Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

..Ameshindwa kukupa hela (kwa mkopo) ili umtibu mama yako, kwa kisingizio kuwa hana. Kumbuka huyo ni mama mkwe mtarajiwa.
...Ameshindwa hata kuja hospitali kumuona mama mkwe mtatajiwa kwa mda wa wiki mbili, sababu kuu ikiwa ubize wa kazi za ofisini.
..Wakati huo huo mpo katika vikao vya maandalizi ya arusi, ili aje kuwa sehemu ya familia yako.
Kiongozi una mtihani mkubwa, ninavyowajuwa wanawake walio wengi, angetumia mda huo kuonyesha kwako na familia yako kuwa yeye ni chaguo bora kuliko wote kwako. Yeye ameonyesha tofauti kabisa, tena si ndani ya ndoa. Huyo ana walakini tena mkubwa, wala sihitaji hadithi ya upande wa pili kufanya maamuzi. Kwa utafakari upya, uchumba unaweza kuvunjwa na hakuna atakayesema nyoko.

Words Eli79 mwema utamjua kwenye matatizo.
Pia ndoa haina mbadala ukikosea umekosea.
Mtoa mada una wakati mgumu sana
Poleee
 
Last edited by a moderator:
Uamuz mzur ndo uanaume oa acje kukulibwata mkuu huyo hakufai
 
Kumuacha huyo ni sawa! Hafai ila kukurupuka na huyo mwingine haifai kabisa! Sasa tulia kwanza!

UOTE=boby-;12470042]Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni
10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri
[/QUOTE]
 
Kazi kweli kweli...

Najaribu kufikiria namna ambavyo binti mpenda gari alivyobanwa na chupi sasa kwani muda si mrefu aachwa solemba...

Mwanawake huyu namfananisha na wanawake wa kizazi cha leo ambao huwa katika mahusiano...

Kazi yao kubwa huwa ni kuwachuna maboifrendi zao ilihali wazazi au ndugu wa maboifrendi wapo dhoofu ili hali kiuchumi na kiafya...
 
Mtu achune kiasi, lol, kuna wengine hatari
 
Huyo bibie wa gari piga chini tafadhali, ila khs bi harusi mpya be hesitant kwanza kufanya maamuz drastically namna hiyo usije muumiza binti wa watu in the long run coz of making permanent decisions on temporary feelings.. Im sure you were just in awe of how supportive she turned out to be but kumpenda serious kiasi cha kukuweka ndani nehiiii batchao!!! Jipe muda kwanza kutafakari
 
Uchunguzi 99% ya wachangiaji wamesema piga chini oa bibi harus no2
Wengi wape Mkuu.
 
Wakuu narudia tena kuwashukuru kwa Upendo wenu
Kiukweli napitia kipindi kigumu sana
Maana kuna vikao vinaendelea usiku na mchana kutatua tatizo hili
Nilikuja kuomba ushauri hapa wakati vikao vinaendelea ili kupata nguvu zaidi hivyo nawashukuru wote

Pia kazini kuna mgogoro umejitokeza juu ya jambo hili
Lakini unaendelea kutatuliwa kiutu uzima na uongozi

Tukifika mwisho Wa hii tufani nitawapa mrejesho
Kila nikipitia hizi comments zote nakua kama napona rohoni
Nawashukuru sana
 
haaa kwanza asante kwa kunijuza ulinunua plot ya ten million turud kwenye mada wanasema vitu vidogo vina maana kubwa sana katika mapenzi ni ngumu kukushaur uachane nae au uendelee nae kwa kua mwisho wa siku wewe ndo mwenyw maaumzi ndo unajua ni vipi moyo wako umemuelemea huyo dada ila kibinaadam amekosea sana gari na uhai asee mh hajui kama bila huyo mama asingekuona wewe ??
Habari za siku madame
 
Wanawake wapo kimaslahi tumia akili kuwaza na sio moyo
 
Attachments

  • 1429255426992.jpg
    1429255426992.jpg
    22.3 KB · Views: 176
Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni
10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri

mkuu unaamuaje kwa jema moja tu, uamzi wa kumwacha bibi harusi wa zamani upo sahihi, lakini jipatie muda kidogo wa kufikiria kwa kina juu ya huyo mpya usije ukaingia kwenye mtego, ndoa ina mambo mengi hivyo kusaidia tu hela hakutoshi, maamuzi ukiwa katika hasira si mazuri, ila huyo wa zamani usirudi hafai.
 
Kama huyu ameweza kukusaidia tena akijua uko kwenye mipango ya kuoa hata kama mliwahi kuwa na mahusiano na jinsi ninavyojua wivu walio nao dada zetu... Hakika nakuambia huyu ndiye mke wa maisha yako. Aina ya wanawake kama huyo asiyejali uhai wa binadamu na vitu ni wasumbufu sana rafiki mfano mzuri ni huyu kaka yangu yaani hadi ndugu tumebaki kwenye maombi maana chake chake cha kaka chao na anatumia nguvu zoote kuhakikisha yeye ni jembe na jamaa ni lofa. Kwa ishara hii nakushauri ufanye maamuzi magumu kama ya nchi kuingia vitani. Gooooooooooood day.
 
Back
Top Bottom