HITIMISHO
Ingawaje mie leo nimeonekana kama mchezaji wa akiba ila mjue tu kuwa uhai wa huyu Babu unakuwa -backed up na mie mshika, mtundika na mtoa madrip. Bila haya madrip huyu mnayemuita Babu yenu leo ii asingekuwa na uwezo wa kutuma post hata moja achilia mbali kupokea simu.
Ninawashukuru wote kwa kumfanikishia huyu Babu siku njema na ninawaomba mmalizie malizie kwani mie kesho alfajiri ninapiga hodi chumbani kwake na drip yangu.! Babu kumbuka pia kuwa una dozi ya sindani 3 za kwenye makalio so jiandae, masuala ya kutusumbua hadi tupate watu wa kukushika hatutaki.