbishi tu ila ushahidi wa kimazingira unaonesha kunguru ni huyu bwana na hapa alikuwa ameshamchoka mwenzie ila ni sababu tu alikuwa anatafuta....a

Wakuu habari za mida,
.........
Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri
 
Aiseee kuna wanawake ni selfish Sana, wa namna hiyo wapo wengi Sana.
Wewe sogeza tarehe ya harusi hata mpaka mwakani ukae sawa emotionally hlf uchukue mtu mwenye utu.
Pole Sana , inaumiza mno.
 
hiyo siyo sababu ya kumwacha sema humpendi tu umepata sababu
 
wewe kama ungekuwa ni muumini na hivyo msomaji wa maandiko matakatifu, ungeachana na mpango wa kuoa mara moja baada ya kukutana na challenge hiyo.

jifunze zaidi......

1. usijiingize kwenye mambo ya ndoa eti kwa vile tu muda wa kuoa/kuolewa umefika. huo siyo mpango wa Mungu

2. mke/mume ni neema kutoka kwa Mungu. ushauri wa hapa JF hautakupa solution ya hiyo stalemate uliyo nayo sasa. go back to the drawing board na utapata mke bora kuliko hao wawili, na kwa wakati.
 
hiyo siyo sababu ya kumwacha sema humpendi tu umepata sababu


Duh!kuna sababu zaid ya hyo?bila shaka nawe unatabia hyo

ww mtu kakusaidia kifedha mpka familia yako unashindwa kulipa fadhira?
hata hasingekuwa mchumba ile tu kibinadamu ni vibaya kushindwa kumsaidia alyekusaidia
nipe sababu ya ww kumuacha mwenza wako??
 
Duh!kuna sababu zaid ya hyo?bila shaka nawe unatabia hyo

ww mtu kakusaidia kifedha mpka familia yako unashindwa kulipa fadhira?
hata hasingekuwa mchumba ile tu kibinadamu ni vibaya kushindwa kumsaidia alyekusaidia
nipe sababu ya ww kumuacha mwenza wako??

so anaenda kwa yule sababu kamkopesha milion2 na siyo kwamba kampenda
 
Mwanamke siyo ndugu yako. Na wewe umekosea, alivyosema twende hata tukaangalie wote, mngeenda kweli baada ya kuzikuta sasa ungekuwa na sababu nzuri sana.
 
Mkuu kuna watu huwa wanabisha eti mungu haku waonyesha mke mwema sasa wewe unataka Mungu akufunulie mara ngapi ndo ujue hapoa hakuna mke????? yani ungekua karibu na amimi ninge kuzaba vibao kwa kutokuskia sauti ya Mungu...
 
Duh
Mdada ana roho ngumu....gari over afya/uhai wa mkwewe
 
Badilisha na tarehe ya kuoa uanze upya kutafuta mchumba huyo unayesema alikukopesha siyo chaguo lako, unaoa Kwa kukopeshwa pesa??? Kama ungekopeshwa na ofisi ungeioa? Hapo huna la kujitetea na nilivyokuona unapenda mteremko ndo maana unashindwa kujipa muda Wa kutafuta upya Kwa utulivu nasiyo kukimbilia huyo aliyekupa msaada kwa moyo Wa utoaji nasikwamba ndo Mke mwema.
 
Achana na huyo mchaga.wachaga wote ni pesa mbele mapenzi baadaye


Lakini pia kuhusu kumuoa huyo aliyekukopesha hela si shauri jaribu kuanglia na sifa zingine.vipi kama angekuwa amekukopesha mwanaume mwenzio ungesemaje?unaweza mfanya kuwa rafiki mwema na siyo mke kama sifa zingine hana.yaani kama umevutiwa tu na jinsi alivyokusaidia siyo sifa toshelezi.
 
Elli nakuheshimu na umeongea kwa busara sana... Mimi sitakuwa na mengi lakini naomba kutofautiana na wewe kitu kimoja hasa kulinganisha mgogoro wa maamuzi ya ununuzi wa Plot, Gari na ugonjwa wa mzazi?? Kwa hapo Ndugu yangu Robby sijui Bobby angalia .......Kilichobaki ni wewe wengi wameongea na wameleweka.
Hakika Ugonjwa ni Ugonjwa Mzazi ni Mzazi hapatikani mara mbili, wewe usiye nifaa muda mbele ya wazazi wangu hutanifaa nikiwa sina pa kuegemea.

MWISHO WANAWAKE WENGI WANA TABIA HIYO KIKUBWA JAPO WANALILIA KUOLEWA LAKINI ROHO YA UBINAFSI WANAZO SANA NDICHO CHANZO CHA MIGOGORO MINGI KWENYE MAHUSIANO. TUMEAMBIA NI SEHEMU YA MBAVU ZETU LAKINI BIBLIA ITAKUWA ILIKOSEA.

nilichukua likizo mhula mzima kukaa na wa wakwe kuuguza nilirisk kazi yangu ili kujipendekeza ndoani
nashangaa mwanamke anaedharau wakweze au kwa kua mie mama mzazi amekufa?!!!
yule mama ananipenda mpk najiskia raha yaani kupendwa vile
huyu mdada kimeo tu
pesa ktu gani mbele ya uhai
 
Ndugu kigugumizi cha nini tena hapo? au unataka utuudhi? akufaaye kwa dhiki ndio rafiki! mzazi mgonjwa bibie ana save anunue motokali hivi hapo kulikuwa na haja ya kufungua uzi kwa jambo hili! kibadilika ni jambo gumu kwa hatu ambao hawako tayari kubadilika na utu huonyeshwa waqt wa matatizo so chukua chuma hicho kilichokufaa huyo wa motokali atawapate wenye roho kama yake.
 
Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni
10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri

mama ndo kila kitu kama kamnyima mama pesa ya matibabu unataka mpaka kumnyima ugali nyumbani ndo uchukue hatua?acha kabisa hizo mambo,uzuri Wa mwanamke tabia na huyo hana Tabia nzuri tena umeona mwenyew wala si Wi-Fi kuwa anapakaziwa,hayuko tayari kwa ndoa kwa jicha la 3,mwambie aendelee kujifunza utu
 
Nipo njia panda.

Wakuu ushauri

Hapo hakuna cha njia panda, mbona njia ni nyeupe kabisa ya kumuacha?
Hakuna njia panda hapo,uko high way ya kumuacha. Achana na huyo kenge mkuu. Huyo nyoka mwenye makengeza ameishaonyesha tabia yake,piga chini mkuu.
 
akija ndani sasa siku unafulia ww atatoa kweli pesa yake akanunue mboga?kama wake zetu?cjui.....
 
Nimejaribu kufikiria cha kushauri nimeshindwa, labda nikuachie usemi usemao " AKUFAHAYE KWA ZIKI NDIYE RAKIKI"
 
Back
Top Bottom